CCM, mshindi ni nani?

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Vikao vikuu vya CC na NEC vimemalizika Dodoma kwa Edward Lowassa kulipua bomu kuwa Rais alikuwa anajua kila kilichokuwa kinaendelea kuhusu richmond. Pamoja na yote yaliyojadiliwa, hoja ya kuvuana magamba imerudishwa kamati kuu na pia Chiligati na Nape nao watafikishwa katika kamati ya maadili na ikibainika kuwa wametenda makosa hatua za kinidhamu juu yao zatachukuliwa.

Swali langu ni hili, tuliambiwa wamewapa siku 90 watuhumiwa wa ufisadi wajiondoe ktk chama. WATUHUMIWA HAWAJAJIONDOA except RA. Je, katika vuta nikuvute hii, nani ameibuka mshindi???
 
Wote wameshindwa. Alichofanya Lowassa ni kuonyesha kiwango cha uchafu uliomo CCM. Mwakyembe alificha kwenye ripoti yake na kutuambia kuwa ameacha kusema mambo fulani kwa ajili ya kuilinda serikai. Lowassa kaamua kutoboa baadhi ya hayo yaliyofichwa ambayo yanaonyesha kuwa hata Kikwete alihusika kwenye sakata la Richmond. Wote wamechafuka
 
Kwa vile lengo lao, ilikuwa kumvua gamba Lowasa, na kama tulivyosoma ni kuwa Lowasa ametoa utetezi usio na shaka kuwa kila alichofanya kilikuwa na baraka za bosi wake JK, hivyo hoja ya kuvuana gamba ikafa natural death, basi fisadi Lowasa kashinda tena kwa KO, kwa sababu Nape na Chiligati watesi wake ndiyo sasa watawekwa kikaangoni. Nafurahi sana hili movie la magamba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom