CCM sasa ni kama Dereva wa Basi la abiria aliyeacha usukani wake na kuanza kubishana na abiria wake

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,601
338
Jamani wanaJF kwa kweli CDM inawafanya CCM hawalali siku hizi. Mi nawalinganisha CDM kama mtu aliyeshika remort ya TV ambayo ukiiambia zima unaissue comand na inazima. TV hapa ni CCM maana wao sasa wanaonekana they cannot control themselves.

Mbaya zaidi ni kwamba sasa CCM inaonekana kama dereva wa basi la abiria ambaye ameacha usukani wake na kuangalia barabara sasa amewageukia abiria na kuanza kubishana nao. Kinachofuatia hapa ni ajaali mbaya kabisa. Hivyo CCM wameacha wajibu wao wa kuongoza nchi na kuwaletea watz maendeleo sasa juhudi zao ni kwuimaliza CDM, kinachofuata hapo ni kuanguka kabisa kwa CCM. Hususani tunaona kuna kero nyingi sana sasahivi kama ya umeme, maji nk. Mi ningewashauri CCM kuwa kujisafisha kwao kusiwe kutaka kuiangamiza CDM bali wapambane na kero za wananchi (recovery process) na ndipo hapo watakuwa wamejisafisha. Kinyume na hapo wasitegemee mabadiliko zaidi. Tunategemea 2015 watuambie hakuna tatizo la maji kadhalika umeme. Nyie vibaraka mliotumwa na wanamagamba wa CCM muende mkawaambie waje wajibu hoja wao wenyewe na si vinginevyo.
 
Ukweli haupendwi hata siku moja utaambiwa unahatarisha amani na utulivu. Lakini bado natafakari hili basi ambalo dereva wake ameacha majukumu yake anabishana na abiria tuombe kuwa hatuko sehemu zenye milima au mabonde makubwa kwani ajali yake ni mbaya sana. Mungu ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom