CCM na falsafa ya bomoa tutajenga kesho, itatufikisha wapi?

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Kwa kufuatilia mtiririko wa namna CCM inavyofanya kampeni katika chaguzi mbalimbali tangu mwaka 2010 na kuendelea ni rahisi kugundua kuwa chama hicho sasa kinatumia falsafa ya bomoa tutajenga kesho. Falsafa hii iliwahi kuiimbwa na mwanamziki mmoja nchini kwetu kama hivi ifuatavyo: "bomoa ee, bomoa ee, bomoa mama tutajenga kesho...". kwa kufuata falsafa hii Kigogo mmoja wa CCM baada ya uchaguzi wa 2010 aliwahi kusema kuwa sasa ni wakati wa kuponya majereha ambayo nchi imeyapata wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010.

Falsafa hii ya bomoa tutajenga kesho imetumika Arusha na sehemu nyingine na sasa imehamia Igunga. Hii ni falsafa ya kubomoa misingi ya umoja wa nchi yetu ilimradi tu CCM wapate kura. Hivi karibuni CCM na wapambe wao wameanza kutumia falsafa ileile.

Safari hii wanamtumia mkuu wa wilaya aliyebabwa akiwa na mtandio wake akifanya kampeni za CCM kwa kutumia nafasi yake ya serikali kama DC. Magazeti yanayotumiwa na CCM yaani Habari leo na vyombo vingine vya habari vinaendelea kubomoa, eti kavuliwa hijabu na hivyo kadhalisha imani ya watu fulani. Lakini falsafa hii ya kupata kura kwa kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini itatupeleka pabaya ambako baada ya CCM kubomoa sijui kama nchi itajengeka tena.
 
Back
Top Bottom