CCM NA SERIKALI YAKE IMESHINDWA KAZI iliyopewa na WATZ

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
amka2.gif

JUZI Waziri Mkuu ambaye Kikatiba ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za siku kwa siku za serikali akiwa msaidizi mkuu wa Rais na Makamu wa Rais, alizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu maswala mbalimbali yahusuyo serikali na taifa kwa ujumla.
Tukiwa na jukumu la kuelimisha umma juu ya mambo mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya taifa letu, tunaona kama serikali kupitia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, haijakata kiu ya wananchi.
Katika siku za karibuni kumekuwa na mjadala mkali juu ya hali ya maisha ya Watanzania ambayo inazidi kuwa ngumu kila kukicha.
Bei ya mafuta, nauli, sukari, vyakula na bidhaa zote zilizobaki zikiwemo zile za lazima kwa mahitaji ya binadamu, zote zimepanda kwa kiwango kikubwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu (TEC), Askofu Ruwaichi, akizungumza mbele ya Waziri Mkuu mjini Bunda hivi karibuni alisema, “Ugumu wa maisha unaoshuhudiwa nchini kwa sasa haujapata kutokea tangu wakati wa vita vya Idd Amin miaka ya sabini.”
Hii ni kauli nzito kupata kutolewa na mtu mzito ndani ya nchi yetu kama Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu, tena mbele ya mtu mzito kama Waziri Mkuu.
Kinachotushangaza ni kwamba Waziri Mkuu hakuzungumzia kauli hiyo ya askofu kwenye ibada ile iliyofanyika mjini Bunda wala hakuzungumzia hali ya ugumu wa maisha juzi alipozungumza na waandishi wa habari.
Badala yake katika saa mbili alizozungumza na wana habari, alitumia dakika 45 kuzungumzia tiba ya kiimani inayotolewa na Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwaisapile kule Loliondo.
Ni hivi karibuni tu alipolazimika kuiongelea hali ya ugumu wa maisha inayowakabili Watanzania, Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo alitamka: “Hali ya uchumi ni ngumu, kila Mtanzania abebe mzigo wake mwenyewe.”
Kauli kama hii kutoka kwa waziri mwandamizi ndani ya serikali tena anayeshughulikia fedha na uchumi, si tu haikupaswa kutolewa na waziri bali pia iliivua serikali nguo na kuiacha uchi kwa kuonyesha kwamba wale waliopewa dhamana ya kuiendesha nchi hii hawajui walitendalo.
Lakini kabla hatujakata tamaa na serikali hii tulisikia kwamba Waziri Mkuu angeongea na wana habari, tukapata matumaini ya Pinda kurekebisha makosa katika kauli ya waziri wake wa fedha akiwa ndiye mtendaji mkuu wa serikali.
Tumesikitishwa na kitendo cha Waziri Mkuu kutoongelea jambo hili muhimu ikiwa ni pamoja na kueleza hatua madhubuti zinazochukuliwa na serikali yake kurekebisha uchumi na kupunguza makali ya maisha kwa watu wake. Kweli serikali haijakata kiu ya wananchi maana wananchi wengi walitamani kusikia ni nini kitafanywa na serikali ili bei za vyakula na bidhaa nyinginezo muhimu zishuke na kuboresha kidogo maisha yao.

h.sep3.gif

amka2.gif

JUZI Waziri Mkuu ambaye Kikatiba ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za siku kwa siku za serikali akiwa msaidizi mkuu wa Rais na Makamu wa Rais, alizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu maswala mbalimbali yahusuyo serikali na taifa kwa ujumla.
Tukiwa na jukumu la kuelimisha umma juu ya mambo mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya taifa letu, tunaona kama serikali kupitia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, haijakata kiu ya wananchi.
Katika siku za karibuni kumekuwa na mjadala mkali juu ya hali ya maisha ya Watanzania ambayo inazidi kuwa ngumu kila kukicha.
Bei ya mafuta, nauli, sukari, vyakula na bidhaa zote zilizobaki zikiwemo zile za lazima kwa mahitaji ya binadamu, zote zimepanda kwa kiwango kikubwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu (TEC), Askofu Ruwaichi, akizungumza mbele ya Waziri Mkuu mjini Bunda hivi karibuni alisema, "Ugumu wa maisha unaoshuhudiwa nchini kwa sasa haujapata kutokea tangu wakati wa vita vya Idd Amin miaka ya sabini."
Hii ni kauli nzito kupata kutolewa na mtu mzito ndani ya nchi yetu kama Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu, tena mbele ya mtu mzito kama Waziri Mkuu.
Kinachotushangaza ni kwamba Waziri Mkuu hakuzungumzia kauli hiyo ya askofu kwenye ibada ile iliyofanyika mjini Bunda wala hakuzungumzia hali ya ugumu wa maisha juzi alipozungumza na waandishi wa habari.
Badala yake katika saa mbili alizozungumza na wana habari, alitumia dakika 45 kuzungumzia tiba ya kiimani inayotolewa na Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwaisapile kule Loliondo.
Ni hivi karibuni tu alipolazimika kuiongelea hali ya ugumu wa maisha inayowakabili Watanzania, Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo alitamka: "Hali ya uchumi ni ngumu, kila Mtanzania abebe mzigo wake mwenyewe."
Kauli kama hii kutoka kwa waziri mwandamizi ndani ya serikali tena anayeshughulikia fedha na uchumi, si tu haikupaswa kutolewa na waziri bali pia iliivua serikali nguo na kuiacha uchi kwa kuonyesha kwamba wale waliopewa dhamana ya kuiendesha nchi hii hawajui walitendalo.
Lakini kabla hatujakata tamaa na serikali hii tulisikia kwamba Waziri Mkuu angeongea na wana habari, tukapata matumaini ya Pinda kurekebisha makosa katika kauli ya waziri wake wa fedha akiwa ndiye mtendaji mkuu wa serikali.
Tumesikitishwa na kitendo cha Waziri Mkuu kutoongelea jambo hili muhimu ikiwa ni pamoja na kueleza hatua madhubuti zinazochukuliwa na serikali yake kurekebisha uchumi na kupunguza makali ya maisha kwa watu wake. Kweli serikali haijakata kiu ya wananchi maana wananchi wengi walitamani kusikia ni nini kitafanywa na serikali ili bei za vyakula na bidhaa nyinginezo muhimu zishuke na kuboresha kidogo maisha yao.

h.sep3.gif

Hapo penye red ni kama hapa chini,......

Mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Igunga, Rostam Aziz katika uwanja wa SabaSaba mjini Igunga leo.

Kikwete akisalimiana na Wananchi wa Igunga.

Rostam Aziz akihutubia umati wa watu katika uwanja wa SabaSaba mjini Igunga.

Back
Top Bottom