CCM na Mategemeo yao JKT

MKUU NI KWELI KABISA HAYO ULIYOWATAARIFU KURUTA WATARAJIWA.MIMI NILIKUWA KAMBI YA JKT MGAMBO ILIYOPO KABUKU WILAYA YA HANDENI.SIKU MOJA NILIMTOKA MP ALIYETAKA KUNIPA DRILL NIKAJONGOMEA KWENYE SHAMBA LA michungwa nikawa nashindia na kulalia machungwa (yaani kula lunch na diner ya machungwa tu) kwa siku mbili mfululizo.
 
Hapa umeua mwana wane!

Yaani nimecheka pamoja na kwamba niko peke yangu kwenye computer! Lunch na dinner ya Machungwa hii ni noma mwanangu sijawahi kuisikia. Ilikuwaje mkuu hiyo lunch na dinner? Yaani huu uhondo niliukosa kwa ncha ya sindano Nyamb..f zao waliopitisha maamuzi ya kufuta JKT kipindi cha mwaka 1994. Niliishia kujaza fomu na kupokea joining instructions nikiwa nimepangiwa MLALE JKT. Kitisho kikubwa ilikuwa mnaenda kwenye shamba la mahindi linaloitwa DUNIA. Mkuu nilikuwa nimejiandaa kikamilifu.

Tunajiandaa Januari tuende kulipoti shenzi wakafuta JKT aaaagh!!! Hao vijana ngoja waende. Wallah hata mimi umri ungekuwa bado unaruhusu ningejiandikisha. HONGERA ZENU WAKUU MLIOPITIA HUKO!!
 
Duuh Makutu acha kabisa nimekumbuka mengi sana vile visimama vya bustani,uliyosema ndiyo ukweli wenyewe. Mimi nilikuwa ST kombania ADMINISTRATION COY nimeipenda hasa MAKUTOPORA naijua vizuri sana nami nimepita pale kupata huduma ya JKT.
 
Misamiati zaidi......
Serengeti
Selule
Alpha
Bravo
Charlie
Danger
Eagle
HQ...
......
 
Na nyimbo za ajabu ajabu ndo usiseme... mmoja kwa maselule ulikuwa:-

" sisi ni wagonjwa, lakini hatuuuumwwiii"

Kwa hakika kila mtu anahitaji kwenda JKT hasa watu wenye tabia ya umbea umbea
 
Hapa umeua mwana wane!

Yaani nimecheka pamoja na kwamba niko peke yangu kwenye computer! Lunch na dinner ya Machungwa hii ni noma mwanangu sijawahi kuisikia. Ilikuwaje mkuu hiyo lunch na dinner? Yaani huu uhondo niliukosa kwa ncha ya sindano Nyamb..f zao waliopitisha maamuzi ya kufuta JKT kipindi cha mwaka 1994. Niliishia kujaza fomu na kupokea joining instructions nikiwa nimepangiwa MLALE JKT. Kitisho kikubwa ilikuwa mnaenda kwenye shamba la mahindi linaloitwa DUNIA. Mkuu nilikuwa nimejiandaa kikamilifu.

Tunajiandaa Januari tuende kulipoti shenzi wakafuta JKT aaaagh!!! Hao vijana ngoja waende. Wallah hata mimi umri ungekuwa bado unaruhusu ningejiandikisha. HONGERA ZENU WAKUU MLIOPITIA HUKO!!

Mwisho wa umri ni 45 Mwalimu Baba wa Taifa, Mzee Kawawa, Mzee Kahama et al.. walienda wakiwa watu wazima zaidi.
In fact wabunge wote ambao hawajapita JKT inafaa waende labda wata behave inavyostahili huko Bungeni.
Pia nadhani ingekuwa ni sifa mojawapo kwenye CV kwamba ni COMPULSORY kuwa umepita JKT ndipo ugombee ubunge, udiwani, etc.
 
uliyosema sawa ila ni upande mmoja wa shilingi. kruta, wa kije angeweza kuamrishwa kwenda, kwa afande na kubakwa kwa amri ndiyo afande, mambo hayo yasirudiwe tena, sasa hivi kuna magonjwa mengi
 
Mwisho wa umri ni 45 Mwalimu Baba wa Taifa, Mzee Kawawa, Mzee Kahama et al.. walienda wakiwa watu wazima zaidi.
In fact wabunge wote ambao hawajapita JKT inafaa waende labda wata behave inavyostahili huko Bungeni.
Pia nadhani ingekuwa ni sifa mojawapo kwenye CV kwamba ni COMPULSORY kuwa umepita JKT ndipo ugombee ubunge, udiwani, etc.

Mkuu hawa jamaa wa sasa hivi hawawezi kutuvunja miguu? Miaka 45 mbona ni kasheshe? Ila hawa wabunge kwa kweli inastahili wapelekwe huko. Hayo matusi yakina Lusi labda yatapungua. Ila nina wasiwasi na hao jamaa wa gheshi letu kama hawatatoa upendeleo! Utakuta jamaa wanapangiwa vitengo vizuri vizuri ili wapumue. Huyu Mr. DHAIFU naye si ashauri watu wote ambao hawakupitia JKT warudi huko japo kwa miezi 6 tu kama alivyofanya baba wa Taifa miaka ile.
 
MKUU NI KWELI KABISA HAYO ULIYOWATAARIFU KURUTA WATARAJIWA.MIMI NILIKUWA KAMBI YA JKT MGAMBO ILIYOPO KABUKU WILAYA YA HANDENI.SIKU MOJA NILIMTOKA MP ALIYETAKA KUNIPA DRILL NIKAJONGOMEA KWENYE SHAMBA LA michungwa nikawa nashindia na kulalia machungwa (yaani kula lunch na diner ya machungwa tu) kwa siku mbili mfululizo.

kuna afande alikua anaitwa milambo na magazi unawajua
 
Kwetu mbali nyumbani mbali tukumbukane kwa barua. Yanyukwe. Nyimbo za disko la usiku. Maisha yale yalikuwa safi sana hakuna cha nani wala nani wote sawa.
 
Hii inanikumbusha mbali, enzi za top layer kwenye kofia.
Paint kubwa ya chuma. Unalia hiyo hiyo na kuogea.
Hapa Freeman Mbowe ilibidi awe daktari wa ng'ombe bila kupenda!(Vet-officer afande).
Back on the day's when men were young. If only I' could turn back the hands of time.
 
Mkuu hawa jamaa wa sasa hivi hawawezi kutuvunja miguu? Miaka 45 mbona ni kasheshe? Ila hawa wabunge kwa kweli inastahili wapelekwe huko. Hayo matusi yakina Lusi labda yatapungua. Ila nina wasiwasi na hao jamaa wa gheshi letu kama hawatatoa upendeleo! Utakuta jamaa wanapangiwa vitengo vizuri vizuri ili wapumue. Huyu Mr. DHAIFU naye si ashauri watu wote ambao hawakupitia JKT warudi huko japo kwa miezi 6 tu kama alivyofanya baba wa Taifa miaka ile.

Siku hizi watu mayai mayai sana. Kwa kweli muhimu viongozi wote kwenda JKT na KIVUKONI
 
832KJ ; Operesheni KAMBARAGE, F COY :
CO ni Luteni Mnyomole
Sajini major ni Sanga
Staff sajini ni Rajabu
Sajini Said Omari(huyu baadae alienda Mgulani JKT Sekondari kusoma)
Sajini Mahundi
Sajini Maingu
Koplo Kupaza
Lansi Koplo Kaumbu

Jioni kabla mlo tunasikiliza BBC SWAHILI wakati GEORGE BUSH SR na marafiki zake wanamtoa SADAM HUSSEIN KUWEIT katika ile ilioitwa operesheni Desert Storm ikiongozwa na Gen. Collin Powell na Gen. Schwarzköpf.
Waacheni waende wakamtafule Malela sijui kama watampata.
 
Monday, 16 July 2012 21:10

NI KUANZIA MWAKA HUU WA FEDHA,PIA WAMO WA KIDATO CHA SITA

Neville Meena na Boniface Meena, Dodoma

WABUNGE vijana walioko katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watapaswa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa Mujibu wa Sheria kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2012/13.

Waziri wa Ulinzi na JKT, Shamsi Vuai Nahodha alisema hayo alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya wizara yake bungeni jana. Alisema wabunge vijana watakuwa sehemu ya kundi la kwanza la vijana 5,000 katika mafunzo yatakayoanza Machi, mwakani.

Alisema wizara hiyo imelifanyia kazi ombi la kuandaa mafunzo ya JKT kwa wabunge vijana kama ilivyoombwa mwaka jana na kwamba wabunge hao wameandaliwa mafunzo hayo ya wiki tatu.

"Nafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba Wizara yangu imelifanyia kazi ombi hilo na kuandaa utaratibu wa mafunzo maalumu ya wiki tatu kwa waheshimiwa wabunge vijana," alisema Nahodha na kuongeza:

"Kwa hiyo wabunge vijana wataungana na kundi la kwanza la vijana 5,000 niliowaeleza hapo juu… naomba waheshimiwa wabunge mjiorodheshe kwa maandalizi ya mafunzo haya."

Waziri Nahodha alisema ni imani yake kuwa, pamoja na wabunge kunufaika na mafunzo hayo, watahamasisha urejeshwaji wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na kutoa taswira nzuri ya mafunzo hayo kwa jamii.

Alisema JKT tayari imefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kambi tano zenye uwezo wa kuchukua vijana 20,000 kwa wakati mmoja zimeshaandaliwa kwa ajili hiyo.

Alizitaja kambi hizo kuwa ni Bulombora na Kanembwa za mkoani Kigoma, Mlale ya Ruvuma, Msange mkoani Tabora na Oljoro hukoArusha.

Hata hivyo, alisema gharama ya kuendesha mafunzo hayo ni kubwa hivyo JKT haitaweza kuchukua vijana wote na ndiyo maana imeamua kuanza na hao 5,000.
"Vijana hao ni miongoni mwa vijana 41,348 ambao watahitimu mafunzo ya kidato cha sita katika mwaka 2013," alisema Nahodha.

Kuhusu utaratibu wa kujiunga na kambi hizo, Nahodha alisema uandikishaji wa vijana shuleni utafanyika kati ya Desemba mwaka huu na Januari 2013 na kwamba kambi zitawapokea kati ya Machi 7 na 16, mwakani.Alisema mafunzo hayo ya miezi sita yataanza Machi 17 mwakani na kuendelea hadi Agosti 16.

Wanajeshi Syria

Katika hatua nyingine, Nahodha alisema wanajeshi wa Tanzania kati ya 100 na 200 wanatarajiwa kwenda Syria kuwa waangalizi wa amani ikiwa ni kuitikia ombi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa Serikali.

Alisema ombi hilo linatokana na utendaji mzuri wa jeshi hilo na kwamba tayari Serikali imelikubali.

Nahodha alisema tayari Makao Makuu ya Jeshi yameanza maandalizi ya kuwapeleka waangalizi hao.

Alisema Tanzania ina wajibu wa kushirikiana na nchi nyingine kulinda amani duniani na imekuwa ikishiriki katika operesheni mbalimbali za kulinda amani.

Katika hatua nyingine; Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Christowaja Mtinda alilalamikia kitendo cha Wahindi kuuza bidhaa za maduka ya jeshi kwa gharama za juu, wakati bidhaa hizo hazilipiwi kodi.

Alisema ni lazima Serikali ieleze Wahindi hao wanauzaje bidhaa za kwenye maduka ya jeshi kwa gharama kubwa wakati maduka hayo yanatakiwa yauze bidhaa hizo kwa bei ya chini.

"Ukienda sasa hivi wanauza sukari Sh1,800 wakati nje ya maduka hayo sukari kilo ni Sh2,000, hili haliwezekani. Wanauza friji, tv kwa bei ya juu na TRA, maofisa wa jeshi wa ngazi za juu wote wanajua," alisema.

Mtinda alitaka suala hilo litafutiwe ufumbuzi ili bidhaa ziuzwe kwa bei inayotakiwa. Pia alilalamikia nyumba za maofisa wa jeshi akisema haziridhishi na kwamba zinahitaji kukarabatiwa upya.

"Nyumba za maofisa wa jeshi zinatia aibu, hazijakarabatiwa kitu ambacho kinasababisha wafanye ukarabati kwa fedha zao wenyewe," alisema.

Wapinzani wang'aka

Kwa upande wake, Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu wizara hiyo, Mchungaji Israel Natse aliitaka Serikali kutoa maelezo ya matumizi ya Sh4.048 bilioni ambazo zilitumika kuondoa matrekta bandarini.

"Hakika fedha hizi ni nyingi sana kwa kazi ya kuondoa tu matrekta bandarini, Kambi ya Upinzani inataka kupata majibu ni matrekta mangapi yaliondolewa na gharama ya kuondoa trekta moja ilikuwa kiasi gani?" alisema Natse alipokuwa akitoa maoni ya kambi hiyo.

Natse ambaye pia ni Mbunge wa Karatu (Chadema) alisema malipo hayo yanatia shaka na kwamba Serikali lazima ieleze fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi gani.

Kuhusu migogoro ya ardhi, mbunge huyo alisema kumekuwapo na migogoro kwa muda mrefu baina ya wanajeshi na wananchi kwenye maeneo mbalimbali ya nchini na kwamba ni kama hakuna dalili kwamba kuna nia ya dhati ya kumalizwa kwa matatizo hayo.

"Migogoro hii imesababisha kuwapo kwa mvutano baina ya wananchi na jeshi letu kwa upande mmoja na viongozi wa wananchi kwa upande wa pili," alisema Natse.
Alitoa mfano wa maeneo hayo kuwa ni Ilemela, Tarime, Kunduchi na mengine mbalimbali ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wabunge kwa muda mrefu.

"Mara zote Serikali imekuwa ikitoa majibu kuwa itawalipa fidia wananchi ili waweze kuondoka na kuyapisha maeneo hayo kwa ajili ya jeshi, kwa mwaka huu wa fedha 2012/13 zimeombwa kiasi cha Sh1 bilioni kwa ajili ya kulipa fidia ya ardhi maeneo ya Mapinga, Shinyanga na Arusha."

Alisema kutokana na fedha hizo ni dhahiri kwamba hakuna nia ya dhati ya kumaliza migogoro baina ya jeshi na wananchi kwani kiasi hicho kilichotengwa ni kidogo na ni kwa ajili ya kulipa fidia na sehemu chache tu.

"Tunaitaka Serikali iwe na nia ya dhati ya kuwalipa wananchi fidia ili kumaliza migogoro hii ambayo inawafanya wananchi walichukie jeshi lao," alisema.
 
OH YES

1.MWINGULU MCHEMBA
2.ALI MWINYI
3.NAPE NNAUYE
4.WILLIAM MALECELA
5.JANUARY MAKAMBA

Yes, Na zaidi Hawa watoto wa wakubwa AZIMIO la ZANZIBAR LILIWACHUNGA na Kuvunja JKT sasa wanaona

Ubaya wake? Too late President Mwinyi; Oh Kikwete Riz1 atakwenda?
 
CCM imeishiwa sera sasa inalenga kuwakomoa wabunge vijana wa Chadema. Hizo ni sera za CCM si lazima zifuatwe na upinzani.
 
Huu ni upuuzi kabisa, unakopa hela kwenda kupoteza kwenye programu iliyoisha feli miaka iliopita.
Kitu wasichojua ni kuwa wanaenda kuwafundisha vijana kupigana ili wawatoe kwa mtutu wa bunduki vizuri pale watakapo chakachua. Nasema kwa unyenyekevu kila la kheri serikali hii tukufu, hamjui manafanya nini. Hizo fedha bora mngezitumia kuimarisha makazi ya maafande, mapolisi na wanamagereza.
Jkt ilikuwa sera iliyobuniwa toka china na ulaya mashariki wakati wa utawala wa kiimla wa chama kimoja, sasa hivi, ni kila la kheri. Naona mwakani mtatuburuza kwenye mafunzo ya mgambo.
 
Back
Top Bottom