dosama
JF-Expert Member
- Dec 25, 2010
- 912
- 957
Source Mwananchi
Chama cha Mapinduzi CCM kimekiri kuwa Makundi yanakiuwa chama na ugomvi na vurugu hizo ni sawa na ugomvi wa Nato na G8 na wakati huo huo Maige kamtaja Nape kama gamba sugu linalotakiwa kung'olewa ndani ya chama na Amemtahadharisha Spika Makinda kuwa katika kikao cha Bajeti atasema madukuduku yake yote yanayomsumbua.
Nchi zinazounda G8 ni Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Russia na Uingereza ambazo pia baadhi yao, ndizo zinazounda Nato, umoja wenye wanachama 28.
Mukama alitoa kauli hiyo juzi wilayani Rufiji wakati akizungumza na umati wa wananchi na wanachama wa chama hicho waliofurika katika Viwanja vya Corecu, Kata ya Kibiti.
Alisema baadhi ya wanachama wa CCM wamekuwa ni wasaka madaraka na wanapokosa huamua kuunda makundi ya uhasama ambayo hawataki kuyavunja pindi mchakato wa kutafuta mgombea unapomalizika.
Makundi yaliyoundwa tangu 2005 na 2010 yanaendelea kukitafuna chama, wanachama wakinyimwa uongozi wanaanza uhasama, hatufiki malizeni makundi, alisema.
Alisema makundi hayo pia yako katika Wilaya za Mkuranga na Rufiji, ambako katika ziara yake amebaini mpasuko mkubwa unaotokana na fitina na uhasama miongoni mwa wapenzi na makada wa CCM na kusisitiza kwamba hayafai na ni hatari kwa mustakabali wa chama hicho kikongwe barani Afrika.
Nikiwa Mkuranga nilitaarifiwa kuwa kuna makundi ya Nato na G8 na sasa nimefika Rufiji nimeyakuta makundi hayo. Jamani makundi hayo ya nini?
Mukama ambaye aliwahi kushika nafasi mbalimbali za kiutendaji zikiwemo za Ukuu wa Wilaya ya Mafia akimrithi mtangulizi wake Hemedi Mkali, alisema aliwahi kugombea ubunge wa viti vya Taifa kupitia Juwata (iliyokuwa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania), na aliposhindwa alikubali matokeo.
Alisema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema bila CCM imara nchi yetu itayumba, akimaanisha kuwa hakuna chama mbadala cha kuongoza nchi zaidi yake.
Alitoa mfano wa Chama cha Democrat cha Marekani kwamba wanachama wake hawana kadi, bali mapenzi ya chama yako mioyoni mwao na wanapojiunga hawafanyi hivyo kwa lengo la kusaka madaraka... Hii ni tofauti kubwa na nchi zetu ambako mtu akijiunga na chama kitu kwanza kufikiria ni kusaka madaraka, alisema.
Alisema chama hicho kina mkakati madhubuti wa kupambana na watu wachache wanaotaka kukimiliki wakitumia nguvu ya fedha.
Alisema baadhi ya wanachama wa kawaida wamejiona kuwa hawana nafasi katika chama chao wakiamini kuwa kimetekwa na wenye fedha na kuongeza kwamba mwanachama wa kawaida hawezi kuongoza bila rushwa.
Katika Tanzania Daima Ya Nape na Maige
KATIBU wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye ametajwa kuwa gamba namba moja linalotakiwa kuvuliwa, kwa kile kilichodaiwa kutoa matamshi mengi ambayo yamekivunjia heshima na kukidhohofisha chama hicho.
Nape pia ameshutumiwa kwa kushindwa kwake kubuni mbinu za kuingiza wanachama na zaidi kupambana na wimbi la kuhama kwa viongozi, makada na wanachama wa CCM.
Shutuma hizo nzito zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Ezekiel Maige (CCM) jana wakati akizindua matawi mawili ya wakereketwa wa chama hicho ambao ni wajasiriamali, katika Kijiji cha Isaka wilayani hapa.
Maige alisema kuwa Nape amekuwa akitoa kauli ambazo si za msingi, zisizojenga bila kujua kuwa zinakidhohofisha chama hicho tawala.
Mbunge huyo ambaye amepata kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema kwa sasa kuna wimbi kubwa la wana CCM wanaohamia vyama vya upinzani, ambalo ilitegemewa kuwepo kwa juhudi za makusudi za kuzuia chini ya usimamizi wa katibu huyo wa itikadi na uendezi.
Kitendo cha CCM kupoteza wanachama zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja mkoani Arusha na sehemu nyingine wanachama 3,000, kinashitua, na ilitegemewa Nape kusimama imara na kuhakikisha chama hakiendelei kupoteza wanachama wake, lakini ndio kwanza anasema hajali na eti hao ni makapi, alisema kwa kushangaa.
Nape akihutubia vijana mjini Bukoba siku chache zilizopita, alidai kuwa hata kama wanachama wote watahama, yeye (Nape) atabaki peke yake na CCM haitakufa.
Alidai kuwa kasi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) haiwezi kupuuzwa na kiongozi makini, na kuongeza kuwa zinahitajika busara na bidii za kuwapa moyo waliopo ili nao wasiondoke na si kuwasimanga.
Jamani Nape anachokifanya sasa ndani ya chama mimi ninaweza kuamini kwamba anatumika na kukidhi matakwa ya waliomtuma na si manufaa ya chama.
Ninalolisema hapa lisitafsiriwe kwamba nalilia uwaziri, hapana, ila ni uchungu nilionao kwa chama changu kuona kila siku tunavyopoteza idadi kubwa ya wanachama, tuliyemkabidhi jukumu la uenezi anasema hajali, sasa huyu si atupishe mapema kabla mambo hayajaharibika?
Maige alimwomba Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja kutumia nafasi yake kuwashauri wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuchukua hatua za haraka dhidi ya Nape.
Wakati Maige akitoa maneno hayo mazito, Mgeja alikuwa ameinamisha kichwa chake chini, lakini mamia ya wana CCM pamoja na wananchi wengine walishangilia kwa nguvu.
Jk chama kinamfia mikononi mwake