CCM msiendelee kutumia mtaji wa adui mliyeshindwa kumuondoa

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
Inasikitisha sana kuona wanasiasa wakiwekeza kwenye uelewa mdogo wa watu.
Inakera kuona watu badala ya kuelimisha wanazidi kusambaza ujinga kwa watu wakati wa kampeni.

MSEMO KUWA MCHAGUENI ATAKAYESIKILIZWA NA SERIKALI ni kauli inayopaswa kukemewa kwani inapotolewa na wanasiasa ambao ni viongozi katika jamii inasikitisha. UJINGA ni miongoni mwa maadui wealiokuwa wawe wameondolewa kama vita hivyo vingekuwa vya kweli. Lakini inaonekana watawala wanapenda ujinga kwa faida yao binafsi.
Ni heri ushindwe uchaguzi lakini wananchi wakamshinda adui ujinga kwa msaada wako. Kampeni zingetumika pia kama elimu isiyo rasmi. Tafadhali CHADEMA msiache kujibu hoja hizi kwani madhara ya ujinga ni makubwa. ( Ujinga ni adui aliyeshindwa kuondolewa na viongozi wetu)
Wapeni mifano ya jinsi halmashauri zinazoongozwa na upinzani zinavyofanya vizuri. Kwa miaka kadhaa manispaa ya Moshi haina mbunge wa CCM. Maeneo ya jirani na Arumeru kama Karatu, Arusha mjini, Hai, Rombo, Vunjo kote ni wapinzani.
Hii mifano ni ya muhimu kuliko mnavyoweza kuamini. CCM inaendelea kula matunda ya ujinga ( uelewa mdogo) wa wananchi. Elimu ya uraia iendelee kutolewa wakati huu wa kampeni.

Wakumbusheni tena kuwa maeneo yenye wapinzani ndiyo yenye maendeleo zaidi. Hoja hizi zisingekosekana.
Mimi sio mwanachama wa CDM wala CCM ila ninachukia kuona viongozi wanaopaswa kueleza mambo ya muhimu wakiwafanya watu wajinga.
 
  • Thanks
Reactions: GIB
Back
Top Bottom