CCM Mwanza tifutifu - mbunge Ndasa atimuliwa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,894
mbunge%2Bwa%2BSumve%2BRichard%2BNdasa%2Bakichangia%2Bhoja%2Bya%2Bwizara%2Bya%2Bviwanda%2Bna%2Bbiashara.JPG

HOT NEWS....CCM MWANZA KIMENUKA ,MBUNGE NDASA ATIMULIWA

KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, imemfukuza kwenye kikao, Mbunge wa Sumve wilayani humo, Richard Ndassa, kwa madai kwamba ameanza kuunda makundi na mgogoro kwa madiwani wa halmashauri hiyo, ili madiwani hao wamkatae mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa maslahi yake binafsi; imedokezwa.

Imeelezwa kwamba, Ndassa anatuhumiwa kuanza kuwarubuni baadhi ya madiwani wa CCM, ili wamkatae mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Zephania Masangu (CCM), na kwamba siku hiyo ya kikao cha kamati ya siasa kilichofanyika Novemba 3 mwaka huu, mbunge huyo alifukuzwa ndani ya kikao ili wajumbe waweze kumjadili kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kuanzisha mgogoro ndani ya halmashauri hiyo inayoongozwa na CCM.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mwanza Sitta Tumma anaripoti kuwa ,taarifa zilizoifikia mwandishi wa mtandao huu kutoka jijini Mwanza, Sitta Tumma, kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, zimeeleza kwamba, Ndassa ameanzisha harakati hizo za kutaka kumg'oa mwenyekiti huyo, ili aweke mtu anayemtaka yeye, kinyume cha taratibu na kanuni za chama, na kwamba siku hiyo ya kikao alitolewa nje na hakurudi hadi tena kikaoni.

Kwa mujibu wa habari hizo, kamati hiyo ambayo iliwaita na kuwahoji madiwani wake mmoja baada ya mwingine kuhusiana na mgogoro huo, inatarajia kutoa maadhimio yake Novemba 10 mwaka huu, na huenda ikamwadhibu vikali mbunge huyo pamoja na madiwani anaoshirikiana nao kupanga njama hizo chafu za kutaka kumng'oa mwenyekiti Masangu katika nafasi yake hiyo.

"Ndassa ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya, lakini siku ya kikao alitimuliwa na hakurudi tena. Kisa cha kufukuzwa kwenye kikao hiki ni njama zake za kuanza kuwarubuni baadhi ya madiwani wa CCM ili wapitishe maazimio ya kumkataa mwenyekiti wa halmashauri kwa maslahi yake binafsi na jamaa zake.

"Kimsingi tunaiomba sana kamati yetu imwadhibu huyu Ndassa na ikiwezekana afukuzwe uanachama, maana ameanza kuigawa CCM. Ndassa hamtaki mwenyekiti wa halmashauri (Masangu), kwa vile anatetea sana maslahi ya wananchi wa Kwimba, na anapiga vita mambo ya kifisadi", kilisema chanzo kimoja cha habari kutoka ndani ya kamati hiyo.

Huyo Ndasa anakiburi sana!! Inabidi wajipange hiyo kamati maana ni mbishi!! Ila ningependa kama kweli anakwamisha mambo ya msingi kwa wananchi basi wamtose tu bila kujali ni magamba au nani.
 
kwa sababu ulizozitoa huyo m/kiti ndiye atakaye ng'oka maana mafisadi wana nguvu sana ktk nchi hii na hawakamatiki
 
Wajameni Mhe. Richard Mganga Ndassa, namfahamu fika, ni mtu makini. Kama ni kweli alipiga ndogondogo kumng'oa Mwenyekiti wa Halmashauri yake, then mwenye matatizo ni huyo Mwenyekiti.

Mwendishi aliyeileta hii habari, ni wale wanahabari wa 'petty cash journalisim' ambaye ameegemea upande mmoja. Kwa nini hakumtafuta Ndasa kuupata upande wa pili ili abalance story yake?.

Binafsi namuaminia Ndasa, hivyo lazima kutakuwa na madudu ya huyo mwenyekiti na yataibuliwa na atakwenda na maji.
 
Sifahamu unamfahamu vp huyu Ndasa. Mimi pia namfahamu. Ni mbunge wa jimbo langu. Ni mmoja wa wabunge 'bogus' waliopata kutokea Tz. Ni tajiri huyu ndugu, akiaminiwa kujitajirisha kwa nguvu za giza. Kwa kutumia pesa yake naamini M/kiti wa Halmashauri hana chake!
 
Hakuna kiongozi msafi CCM labda Mwenyekiti wa kijiji chetu ambaye it happens ni Baba yangu mzazi!
 
Wajameni Mhe. Richard Mganga Ndassa, namfahamu fika, ni mtu makini. Kama ni kweli alipiga ndogondogo kumng'oa Mwenyekiti wa Halmashauri yake, then mwenye matatizo ni huyo Mwenyekiti.

Mwendishi aliyeileta hii habari, ni wale wanahabari wa 'petty cash journalisim' ambaye ameegemea upande mmoja. Kwa nini hakumtafuta Ndasa kuupata upande wa pili ili abalance story yake?.

Binafsi namuaminia Ndasa, hivyo lazima kutakuwa na madudu ya huyo mwenyekiti na yataibuliwa na atakwenda na maji.

Pasco,

Pamoja na imani uliyonayo kwa Ndassa bado haiondoi ukweli kwamba si mtu makini na ni fisadi. Bila shaka utakuwa unakumbuka lile sakata la kamati ya bunge iliyowahi kuundwa kwa ajili ya kuchunguza tuhuma fulani(sikumbuki ni tuhuma gani) na Ndassa akiwa mjumbe na ikaja kubainika kwamba walikula rushwa wakapindisha ukweli na kutoa taarifa ya uongo iliyopelekea wabunge wale kusimamaishwa kuhudhuria vikao vya bunge.

Unaikumbuka hiyo skendo? Je katika hali kama hiyo bado unadhani Ndasa ni mtu makini?
 
Sifahamu unamfahamu vp huyu Ndasa. Mimi pia namfahamu. Ni mbunge wa jimbo langu. Ni mmoja wa wabunge 'bogus' waliopata kutokea Tz. Ni tajiri huyu ndugu, akiaminiwa kujitajirisha kwa nguvu za giza. Kwa kutumia pesa yake naamini M/kiti wa Halmashauri hana chake!

Kuna skendo moja ya rushwa iliwahi kuikumba kamati teule ya bunge Ndasa akiwa mjumbe, walituhumiwa kula rushwa na kutoa ripoti ya uongo hali iliyopelekea kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge, unaikumbuka?
 
Me nilijua amevuliwa uanachama na jimbo liko wazi...aaaargh!

CCM hawana hiyo jeuri sasa hivi maana hawana uhakika wa kulitwaa jimbo Kama watamfukuza mbunge. Ingekuwa zamani walipokuwa na uhakika wa kulirejesha jimbo wangethubitu, lakini sasa hivi ng'ooooo.
 
mimi nilifikiri katimuliwa chamani ili tuanze maandalizi ya kugombea jimbo? kumbe katimuliwa kikaoni tu, ushanika stimu kabisaaaaaaaaaaaaaam. ngoja nitoke nikapunge upepo.
 
hao watumikia tumbo wanakazi kwelikweli kila kukicha wanagombania kujaza tumbo tu.
 
Back
Top Bottom