Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,045
Hivi majuzi, kuna Mwana-JF alianika hapa JF mikakati iliyomo katika Waraka wa siri ulioandaliwa na ccm kuwamaliza CDM. Baada ya kuusoma nilihitimisha kwa kujisemea kuwa, haya ni mawazo yanayoletwa na hisia binafsi za Mwandishi. Na haya mawazo yanatokana na mapenzi yaliyomzidia Mwandishi kwa chama chake, kiasi kwamba anashindwa kutafakari taarifa kwa kina. Nilihitimisha hivyo kwa sababu kuu moja; ccm imekuwa ikikituhumu CDM kwa UKATOLIKI na UCHAGA na hivyo kuingiza UGAIDI wa Afghanistan na Libya ingekuwa ni kuua hoja ya UKATOLIKI. Na muendelezo huu ungeisaidia CDM badala ya ccm.
Tuhuma ya UKATOLIKI imefanikiwa kwa kiasi cha kuchelewesha uhuru wa pili Tanzania. Wananchi wameshikwa kisawasawa na hoja ya UDINI kiasi kwamba hawajadili hoja bali huegemea ni mwenzetu. Hawajali njaa, bei ghali ya bidhaa wala ugumu wa maisha ilimradi aliyesababisha ni mwenzao. Kwa sasa udini unasafisha na kurasimisha kila aina ya ovu na dhambi. Haya ni mafanikio kwa ccm ambayo kwa mpanga-mkakati ya kisiasa mzuri angependa kuyaendeleza na kuyakomaza. Mbinu ya kuyakomaza ingekuwa kujenga hoja endelevu juu ya UDINI tena udini wa KIKATOLIKI. Hivyo basi nisingetegemea mtu makini ndani ya ccm kuendeleza hoja ya UKATOLIKI kwa kuingiza UGAIDI ambao maarifa yake yamesemekana kupatikana kutoka Afghanistan na Libya. Nasema hivi kwa sababu iwe ni propaganda ama kweli, UGAIDI umehusishwa zaidi na dini nyingine tofauti na UKRISTU achilia mbali tukio la hivi karibuni huko Norway. Nyongeza ya hapo, hakuna muunganiko kati ya UKATOLIKI na Afghanistan na Libya. Imani katika nchi hizi za Afghanistan na Libya haitoi mwanya wa kuwa na uhusiano na Ukatoliki (wanaita Ukafiri) na hasa katika mahusiano ya kimataifa. Hoja ya Ukatoliki wa CDM ingepata mashiko zaidi kama ingezidi kusukumwa kwa kuunganishwa na UMAFIA kuliko kuingiza UGAIDI. Asili ya UMAFIA ni Italy ambako Ukatoliki una mizizi. Na ni huko huko Italy ambako mlenga wa ccm ndani ya CDM alipata sehemu kubwa ya elimu yake. Kidogo hapa kungekuwa na muunganiko ambao ungeweza kuleta uhalisia wa kughushi.
Baada ya kusoma aliyosema Wilson Mukama jana katika mkutanao wake na Waandishi wa Habari, nimekubali kuwa kumbe mimi ndiye sikuwa sahihi na Mwana-JF aliripoti kitu cha kweli kabisa. Kukiri kwangu kutokuwa sahihi ni kudhihirisha udhaifu wa hali ya juu wa ccm katika kupanga mikakati ya kisiasa na kuiendeleza. Siungi mkono mikakati ya kipuuzi yenye kuegemea katika udini, dhuluma au kuwagawa watu kibaguzi bali najaribu kuonyesha umuhimu wa kuwa thabiti (consistent) unapo panga Mkakati. Kwa kosa hili la kuchanganya UKATOLIKI na UGAIDI wa Afghanistan na Libya CDM wamepata upenyo mzuri amabo wakiutumia vema wanaweza kupunguza upinzani unaotokana na UDINI.
Kazi ni Kwenu .