CCM Mnawafahamu Hawa, John Ayo na Mrs.Kirilo??

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,995
2,494
John Ayo alikuwa kada mtiifu wa CCM kwa muda mrefu saaana na diwani, lakini Sasa ameukubali ukweli na kusimamisha Bendera ya CHADEMA nyumbani kwake, na Kadi ya CHADEMA mfukoni. Pia ni mhamasishaji mkubwa wa Chagua Nassari maeneo ya Nkoaranga. CCM fungueni macho muone na mjiulize kwanini mnapoteza hazina zenu?
Naamini ni kwasababu mnachoamini na kutenda ni tofauti na mnachohubiri.

Mama Kirilo.
Huyu mama ni mke wa Marehem Mheshiwa J. Kirilo, mzee alepigania uhuru, mwananchi wa kwanza kwenda Leaugue of Nation kuomba uhuru wa Ardhi ya Meru, kati ya waasisi wa CCM lakini sasa na yeye kapandisha Bendera ya CHADEMA nyumbani kwake, na alimpa Nassari baraka zote.

Nionavyo:
Kama makada na walofaidika na ccm wameanza kujitoa waziwazi bila uoga basi ccm inakufa haraka sana. Na hii ni kutokana na matendo yao. Kutoka "Nyundo Na Jembe" to "Wizi Na Ufisadi"
 
Pilipili usiyoila inakuwashia nini? Hao watu umewataja kwa ridhaa yao au maamuzi yako na unataka washughulikiwe? Nadhani ujumbe umefika
 
Back
Top Bottom