CCM mmeridhika na Livingstone Lusinde?

Wasipomshtaki huyu jamaa! CDM inawalakini

Thats why I admire Mtikila!

CDM maneno mengi sana...yaani uccm mwingi mno..huyu jamaa anatakiwa kufunguliwa mashtaka, na adhabu yake jimbo linaenda kwa CDM uko mtera
 
Mkuu wa sheria wa CDM chukua maoni ya wadau.Huyu mwehu lazima ashtakiwe.
 
Bangi mbaya sana wajameni si matusi ya bure hayo na wakati huo anayatoa atakuwa alikuwa amevuta si bure kutamka maneno ya aibu kiasi hicho mbele za watu wazima na akili zao.
Hata waliokuwa wanamsikiliza na kumshangilia wote wapuuzi kwa mtazamo wangu HAIWEZEKANI jamaa linawatukana hata wao halafu mnashangilia na kusikiliza ujinga na upuuzi.
Mtu mzima ovyo LUSINDE!!!!!
 
No comment. Sijawahi sikia matusi ya nguoni namba hiyo. Anazo akili timamu?
 
eti lusinde kasimama jukwaani anatamka kwamba yeye ni kichaa wa kuzaliwa ..sijui waliokuwa wanamsikiliza kichaa na kushangilia tutawaitaje?je walio mchagua jimboni kwake wakoje? mpaka wakamchagua kichaa?

cdm pelekeni mtu mwenye akili timamu akachukuwe jimbo 2015
 
Afadhali ccm wangemwachia Mzee Malecela aendelee kama huyu kijana mwenzetu ndo hivi. Sijui hata wapiga kura wake wanajisikiaje huko jimboni. Poleni wana Mtera hili ni janga.
 
Booooonge la hotuba, cdm wakimwaga mboga ccm tunamwaga ugali.....jino kwa jino wakijamba tunaharisha!
wewe kweli pumb-a. Kune ubonge gani katika hotuba ambayo hata mtoa hotuba mwenyewe kaomba radhi kwa ***** alioumwaga hadharani! Msifie mtu kwa sera zenye mantiki, sio kushoboka
 
Lusinde alihamia CCM toka CDM, na bado tunaendelea nae kumrekebisha maana maadili na hayo anayoyapractise kayatoa huko alipotoka.
 
Mzazi wa Mh. huyu angekuwepo siku ya hotuba hii, angejisikia vibaya kuleta kiumbe kama hiki duniani.
 
Do huyo ndie aliepiga chini kwa mzee Malecela! Naomba niletewe na ya Lema nilinganishe au wenyewe hawana matechinician wa kutunza kumbukumbu?
 
Kweli huyu bwana alikosa sera, Chama cha Mapinduzi kisipomwajibisha huyu bwana basi nitajua kumbe ndo lugha ndani ya vikao vyao. Lakini si-shangai sana; maana Nape N. alinukuliwa akiwa viwanja vya magomeni-Kirumba Mwanza, watu walipoanza kumuuliza maswali, kaishia kutukana; matokeo yake uchaguzi umekuja wamepoteza.
 
Lusinde alihamia CCM toka CDM, na bado tunaendelea nae kumrekebisha maana maadili na hayo anayoyapractise kayatoa huko alipotoka.
Mkuu wana ccm wenye akili timamu hawawezi kusifia matusi ya Lusinde , kimsingi ukirejea kauli za wazee wetu Bujiku na Kitine hawa ndio wanaoua ccm taratibu
 
mkuu ngosha kitoga,mi cpati picha mwanae akimkosea anavyomuogesha mitusi,jamaa ni noma khaaa
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom