CCM Sengerema si shwari, wamkataa Katibu wao

JOB SEEKER

Senior Member
Aug 1, 2011
145
33
ccm.png


HALI ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza si shwari, baada ya kile kinachodaiwa Kamati ya Siasa ya CCM kumkataa Katibu wa chama hicho wilayani humo, Rahel Washa, kwa tuhuma za kuanza kupanga safu ya viongozi wa kambi ya kigogo mmoja wa chama, kwa lengo la kutafuta ushindi wa Ubunge mwaka 2015; Imeelezwa.

Inadaiwa kwamba, Katibu huyo wa CCM wilaya ya Sengerema, ameonekana dhahiri kuanzisha makundi ya kukigawa chama kwa maelekezo ya kigogo huyo (jina na nafasi yake ya uongozi tunalo), na kwamba hali hiyo hawaikubali maana imelenga kukibomoa chama na kutoa nafasi kubwa kwa wapinzani hasa Chadema kushinda kwenye Uchaguzi mwaka 2015.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM wilaya ya Sengerema zinaeleza kwamba, Katibu Washa (53), alikataliwa na wajumbe wanane kati ya 12 wa Kamati ya siasa ya wilaya hiyo Januari 7 mwaka huu, mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya chama hicho mkoa wa Mwanza, walipokutana kwenye kikao cha usuluhishi mjini Sengerema.

“Wajumbe wanane kati ya 12 waliohudhuria kikao walisimama na kutaka Raheli Washa aondoke Sengerema. Walisema haya tena mbele ya katibu wa mkoa na wajumbe wa kamati ya maadili ya chama mkoa.

Endelea kusoma: http://www.fikrapevu.com/habari/ccm-sengerema-si-shwari-wamkataa-katibu-wao
 
Wewe binafsi unasemeaje ishu hiyo?
Vinginevyo unaonyesha hujathubutu kuisoma kabisa!
 
Alisema, mwanzo hadi mwisho wa kikao hicho hakuna mjumbe aliyesimama na kumtuhumu kwa hayo mambo, badala yake walizungumzia mgogoro uliopo kati ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sengerema, Jaji Tasinga Gabanyaga na mbunge wa Buchosa, Dk. Charles Tizeba.

Hivi huyo mwenyekiti wa CCM wilay ni Jaji kweli kweli in the meaning of Judge au?? Siamini kama Jaji wa kiukweli anaweza kujishusha hadhi yake namna hiyo na kuwa mwenyekiti wa chama wa wilaya??
 
Hivi huyo mwenyekiti wa CCM wilay ni Jaji kweli kweli in the meaning of Judge au?? Siamini kama Jaji wa kiukweli anaweza kujishusha hadhi yake namna hiyo na kuwa mwenyekiti wa chama wa wilaya??



ni jina lake mkuu...ni mtu anayetumiwa sana na ngereja kuiharibu ile wilaya na kuleta mkanganyiko mkubwa...ana duka lake la madawa pale sengerema mjini barabara ya kwenda sengerema sekondari/sengerema parokiani...hana shule ya maana ila mdomo unamuwezesha kuishi pale wilayani....anautumia vyema
 
Sometimes huwa naona tuwaache tu hawa CCM because they are creating their own downfall, wala hatuhitaji kuandamana.
 
Back
Top Bottom