CCM siasa mnayoieneza Arumeru iko siku ita-backfire

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
79
Jamani nimepitia You tube na nikaikuta clip moja imewekwa ya Kijana Livingstone Lusinde Mbunge wa Jimbo la Mtera, aliyoyaongea wakati anampigia kampeni Mgombea wa CCM yanashangaza na huwezi amini kuwa yanatolewa na mtu ambaye ni mbunge. Ni Matusi mazito yasomithilika, nashindwa kuelewa je anayetukanwa hawezi fungua kesi kwa haya???
Hebu angalia clip hii:

Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru - YouTube

nawasilisha
 
dah dah dah, nimeshindwa kumaliza kuangalia huu usengerema
 
Tumesharushiwa hii kitambo. Kwa utuuzima wangu nimeweza kuisikiliza maramoja Tu. Kwasasa hata unipe milioni siwezi thubutu kuyasikiliza matusi makubwaa haya toka Kwa kiongozi wetu Muhimu kichama na kiserikali ambaye anatuwakilisha Bungeni na kutuamulia mambo makubwa ya kitaifa. Pia Sijui tunawafundisha mini vijana wetu.
 
Kwa huu mtindo wa kampeni tujiandae na vita tu, chuki inayoenezwa ni bora kila mtu tayari kwa lolote.
 
Natafuta sred inayounga mkono matusi haya.. Wapi rejeo wapi mama porojo.. Umeona jinsi mimba inavyochukuliwa Kama katuni Jukwaani .. Embu niwaone hapa.. Tuweni waungwana kwenye kosa tuseme ni kosa sio kuhalalisha everything..
 
Natafuta sred inayounga mkono matusi haya.. Wapi rejeo wapi mama porojo.. Umeona jinsi mimba inavyochukuliwa Kama katuni Jukwaani .. Embu niwaone hapa.. Tuweni waungwana kwenye kosa tuseme ni kosa sio kuhalalisha everything..

Kuna wakina chinchilla na jacksonmichael/michael jackson ndio ambao nahisi kwa leo wapo on duty!!!
 
Back
Top Bottom