CCM na Urafiki wenye Mashaka!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Well.. habari ndiyo hiyo! Ukitaka nakala yako kila wiki fuata maelekezo kwenye kijarida ili ujiandikishe.

toleo13_phixr.jpg
 

Attachments

  • TOLEOJIPYA13.pdf
    307.1 KB · Views: 135
Last edited by a moderator:
Hivi hii vita ya ufisadi ni kiini macho au?

Kwa chama kupokea mchango kutoka kwa mtuhumiwa maana yake ni kuwa yeye ni untouchable na ni matusi kwa watanganyika wenye kuipenda nchi yao.
 
Hivi hii vita ya ufisadi ni kiini macho au?

Kwa chama kupokea mchango kutoka kwa mtuhumiwa maana yake ni kuwa yeye ni untouchable na ni matusi kwa watanganyika wenye kuipenda nchi yao.

huu ndio unaitwa urafiki wenye mashaka..
 
Namuona RA "far left- last row" katikati ya Msekwa na Nchimbi....!!!! The King-Maker anawasanifu WA-Tz na njaa na tamaa kali na anampongeza fisadi mwenzake kwa kazi nzuri....

SWALI - Huu urafiki wa mashaka mpaka lini? mbona mashaka yanzidi kuongeza na urafiki unazidi kuongeza? could it be that mashaka na urafiki they are "directly propotional" Kwa hakika SIPATI PICHA
 
Kuna picha moja niliwahi kuiona ila sijaona version yake ya kiingereza ikoje ambayo ndiyo inaitwa "Urafiki wenye Mashaka"..
 
CCM na mapesa ya matajiri hawa!

John Bwire Novemba 12, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

BABA wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliwahi kukiasa Chama cha Mapinduzi kwamba siku ambayo kitawakumbatia matajiri na kuwapa hatamu za uongozi kitakuwa si chama cha kutetea tena haki za wanyonge; bali kitakuwa chama cha kutetea kikundi fulani cha wachache wenye mapesa.

Pamoja na tahadhari hiyo ya Mwalimu Nyerere, aliyoitoa miaka zaidi ya 12 iliyopita, CCM bado hakijabadilika. Bado kinaendelea si tu kuwakumbatia wafanyabiashara matajiri wakubwa na kuwahamasisha kugombea uongozi; bali pia kimeendelea kupokea misaada ya mapesa yao.

Mfano wa hivi karibuni ni wa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo vyombo vya habari viliripoti taarifa za mfanyabiashara anayeitwa Tanil Somaiya kuipa jumuiya ya CCM ya vijana (UVCCM) msaada wa Shilingi milioni 400, fulana 1,000, mabegi 1,000 na kofia 1,000 kwa ajili ya kuendesha uchaguzi wake mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Msaada wa mfanyabiashara huyo ulikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, mjini Dodoma ambaye aliufurahia; kiasi hata cha kumwomba pia atengeneze hata bendera za chama hicho.


Hatuna ugomvi na Somaiya kuonyesha ukereketwa na ukada wake kwa CCM kwa kuimwagia mapesa hayo, lakini hatupendezwi na tabia ya chama hiki tawala kuendelea kuwa tegemezi kwa mapesa ya wafanyabiashara matajiri ili kuendesha shughuli zake.

Na hofu yetu ni ya dhahiri. Wafanyabiashara kote duniani ni watu wanaowekeza mahali ambako wanatarajia kuvuna baadaye. Mfanyabiashara hawezi kutumbukiza mamilioni ya pesa bila kutegemea kunufaika na pesa zake hizo, kwa njia moja au nyingine, mbele ya safari.

Hatuna hakika wafanyabiashara wananufaika vipi na mapesa hayo wanayoyatoa kusaidia kufanikisha chaguzi za Chama, lakini tuna hakika ya kitu kimoja; nacho ni kwamba mapesa hayo yanawafanya wawe ni watu maalumu na wapekee kwa CCM na serikali yake.

Hali hiyo ya kuwafanya waonekane ni watu maalumu na pekee hujenga mazingira ya kuwapo, huko mbele ya safari, kwa mgongano wa maslahi katika utendaji wa Chama na Serikali.

Hiyo iliwahi kuthibitishwa na kauli iliyopata kutolewa miaka michache iliyopita na Waziri Mkuu wa zamani ambaye ni mjumbe wa NEC ya CCM, Frederic Sumaye aliyesema kwamba wafanyabiashara wanaotaka mambo yao yawanyookee waiunge mkono CCM.

Kauli yake hiyo, ambayo mpaka leo haijakanushwa au kufutwa na CCM yenyewe, ilimaanisha kwamba kuna upendeleo maalumu kwa wafanyabiashara wanaoiunga mkono CCM. Na hilo si jambo la kujivunia hata kidogo.

Ndiyo maana ushauri wetu kwa CCM ni ule ule alioutoa Mwalimu Nyerere miaka kadhaa iliyopita; nao ni kwamba chama hicho tawala kiache kukumbatia wafanyabiashara wakubwa, na kiache kukumbatia mapesa yao.

Badala yake kiimarishe miradi yake ya uchumi na pia kitumie vizuri ruzuku kinachopata ili kuendesha vyema mambo yake; ikiwa ni pamoja na kusaidia kifedha jumuiya zake kukamilisha chaguzi; pale inapobidi kufanya hivyo.

Lakini kama itabidi kichangiwe na wanachama wake, wakiwemo wafanyabiashara wakubwa, basi, kuwe na kikomo cha pesa ambacho mtu mmoja anaweza kukichangia.

Kuweka kikomo cha mchango wa mtu mmoja ndivyo wenzetu waliokomaa kidemokrasia huko nje (ikiwemo Marekani), wanavyofanya katika chaguzi zao.

Hatuoni ni kwa nini CCM, kama chama tawala na kongwe nchini, kisionyeshe mfano huo mzuri ili vyama vingine viige.

Vyovyote vile, hakiwezi kuwakumbatia wafanyabiashara matajiri na kikaweza kuendelea kuwatetea vyema wanyonge wa nchi hii ambao ni wakulima na wafanyakazi.
 
Back
Top Bottom