CCM Mwanza haijatulia

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

5.png
0.png
7.png
1.png
7.png

[h=2]
[/h]JUMATANO, JULAI 11, 2012 06:24 NA JOHN MADUHU, MWANZA

WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, wamemtuhumu mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Clement Mabina kuwa ni mmoja wa viongozi wanaokiangusha chama chao.

Mabina, alishushiwa tuhuma hizo nzito katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho, kilichofanyika Chuo cha Veta Nyakato, kilitawaliwa na maneno ya kejeli,vurugu na ubabe, huku baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakitishiana kutaka kupigana ngumi kavu kavu kutokana na kutofautiana kauli.

Wajumbe wa kikao hicho, inaelezwa walikuwa wakitofautiana na wakati mwingine kuzomeana au kupigiana makofi kutokana na tofauti zilizopo.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zinasema tuhuma za Mwenyekiti kujihusisha na rushwa na kushindwa kukiongoza chama hicho na kukisababishia kupoteza baadhi ya majimbo zilirushwa kwake na wajumbe wa Halmashauri ya Mkoa, Richard Rukambura pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman.

Taarifa za uhakika, zinasema aliyeanza kumshambulia Mabina ni Rukambura ambaye alikieleza kikao hicho kuwa suala la kupinga rushwa katika chaguzi limekuwa zito kutokana na viongozi waliopewa dhamana ya kupiga vita rushwa wamekuwa wakijihusisha na rushwa.

“Tuanze nawe Mabina,wewe ni mpokeaji wa kitu kidogo namba moja,umekuwa ukipokea rushwa katika chaguzi mbalimbali kwa ajili ya kuwapendelea baadhi ya wagombea,hivyo hufai kuendelea kuwa Mwenyekiti",alisema Rukabura.

Kutokana na madai hayo, alikuja juu na kumtaka mjumbe huyo aketi chini ambapo hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu, Kache aliingilia kati na kumtaka Mabina kumuacha mjumbe huyo azungumze suala hilo hadi mwisho.

Kiongozi mwingine, aliyemtuhumu Mabina ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman alidai mwenyekiti huyo ameshindwa kuunganisha chama.

Akijibu tuhuma hizo, Mabina aliiambia MTANZANIA kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake hazina msingi wowote, zaidi ya wajumbe hao kuwa na chuki zao.

“Haya ni mambo ya kupangwa ili kuvuruga kikao,mimi sio mla rushwa, nafuata taratibu katika kusimamia haki na sio vinginevyo",alisema Mabina

ndio unadhani watamuita Lau Masha tena kuwa mbunge? asahau
 
Yaani ukiwa mchawi ukimaliza woote utawageukia hadi wanao mwisho utajimaliza mwenyewe!
 
Mabina anajulikana sana kuwa ni mtoto wa mjini. Amekuwa mtu wa mention town tangia bia za magendo miaka ya 90 pia alikuwa anajihusisha na uvamizi ziwani.

Kwa umri wake hayo hayawezi tena bali ni kuchukuwa chako mapema tu, rushwa nk. Kwa sasa anashirikiana na dc wa misungwi, mawe matatu na mh ngereja katika mkakati wa kuwalinda wachimbaji wadogo wadogo kule kitongo.

Hawa wachimbaji wanapeleka asilimia 30 ya uzalishaji ili walindwe.

The guy is so corrupt to the teeth
 
Well said. Mabina is one of the very corrupt leaders CCM is having. Wachimbaji wale wadogo wa dhahabu wamekuwa mradi wa Mabina na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi. Kila mara wamelazimika kuchanga fedha na kuwapa viongozi hawa ili wawatetee wasiondolewe kwenye eneo ambalo ni la Mwekezaji. Huyu Mabina ni mhalifu ambaye hafai hata kuwa raia wa kawaida achilia kuwa kiongozi wa ngazi yeyote ile.
 
Kwa kuwa nguvu ya dola imeshindwa fanya kazi hasa PCCB, Naomba tujaribu Nguvu ya Umma
 
Sio huko Mwanza. Hata huku kwetu na sehemu zote itakuwa hivyo kabla ya kale kauchaguzi kao. Na 2015 ndio itakufa rasmi.
 
Kwani PCCB wanafanyakazi gani ? They all corrupt therefore, they cannot persecute no one. PCCB is there for JK and his corrupted guys. In the long run I do not think we need PCCB because they are hopeless; they leave the BIG FISHES and net the small people. WHY

Mabina alikuwa mwizi wa magari wa kujulikana katika hiyo miaka ya nyuma. hata alimtumia cousin wake mmoja katika kuiba magari bahati mbaya akakamatwa na kuwekwa lupango hapo dar(kisutu), mipango ikafanyika akawekewa dhamana siku ya hukumu hakushow-up kesi ikawa imezimwa kiana na yule mtu aliyemwekea dhamana haubughudhiwa lakini Mungu wa mema yule mwizi alikokimbilia alichukua mzinga wa gari na kufa...labda ilikuwa ni kutoa kafara. binafsi huwa naona nchi hii ni jalala. kuna kipindi alijifanya mfanyabiashara wa bia kutoka kenya via ziwa victoria akiungana na jamaa mmoja wa magnum company wakikwepa ile mbaya kulipia ushuru kwa kuingiza bia katika fukwe za kichororoni.this guy is thief na ninashangaa hii ccm wanaitakia kheri tanzania? lkn tetesi kataka mlango wa nyuma kuna biashara chafu inafanyika na jamaa mmoja huko dar amejipenyeza na kupata access ngazi tawala ndiyo kinara plan nzima ya mabina....game not over yet.
 
Well said. Mabina is one of the very corrupt leaders CCM is having. Wachimbaji wale wadogo wa dhahabu wamekuwa mradi wa Mabina na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi. Kila mara wamelazimika kuchanga fedha na kuwapa viongozi hawa ili wawatetee wasiondolewe kwenye eneo ambalo ni la Mwekezaji. Huyu Mabina ni mhalifu ambaye hafai hata kuwa raia wa kawaida achilia kuwa kiongozi wa ngazi yeyote ile.

Magu lazima ikombolewe, akina mabina wameshindwa kazi, nasikia anataka kugombea jimbo la Magu baada ya Dr. Limbu kushindwa kuliletea maendeleo jimbo hilo, hakika sijawahi kuona Dr Mchovu kama Limbu, huyu bwana angerudi kwenye academics ili afundishe maana ni mtaalamu sana wa uchumi, lakini siasa imemuacha. Tuungane kukaikomboe magu.
 
Mabina siyo mla rushwa tu, ni Jambazi toka siku za nyuma, ukiingia kwenye anga zake unakufa. Pia alikuwa mfanya magendo sana toka kenya kupitia ziwani wakiwa na kishimba, Kitano na wengine wafanyabiashara hapa Mwanza.

5.png
0.png
7.png
1.png
7.png

JUMATANO, JULAI 11, 2012 06:24 NA JOHN MADUHU, MWANZA

WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, wamemtuhumu mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Clement Mabina kuwa ni mmoja wa viongozi wanaokiangusha chama chao.

Mabina, alishushiwa tuhuma hizo nzito katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho, kilichofanyika Chuo cha Veta Nyakato, kilitawaliwa na maneno ya kejeli,vurugu na ubabe, huku baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakitishiana kutaka kupigana ngumi kavu kavu kutokana na kutofautiana kauli.

Wajumbe wa kikao hicho, inaelezwa walikuwa wakitofautiana na wakati mwingine kuzomeana au kupigiana makofi kutokana na tofauti zilizopo.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zinasema tuhuma za Mwenyekiti kujihusisha na rushwa na kushindwa kukiongoza chama hicho na kukisababishia kupoteza baadhi ya majimbo zilirushwa kwake na wajumbe wa Halmashauri ya Mkoa, Richard Rukambura pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman.

Taarifa za uhakika, zinasema aliyeanza kumshambulia Mabina ni Rukambura ambaye alikieleza kikao hicho kuwa suala la kupinga rushwa katika chaguzi limekuwa zito kutokana na viongozi waliopewa dhamana ya kupiga vita rushwa wamekuwa wakijihusisha na rushwa.

“Tuanze nawe Mabina,wewe ni mpokeaji wa kitu kidogo namba moja,umekuwa ukipokea rushwa katika chaguzi mbalimbali kwa ajili ya kuwapendelea baadhi ya wagombea,hivyo hufai kuendelea kuwa Mwenyekiti",alisema Rukabura.

Kutokana na madai hayo, alikuja juu na kumtaka mjumbe huyo aketi chini ambapo hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu, Kache aliingilia kati na kumtaka Mabina kumuacha mjumbe huyo azungumze suala hilo hadi mwisho.

Kiongozi mwingine, aliyemtuhumu Mabina ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman alidai mwenyekiti huyo ameshindwa kuunganisha chama.

Akijibu tuhuma hizo, Mabina aliiambia MTANZANIA kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake hazina msingi wowote, zaidi ya wajumbe hao kuwa na chuki zao.

“Haya ni mambo ya kupangwa ili kuvuruga kikao,mimi sio mla rushwa, nafuata taratibu katika kusimamia haki na sio vinginevyo",alisema Mabina

[/QUOTE]
 
mfa maji haachi kutapatapa so sioni hilo jambo kama ni geni kwa ccm na kwanza wameanza mapema sana mtulie tu myaone mengi kwenye siasa hiyo tuendayo 2015
 
kweli ccm imejaa rejects,hadi huyu ? Mwizi maarufu toka niko darasa la kwanza pale nyamagana miaka hiyo ? Lol. Ccm is like music, no matter what the music changes,it keep on dancing !
 
Mabina anajulikana sana kuwa ni mtoto wa mjini. Amekuwa mtu wa mention town tangia bia za magendo miaka ya 90 pia alikuwa anajihusisha na uvamizi ziwani.

Kwa umri wake hayo hayawezi tena bali ni kuchukuwa chako mapema tu, rushwa nk. Kwa sasa anashirikiana na dc wa misungwi, mawe matatu na mh ngereja katika mkakati wa kuwalinda wachimbaji wadogo wadogo kule kitongo.

Hawa wachimbaji wanapeleka asilimia 30 ya uzalishaji ili walindwe.

The guy is so corrupt to the teeth

Mwambie aliewatuma kakosea step. Baada ya thread ya jana ya madiwani 22 kuhamia CDM kufail naona mmekuja kivingine. Mabina sitomzungumzia sana na kwa kuwa mimi kama mimi najua lengo ni kumchafua mawe matatu na si vinginevyo. Mmenoa. Polly Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi ndiyo amewatuma hapa nadhani. Naomba mtambue kitu kimoja. Watanzania wameamka sana. No more CCM katika jimbo la Misungwi kama mawematatu hatakuwapo. Kaeni mkilijua hilo. Pollycap ni mwizi na ndiyo anajaribu kupanga haya. Ni kweli Clement alifanya haya magendo ya bia miaka uliyoitaja na hayakuwa ya kupendeza. Na ni kweli pia alikuwa mtoto wa mjini sana na kwa sasa sijui ana behave vipi. Lakini kwa mawe matatu umechemka. He is innocent na ni mtu aliyestragle mwenyewe kwa shule na kufanikwa kuwa na miradi yake halali. Jipangeni upya. Polly mwizi na hamtamuosha kwa jinsi hii.
 
Mabina alikuwa mwizi wa magari wa kujulikana katika hiyo miaka ya nyuma. hata alimtumia cousin wake mmoja katika kuiba magari bahati mbaya akakamatwa na kuwekwa lupango hapo dar(kisutu), mipango ikafanyika akawekewa dhamana siku ya hukumu hakushow-up kesi ikawa imezimwa kiana na yule mtu aliyemwekea dhamana haubughudhiwa lakini Mungu wa mema yule mwizi alikokimbilia alichukua mzinga wa gari na kufa...labda ilikuwa ni kutoa kafara. binafsi huwa naona nchi hii ni jalala. kuna kipindi alijifanya mfanyabiashara wa bia kutoka kenya via ziwa victoria akiungana na jamaa mmoja wa magnum company wakikwepa ile mbaya kulipia ushuru kwa kuingiza bia katika fukwe za kichororoni.this guy is thief na ninashangaa hii ccm wanaitakia kheri tanzania? lkn tetesi kataka mlango wa nyuma kuna biashara chafu inafanyika na jamaa mmoja huko dar amejipenyeza na kupata access ngazi tawala ndiyo kinara plan nzima ya mabina....game not over yet.

Jamaa wa Magnum alikuwa anaitwa Mamata na walikuwa kundi moja na wahaya fulani jina sina na Polly mwenyekiti wa Misungwi akiwemo.
 
Back
Top Bottom