CCM mna mkakati gani dhidi ya Lema?

Toka asimamishwe ubunge wa Arusha mjini, Godbless Lema amekuwa akifanya harakati kubwa sana za kisiasa dhidi ya CCM, akipita kijiji kwa kijiji akitumia uwezo wake wa kuzungumza kwa ujasiri na hoja zinazogusa wananchi wa ngazi ya chini kabisa,

Sio siri tena athari kadhaa kubwa zimeanza kuonekana waziwazi kwenye kila eneo alilopita, kwa mfano:
1/Makada wengi kutoka CCM wamejiunga na Chadema.
2/Chadema imeanza kuota mizizi vijijini.
3/Chuki dhidi ya Serikali imeongezeka.
4/Woga wa kifikra miongoni mwa wananchi umeanza kutoweka.
5/Chadema imepata wanachama wengi sana maeneo mapya.

*Swali langu kuu kwa viongozi na makada wa CCM, mmejipangaje kukabiliana na hii hali, maana msipochukua hatua sasa mwisho wa siku ni kilio.

Nawashauri arejeshewe Ubunge wake, apangwe kwenye kamati mojawapo ya changamoto nyingi kama nishati; kwa ziara zote zinazohitaji uwepo wa wabunge apangwe ili kumtenganisha kabisa na sisi wa tabaka la huku chini
 
Back
Top Bottom