CCM: Ni Nani aliye Msafi Aanze Kumtupia Jiwe Lowassa?

Polonium210

Member
Nov 24, 2011
58
39
Natambua kwamba Lowasa Ni Fisadi kwa maana hakuna aliye msafi ndani ya CCM. Nimefatilia Sarakasi za Cheusi Chekundu zinazochezwa na CCM kujivua gamba na Namna ambavyo akina Nape wanavyojaribu kutuaminisha kwamba Wakimfukuza Lowasa na Chenge basi CCM kitakuwa ni Chama safi machoni mwa Watanzania na kwamba sasa wananchi watakipokea tena na kukipa Free Pass ya Kutawala Nchii hii kwa miaka mingi Ijayo. Well Yeyote anayeamini kwamba Kuondoka kwa Lowasa kutakifanya CCM kuwa Chama Safi kisicholea Ufisadi huyo sina jina lingine la kumwita isipokuwa ni JUHA. Ningependa kuuliza maswali yafuatayo

1. Nani alikuwa AG wakati Serikali ina sign Mkataba wa Buzwagi? Yuko wapi huyu Mtu
2. Ni nani aliyesema Richmond ni Safi haina Tatizo? Yuko wapi huyu mtu
3. Ni akina nani waliounda Mtandao Ulioiba Pesa Benki kuu kugharimia JK awe Rais 2005? Wako wapi hawa wanafanya nini?
4. Ni nani aliyesign Mikataba ya IPTL? Yuko wapi huyu?

Kinachoendelea Dodoma ni mazingaombwe na Sarakasi za lile Kundi la Kimafia ambapo hapa kwetu limesajiliwa kama Chama cha Siasa kwa jina la CCM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom