Elections 2010 CCM kweli hawana haya...yaani wataka kumvua ubunge huyu dogodogo...........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Jimbo la Muhambwe ambalo limebebebwa na NCCR-MAGEUZI huenda likaamuliwa na mahakama kuu baada ya mgombea wa CCM kuamua kujitosa mahakamani kudai haki yake kama ipo..................SOURCE: Habari Leo............


Kwa maoni yangu..............

Ikumbukwe jimbo hilo limechukulia na Mbunge mpya na mwenye umri mdogo kuliko wote bungeni Mheshimiwa Felix Mkosamali........ungelifikiria CCM kama kingelikuwa ni chama makini kingelizingatia utata wa NEC ilivyosimamia chaguzi hii wangeliwaagiza wagombea wao waliobwagwa kuachana mara moja na kukimbilia mahakamani ili kuleta maelewano ya kiutaifa na hasa ukizingatia kijana Mkosamali ndiye chipukizi kuliko wote bungeni.............

Oneni aibu CCM.....kura muibe na bado mwataka sasa mahakama iwaongezee majimbo isivyo halali na kinyume cha sheria...huu ulafi utaisha lini?
 
kama mwnyekiti wa chama ndo master mind wa uchakachuaji, wanachama itakuaje?
 
KUMBUKA ANA KESI NA KANISA KATOLIKI......... TAKUKURU WILAYA AMENUNULIWA GARI(?)....... TAKUKURU WALIKUWA WAKIMPIGIA KAMPENI HADHARANI(?)....... SI MAJUNGU ULIZA MWANA KIBONDO NA ASEME FROM THE HEART WHO THE MAN IS....!
tusubiri tuone
 
KUMBUKA ANA KESI NA KANISA KATOLIKI......... TAKUKURU WILAYA AMENUNULIWA GARI(?)....... TAKUKURU WALIKUWA WAKIMPIGIA KAMPENI HADHARANI(?)....... SI MAJUNGU ULIZA MWANA KIBONDO NA ASEME FROM THE HEART WHO THE MAN IS....!
tusubiri tuone

Hueleweki kabisa! Nani ana kesi?
 
we unaejiita mahesbu ni mbumbumbu sana tena toa picha ya nyerere hapo, unataka kusema TAKUKURU wamemhonga jamaa wa NCCR na kumpigia kampeni? kwakweli wwe ur nul in ur head!kanisa na takukuru wanauhusiano gani? na huyo ccm why hakupigiwa debe na takukuru, hope this is another crap
 
Tuache ushabiki Kukata rufaa ni haki ya wagombea wa vyama vyote, kama hana ushahidi mahakama itatupa rufaa yake.
 
KUMBUKA ANA KESI NA KANISA KATOLIKI......... TAKUKURU WILAYA AMENUNULIWA GARI(?)....... TAKUKURU WALIKUWA WAKIMPIGIA KAMPENI HADHARANI(?)....... SI MAJUNGU ULIZA MWANA KIBONDO NA ASEME FROM THE HEART WHO THE MAN IS....!
tusubiri tuone
Sijaelewa kitu hapa....unaidhalilisha picha ya Mwalimu broda...
Kwanini harakaharaka?..andika kitu kinachoeleweka, ndiyo nia ya msingi ya upashanaji habari!
Unakuwa kama Kiranga-fulani bana!
 
CCM yapitisha aliyetajwa kuuza viungo vya Albino

lC.gif
Mwandishi Wetu​
Agosti 18, 2010
rC.jpg

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) iliyokutana Dodoma kuchuja na kupitisha majina ya wagombea wake wa ubunge, imepitisha jina la mgombea ubunge aliyewahi kupigiwa kura na wanakijiji akitajwa ni muuaji na mnunuzi wa viungo vya maalbino, Raia Mwema imebaini.
Mgombea huyo (jina linahifadhiwa) ambaye sasa atakuwa ameweka rekodi ya kushinda kura ya maoni CCM pamoja na kura ya maoni ya mauaji ya maalbino iliyowahi kuendeshwa na Serikali, ni kutoka katika jimbo moja (jina linahifadhiwa) mkoani Kigoma.
Gazeti hili limefanya uchunguzi na kuwasiliana na vyombo vya usalama, na kuthibitishiwa na baadhi ya wakazi jimboni humo ambako mgombea husika ameteuliwa kugombea ubunge.
Taarifa tulizo nazo zinaelekea kumshutumu mteule huyo wa CCM kwa makosa kadhaa ya jinai, na mshangao ni wa jumla kuhusu uteuzi wa mtu anayeonekana hafai kwa kigezo chochote isipokuwa matumizi ya fedha na ufadhili wake kwa wakuu wa chama.
Aidha mawasiliano na baadhi ya wajumbe wa NEC walioshiriki kikao cha Dodoma hivi karibuni, yanabainisha kuwa mchujo wa mgombea huyo ulizua utata mkubwa kwenye kikao hicho, utata ambao msingi wake ni mvutano kati ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kigoma na Kamati ya Siasa ya Wilaya anakotoka mgombea.
Katika kikao hicho, jina la mgombea huyo liliwasilishwa NEC kutoka Kamati Kuu na lilipofikia hatua ya kujadiliwa ndipo mvutano ulipojitokeza.
Katibu wa CCM ngazi ya Mkoa wa Kigoma anatajwa kutoa maelezo akibainisha kuwa mgombea alikataliwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya kwa tuhuma mbalimbali zikiwamo za mauaji ya maalbino, tuhuma ambazo zimetokana na wananchi kumpigia kura za maoni wakati Serikali ilipoendesha upigaji kura ya maoni kufichua wauaji maalbino.
Kiongozi huyo alibainisha kuwa mbali na kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ambako kwa pamoja jina la mgombea huyo lilikataliwa, katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kulitokea mvutano uliomlazimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo kuwasilisha taarifa za madhambi ya mgombea huyo ambayo ni mauaji ya maalbino, ujambazi na uhusiano mbaya na viongozi wa dini ngazi ya wilaya.
Kanali Simbakalia aliwasilisha madhambi ya mgombea huyo ili kushawishi kikao cha kamati hiyo ya siasa ya mkoa kuondoa jina lake lakini kutokana na maandalizi ya mgombea huyo akidaiwa kutumia fedha, juhudi hizo za Mkuu wa Mkoa ziligonga mwamba, na jina hilo likapitishwa hadi Dodoma, ambako katibu huyo wa CCM Kigoma alijaribu kuendeleza juhudi za Kanali Simbakalia.
Ndani ya kikao cha NEC Dodoma wakati katibu huyo akiwasilisha taarifa hizo, baadhi ya wajumbe wa NEC walimzomea na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kuwataka wamruhusu amalizie kutoa taarifa yake.
Kutokana na hali ya kuzongwa, katibu huyo aliwaeleza wajumbe kuwa hata wana-CCM ngazi ya Wilaya wameahidi kutoshiriki kampeni za mgombea huyo kama atapitishwa na chama.
Baada ya maelezo hayo, kiongozi huyo alisema ni vema aeleze hali halisi ili CCM itakaposhindwa jimboni humo lawama zisielekezwe kwake. Lakini maelezo hayo yalipingwa na kiongozi mwingine wa juu CCM ngazi ya Mkoa ndani ya kikao cha NEC akifikia hatua ya kumshambulia Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, kwamba anamwandama mgombea huyo bila sababu za uhakika.
Simbakalia anatajwa kushambuliwa kutoka katika maelezo ya mjumbe mmoja aliyekuwa akimtetea mgombea huyo akisema kuwa kama kweli Mkuu huyo wa Mkoa anaeleza kuwa mgombea mtarajiwa ni mtuhumiwa ni kwa nini ameshindwa kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
Miongoni mwa hoja za kumshambulia Mkuu huyo wa Mkoa na kumtetea mgombea huyo zinatajwa kutolewa na mfanyabiashara mmoja maarufu mwenye vitega uchumi katika mikoa mbalimbali ikiwamo Kigoma.
Nguvu za mgombea huyo akisaidiwa na wafanyabiashara wakubwa mkoani Kigoma na wengine ambao ni wajumbe wa NEC-CCM na mmoja akiwa ni mjumbe wa Kamati Kuu, zinatajwa kwamba ndizo zilizohakikisha kwamba mfanyabiashara huyo haenguliwi na NEC.
Kutokana na hali hiyo, gazeti hili liliwasiliana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, ambaye alitetea uamuzi wa NEC kumpitisha mgombea huyo akisema ni sahihi kwa kuwa zinazoelekezwa kwake ni tuhuma tu na kwamba mgombea angepoteza sifa kama angekuwa amehukumiwa na Mahakama.
Hata hivyo, wiki iliyopita gazeti hili lilimnukuu Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa, akisema chama hicho hakikuwa na muda wa kutosha kuchambua wagombea wote.
Katika maelezo yake hayo, Msekwa alisema si rufaa zote zitakazoweza kusikilizwa kutokana na wingi wake na muda wa kufanya hivyo kuwa mfupi, akiahidi mchakato huo utaendelea na ikibidi wagombea walioshinda wakiwa na kasoro wanaweza kuenguliwa.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Msekwa inachukuliwa kama utani, kwani kesho Agosti 19, wiki hii ndiyo siku ya mwisho ya vyama vya siasa kuwasilisha majina ya wagombea wateule katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na hakuna dalili kwamba CCM-NEC inaweza kukutana tena kabla ya hapo.
Taarifa kutoka vyombo vya usalama nchini zinabainisha kuwa mgombea huyo mshindi wa kura za maoni CCM na mtuhumiwa wa mauaji ya maalbino naye pia ni mfanyabiashara mwenye uhusiano na mbunge na mfanyabiashara maarufu, ambaye pia ni mjumbe wa vikao vya juu vya CCM.
Raia Mwema iliwasiliana na baadhi ya wakazi wa jimboni anakotarajiwa kuwania ubunge mfanyabiashara huyo wakieleza kushangazwa na uamuzi wa CCM.
"Mimi ni mwana-CCM tumeshangaa huyu mtu amepitishwa kugombea ubunge. Huku alishinda kwa nguvu za fedha, sasa tulidhani katika vikao vya juu atakwamishwa lakini amepita…sidhani kama anastahili kuwa mwakilishi wa wakazi wa Jimbo hili," alisema mkazi mmoja ambaye jina linahifadhiwa kwa sababu maalumu.
Mwananchi huyo ambaye ni kiongozi wa kijiji kimojawapo kwa tiketi ya CCM anasema uteuzi wa mgombea huyo umesononesha hata viongozi wa dini jimboni humo.
Mwananchi mwingine aliyezungumza na Raia Mwema amebainisha kuwa wakati umefika sasa kwa CCM kutokuwa na mbunge katika jimbo hilo akisema, watampigia kura mgombea wa CHADEMA.
Itakumbukwa kuwa baada ya mauaji ya albino kushamiri kwa kasi nchini, Serikali kupitia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, iliratibu upigaji kura ya maoni kuwataja wahusika wa mauaji wa maalbino karibu katika kila mkoa nchini.
Katika kuhakikisha Serikali inapambana na mauaji ya maalbino, Waziri Mkuu Pinda pia aliwahi kutangaza kufuta leseni za waganga wa kienyeji na baadaye kurekebisha uamuzi huo.
Pia Waziri Mkuu aliwahi kutoa kauli yenye kuashiria wauaji wa maalbino nao wauawe lakini baadaye alirekebisha kauli hiyo bungeni.
Mbali na juhudi hizo za Serikali, Oktoba, mwaka 2008 Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Chama cha Maalbino Tanzania na wadau wengine walilazimika kuandaa mkakati wa kupambana dhidi ya mauaji ya maalbino.
Katika mkakati huo, namba maalumu za simu sambamba na tovuti zilianzishwa ili kuwawezesha wananchi kutoa taarifa za moja kwa moja dhidi ya watu wanaohisi wanapanga mipango ya kufanikisha mauaji hayo. Mkakati huo uliitwa Zuia na Pambana na Mtandao wa Mauaji.
Kwa wakati huo, watuhumiwa 53 walikamatwa katika maeneo mbalimbali nchini wakituhumiwa kwa mauaji hayo.
Inasadikika kuwa maalbino wamekuwa wakiuawa kutokana na imani za kishirikina na viungo vyao kuuzwa kwa wafanyabiashara wakubwa wakiamini ni nyezo ya kustawisha biashara zao.
hs3.gif



Source: CCM yapitisha aliyetajwa kuuza viungo vya Albino
 
Waache waendelee kutapatapa kichapo chetu si wamekiona, toka 80% mwaka 2005 hadi 61% mwaka huu, come twenty fifteen watatueleza tu. Na hata kesi ikiamuru uchaguzi urudiwe ndo watatujua!
 
PAKAJIMMY
usipoteze energy kujibizana na watu wasiotaka kuelewa na kuelimika.
tukaze uso wetu kuiangalia safari ya kuwakomboa watanzania.
I hate hawa wanaobeza na kushabikia wizi wa kura za wananchi uliofanywa na ccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom