CCM na Rushwa: Uchaguzi CCM Mkoa Pwani wavunjwa kwa Rushwa.....

TAKUKURU walikuwa wakitafuta idhini ya Mkuu wa Mkoa ili awashauri cha kufanya. Ukizidi kuwahoji watakwambia uwapelekee ushahidi. CCM Oyeeeeee! Rushwa Oyeeeeee!
 
Tangu lini ccm inafanya shuhuli zake bila rushwa???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
!Tasisi ya Moh ibrahim imetaja Tanzania kuwa top 10 kwa utawala bora africa
 
umeisoma habari hii kabla ya
kuipost? maana takukuru ndio waliomtonya RC kuhusu uwepo wa rushwa


HIVI KWELI TAKUKURU HAWAWAONI WATOAJI RUSHWA NA
KUWAKAMATA???????
Inakuwaje sasa Takukuru waone rushwa washindwe kukamata wahusika halafu waende kulalamika kwa RC kuwa kuna rushwa?
 
Ukiona hivyo ujue upepo uligeuka sasa wakaona njia ya kujiokoa ni kuahirisha mkutano.
Mbona Sumaye alipolalamika TAKUKURU hawakuyafanyia uchunguzi malalamiko yake?
 
Aibu kwa TAKUKURU badala ya kuwashika watoa na wapokea rushwa ina wasiliana na kiongozi wa wao emu.
 
Hao maofisa wa TAKUKURU nao bogus kabisa. Kama wamegundua kuna vitendo vya rushwa kwanini wasiwakamate wahusika badala ya kwenda kuripoti kwa mkuu wa mkoa?

Nakubaliana na mdau mmoja aliyesema maana halisi ya TAKUKURU ni Taasisi ya Kuboresha na Kukuza Rushwa!
 
TAKUKURU are embedded! they are part and parcel of the same corrupt system, A boer can not commit suicide.
 
Hali halisi ndani ya CCM ni kama vile RUSHWA imehalalishwa kwani kila kukicha ni hadithi za Rushwa tu kwenye chaguzi za ndani za CCM. Leo hii katika kipindi cha Habari cha TBC mchana huu ni aibu kubwa mkutano wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Pwani umeahirishwa kwa kile kilichotajwa kuwa ni kukithiri kwa vitendo vya kutoa na kupokea Rushwa miongoni mwa wagombea na wapiga kura - tena WAZI WAZI kabisa.

My Take: Taasisi ya TAKUKURU ni bora tu isiwepo kwa maana sioni kama kweli wanadhirisha uwepo wao au ndiyo kusema haya yanayo tendeka kwenye chaguzi za CCM hawayaoni au RUSHWA ndani ya CCM ni ruksa? Au ndiyo vile tena kuwa ni matokea ya serikali dh***u?
 
Jamani mbona mnaposha? sio RUSHWA ni TAKRIMA!!!!!!!!!!!!!chama chetu takrima nimoja ya sera zetu,ikshatoka kwenye ngazi ya chama na kuwa sirikari kuu ndiyo ileeeeeeeee mnaita 10%.kwetu nivitu vya kawaida au kwa lugha nyingine wagombea wanatoa FUNGU LA 10 kwa wapiga kura wao.
 
Kwenye alama nyekundu hao ndio walisababisha kikao kuvunjika kwa kuwa ilionekana mtu wao hawezi kupita wakaleta kisingizio cha rushwa, mbona sehemu nyingine rushwa ilikuwepo waziwazi na uchaguzi ukafanyika. Mkuu wa Mkoa alikutana nao kupewa maelekezo ya kufanya,maana kila mkutano una msimamizi ambaye ndiye mwenye mamlaka kwenye mkutano huo, sasa kupata ushauri wa wajumbe wawili ina maana gani? Au kwa kuwa kuna mtoto wa RAISI?

Naweza kukubaliana nawe, why akutane na hao wawili tu badala ya kukutana mwenyeiti mwenyewe wa mkoa labda na sekretarieti nzima ya CCm mkoa?
 
Ajabu PCCB hawaoni haya mambo
Rushwa yavunja uchaguzi CCM Pwani Send to a friend
Wednesday, 17 October 2012 21:40
Na Julieth Ngarabali, Kibaha TUHUMA za kushamiri kwa vitendo vya rushwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CCM mkoani Pwani, jana vilimlazimisha mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Mwinshehe Mlao kuvunja mkutano huo. Uchaguzi huo uliokuwa ufanyike kwenye Jengo la Mkuu wa Mkoa wa Pwani, uliahirishwa saa chache, kabla ya upigaji kura kuanza kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba baadhi ya wajumbe walikuwa wakitoa na kupokea rushwa ili kushawishi ushindi wa baadhi ya wagombea. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza aliwaeleza wajumbe hao kuwa amepata taarifa kutoka vyombo vya usalama kuwa uchaguzi huo umegubikwa na vitendo vinavyoashiria kuwapo na rushwa. Akiahirisha mkutano huo jana, Mlao alisema amelazimika kusitisha uchaguzi huo hadi utakapotangazwa tena, kutokana na baadhi ya wajumbe kukidhalilisha chama kwa kujihusisha na rushwa. “Kwa haya yaliyotokea lazima tuwasiliane na wenzetu makao makuu. Baada ya kusema haya natangaza kuahirisha kikao hadi tarehe ya uchaguzi itakapotangazwa tena,” alisema Mlao. Akizungumza katika mkutano huo, Mahiza alilaani kitendo hicho akisema kuwa kimeidhalilisha CCM na ofisi yake. Awali Mahiza alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa maofisa wa Takukuru kuhusu kuwapo kwa mazingira ya rushwa yanayofanywa na wajumbe wa mkutano huo na baadaye alifika katika ukumbi wa mkutano. “Baada ya kupata taarifa kuhusu mazingira ya rushwa, nilitoka nje na kweli ukumbini sikukuta watu. Niliposhuka chini niliwakuta wajumbe wengi wakiwa wamesimama makundi. Sikujua na wala sikushuhudia nani aliyekuwa anatoa rushwa ila maofisa wangu wameliona hilo," alisema Mahiza. Mkuu huyo wa mkoa aliendelea kusema, "Najua nitabeba lawama kubwa sana, nitatukanwa sana na baadhi yao, lakini hili sitalivumilia.” Nafasi iliyodaiwa kuwa ndiyo iliyokuwa ina wagombea waliokuwa wakichuana vikali zaidi ni katibu wa uchumi ambayo wagombea wake ni, Imani Madega na Haji Abuu Jumaa. Baada ya kuahirishwa kikao hicho, Mahiza alifanya kikao cha ndani na wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (NEC) wa mkoa huo, Ridhiwan Kikwete na Rugemalila Lutatina. Alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema, " Waseme wenyewe wa Pwani. Kama imetokea leo siwezi kupata taarifa leo." Aliendelea kusema," Kama imetokea wataleta taarifa, zikifika tutakuwa na cha kuzungumza, lakini leo waache waseme wao kwanza." HIVI KWELI TAKUKURU HAWAWAONI WATOAJI RUSHWA NA KUWAKAMATA???????
Nimeshuhudia ITV jinsi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani na Mkuu wa Mkoa wakilaani tukio hili..... inasikitisha sana ...... Hivi hawa Takukuru wako maeneo ya mengine ta TZ na sio Kibaha? Mh. Hosea jana alinukuliwa kwamba viongozi wa siasa ni wanafiki katika swala la rushwa
 
Hao maofisa wa TAKUKURU nao bogus kabisa. Kama wamegundua kuna vitendo vya rushwa kwanini wasiwakamate wahusika badala ya kwenda kuripoti kwa mkuu wa mkoa?

Nakubaliana na mdau mmoja aliyesema maana halisi ya TAKUKURU ni Taasisi ya Kuboresha na Kukuza Rushwa!

Takukuru wanatutia hasara walipakodi sie maana wanatumia pesa yetu bila kutuletea faida yoyote. Natamani hii tasisi ivunjwe haraka
 
Nimeshuhudia ITV jinsi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani na Mkuu wa Mkoa wakilaani tukio hili..... inasikitisha sana ...... Hivi hawa Takukuru wako maeneo ya mengine ta TZ na sio Kibaha? Mh. Hosea jana alinukuliwa kwamba viongozi wa siasa ni wanafiki katika swala la rushwa

Haiingi akilini waone rushwa halafu hawajakamata mtu hata mmoja.

Haiingii akilini wana-CCM walalamike kuwa kuna rushwa, halafu TAKUKURU haioni wala kusikia. Au kuna mtu kwaroga hawa takukuru wetu hadi wanashindwa kuona???

Haiingii akilini Sumaye aone rushwa, takukuru hawaioni. Nape anakiri kuna rushwa, Hoseah anasema watajwe watoa rushwa. tuna matatizo makubwa sana
 
Inasikitisha sana. Nimemuona mkuu wa mkoa wa pwani akivunja mkutano huo na kuamuru viongozi wa ccm mkoa kutafuta ukumbi mwingine na sio ofisini kwake tena.

CCM bila rushwa haiwezekani.
 
umeisoma habari hii kabla ya
kuipost? maana takukuru ndio waliomtonya RC kuhusu uwepo wa rushwa



HIVI KWELI TAKUKURU HAWAWAONI WATOAJI RUSHWA NA
KUWAKAMATA???????

Nimeisoma tena kwa kituo.

Good wameona na wakamwambia RC. Then wamemkamata nani kwa rushwa hapo Kibaha????

Who is RC at all katika kushughulikia rushwa ndani ya CCM?

Umesikia alichosema Hoseah kuhusu rushwa ndani yan CCM?
 
Acha wafu wazike wafu wao! Kitendo cha kufanyia mkutano wa chama kwenye jengo la serikali i.e ukumbi wa mkuu wa mkoa, ni kitendo cha kiisadi na matumizi mabaya ya mali za umma!
 
natamani aje mtu atuthibitishie ni sehemu ipi katika chaguzi za magamba pesa haikutumika?
 
CCM na rushwa damu damu, wala sishangai!!!

Kuitenga CCM na Rushwa ni sawa na Kuutenga mzoga na funza/inzi waliouzingira huo mzoga, it is practically impossible. lakini walipofikia ni patamu hapo panaitwa mwenye kisu kikali.................................ndo mla nyama, kama huna kanunue au noa kuongeza makali
 
Rushwa ni sera za CCM

Na mbaya zaidi kama rushwa hiyo ya kutisha inafanyika nyumbani kwa President Kikwete, halafu bado tutaendelea kujitapa kuwa tuna chombo cha kupambana na rushwa hapa nchini, yaani TAKUKURU, kwanza wa-TZ tunashindwa kuelewa ni kwanini Dr Hoseah, hachukui uamuzi wa kujiuzuru wadhifa wake, kutokana na chombo chake cha TAKUKURU, kushindwa kabisa hii vita ya rushwa kubwa, hasahasa kwenye chaguzi za CCM, badala yake amekuwa bingwa wa kukamata vidagaa, kama vile askari wa Traffic, wanaokimbizana na vidaladala vinavyotanua mabarabarani! Kweli naamini Tanzania hivi sasa ni miongoni ya maajabu saba ya Dunia!!
 
Back
Top Bottom