CCM na Serikali za Mitaa wanaandaa wizi wa kura Oct 2010

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Ndugu zanguni habari nzito na ushahidi zinaonyesha jinsi gani CCM na Seeikali za Mitaa yaani Tamisemi wanavyo weka mbinu za wizi wa kura katika uchaguzi mkuu .Madiwani wote na watumishi wa Halmashauri za Watumishi wa Halmashauri kwa muda sasa wamekuwa wakihaha kila kona kutafuta mbinu za kura .Kuhakikisha CCM inashinda na si Upinzani kwa kuwa wengi wana ogopa upinzani kuingia katika Halamshauri unazuia kula yao na kuleta hoja nzito kweney vukao . Maneno haya nina uhakika nayo na kama huamini kuanzia sasa fuatiliani vikao vya siri kweney Halmashauri hizo na viongozi wa CCM.

Ushahidi kamili ni ule wa uchaguzi wa Oct ambapo Serikali za mitaa waliamua kufanya uhuni wa kuchapisha karatasi za kura ki ajabu na bado watgu wakaingia nazo kwenye uchaguzi .Baada ya kufanikiwa lile la karatasi za kura na watanzania kama kawaida hakuna aliye hoji ndipo Tume ya Taifa NEC imeamua kufanya maajabu yale yale na kwa uhakika nia yao ni kuguat wapinzani Bungeni mwaka 2010.

Do something now vinginevyo mwaka 2010 Bunge zima ni la CCM na wataendelea kupeta .
 
wakati fulani mdomo ulimponza kichwa na vita ya majimaji ilianzishwa na watu dizaini kama hii. KIla mtu anamkutano wake usitengeneze uhalali wa maneno ya laana ukiwa bado katika jua bila kujua
 
wakati fulani mdomo ulimponza kichwa na vita ya majimaji ilianzishwa na watu dizaini kama hii. KIla mtu anamkutano wake usitengeneze uhalali wa maneno ya laana ukiwa bado katika jua bila kujua

Fafanua ama jenga hoja upinge niliyo yasema kabla sijaanza kuweka ushahidi hapa ila wenzako wanajua ukweli huu huhitaji University Degree
 
Mwoga daima hawezi kushinda, wizi na mikakati ya kuiba kura imekua ikijirudia katika mijadala mbalimbali kila siku hatua gani imechukuliwa kulalamika tu, Hapana ni lazima twende mbali zaidi ni kiasi gani umma umeandaliwa kwa mabadiliko kama umma haujaandaliwa ipasavyo kila siku tutaongea wizi wa kura. Khomeni alimuondoa Mfalme Shah kwa vipeperushi na mikanda ya hotuba za kujenga hasira kwa umma na kuwapa matumaini. Mizinga na vifaru vya shah havikuzuia mageuzi chimbuko la mageuzi yeyote ni watu (umma) watanzania wako tayari ? Nionavyo mimi ni ujinga wetu na ujasiri wa kuzoea maumivu kama Kaunda aliondoka kwa kwa kura kwa sababu ya kupanda bei kwa sembe tu Watanzania tunazo sababu nyingi na za wazi za kuwaondoa ktk mamlaka viongozi walioshindwa. Tusilaumu tulipoangukia tutazame pale tulipo jikwaa au wizi wa kura utabakia wimbo wa taifa
 
Huu wote ni uongo na uzushi mtupu. Kila mwaka hadithi ya kuiba kura, mbona sijaona wezi wakifikishwa mbele ya vyombo vya sheria ?? .......Acheni zile za jamani tuamueni.... ......huyu mke nitamuumiza ...............kumbe wewe ndiye unapigwa.
 
Back
Top Bottom