CCM Madarakani: Sababu za kuitoa, ugumu wake na mbinu mbadala za kuing'oa

Nina sababu tatu za msingi ambazo zimenifanya niichukie na kutopenda kuiona timu ya CCM na vibaraka wake wakiendelea kunitawala.
1. Wameshindwa kushughulikia kikamilifu suala la miundombinu - wote tunajua kuwa miondombinu ni sawa na sensory nerves kwenye mwili wa binadamu, bila kuwa na miundombinu inayofanya kazi na inayokidhi mahitaji ya leo na ya miaka angalau 50 ijayo basi maendeleo itakuwa ndoto.
- Mabarabara yanayojengwa hayakidhi mahitaji yaliyopo, achilia mbali ya miaka 5 ijayo {mfano barabara za jiji la DSM ambazo zimejengwa ktk awamu ya nne - Mandela, Kilwa, etc, sehemu nyingi za nchi hii bado hazifikiki (yakiwemo maeneo yaliyoko mjini kama Kibamba) tangu tupate uhuru miaka 50 sasa.
- Wameshindwa kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala la msongamano wa magari jiji Dsm, licha ya kufanya ziara elfu kidogo nchi za nje zenye mifumo inayoeleweka kwenye majiji yao na wasijifunze lolote.
- Tanzania ni moja ya nchi chache duniani ambayo haina shirika la ndege linalofanya safari za kimataifa, na hakuna jitihada za dhati za kuwawajibisha wale wote walioshiriki kulifilisi shirika letu la ATC.
- Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na mpaka na njia kuu ya usafirishaji (bahari) na imeshindwa kuitumia kuwakomboa wananchi wake. Badala ya kuendeleza bandari na miundombinu inayoingia kwenye bandara ya Mtwara kwa ajili ya kuhudumia nchi jirani za Malawi, Zambia, DRC, Mozambique, serikali ya CCM inaelekeza nguvu kuendeleza bandari ya Bagamoyo bila sababu zozote za kuridhisha.

2. Imeleta na inaendeleza matabaka katika jamii, ubaguzi wa aina yoyote ile ilikuwa sababu mojawapo iliyowalazimu mababu zetu wadai uhuru kutoka kwa wakoloni. Lakini miaka 50 baadaye serikali imeshindwa kusimamia usawa wa fursa za kujikwamua na changamoto katika maisha yao. Kwa sasa kuna matabaka katika kutoa huduma za jamii kama vile elimu, afya na nyingine nyingi. Viongozi wa serikali yetu hawatumii huduma za elimu, afya zinazotolewa na serikali wanayoiiongoza na badala yake huduma hizi zimebaki kuwa duni zisizokidhi mahitaji na hakuna jitihada zozote za msingi kulirekebisha tatizo hili ambalo baadaye linaweza kusababisha migogoro katika jamii yetu. Leo hii kuna watanzania wachache ambao wanaweza kuvunja sheria yoyote bila kuguswa na chombo chochote cha serikali huku wengine wakiandamwa ili kuwakomesha, haya tumeyaona kwa macho yetu kwenye mchakato wa kura za maoni za ccm ambapo rushwa na vitendo visivyo vya kistaarabu vilitawala lakini ni baadhi tu ndio waliowajibishwa richa ya kuwepo vyombo vyo dola katika kona zote za nchi hii. Ni aibu kwa TAKUKURU kuutangazia ulimwengu kuwa ni Iringa peke yake ndiko kulikuwa na vitendo vya rushwa!

3. Imeshindwa kusimamia rasimali za taifa hili kikamilifu na kushindwa kuwawajibisha wale wote ambao wameliingiza taifa katika mikataba ya kinyonyaji na wageni au watu wengine.

Kwa sababu hizi na nyingine nyingi za msingi, nimeamua kuwanyima kura yangu, naomba uniunge mkono ili tulikomboa taifa hili kwa kuwanyima CCM kura
 
Ni kweli wamegeuka kuwa ngedere na kula mahindi shambani badala ya kuyalinda, wamekuwa watembeza bakuli bila aibu eti kuna njaa, wakati hawajui njaa inasababishwa na nini. Hawafai kabisa kukabidhiwa shamba tena!!

Tunahitaji mabadiliko sasa, wakuu ni muda wa mabadiliko tusidanganyike, tunahitaji kubadilisha walinzi shambani kwetu, mabadiliko yanaanza na mimi na wewe!

Tuamkeni kutoka katika huu usingizi!
 
jk....ameweza amefanya mengi.....nchii hii ni maskini...na watu ni wavivu.....na wapenda dezo......nchi inapokuwa masikini watu wanajituma sana kote duniani tofauti hapa kwetu walizoea bure kila kitu.......haya mashirika yamekufa kwa sababu hizo ....ufisadi ulikuwemo lakini na watu sio wabunifu......sasa kikwete mnatka akujazeni mapesa mfukoni ?
ukweli utabaki hatujapata kuwa na rais mstarabu na muungwana wa kweli zaidi ya kikwete..ni mkweli kwa juu...hakuna raia amedhulumiwa tangia amengia madarakani, hatujasikia mabomu ya machozi , police sasa angalau wanafanya kazi zao bila kuonea onea, raia wameanza kujua haki zao , bunge limekua huru kuliko wakati wowotw wa tanzania.....uhuru wa kusema na kukosoa umekua mkubwa sana hakuna kiongozi anemfikia
,huyu jamaa ameweza na hakuna kati ya wanao gombea anamshinda........na ukweli atashinda sababu anazo,uwezo anao, na nia anayo.......ni kiongozi bora amabye tumepata anaheshimika dunia nzima,,,, heshma anayopata inatokana na uongozi wake wa busara na kuwajali watu wake...anahangaika kwa ajili ya sote.....mpeni kura zenu...
 
Mkuu ni haki yako. Lakini kusema watanzania ni wavivu ni tusi.

Hii serikali unayosema ianawajali watu imewezesha nini ili uzalishaji uongezeke?
Miundo mbinu tu angalau, wapi?
Dar ndiyo mkoa unaochangia mapato y anchi zaidi ya 60%, ona hiyo foleni!!! Wamefanya nini?
Ona umsikini!! Unajua 2005 sukari ilikuwa shs ngapi mkuu? Linganisha na leo?

Ukweli ni kuwa CCM hakuna jipya.... wanapumulia mashine tu!!!
Sasa hivi kwa vitendo vyao, kila kijana aliyeajiriwa serikalini amekuwa mwizi. Why? Hakuna uzalendo na ndo hao hao wanao-process mahela ya wizi kwa wakubwa!!! Tenda hewa.... mkuu tafakari tena, haya unayoyaona kwa juu ni danganya toto, maana wanajua mdanganyika wa kawaida ndo anayoweza kuayaona kirahisi ili kujustfy kurudi madarakani.

CCM is a crap....rotten and corrupt party. Leo hii, wezi wao wameshapanga mpaka serikali ya 2015. Bado unasema watu hawa!!!!
 
Mawazo ya kupenda kupangiwa mipango ya maendeleo yana tabu sana. Ndio maana kulifanyika mkutano wa Rio de Janeiro mwaka 1992 kuondokana na mambo ya kupangiwa kupangiwa kila kitu.
 
Mawazo ya kupenda kupangiwa mipango ya maendeleo yana tabu sana. Ndio maana kulifanyika mkutano wa Rio de Janeiro mwaka 1992 kuondokana na mambo ya kupangiwa kupangiwa kila kitu.

Mkuu hapa sijakupa, unataka kusema nini, hebu fafanua kido.
 
Aibu yako milele. Mbona hapa unakua mvivu wa kufikiri kiasi hiki?
Hukusikia mabomu na kuchomewa moto wakazi wa loliondo? Hukusikia juu ya kilichotokea North Mara kwa sumu kudhuru wananchi?
Ushahidi waonyesha amengia ikulu kwa fedha za EPA. Ukikinzana na mwanae lazima akushughulikie kikamilifu.
Serikali yake imeshindwa uthibiti mfumuko wa bei? Ufaulu wa wanafunzi sekondari umeshuka mwaka hadi mwaka.
Amewajibu wafanyakazi kwa dharau walipodai maslahi yao. Ni Katika serikali yake ata walimu walifikia hatua ya kuitisha mgomo.
Amekosa umakini na kusingizia kadanganywa kwa kusaini sheria ya uchaguzi bila kuisoma na kujua imechakachuliwa. Kafungua hoteli leo kesho tanroads wakaivunja uzio wake.
 
Ahsante, nimepata sababu zingine za msingi kuwachukia na kutotaka wasogee Ikulu.
 
...Imeleta na inaendeleza matabaka katika jamii, ubaguzi wa aina yoyote ile ilikuwa sababu mojawapo iliyowalazimu mababu zetu wadai uhuru kutoka kwa wakoloni....

hakuna ubaguzi mbaya kuliko ule wa matabaka na hasa tabaka la uongozi (mtandao); wale wote waliokosa tabaka hilo na hasa kupitia ubunge na udiwani wameambiwa waondoke tena watasindikizwa na chama; mfano shibuda, selelii, shelukindo, bhanji...

nawashanga watu kama kina MS mmeamua kujipofua wenyewe hamuoni ukweli huo kuwa wenye chama ni hao waliopo mtandaoni; ninyi ni vyombo tu vya kuwatengenezea ulaji.
 
Pamoja na juhudi nyingi zinazofanywa na CCM kuinusuru na anguko kuu lililotabiriwa na nabii wao (Nyerere), ishara zote zinaonyesha machweo yamewajia vibaya kiasi kwamba imebidi hata vitisho vya kijeshi vitumike

Hata hivyo, anguko la CCM halikwepeki this time..... the unbeliavable shall be the believable...........

Follow the link for illustration http://www.youtube.com/watch?v=CXQE7C1CPWM
 
Kama vyama hivi vya upinzani vitainyamazia Tume za Uchaguzi bila ya kuzichukulia hatua yeyote ,basi tuelewe kuwa CCM itatawala nchi hii milele na milele.

Kuna idadi ya WaTanzania ,kuna idadi ya waliojiandikisha kama wapiga kura ,kuna waliopiga kura , pia kuna huu msamiati tunaousikia siku hizi wa Uboreshaji wa Daftari la kupigia kura.
Haikubaliki tupo waTz zaidi ya milioni 50 wanaopiga kura hawazidi hata milioni 20.
hayo ya mahesabu weka kando kwani wakiwa wengi au kidogo Tume hazihusiki wala hazipati tabu kuseti nambari hizo ,kwa vile watakalolitamka wao ndio lishapita.

Tumeona katika maandishi Lowasa akimwita Slaa mwongo ,katika barua alimwambia Slaa asihadaike na wingi wa watu wanaohudhuria mikutano, ni lazima akae na kujua siasa za Tanzania zinaendeshwa vipi ,something like that...! Hii ni kukatisha tamaa kisaikolojia iweje yeye Lowasa aliweka kambi huko kwake hivi akizungumza na miti ???

Vyama ni lazima vidai tume hizi za Uchaguzi ziwe huru kabisa zisizohusiana na chama chochote kile hata kama itabidi kukodi wazungu waje watusimamie shughuli za uchaguzi tokea uandikishaji hadi upigaji kura ,tume hizi ni lazima zibadilishwe kikamilifu kama si hivyo basi hakuna siku upinzani utashinda.
 
Hakika Mwiba hicho cha kudai tume huru ndo cha msingi. Lakini naona wanapambana maana hata Lipumba jana kwenye kumtangaza Jk aliiongelea. Nafikiri ni kazi ya wadau wote kuwapigia kelele ccm na serikali yake tume ibadilishwe ASAP
 
Back
Top Bottom