Ccm sasa shule hadi shule

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
298
Jumuia ya wazazi CCM mkoa wa Kilimanjaro sasa wanapita shule hadi shule wakihamasisha maadili kwa wanafunzi.

Walijaribu kutolea mifano ya vurugu za Tegeta na ishu ya wanachuo wa UDOM kutaka kuingia ukumbini kujadili muswada, Walidai maadili yangekuwepo yasingetoke mambo yale.

Walisisitiza kuwa hawakuja kwa ajili maswala ya kichama japo wao ni wana CCM. Hayo yalitoke shule ya sekondari Mawenzi- Moshi. ilikuwa ijumaa tar 8 april 2011.

Wiki hiyo hiyo Mwenyeketi wa wazazi CCM Ngawaiya alitembelea Kawe Sekondari, ambako aliituhumu CDM kuwa inapokea fedha toka U.S.A ili kuleta vurugu.

Siujui ni kurejesha imani kwa wananchi hasa vijana ili zomeazomea isiwakumbe watakapoanzisha maandamano ya kumpongeza JK kwa kilichoendelea Dodoma.
 
Wamechelewa sana watoto wa kimaskin hawatakubali kudanganywa kwa peremende na pipi na do sababu sie shule tunawafundisha Education for Liberation/Emancipation and not for reterdation...
 
Wamechelewa sana watoto wa kimaskin hawatakubali kudanganywa kwa peremende na pipi na do sababu sie shule tunawafundisha Education for Liberation/Emancipation and not for reterdation...
Inawezekana wamechelewa kwani wakati wanajitambulisha karibu ilete tafrani, waliposema tu wanatoka CCM, wanafunzi walianza kuguna.
 
kheee kweli hawa jamaaa wanajivua magamba...wanaenda mpaka mashuleni sasa
 
Hatuwatambui hao,tena ni vema wakasitisha zoezi hilo.Wao ni jumuiya ya wazazi wa CCM na si wazazi Tz.Hilo zoezi lao walifanyie huko huko kwao si wana kikundi cha chipukizi?eboo....
 
Hawana jipya wameishiwa ndo sababu wameona watoto ni waoga wa vitu kama vifo hivyo wakaanza kuwatisha kwa kutumia mifano ya tegeta, what i know ni kwamba haiwezi kusaidia, sana itaharibu kwani wanatakiwa kuwafundisha sababu zilizo pelekea watu kuuana na ninani aliye husika? By the way migogoro ya ardhi kama kule Tegeta ni tatizo kubwa ambalo kwa mtoto wa kawaida kumfundisha ni kumuonea kwakuwa hawezi kuelewa kirahisi, ni vizuri wafundishwe kujitetea pia pindi watakapo onewa na si kila jambo kulinyamazia tu.
 
Kama waliwapeleka watoto ukumbini saa 11 asb, watashindwa nini. Hawana aibu
 
Hatuwatambui hao,tena ni vema wakasitisha zoezi hilo.Wao ni jumuiya ya wazazi wa CCM na si wazazi Tz.Hilo zoezi lao walifanyie huko huko kwao si wana kikundi cha chipukizi?eboo....

Sijui CDM au vyama vingine vikiomba nafasi ya kuongea na wanafunzi kama uongozi wa hizi shule watatoa nafasi.

Ningetamani vyama vya upinzani wauombe nafasi ya kuongea na wanafunzi.
 
Wapeleke ujinga wao sehemu nyingine sio kwenye vichwa vya wadogo zetu na watoto wetu...............................
 
Back
Top Bottom