Poor thinking.
Chama kinataka kugawanyika vipande vipande. haya tusubiri yetu macho na masikio!
Poor thinking.
Chama kinataka kugawanyika vipande vipande. haya tusubiri yetu macho na masikio!
Mkuu Mchambuzi,
Nimechukua hiyo para ya kwanza tu ili tuweze kuijadili kwa marefu na mapana dhana nzima ya haya mabadiliko. Wajumbe wa NEC ambao watakuwa ni full time job ni wa kutoka wilayani tu. So, mawaziri na wabunge bado wana opportunity ya kuingia kwenye NEC na CC kupitia matundu yafuatayo:
Kwa hiyo mawaziri na wabunge bado wanaweza kupitia kwenye tundu la NEC (Taifa), wawakilishi wa wabunge wa CCM au kupitia kwenye Jumuiya za Chama na haswa UWT.
Tatizo la mabadiliko haya ya Katiba, hayalengi kuipatia CCM viongozi waadilifu wala kupunguza mlundikano wa vyeo kwa mtu mmoja. Mfano mdogo tu, je, baada ya haya mabadiliko, Januari Makamba, Mwigulu Nchemba na Chilligati watabaki kuwa wajumbe wa Secretariat ya NEC ambao wanahudhuria vikao vyote na bado ni wabunge? Mwenyekiti wa UWT Taifa ni waziri, mjumbe wa NEC na CC. Anna Makinda ni Mbunge, Spika, Mjumbe wa CC na NEC, Eng. Stella Manyanya ni Mkuu wa Mkoa, Mbunge na Mjumbe wa NEC kupitia UWT.
Katiba za UWT, Wazazi, na UVCCM hazijabadilishwa katika kuweka sifa za wagombea wa ujumbe wa NEC kupitia Jumuiya hizo. Wala wagombea wa NEC Taifa haijasemwa kwamba wasiwe mawaziri. Contradiction iko kwenye kundi la wawakilishi wa wabunge, what if mwakilishi wa wabunge ni Waziri?
Kwa mtazamo wangu, mabadiliko haya hayajafanyiwa kazi kwa kina na kwa umakini. Wangeweka wazi kwamba nafasi za NEC Taifa wabunge wote hawaruhusiwi kugombea. Pia futa kundi la wawakilishi wa wabunge kwenye NEC.
Haya ni matunda ya kushindikana kwa operation vua gamba kwa kuwa tayari Chama kilishatekwa na matajiri na hawajui namna ya kukirudisha kwa walalahoi. Kila njia wanayopendekeza inaonekana kama vile haifanyi kazi. Walianza na kuvua magamba, imeshindwa. Wamekuja na mabadiliko ya Katika, nayo itashindwa bado kuna watu wataendelea kuwa na influence kwenye vikao vya NEC na CC. Mwisho wanataka kuunda Kamati ya Maadili na Nidhamu [ingawa ilikuwepo ambayo ilikuwa inaongozwa na JK]. Sasa kwa sababu JK hataki kuonekana yeye ni mbaya, anataka kusukumia watu wengine wafanye kazi ya kudhibiti mafisadi. Sasa kama NEC na CC wameshindwa kuwadhibiti, hiyo Kamati mpya ya maadili itawezaje kuwashughulikia wale wote ambao wanaonekana kwamba ni magamba?
Mfumo wa Uhongaji ndani ya CCM hauhitaji uwepo wa mhusika mkuu, bali ni swala la mhusika mkuu kutafuta mtu wake na kuhakikisha kwamba anasimamia kila kitu ili kuhakikisha kwamba mgombea wao anashinda.
Mfumo huu wa sasa utawabeba wenye fedha tu!! Unajua wajumbe wengi kule mawilayani hawakuingia katika nafasi hizo kupigania chama bali kutafuta ulaji. Ndiyo maana katika kura za maoni pesa inatembea katika majimbo kama njugu. Sasa wameongezewa tena kiosk kingine cha wajumbe wa NEC. Hvyo wanaotaka nafasi watapaswa kuwa na fedha ili kuchaguliwa mawilayani. Kama hawana fedha itabidi watafute mapema godfather. Hapo ndipo hao wazee watakapoingia. Wao wala hawataenda mawilayani. siku hizi mpaka m pesa na tigo pesa zinapeleka hela. Unadhani nani ata monitor mambo haya?