CCM na mapinduzi visiwani

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
JINA CCM LIMETOKANA NA NINI
Naomba kuchukuwa muda wenu kidogo kujadili kitu hichi kama kinawezekana , nimekuwa nawaza kuhusu jina la CCM yaani chama cha mapinduzi yaani hili jina lake lilitokana na nini haswa kuhistoria inasemekana ni muungano wa TANU ana chama kingine huko visiwani ndio kukazalishwa CCM .
Huko visiwani ndio kulikuwa na mapinduzi na sio Tanzania bara sasa ni kwanini chama hiki kiitwe chama cha mapinduzi wakati mapinduzi yalifanyika visiwani peke yake ? mapinduzi yaliyofanyika huku bara ni yapi hayo tuelezwe .
Pia kuna baadhi ya maandiko yanasema kwamba aliyetekeleza mapinduzi hayo ni okello ambaye alikuwa raia wa Uganda na sio Karume kama wengi wanavyojaribu kupotosha habari yenyewe hata hivyo mimi sio mjuzi sana katika masuala ya historia hii naomba niwaachie wenyewe .
Kuna habari zingine zinazosema kwamba Karume alikuwa Raia wa Malawi , kule visiwani alikuwa anafanya kazi za ubaharia , sasa haieleweki wakati wa mapinduzi hayo kama karume alikuwa anajuana na okelo au okelo alikodishwa kwa ajili ya kazi hiyo pekee au kuna maslahi Fulani alikuwa anatafuta kupitia mapinduzi hayo .
Na je Rais wa Tanganyika enzi hizo alikuwa anajua habari hizi za mapinduzi kabla ya kutekelezwa kwake ? kwa sababu miaka 4 iliyopita kabla ya mapinduzi nyerere aliwahi kukutana na baadhi ya viongozi wa kiarabu huko visiwani na dare s salaam kuwatoa hofu kuhusu nia yake y akudai uhuru , ukipatikana hawata umia kwa chochote .

Lakini mapinduzi yalifanyika muda mfupi baadaye , kisha nchi kuungana na kutengeneza chama kimoja cha kisiasa ambacho ni CCM chama cha mapinduzi , je huu ulikuwa ni mpango wa muda mrefu ambao hata raisi wa tanganyika alikuwa anaujua ?
Baada ya hapo tumeona visasi vya kisiasa visiwani kuanzia wapinzani kunyanyaswa , wengine kupotea na aina nyingine nyingi sana za vitisho .
Hata hii vita tuliyopigana na Uganda nahisi kuna vitu vilivyofichwa ambavyo visasi vyake vinaweza kuwa vinatokana na mapinduzi ya Visiwani vilivyoendeshwa na Okelo
 
Kwa kirefu ni : Christian Conservative Movement. lakini viongozi wa zenj kwa ukosefu wa elimu,ulimbukeni na kutoona mbali waliamini kuwa ni chama cha mapinduzi na ndio maana si hasha leo Pinda anawambia zanzibar sio nchi . (ukweli unauma ,Msema kweli ni kipenzi cha Mmungu)
 
Kwa kirefu ni : Christian Conservative Movement. lakini viongozi wa zenj kwa ukosefu wa elimu,ulimbukeni na kutoona mbali waliamini kuwa ni chama cha mapinduzi na ndio maana si hasha leo Pinda anawambia zanzibar sio nchi . (ukweli unauma ,Msema kweli ni kipenzi cha Mmungu)

Dini, dini, dini, dini, dini, kweli bongo ni mnara wa babeli!!
 
Back
Top Bottom