CCM na ushindi serikali za mitaa

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Najiuliza maswali mengi, imekuwaje CCM ipite bila kupingwa sehemu nyingi za TZ kwenye uchaguzi wa mitaa na vijiji?

malalamiko yalikuwa kwa tume ya uchaguzi, sasa yenyewe imesema haitasimamia,

Ina maana hiki chama bado kinakubalika kiasi hiki? au ni kiini macho,

kama ni hivyo basi sisi waTz sio wakweli, tunapiga kelele sana kuwa hatukitaki hiki chama, kumbe tunakipitisha bila kuweka wagombea INAKUWAJE?????!!!!
 
CHADEMA, CUF, NCCR walia faulo

na Nasra Abdallah

[Source Tanzania Daima]

VYAMA vya upinzani vimelalamikia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu, kuwa ni wa wizi mtupu baada ya baadhi ya wagombea wao kuenguliwa, huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikitumia mbinu chafu kujipatia ushindi.

Vyama hivyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF).

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema wagombea wa vijiji 104 wilayani Handeni mkoani Tanga wameenguliwa bila sababu za msingi.

Alisema wagombea kutoka vijiji hivyo, walienguliwa na Mkurugenzi wa wilaya hiyo kwa madai kuwa wamepiga mihuri katika ofisi za chama badala ya kata.

Kutokana na madai hayo, Profesa Lipumba alisema hawajaridhika na hatua hiyo, kwa kuwa sheria ya uchaguzi inamruhusu mgombea kupigiwa muhuri na ofisi za chama ili mradi tu awe ametimiza vigezo vinavyohitajika.

Pia katika mkutano huo, mwenyekiti huyo aliwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya karatasi za kupigia kura ambazo alidai tayari CCM inazo, jambo ambalo alisema litavinyima haki vyama vingine vya siasa.

“Hebu fikiria, hadi saa hizi, wenzetu tayari wanamiliki karatasi za kupigia kura, kitendo ambacho kinaweza kuwapa nafasi ya kuwapa watu mitaani ili wajaze na inapofika siku ya kupiga kura, wanakwenda tu kutumbikiza karatasi hizo,” alisema Profesa Lipumba.

Kutokana na hali hiyo, alisema wanafanya taratibu na wanasheria wao ili kuweza kufungua kesi mahakamani kupinga vitendo hivyo.

Maeneo mengine ambayo CUF inalalamika kuchezewa rafu katika mchakato wa uchaguzi huo, ni pamoja na Wilaya ya Temeke, ambako mgombea wake Omar Lwambo katika Kata ya Tambukareli, alienguliwa kwa madai kuwa hajui kusoma na kuandika.

Lipumba alisema mgombea huyo alijaziwa fomu na mtu mwingine na baadaye aliweka saini, jambo ambalo alidai si kosa kwani hata yeye wakati akijaza fomu za kugombea urais, alijaziwa na mtu mwingine na baadaye aliweka saini yake.

Faulo hizo za uchaguzi, zinadaiwa pia kufanyika mkoani Tabora ambako Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Chemchem, amewapitisha wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa Serikali za Mitaa Kata ya Chemchem waliodhaminiwa na Ofisi ya Katibu Kata CCM badala ya Katibu wa Tawi.

Lipumba alisema hali hiyo ni kinyume na kanuni za uchaguzi kwani mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa katika mamlaka za miji za mwaka 2009, zinasema mkazi yeyote wa mtaa anaweza kugombea uenyekiti wa mtaa au ujumbe ikiwa ni mwanachama na amedhaminiwa na chama cha siasa.

Malalamiko kama hayo, pia yalitolewa jana na CHADEMA baada ya mgombea wake, Yohana Kabiza kutishiwa kuuawa endapo ataendelea kufanya kampeni.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam jana, Kabiza anayegombea nafasi hiyo, Mtaa wa Migombani, Segerea, jijini Dar es Salaam, alisema vitisho hivyo vimetolewa na mmoja na wapinzani wenzake kutoka vyama vingine wanaowania kiti hicho.

Alisema kabla ya kupata vitisho hivyo, juzi majira ya saa 12 jioni alikuwa katika kituo cha daladala cha Kona akigawa vipeperushi kwa wananchi waliokuwa wakishuka kwenye daladala na ghafla akatokea mtu asiyemfahamu na kumnyang’anya vipeperushi hivyo huku akidai yeye ni polisi.

“Kabla hajaninyang’anya vipeperushi hivyo, aliniambia nimpe nikakataa…alinitisha nikampa vipeperushi 20, aliendelea kuniambia nitampa vipeperushi nilivyobaki navyo au simpi na kusema yeye ni polisi, ndipo aliponinyang’anya vingine 70,” alisema Kabiza aliyemaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Nacho chama cha NCCR Mageuzi, kimelalamikia mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa serikali kutaka kuipatia ushindi CCM katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ya chama hicho jijini Dar es Salaam, jana, Mkuu wa Idara ya Sheria na Haki za Binadamu, Dk. Sengondo Mvungi, alisema CCM imekuwa ikitumia mtandao wa serikali kwani kuna ushahidi wa barua iliyokamatwa na chama hicho.

Alisema barua hiyo iliyoandikwa na katibu tawala kwenda kwa afisa uchaguzi wa wilaya, inamtuhumu Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kasulo wilayani Ngara, Abdu Ngangula kwa kushindwa kumpigia kampeni mgombea wa CCM, hivyo anapaswa kuondolewa.

“Kwa kweli inatia shaka na inaonyesha ni jinsi gani CCM ilivyoamua kuendesha demokrasia ya kihuni na hata ikitokea wameshinda uchaguzi, tunaamini ni kutokana na uhuni wanaoufanya,” alieleza Dk. Mvungi.

Aidha alieleza kuwa matumizi mabaya ya vyombo vya dola, yamezidi kugubika, huku CCM ikifanya hivyo kwa kuelewa kuwa vyama vya upinzani vinaweza kususia.

“CCM imekuwa ikitumia mtandao wa serikali kujua ni maeneo yapi hakuna wagombea, hivyo kujitangazia maeneo hayo kuwa ni washindi,” alifafanua Dk. Mvungi.
 
Huu wizi wa kura na mafia style ukichanganya na ujinga wa wapiga kura itakuwa safari ndefu sana kuondoa hawa taleban,ila napata wasiwasi sana maana nilitegemea sehemu kama Dar,Mwanza ,Arusha wapinzani wangeweza kushinda kirahisi lakini ni kinyume,wapiga kelele wa migawo ya umeme na hali mbaya ya maisha na ufisadi na wanaojiita wasomi na kuelewa demokrasi wamejaa wako Dar lakini upinzani wa kweli uko mikoani kama Mara...nina mpango wa kumshauri Mrema arudi kugombea ubunge Temeke ili akawabwatukie bungeni maana inaweza kusaidia kidogo wasiibe sana
 
<b>kama ni hivyo basi sisi waTz sio wakweli, tunapiga kelele sana kuwa hatukitaki hiki chama, kumbe tunakipitisha bila kuweka wagombea INAKUWAJE?????!!!!

Ni kweli Watanzania hawakipendi chama, ila chama kinajua kucheza sarakasi ili kiwepo madarakani. Sababu kubwa ni njaa na njaa hiyo inaweza kugawanyika katika sehemu mbili.Njaa ya kweli, hii ni ile njaa ya wananchi wa vijijini ambao kwao nguo mpya huvaliwa kila baada ya miaka mitano na pilau ya nyama huliwa kila baada ya miaka mitano. Mara baada ya walalahoi hao kurubuniwa huwa hawana jinsi bali kuchagua chama wasichokipenda.Njaa nyingine ni watu wa mjini ambao wanaona ili kukidhi mahitaji yao njia pekee ni kuwa jirani na chama. Hawa wanakipenda chama kwa maslahi ya kiuchumi tu na si vinginvyo.Woga, hii ni shauri majority ya voters hawajui haki zao za kiraia, na hii kwa kiasi kikubwa ni kuwa asasi zisizo za kiserikali haziwezi kutoa elimu hii kwani sheria ya uchaguzi imekataza kufanya hivyo, wanaoruhusiwa ni tume ya uchaguzi tu.
 
People are despared!..Thats all, and hence they dont expect any changes!
 
Kila che mwanzo kina mwisho . Watu wa mikoa iliyo tajwa hawana tofauti wajuvi wa JF ambao huwanyooshea vidole akina Zitto na Mbowe wakati wako Ulaya na USA machungu ya Kinondoni hawajui .Typical Watanzania bwana
 
wa TZ wachache wenye access ya Jf watanzania wengi sikuhizi wanaona TBC na TBC radio
 
Back
Top Bottom