CCM na magari ya uchaguzi...

Kwa hali ilivyo sasa, nina uhakika mkubwa kabisa kwamba CCM haiwezi kufanya upuuzi huo... ila tusubiri tuone

Waliweza kufanya upuuzi wa Meremeta, kagoda, EPA, utakuwa huu? Kuna jambo la kipuuzi ambalo CCM hawajafanya? Wameweza kuitana vichaa na bado wanaendelea kuwa mawaziri na ukichaa wao, itakuwa hili? Wenzako wala hawaoni kama ni tatizo, watakujibu kirahihi kabisa kuwa ni wivu au chuki? I mean this party can't do anything sensible hapo ilipofikia!
 
Waliweza kufanya upuuzi wa Meremeta, kagoda, EPA, utakuwa huu? Kuna jambo la kipuuzi ambalo CCM hawajafanya? Wameweza kuitana vichaa na bado wanaendelea kuwa mawaziri na ukichaa wao, itakuwa hili? Wenzako wala hawaoni kama ni tatizo, watakujibu kirahihi kabisa kuwa ni wivu au chuki? I mean this party can't do anything sensible hapo ilipofikia!

Unanifurahisha sana na hoja zako! Eti wameitana vichaa na bado wanaendelea kuwa mawaziri na ukichaa wao....very funny and true.
 
CCM si ndo inaongoza serikali? Lazima wajipendelee!

Bora mawazo ya Makamba kuliko wewe.
Mawazo kama hayo ndo yanawafanya Waganda kuanza kutunga sheria ya kupambana na wanaopanga ndoa za jinsia moja. Ni kwa kuamini wana matatizo kichwani.

Mwishoni kabisa mwa 2009 bado unaamini ukiongoza serikali basi hulipi kodi!!! na tena uko JF!
 
Waliweza kufanya upuuzi wa Meremeta, kagoda, EPA, utakuwa huu? Kuna jambo la kipuuzi ambalo CCM hawajafanya? Wameweza kuitana vichaa na bado wanaendelea kuwa mawaziri na ukichaa wao, itakuwa hili? Wenzako wala hawaoni kama ni tatizo, watakujibu kirahihi kabisa kuwa ni wivu au chuki? I mean this party can't do anything sensible hapo ilipofikia!

Kitila umenikuna haswa!!! Bottom line UFISADI hauwezi kuwa historia katika hii nchi kama tutaendelea kuongozwa na SSM na viongozi wa sasa wa SSM. Tunahitaji mapinduzi.
 
kama CCM wangelipa hizo pesa zingeweza kusaidia wananchi kibao wanaotegemewa kuadhirika kwa njaa kwa sababu ya kulikupata mavuno ya kutosha msimu huu.......................!!!!!!

Kwani tatizo lako liko wapi??? Huna uchungu na hizo 600 million/Billion???


Sawa kabisa ila naomba Invisible anijibu. Sidhani kama anamaaniosha hivyo.
 
Umesikia makamba adai wamelipa 1 billion kwa baadhi ya gari,na gari sio 200 ni 150.
We ruzuku yote hiyo washindwe kulipia ushuru itakuwa kichekesho.hizi ni porojo za siasa katiaka chadema-wanakurupuka tu- ovyooooooo????
 
Umesikia makamba adai wamelipa 1 billion kwa baadhi ya gari,na gari sio 200 ni 150.
We ruzuku yote hiyo washindwe kulipia ushuru itakuwa kichekesho.hizi ni porojo za siasa katiaka chadema-wanakurupuka tu- ovyooooooo????

Komaa kwanza kabla ya kutoa maoni makali kama haya.

Nani anataka kulipa kodi ktk chama hicho. Chiligati magari 200, Makamba 150, Uko kwa nani wewe? Kumbuka kuna muhuni Makala kama muweka hazina.

CCM hawana pesa za uchaguzi kama unavyodhani. Hawana mradi wowote wa kuweza kupata mabilioni ya EPA-type.

Ndo maana tunasikia sasa hata kikosi cha zima moto kimepewa malengo ya kukusanya pesa toka kwa wenye magari na kuzifisha chama tawala.
 
TRA wanasema eti CCM hawadaiwi..
Ila sawa Mbwa na mwenye mbwa nani mwenye maamuzi..
 
Hawa watu ni wataalamu katika nyanja zote za kujipatia fedha kwa njia za mkato. Ukiziba njia moja wanatoboa nyingine. Baada ya kugutukiwa kukwepa kodi kwa mashangingi hayo watalipa lakini kwa pesa za wizi vile vile si serikali ni yao watabuni njia nyingine tu. Kuna hela za walalahoi za deci zitachotwa zikalipe kodi hiyo . Hawa wamekubuhu kwa umafia.
 
Dah! nakumbuka orodha ya mafisadi aliitoa huyu bwana sasa nimeanza kumuamini the guy is serious
 
SHUPAZA na Wana JF,

Kilichobakia ni kuhakikisha Dr. W. Slaa anakuwa Rais wa nchi yetu mwaka ujao. Kazi ifanyike. Hakuna mbadala.
 
SHUPAZA na Wana JF,

Kilichobakia ni kuhakikisha Dr. W. Slaa anakuwa Rais wa nchi yetu mwaka ujao. Kazi ifanyike. Hakuna mbadala.

kuna methali ya kiswahili inasema kuwa "Baniani mbaya kiatu chake dawa" kwenye hili la CCM kuna jambo CHADEMA wanapaswa kujifunza kwani kuna jambo la msingi CCM wamefanya

Hivi sasa adui namba moja wa CCM ni chadema, wakati CCM inaagiza magari 200 (150?) kwa ajili ya kampeni ya mwakani CHADEMA inayo mangapi?

Hoja yangu hapa ni kwamba wakati katibu wa CHADEMA wa wilaya anatembea kwa miguu kuwafikia wapiga kura, mwenzake wa CCM atakuwa ameshawatembelea wapiga kura mara elfu kumi zaidi.

Kampeni ni vita na vitani Logistic ni kitu muhimu sana, mpaka sasa CHADEMA wana ofisi ngapi za wilaya ambazo zitawawezesha wanachama wake kukutana kirahisi kwa wakati mmoja kwa pamoja ili wapange mikakati ya kuisambaratisha CCM?

Mimi siipendi kabisa CCM,lakini pia sipendi kuishi kwenye njozi. Kama ni lazima viongozi wa kitaifa wawepo ndiyo CHADEMA iwe hai katika eneo husika basi hakuna kitu kama Slaa kuwa rais mwaka 2010 au hata 2015.

CHADEMA makao makuu inaweza kukaa zaidi ya mwezi mzima au hata miezi bila ya kuwasiliana na viongozi wake wa Mikoa, wilaya, na majimbo, sasa chama kama hicho kitaishindaje CCM?

Kimsingi nataka nyie mlio karibu na viongozi wa CHADEMA muwaambie wabadilike. Kafulila na Danda wameondoka CHADEMA baada ya kugundua kuwa kama hauko makao makuu ya chama huwezi kuwa na uwezo wa kupata rasirimali zitakazokuwezesha kushinda kwenye uchaguzi.
 
CCM yahaha kujinasua na kombora la Dk Slaa

Na Exuper Kachenje

UFAFANUZI wa tuhuma alizovurumusha katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa unaonekana kuwakoroga viongozi wa CCM kutokana na kada mwingine kujitokeza kutoa maelezo zaidi ya yale yaliyotolewa na katibu mkuu, Yusuf Makamba na John Chiligati.

Mwanzoni mwa wiki akiwa mkoani Tanga katika Operesheni Sangara inayoendeshwa na chama chake, Dk Slaa alidai kuwa CCM imeagiza magari 200 na kuyaingiza nchini bila kulipia ushuru ambao alisema unafikia Sh600 milioni.

Tayari katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba ameshakiri kuwa chama chake kimeagiza magari hayo na kwamba kimelipia uhuru, huku akipingana na idadi ya magari iliyotajwa na Dk Slaa.

Lakini jana, Amos Makala, ambaye ni katibu wa NEC wa masuala ya uchumi na fedha aliona ufafanuzi huo hautoshi na kutoa ufafanuzi zaidi katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi ndogo ya CCM iliyo Mtaa wa Lumumba.

Alielezea kwa kifupi tuhuma hizo za Dk Slaa kuwa ni uongo,uzushi na propaganda za kisiasa zinazolenga kuichafua CCM, kabla ya kuanza kutoa ufafanuzi zaidi.

Makala alionyesha nyaraka mbalimbali za ukaguzi uliofanywa na TRA, maelekezo ya kiasi cha ushuru walichotakiwa kulipa, risiti za benki zilipolipiwa fedha hizo na kwamba tayari chama hicho tawala kimeshalipia ushuru wa magari 74 kati ya 150 yaliyoagizwa.

"Leo nimekuja ili kufafanua baadhi ya mambo... nirudie kauli kuwa CCM haijakwepa kulipa kodi, pia kuonyesha jinsi Dk Slaa alivyo mwongo," alisema Makalla.

"Ukweli ni kwamba CCM imeagiza magari 150 na siyo 200. Yaliyoingia ni 74 na bado magari 76. Namshangaa Dk Slaa, mtu mzima alivyo muongo."

"Cha kushangaza zaidi Dk Slaa hajui hesabu, magari 200 halafu ushuru uwe Sh600 milioni?, jamani ni hesabu za kitoto hizo. Hayo magari 74 tumelipa Sh1,720,065,031 bilioni," alisema Makalla.

Alifafanua kuwa CCM imelipa ushuru huo Novemba 7 kupitia matawi ya benki ya CRDB ya Azikiwe na Vijana yote ya jijini Dar es Salaam akibainisha kuwa Sh878,875,000 zililipwa kupitia tawi la Azikiwe na Sh841,190,031 tawi la Vijana.

Makalla alidokeza kuwa tayari meli nyingine imewasili nchini ikiwa na magari 76 yaliyosalia na ambayo yataanza kutolewa baada ya taratibu kukamilika, ikiwemo ya kulipia ushuru.

Alizidi kumshambulia Dk Slaa kuwa ni mtu wa fitina, hatari anayestahili kuogopwa na jamii na kuwa hatua ya CCM kuweka hadharani nyaraka walizolipia ushuru ni sawa na kumvua nguo Dk Slaa na kudharaulika.

"Waliomwambia hayo Dk Slaa, wamemwingiza mkenge. Leo hapa tumemvua nguo... Dk Slaa amekurupuka ni aibu kwake na amedharaulika," alisema.
 
Slaa ni Mfitini eh? mbona hoja zingine hawazijibu haraka kwa style hii? Fedha za Kagoda jee? Deep Green? nk? Kama wamelipa sawa, Slaa hongera kwa kuzuia mpango wa kukwepa kulipa. Kinga ni bora kuliko tiba,maana hapa kwetu tiba huwa haipo
 
Hiki Chama Cha Majambazi walipata wapi hizo pesa za kuagiza hayo magari? Isije kuwa ndio wakishinda wanaanza tena kurudisha fadhila.
 
Risiti za meremeta, deep green, kagoda, import support nazo tunataka ziambatanishwe na hiyo nusu deni ya ushuru wa magari waliyotoa na pia B/ce wataimaliza lini? bila kusahau maelezo ya pesa wamezipata wapi isije ikawa ni za mafisana kama hawa waliogandamana nasi sasa mithili ya kupe katika ngozi.
 
BEI ya shangingi moja ni 100 milioni....sasa hawa jamaa wamenunua 150...ina maana jumla kwa kazi hii watatumia 15 BILIONI...sasa kwa chama makini kama ccm inavotaka ionekane...watuambie wamepata wapi BILIONI 15 za kununua magari ambayo hata serikali yenyewe kupitia waziri mkuu pinda aliagiza yasinunuliwe kwa kuwa yana gharama kubwa kununua na kuyahudumia pia....

CCM ninayoijuwa ni wafujaji wakubwa wa mali hasa magari ..laiti ccm wanguwa watunzaji wa magari yao wasingehitaji kununua magari mengi namna hii kila kampeni ...sanasana wangekuwa wananunua machache kama 20 kwa ajili ya kumbeba mgombea na entourage yake ...yaliyobaki wangetumia yaliyopo......lakini ukweli ni kuwa magari ya chama hayatunzwi vema ,hayawekwi vipuri halisi.....inachangia kuharibika mapema........huu ni ufujaji...., nashawishika kuamini kuwa kila baada ya uchaguzi magari huwa wanapeana zawadi..nikiangalia serikalini magari yaliyonunuliwa hata mwaka 1990 mengine bado yanafanya kazi .....kwanini kati ya mashangingi 200 yaliyotumika uchaguzi wa 2005 ...hayaonekani tena.......sana sana ni yale magari ya kihindi ndio yanaonekana yakitumiwa na makatibu wa chama wilaya.........

nadhani CCM wanahitaji kuajiri kampuni ifanye uhakiki wa mali zake.....na kuziwekea codes!!
 
Hiki Chama Cha Majambazi walipata wapi hizo pesa za kuagiza hayo magari? Isije kuwa ndio wakishinda wanaanza tena kurudisha fadhila.

nambiwa hapa kuwa that is PART OF a cut from MULT MILLION DOLORS tender award kununua MATREKTA YA KILIMO KWANZA ...aliyopewa jamaa mmoja ....matrekta yataagiziwa india!!
 
Makala kama kweli ni mkweli yeye alitakiwa kuwapa waandishi wa habari hizi risiti wazione na awape copy waweke hadharani maana si siri ila alitaka ukweli . Tutajuaje kama risiti hizo ni za magari yaliyo bandarini ? Why idadi inapungiua tena na wakati wakubwa wake walisema ni 200 ? Je baada ya kumwita Slaa muongo ndiyo hawaendi mahakamani kama walivyo tamka ? Bado kuna siri kubwa ukweli mwingi umefichwa.Ngojeeni Slaa akiibuka .
 
BEI ya shangingi moja ni 100 milioni....sasa hawa jamaa wamenunua 150...ina maana jumla kwa kazi hii watatumia 15 BILIONI...sasa kwa chama makini kama ccm inavotaka ionekane...watuambie wamepata wapi BILIONI 15 za kununua magari ambayo hata serikali yenyewe kupitia waziri mkuu pinda aliagiza yasinunuliwe kwa kuwa yana gharama kubwa kununua na kuyahudumia pia....

CCM ninayoijuwa ni wafujaji wakubwa wa mali hasa magari ..laiti ccm wanguwa watunzaji wa magari yao wasingehitaji kununua magari mengi namna hii kila kampeni ...sanasana wangekuwa wananunua machache kama 20 kwa ajili ya kumbeba mgombea na entourage yake ...yaliyobaki wangetumia yaliyopo......lakini ukweli ni kuwa magari ya chama hayatunzwi vema ,hayawekwi vipuri halisi.....inachangia kuharibika mapema........huu ni ufujaji...., nashawishika kuamini kuwa kila baada ya uchaguzi magari huwa wanapeana zawadi..nikiangalia serikalini magari yaliyonunuliwa hata mwaka 1990 mengine bado yanafanya kazi .....kwanini kati ya mashangingi 200 yaliyotumika uchaguzi wa 2005 ...hayaonekani tena.......sana sana ni yale magari ya kihindi ndio yanaonekana yakitumiwa na makatibu wa chama wilaya.........

nadhani CCM wanahitaji kuajiri kampuni ifanye uhakiki wa mali zake.....na kuziwekea codes!!
PM,

Kwa akili yako kweli unaamini CCM wameenda kununua magari yao Japan, tena kwa mpigo magari 150. Bado unaamini watanunua hizo gari kwa bei ya zaidi ya milioni 100 kwa moja?

Nipe mimi milioni 70, nitakuletea gari kama hiyo mpya na kubakiwa na kama milioni 10 zangu za kula. Ila ushuru Dar juu yako.

Hata mwandishi hapa chini kaingia mkenge kama wako. Hao Wahindi Dar wanatulangua hayo magari.


CCM yatumia Sh10b kununua magari
YASEMA MECHI BILA MAZOEZI HAKUNA USHINDI,YASISITIZA KULIPA KODI

Mwandishi Wetu

IMEBAINIKA kwamba CCM imetumia takriban Sh70 milioni kununua gari moja kati ya magari 150 aina ya Land Cruiser Hardbody yaliyoagizwa kwa ajili ya kufanikisha mradi wa kuimarisha chama" hicho, lakini bei halisi ya magari hayo ni zaidi ya Sh107 milioni.

Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kuwa CCM itatumia zaidi ya Sh10 bilioni kununua magari yote 150 ambayo yatasambazwa kwenye wilaya zote nchini kufanikisha shughuli za kisiasa za chama hicho tawala.

Taarifa za kuingizwa kwa magari hayo zilifichuliwa na katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wakati alipoituhumu CCM kuwa imeingiza magari 200 na kukwepa ushuru wa takribani Sh600 milioni.

Dk Slaa alitoa tuhuma hizo wakati akihutubia kwenye moja ya mikutano ya Operesheni Sangara mkoani Tanga, lakini CCM ikamkosoa kuwa idadi ya magari iliyoagiza ni 150 na kwamba kiwango cha ushuru ni kikubwa zaidi ya alichokitaja.

Lakini tofauti hiyo ya bei halisi ya magari hayo na kiasi cha fedha kilichotajwa na CCM kuwa kimetumika kugharamia ununuzi wa magari na ushuru, kinaweka maswali kuhusu ukweli wa sakata hilo.

CCM imeeleza kuwa imeshaingiza magari 74 kutoka Japan wakati mengine 76 yapo bandarini yakisubiri kukamilika kwa taratibu za kulipia ushuru ili yatolewe wakati wowote kuanzia leo.

Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kuwa CCM pamoja na kulipa ushuru imenunua gari moja kwa Sh70,451,619.7. Lakini taarifa kutoka kampuni inayouza magari hayo hapa nchini (Toyota Tanzania Limited) zinaonyesha kuwa gari moja la aina hiyo pamoja na kulipia ushuru linauzwa kwa Sh107,813,905, ikiwa ni tofauti ya Sh37,362,285.3.

Katibu wa masuala ya uchumi na fedha wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Amos Makalla alibainisha wakati akiongea na waandishi wa habari kuwa chama hicho kimetumia Sh3,493,354,830 kununua magari hayo na imetumia Sh1,720,065,031 kulipia ushuru.

"Kwa magari hayo 74, tumelipa Sh3,493,354,830, sasa kama wewe ni mwanamahesabu mzuri jumlisha na ushuru tuliolipa wa Sh1,720,065,031 utajua gharama zote," alisema Makalla, ambaye alikuwa kiongozi wa tatu kutoa ufafanuzi wa tuhuma za Dk Slaa baada ya kutanguliwa na katibu wake mkuu, Yusuf Makamba na katibu wa itifaki wa Nec, John Chiligati.

"Ukitaka kujua bei ya gari moja aina ya Toyota Landcruiser Hardbody tuliyonunua, chukua kiasi hicho gawanya kwa 74."
Kwa maana hiyo, jumla ya fedha zilizotumika kununua na kuingiza magari hayo ni Sh5,213,419,861, ambayo ukiigawanya kwa 74 unapata Sh107,813,905, ambazo zilitumika kununulia gari moja kati ya hayo 150.

Kwa maana nyingine, gharama za magari 76 yaliyo bandarini zinakadiriwa kufikia Sh5,354,323,100.5 bilioni zikujumuishwa na ushuru wa Sh1,766,553,275.1 bilioni unaotarajiwa kulipwa kwa ajili hiyo.

Lakini utafiti uliofanywa Toyota Tanzania Limited, ambayo ni wakala wa magari hayo nchini unaonyesha kuwa bei ya sasa ya gari aina ya Toyota Landcruiser Hardbody ni Sh107 milioni baada ya kulipiwa ushuru na kukamilisha taratibu nyingine.

Kiwango hicho kinafanya tofauti ya bei iliyotumiwa na CCM na ile ya kampuni ya Toyota ni takribani Sh33 milioni. Makalla hakupatikana baadaye jana kutoa ufafanuzi kama magari waliyoagiza ni mtumba au ni mapya. Pia wakala aliyeagizia magari CCM hakuweza kupatikana jana.

Mwaka 2005, CCM pia iliagiza shehena ya magari aina ya Mahindra ambayo pia yaliamsha tuhuma kuwa chama hicho tawala kilikwepa kodi wakati wa kuyaingiza.

Makala alithibitisha kuwa magari mengine 76 yataanza kutolewa bandarini muda wowote kuanzia leo, pindi TRA itakapokamilisha taratibu na nyaraka husika zitakazoiwezesha CCM kulipia ushuru.

"Tumeyaleta (haya magari) kwa ajili ya mradi wa kuimarisha chama, lakini zitasaidia pia uchaguzi wa 2010. Tunalenga kuwafikia wananchi wote hata vijijini, tunafanya siasa ambayo bila usafiri haiwezekani, lakini kwa kuwa uchaguzi ni mwakani, tunafanya mazoezi kwani mechi bila mazoezi huwezi kushinda. Sasa tunapiga jalamba," alisema Makalla.

Tangu Dk Slaa amwage hadharani mpango huo, viongozi tofauti wa CCM wamejaribu kutoa ufafanuzi, akiwemo Chiligati ambaye alisema kwa kifupi tu kuwa chama hicho ni kikubwa hivyo suala la kununua magari hayo si la ajabu.

Makamba alifafanua makombora ya Dk Slaa kwa kueleza kuwa alikosea katika idadi ya magari yaliyoagizwa na CCM na kutaja kuwa ni 150 na ndipo Makalla alipoanza kutoa ufafanuzi kwa kuonyesha waandishi nakala za nyaraka za kuagizia magari hayo na risiti za benki za kulipia ushuru. Kuhusu mkakati wa wanaCCM kukichangia chama hicho fedha ili kijitegemee, Makalla alisema wanachama wameitikia wito huo na wengi wameonyesha nia ya kuchangia, lakini akasema baada ya vikao vikuu vya CCM Januari na Februari mwaka 2010 watazindua kampeni hizo za kuchangisha fedha.
 
Back
Top Bottom