CCM sio chama cha siasa, ni kampuni ya Familia za Kifalme

Ingekuwa CHADEMA kingetajwa kama chama cheye mfumo wa kifalme, lakini kwa kuwa ni CCM, sawa tu, A Mornach party. i.e Makamba senior & Junior, Nnauye Senior & Junior, Sumari Senior & Sumari junior, Mwinyi senior & Mwinyi Junior, Karume senior & Karume Junior,
Kikwete & Ridhiwan, Kawawa Senior vs Junior, Wasira senior vs junior, Masauni senior Vs Junior, Mongela senior vs junior, Mapachu senior vs junior, mzindakaya senior vs junior orodha ni ndefu inayotengeneza mpaka mduara wa ufisadi. Na wewe ongezea uwajuao.

Hapo mbona tafauti
 
Nawashangaa sana hawa jamaa toka ASP - TANU - CCM watu ni wale wale hakuna koo zingine tukaona mabadiliko?
 
Umeona mkuu wa-TZ tulivyo mataahira? Eti kuna watu hawaoni kama ni tatizo? Eti wanakwambia uache wivu! Wananitafutia BAN hawa!
 
Umeona mkuu wa-TZ tulivyo mataahira? Eti kuna watu hawaoni kama ni tatizo? Eti wanakwambia uache wivu! Wananitafutia BAN hawa!

Baelezee tu mkuu zama za sasa kwa vijana ni kuambiana ukweli, hawa ndo wanaosubiri kutafuniwa, posho za elf5 baada ya kampeni, pakiti ya chumvi, na khanga ccm kwa wazee wao. wataendelea kuwa watumwa tu.
 
WanaJF,

Ningependa kutoa dukuduku langu kuhusu huu uongozi wa nchi yetu ya Tanzania. Umekuwa na utaendelea kuwa ni uongozi wa kurithiana!

Je, kuna tofauti gani ukilinganisha na nchi zinazotawaliwa kifalme?

Hebu tuangalie mfululizo wa viongozi wetu waliotangulia na hawa wa sasa utagundua Kuwa wengi wao ni watoto wa viongozi waliotangulia;

Ukiangalia Mawaziri wetu na Wabunge, utagundua kuwa hakuna asiekuwa mtoto wa kiongozi fulani.

Tukiangalia kiundani zaidi, utagundua kuwa tunaongozwa na viongozi wa kurithiana kama ufalme kwani wengi wa watoto wa viongozi tunawaona madarakani na wengi wapo njiani kuja kuchukua madaraka mbalimbali.

Swali langu; Je, tupo tayari kuongozwa kifalme?

Je, hakuna wasomi wengine wanaoweza kushika madaraka au kutuongoza isipokuwa ni lazima iwe watoto wa viongozi?

Asanteni sana..

Sasa na tuchangie hii mada..
 
Marekani mpaka sasa bush wawili mtoto na mwanae washakuwa marais, na akitoka obama anaingia bush mjukuu. tuangalie uwezo na sio familia.
 
Kwahiyo hakuna mfano wa kuigwa isipokuwa marekani mbona kwenye maendeleo hufananishi na marekani kihio

Nyoka hazai mjusi wala Simba hatozaa Tembo. Maji hufuata mkondo;

1: Mbona hushangai Peter Manyika v/s Manyika Peter. Halfan Ngassa v/ Mrisho Ngassa. John Tegete v/s Jerry Tegete. Ally Moshi Haruna Moshi?
2: Mohammed Ally v/s Sonia Ally. May weather snr v/s Jnr maywearher.
3: Freeman Aikael(Mbowe) vs Mzee Mbowe ( Mbowe hotels
4: Tx Moshi vs Moshi Jnr. Max bushoke vs Bushoke Jnr.

Kama mtoto ama mjukuu wa kiongozi anazo sifa za kuongoza tusiweke vikwazo.
 
Hata kwenye mpira pia ni kumekaa kifalme. Halifan Ngasa Mrisho Ngasa, Jamhuri Kiwelu Mtwa Kiwelu, Blind yule wa Man U alikuwa na baba yake pia, Watoto wa Beckam wapo Arsenal n.k, Siasa ni mchezo kama ilivyo michezo mingine, so relax kijana.
 
Kwa muelekeo huu tumekwisha hii sumu tulienyweshwa itatumaliza nimeamini ni wengi tuliochukia utumwa na kuukataa na kuupokea utumwa mamboleo kwa mikono miwili hapo ni kawa na kukataa kutumia kitu fulani cha analogy na kuja kukitumia tena kwa njia ya digital ulikikataa na sasa unakitumia tena kisa ni digital
 
Pole jamani cenzo...ama very sorry nimecheka sana pekee yangu barabarani natembea nikahisi kama nakuona mwenyewe...umejipinda kweli kweli ukifikili unavielelezo toshelezi. Lakini uchambuzi wa wenye vigezo tosha kama wa Ipogolo ukashushia na funga kauli ya mcubic..ka umepigwa upper kati au ya chemba ukaa chini taaratibu.

Ukweli dunia imebadilika sana sana tena isivyotalajiwa mno...mojawapo ni ili la GENETICS.
 
Acha akili za bavicha marekani mpaka sasa bush wawili mtoto na mwanae washakuwa marais,na akitoka obama anaingia bush mjukuu.tuangalie uwezo na sio familia.

Hivi hapo yeye kajitambulisha ni kutoka chama gani? Unataka kusema ktk ccm hakuna wanaoweza kuikosoa serikali? Mbona mnatawaliwa sana na itikadi hata ktk mambo ya msingi?
 
Kwa muelekeo huu tumekwisha hii sumu tulienyweshwa itatumaliza nimeamini ni wengi tuliochukia utumwa na kuukataa na kuupokea utumwa mamboleo kwa mikono miwili hapo ni kawa na kukataa kutumia kitu fulani cha analogy na kuja kukitumia tena kwa njia ya digital ulikikataa na sasa unakitumia tena kisa ni digital

Ktk nchi nyingi za kiafrika hii ndio hali halisi na labda tuseme kuwa afrika tunaiga mfumo wa kitawala wa marekani
 
Hata kwenye mpira pia ni kumekaa kifalme. Halifan Ngasa Mrisho Ngasa, Jamhuri Kiwelu Mtwa Kiwelu, Blind yule wa Man U alikuwa na baba yake pia, Watoto wa Beckam wapo Arsenal n.k, Siasa ni mchezo kama ilivyo michezo mingine, so relax kijana.

Duu jamaa upo vizuri kwenye kumbukumbu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom