CCM London na viongozi wao

SNC15067.JPG

Huyu owino ndio nani tena?

Mwanamalundi,

rekebisha picha yako... inaonekana link inapotea
 
Yeboyebo,

Mkuu najua ni makini sana lakini hao jamaa zako kwenye chama ni fake
na utasikia mengi.

Ndio maana wengine tulikuwa tunapinga haya mambo ya vyama Ulaya. Sisi wote ni watanzania na chama cha Watanzania kingelitosha kabisa.

Naona umeguswa na kuwa mkali na mashambulizi kwenye hili. Mimi sishangai
maana kwa watu wanaohangaika na kufungua matawi Ulaya sidhani kama moyo wao uko kwa taifa zaidi ya kujitengenezea njia kwa mwaka 2010.

Mkuu Mtanzania

Nitakuwa mjinga sana nikiamini 100% kuwa hawa watu wanafanya Charity, lakini bado sioni ubaya kwa wanalolifanya maana kama ni siasa na huo uongozi upo wazi kwa yoyote kugombea. Pia, hawa watu wao wameona vipaji vyao nipo kwenye siasa; kwa nini tusiwape nafasi ya kufanya siasa zao bila haya masimango na majungu (so far, hakuna data kamilifu) yasiyo na kichwa wala miguu.

Mimi nafahamu watanzania ambao wamewahi kufanya kazi za kujitolea kwa wazungu ili wapate njia ya kupata kazi za uhakika hapo baadae; wapo waliofanikiwa na wengine wamekata tamaa. Sasa kuna ubaya gani hawa ndugu zetu kuamua kuwatumikia watanzania wenzao kupitia siasa ili hapo baadae wawe viongozi kwenye nchi yetu. Kwa nini tunaheshimu watu wakiwa madaktari, walimu, wameba boksi huku ulaya lakini tunashindwa kuwaheshimu hawa wanasiasa (japo kuwapa benefit of dought) ambao wameona wanaweza kuwatumikia Watanzania wenzao kupitia siasa?

Mimi sioni kama nitadhurika na lolote, na iwapo kuna mwanabodi anaona sisi kama Watanzania hapa tutakuja kudhurika kwa sababu CCM ina Tawi hapa UK basi anielimishe. Lakini mpaka sasa sioni hoja, zaidi ya kashfa na majungu yasiyo na mashiko.

Tukate issues.
 
Mwafika wa Kike

Sioni hoja hapa, Mgaya anataka watu waje wajadili mambo aliyafanya Maina akiwa Sekondari..!!

Nasubiri hayo ya Daruso maana huko walau alikuwa na madaraka na akili za utu uzima.

hawa watu wananichekesha hapa !
 
Yes GT

I never left, hizi tuhuma zisizo na kichwa wala miguu hazina nafasi hapa. Hii Forum ina heshima zake.

Hakuna ushahidi wowote wa kusapoti hoja yako kuwa CCM London walipokea £60,000 kutoka kwa jamaa wa Commonwealth. Labda kama hao Commonwealth nao ni mafisadi. Nina imani na Commonwealth maana kama walitoa hela wangetaka pia kujua zilitumikaje; na mimi kwa macho yangu sioni kilichofanyika ambacho kingerithisha Commonwealth. Hivyo, usiwapake matope Commonwealth kuwa wanatoa hela ili zinafanyiwe ufisadi.

Daruso jamani, hakuna mwenye Data?

nasubiri kwa hamu kusikia ufisadi wa kweli wa huyu jamaa, Lunyungu akiwa mshika dau mkubwa wa facts za huyu jamaa !
 
Yeboyebo,

Nimeahidiwa kupewa namba ya huyu Bashiru. Ingawa pia naambiwa kuwa niulizie Mafuru na Maimu. Hawa ni kina nani?

Mwafrika wa Kike

Nina waziwasi kwa kuwataja hao ndugu majina hapa bodini iwapo watakubali kuwa open kwako. Sijui utatumia njia gani lakini nina mashaka wakijua majina yao yalikuwemo humu wanaseza kukuwekea ngumu. Ni wazo langu tu..
 
Mimi ndio maana naipenda JF, ukweli na uwongo hujitenga wenyewe. Hii ndio faida ya kuja na data.

Mwafrika wa Kike

Heshima yako, umeleta Data ulizopewa hapa, mkuu Kitila Mkumbo kaziona hazina ukweli, FD na Gembe pia wameona hazina ukweli; tena yeye alifuatilia baada ya kutoa tuhuma kama hizi anazopewa Maina Owino. Heshima yako Gembe kwa kumuomba radhi mhusika.

Tanzanianjema

Unakuja kwenye hii hoja na kumwambia Kitila Mkumbo akae pembeni kwa nini, Mhe Kitila ametetea ukweli anaoujua. Sasa kama wewe huo uovu alioufanya Daruso kwa nini usiuweke hapa??????????????????

Weka mambo hapa, walipotia mlimani ni wengi watathibitisha. Tayari tumeshaona data za Kitila na Gembe. Tupe zako, binafsi naangalia Data; sitaki kusikiliza hizi sifa za kuwa huwa husemi na kwamba ukisema basi lazima ni kweli. Wanabodi wana akili zao timamu weka data hapa watu tunyangamue mwenyewe.

Tanzanianjema weka Data; usimfanye Kitila amalize popcorn zake bila sababu.

ndio kwanza mwanzo huuu !
 
Kitila,

Ukisoma habari zinazoingia kuhusu Maina utasikitika. Ninajua kuna watu kibao watakuja na habari zake. Inawezekana Maina alikugeuka kama Mkapa alivyomgeuka Nyerere..... kwi kwi kwi!

Wewe kamata popcorn tayari for the movie....

mimi nasubiria PM ya huyu Bashiru ... inaonekana ana habari nyeti za Maina. Yeyote mwenye habari anipe kwenye PM nitazimwaga hapa na sitataja jina.

Ukisha pata mwaga hapa ndiyo maana ya JF tuchambue wenyewe .
 
wewe ulisema data unazo ! zimwage sasa !

Mkuu Kada,

Nimpe Lunyungu haki yake, alishasema yeye data hana angekuwa nazo angeshazimwaga hapa. Kwa hilo sina shaka kabisa na Lunyungu.

Aliyesema ana data ni Tanzanianjema. Tunasubiri kwa shauku...

Heshima mbele.
 
Yeboyebo,

Nimeahidiwa kupewa namba ya huyu Bashiru. Ingawa pia naambiwa kuwa niulizie Mafuru na Maimu. Hawa ni kina nani?

Bashiru is too high kuingia katika siasa hizi. Mafuru anajua mengi lakini ni corporate elite dont expect any thing there. MAIMU? damn hapa ndio patamu, yanakuwa ya kesi ya EPA kuwapelekea kina ......

Yeboyebo and other concerned CCM's, fanyeni kazi yenu kabla hamjaula wa chuya. Ukisoma post yangu ya mwanzo utaelewa kuwa ni kwa manufaa yenu wana DIASPORA "wakereketwa" kudeal naye wenyewe yasije yakawa ya kina Zitto na Buzwagi na kutoa ushindi wa chee kwa mnaowaita wapinzani wenu. Muulizeni ilichukuwa muda gani kuweza kupata clearance yake MLIMANI na kwanini ilizuiwa? Hilo ni chembe tu ya mengi likiwemo lilomfanya atoke mkuku RORYA 2005.

Hata kama hamuwezi kuzuia jahazi (CCM) lenu kuzama mnaweza kupungusa mwendokasi wa uzamaji wake.....

Tanzanianjema
 
Mkuu Mtanzania

Nitakuwa mjinga sana nikiamini 100% kuwa hawa watu wanafanya Charity, lakini bado sioni ubaya kwa wanalolifanya maana kama ni siasa na huo uongozi upo wazi kwa yoyote kugombea. Pia, hawa watu wao wameona vipaji vyao nipo kwenye siasa; kwa nini tusiwape nafasi ya kufanya siasa zao bila haya masimango na majungu (so far, hakuna data kamilifu) yasiyo na kichwa wala miguu.

Mimi nafahamu watanzania ambao wamewahi kufanya kazi za kujitolea kwa wazungu ili wapate njia ya kupata kazi za uhakika hapo baadae; wapo waliofanikiwa na wengine wamekata tamaa. Sasa kuna ubaya gani hawa ndugu zetu kuamua kuwatumikia watanzania wenzao kupitia siasa ili hapo baadae wawe viongozi kwenye nchi yetu. Kwa nini tunaheshimu watu wakiwa madaktari, walimu, wameba boksi huku ulaya lakini tunashindwa kuwaheshimu hawa wanasiasa (japo kuwapa benefit of dought) ambao wameona wanaweza kuwatumikia Watanzania wenzao kupitia siasa?

Mimi sioni kama nitadhurika na lolote, na iwapo kuna mwanabodi anaona sisi kama Watanzania hapa tutakuja kudhurika kwa sababu CCM ina Tawi hapa UK basi anielimishe. Lakini mpaka sasa sioni hoja, zaidi ya kashfa na majungu yasiyo na mashiko.

Tukate issues.

Yebo yebo naamini mimi na wewe twafahamiana kiasi .Hebu sema .Uko katika Uongozi wa CCM London ana uongozi wa Watanzania UK .Je kuna watu wana kofia 2 mbili kwenye CCM na Chama cah Watanzania hapo UK na wewe upo hivyo ? Maana naona unaumia sana.Nimetoa onyo hapa .Tanzanianjema ni kijana makini hana papara .Fuatilia onyo lake hadi wakaamua kumfuata huko Rorya lazima wanajua mengi .Kitila kasema na huyo Mwalimu kasema lakini nasema hakuna cha Charity UK wacha utaona bomu lilipuke utajua nini nasema hapa .Muulize Bugurunikwamnyamani atakupa picha zaidi .
 
Bashiru is too high kuingia katika siasa hizi. Mafuru anajua mengi lakini ni corporate elite dont expect any thing there. MAIMU? damn hapa ndio patamu, yanakuwa ya kesi ya EPA kuwapelekea kina ......

Yeboyebo and other concerned CCM's, fanyeni kazi yenu kabla hamjaula wa chuya. Ukisoma post yangu ya mwanzo utaelewa kuwa ni kwa manufaa yenu wana DIASPORA "wakereketwa" kudeal naye wenyewe yasije yakawa ya kina Zitto na Buzwagi na kutoa ushindi wa chee kwa mnaowaita wapinzani wenu. Muulizeni ilichukuwa muda gani kuweza kupata clearance yake MLIMANI na kwanini ilizuiwa? Hilo ni chembe tu ya mengi likiwemo lilomfanya atoke mkuku RORYA 2005.

Hata kama hamuwezi kuzuia jahazi (CCM) lenu kuzama mnaweza kupungusa mwendokasi wa uzamaji wake.....

Tanzanianjema

Tanzanianjema

Nina imani kuwa una nia njema kabisa, lakini kwa nini unatufanya kama watoto wadodo (mtoto ndiye anayeambiwa, usifanye hiki; akiuliza kwa nini, unamwambia ukikua UTAJUA). Hilo dodoso uliloweka ni dogo mno kulishika kwa mikoni miwili na kumlima nalo mtu ambaye ni kiongozi wa jamii tena mwenyekiti (CCM London).

Mbona unawawekea kasoro mashahidi wote...kabla ya kujua wamesema nini? hata kama wana la kusema watasema tena kweli?

Yebo yebo naamini mimi na wewe twafahamiana kiasi .Hebu sema .Uko katika Uongozi wa CCM London ana uongozi wa Watanzania UK .Je kuna watu wana kofia 2 mbili kwenye CCM na Chama cah Watanzania hapo UK na wewe upo hivyo ? Maana naona unaumia sana.Nimetoa onyo hapa .Tanzanianjema ni kijana makini hana papara .Fuatilia onyo lake hadi wakaamua kumfuata huko Rorya lazima wanajua mengi .Kitila kasema na huyo Mwalimu kasema lakini nasema hakuna cha Charity UK wacha utaona bomu lilipuke utajua nini nasema hapa .Muulize Bugurunikwamnyamani atakupa picha zaidi .

Naam Lunyungu,

Mimi sio kiongozi wa kuteuliwa au kupigiwa kura kwenye CCM wala Tanzania Association UK. Lakini kama unavyonifahamu; sikubali kamwe watu wapakwe matope bila sababu.

Siko hapa kumtetea mtu, ila kuna tuhuma zimewekwa (kwa bahati mbaya namfahamu mhusika) na mimi ninachoomba na kusisitiza ni data ziwekwe hapa watu tujue pumba na mchele.

Mtu akija na data zenye mashiko hapa mimi nitakuwa wa kwanza kuwa mpole. Wala msije mkadhani nitaona aibu; Ila mpaka dakika hii ni majungu tu.
 
Bashiru is too high kuingia katika siasa hizi. Mafuru anajua mengi lakini ni corporate elite dont expect any thing there. MAIMU? damn hapa ndio patamu, yanakuwa ya kesi ya EPA kuwapelekea kina ......

Yeboyebo and other concerned CCM's, fanyeni kazi yenu kabla hamjaula wa chuya. Ukisoma post yangu ya mwanzo utaelewa kuwa ni kwa manufaa yenu wana DIASPORA "wakereketwa" kudeal naye wenyewe yasije yakawa ya kina Zitto na Buzwagi na kutoa ushindi wa chee kwa mnaowaita wapinzani wenu. Muulizeni ilichukuwa muda gani kuweza kupata clearance yake MLIMANI na kwanini ilizuiwa? Hilo ni chembe tu ya mengi likiwemo lilomfanya atoke mkuku RORYA 2005.

Hata kama hamuwezi kuzuia jahazi (CCM) lenu kuzama mnaweza kupungusa mwendokasi wa uzamaji wake.....

Tanzanianjema

Sasa kama Bashiru ni too high... Mafuru ni Corporate, huyu Maimu ni nani na yuko wapi?
 
Mwafrika wa Kike

Nina waziwasi kwa kuwataja hao ndugu majina hapa bodini iwapo watakubali kuwa open kwako. Sijui utatumia njia gani lakini nina mashaka wakijua majina yao yalikuwemo humu wanaseza kukuwekea ngumu. Ni wazo langu tu..

Yeboyebo,

Kuna njia nyingi za kuwapata hawa. Nimepata message kuwa Mafuru na Maimu walikuwa wote viongozi wa Daruso pamoja na Owino. Sasa kesi ya kwanza hapa ni kuwa. Je wakati wa uongozi wa Owino pale mlimani, pesa za wanafunzi zilitumika bila taarifa maalumu? Je ni kweli kuwa kuna walifunguliwa mashitaka ya ufujaji wa pesa ya Daruso?
 
....

Mtu akija na data zenye mashiko hapa mimi nitakuwa wa kwanza kuwa mpole. Wala msije mkadhani nitaona aibu; Ila mpaka dakika hii ni majungu tu.

Yeboyebo,

je unaamini au huamini kuwa pesa za Daruso zilifujwa wakati Owino akiwa katibu wa chama?
 
Nilikuwa maeneo ya Shirati wakati wa mchakato wa CCM kumpata mgombea wa Rorya. Huyu Maina Owino alikuwa katika wale waliokuwa wanamtia kitimutimu Prof. Sarungi. Wengine wakati huo walikuwa Prof. Bwathondi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), na mwingine kama kumbukumbu zangu alikuwa mfanyakazi ama lecture wa institute moja.

Sasa kuwa Maina Owino alijitoa sababu ya kashfa hilo napingana nalo, na sipingani nalo kuwa namtetea. La hasha sijuani naye, na vile vile sikipendi chama tawala kwa kinachotufanyia, nadhani sina haja ya kuyataja hapa yanayofanywa na CCM.

Ila makubaliano yalikuwa Maina Owino ajitoe, ampishe Mzee. Ili miaka ijayo, yaani 2010, Mzee naye atamsaidia Maina kwa kampeni. Ikumbukwe kuwa wakati wa mchakato huu, kulikuwa na ugomvi wa dhahiri kati ya Sarungi na Bwathondi. Maina akiwa kundi la Sarungi.

Ninayo zaidi, lakini fedha tu za kumwaga, huyu kijana alikuwa nazo. Hivyo kujitoa kwake kulikuwa ni kuwa anasubiri akabidhiwe kijiti.
 
Sasa kama Bashiru ni too high... Mafuru ni Corporate, huyu Maimu ni nani na yuko wapi?

Hawa jamaa wlishawahi kuwa viongozi pale Daruso pamoja na Owino miaka kati ya 1999 na 2000. Maimu alikuwa Rais wa Daruso akitokea engineering, ni kijana machachali sana ukiweka ligi naye atakutoa tu kwa porojo si ajabu naye yuko CCM mahali furani.
 
Yeboyebo,

je unaamini au huamini kuwa pesa za Daruso zilifujwa wakati Owino akiwa katibu wa chama?

I don't know kama hii itatimiza lengo lolote, ila iwapo unapenda kujua mimi nimesimama wapi basi nikujibu kuwa; niko na Maina Owino mpaka pale ushahidi kamilifu utakapopatikana. Mpaka hapo ushahidi utapowekwa mezani nampa benefit of dought.
 
Na huo ushahidi inabidi uwe kwa format ipi? ile iliyomtoa Lowasa au ile ya Abacha wa Nijeria?
 
Back
Top Bottom