CCM siyo chama tena hili ni kampuni la watu fulani wachache wenye hisa zao ndani ya kampuni hili

binti ashura

Senior Member
Jan 14, 2011
118
19
Ndugu zangu habarini za asubuhi!, mie nimekuwa nikifuatilia mwenendo mzima wa chama cha mapinduzi, nikaja gundua kuwa chama hiki sasa kinasimama kama kampuni ambalo lina wakurugenzi, na mameneja wakujitolea ambao ni wenyeviti kuanzia mikoani mpaka ngazi ya mtaa na mabarozi wa nyumba kumi (ingawa hiyo ya nyumba kumi ilishageuzwa siku nyingi mpaka sasa hakuna balozi anaesimamia nyumba kumi tu ila wanasimamia mpaka nyumba 70). mabalozi hao huwa wanathaminiwa wakati wa kampeni tu, ikipita hapo chama kinakuwa cha wakurugenzi tu. tena wale wenye hisa nyingi ndiyo wenye sauti kubwa (hii hainipi shida kwakuwa ni kawaida ya makampuni yote mwenye hisa nyingi ndiye mwenye sauti zaidi katika kampuni). kampuni lenyewe linaendeshwa kibepali wapo tayari watu wapate shida ilimradi wapate faida kubwa. ukiona umeanza kuipenda ccm ujue unaelekea kujengeka kuwa na moyo usiokuwa wa huruma kwako na hata kwa familia yako. naamini hata kama angefufuka leo Nyerere asinge jiunga na CCM. ninaushahidi wa kutosha kuwa asingejiunga CCM, tazama jana hata yule mzee ngombalemwilu ambaye alivaa na suti zile za kipindi kile cha ujamaa kuonyesha kuwa yeye ni mwanaujamaa safi, na alikuwa miongoni mwa waliohamishia taifa hili kwanye mfumo wa ubepari na Juzi tumemsikia akisema taifa lina shida ya viongozi (hapo si anashindwa tu kutoka). poleni sana wana ccm mnaoishi maisha ya unafiki, un..................., na uzandiki.
 
Tukupe pole wewe uliyekaa chini na kuandika huu upupu wote.
 
Kingunge na yeye ni Fisadi tu kama walivyo mafisadi wengine.
Hata akitoa kauli gani namwona ni mnafiki tu!
 
Ulichoongea humu ndicho pia kipo CDM. Sasa sijui hoja yako ni nini? Tena kwa Chadema, wamiliki ni familia mbili tatu tu na wengine hawaruhusiwi hata kujua kinachoendelea.
 
Ulichoongea humu ndicho pia kipo CDM. Sasa sijui hoja yako ni nini? Tena kwa Chadema, wamiliki ni familia mbili tatu tu na wengine hawaruhusiwi hata kujua kinachoendelea.

Mbona jazba jamani? Mtoa thread hajsema cdm siyo ama ni kampuni, kama cdm nayo imekaa ki kampuni kampuni nayo itasemwa katika thread nyingine lakini siyo lengo la mtoa thread hii.

Kwakuwa hii ni thread inayohusu ccm,
mchango wangu ni mfupi tu,
kama makampuni mengi yanavyomilikuwa na matajiri wakubwa, ndivyo ilivyo ccm,
wananchi ni manpower yao,
wamiliki wake walinunua hisa zaidi ya 50 ya ccm ya nyerere,
wauzaji wa hisa hizo hasa ni Mzee Ruksa,Mkapa na kikwete akawaongeza hisa. Walifanya hivi wakati walipokuwa CEO wa ccm ya nyere.
Sijuwi walikuwa na shida gani(ccm ya nyerere) mpaka kuamua kuuza hisa zaidi ya 50 kwa matajiri na familia chache! imeewauza mpaka watendaji wake wakuu waliokuwa waaminifu kwake kama mkapa na kingunge nk.
Nini lilikuwa tatizo hasa mimi sijui.
Tuchukuwe hatua sasa.
 
ni kampuni ya kifamilia zaidi familia za karume,mwinyi,kawawa,nyerere,rupia,bomani,kahama,sykes,makamba,nnauye,kikwete ndizo zenye hisa
 
ndugu zangu habarini za asubuhi!, mie nimekuwa nikifuatilia mwenendo mzima wa chama cha mapinduzi, nikaja gundua kuwa chama hiki sasa kinasimama kama kampuni ambalo lina wakurugenzi, na mameneja wakujitolea ambao ni wenyeviti kuanzia mikoani mpaka ngazi ya mtaa na mabarozi wa nyumba kumi (ingawa hiyo ya nyumba kumi ilishageuzwa siku nyingi mpaka sasa hakuna balozi anaesimamia nyumba kumi tu ila wanasimamia mpaka nyumba 70). Mabalozi hao huwa wanathaminiwa wakati wa kampeni tu, ikipita hapo chama kinakuwa cha wakurugenzi tu. Tena wale wenye hisa nyingi ndiyo wenye sauti kubwa (hii hainipi shida kwakuwa ni kawaida ya makampuni yote mwenye hisa nyingi ndiye mwenye sauti zaidi katika kampuni). Kampuni lenyewe linaendeshwa kibepali wapo tayari watu wapate shida ilimradi wapate faida kubwa. Ukiona umeanza kuipenda ccm ujue unaelekea kujengeka kuwa na moyo usiokuwa wa huruma kwako na hata kwa familia yako. Naamini hata kama angefufuka leo nyerere asinge jiunga na ccm. Ninaushahidi wa kutosha kuwa asingejiunga ccm, tazama jana hata yule mzee ngombalemwilu ambaye alivaa na suti zile za kipindi kile cha ujamaa kuonyesha kuwa yeye ni mwanaujamaa safi, na alikuwa miongoni mwa waliohamishia taifa hili kwanye mfumo wa ubepari na juzi tumemsikia akisema taifa lina shida ya viongozi (hapo si anashindwa tu kutoka). Poleni sana wana ccm mnaoishi maisha ya unafiki, un..................., na uzandiki.
unatumia kinywaji gani mkuu...?
 
Ulichoongea humu ndicho pia kipo CDM. Sasa sijui hoja yako ni nini? Tena kwa Chadema, wamiliki ni familia mbili tatu tu na wengine hawaruhusiwi hata kujua kinachoendelea.
we msengerema sio lazima ulinganishe CCM na CDM
 
Sasa CCM ikiwa kampuni na Chama kinachorithiwa na mkwe utakiitaje? unanchekesha!
 
Sasa CCM ikiwa kampuni na Chama kinachorithiwa na mkwe utakiitaje? unanchekesha!

unafanya kazi nzuri sana, kukitetea chama chetu.
big up! haiwezekani chama kinachafuliwa kiasi hiki wakati nyie wenye nacho mpo. wasaidieni na wenzeno wawe na moyo huohuo. kumbuka chama kwanza Taifa badae!. CCM hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
 
Back
Top Bottom