Ccm kwa sasa wanaendesha nchi kwa maelekezo ya chadema

mm naona ni sawa kabisa maana km chama rasmi cha upinzani hupaswa kuainisha njia mbadala(Plan B).
Kwa hapo wametimiza majukumu yao na chazaidi wanaonekana kuibit kwa mbali sana ile Plan A ya magamba, hivyo WAMETHIBITISHA WANAWEZA
 
Ndugu wana JF na wapenzi wa JF,

Napenda kusema kuwa CHADEMA kimejidhihirisha kuwa ni Chama Makini ambacho kina maamuzi magumu na mazuri kwa ajili ya maslahi ya Taifa letu. Hakika CHADEMA kwa sasa ndicho Chama kinachoendesha nchi hii kikiwa nje ya Ikulu(Remote control). Hii inatuonyesha picha ya kwamba CHADEMA ndicho kilistahili kuwa pale Ikulu (White House)kama isingelikuwa mambo ya uchakachuaji wa Kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010. Nitaeleza.

Kuna mambo matatu makubwa sana ambayo CHADEMA wamesababisha yafanyike ndani ya serikali ya CCM nayo ni haya yafuatayo:

  1. Mchakato wa kuundwa kwa Katiba Mpya. Hii ni HOJA ILIYOANZISHWA NA KUUPIGIWA KELELE NA CHADEMA BUNGENI mpaka serikali ya CCM chini ya Rais wake Kiwete wakaelewa somo na kukubaliana na HOJA hiyo ambayo tayari Tume yake inaanza kazi mwezi wa Mei,2012. Kumbuka CCM hawakuwa na hoja hii kwenye ILANI yao ya Uchaguzi ya 2005/2010. Hoja hii Ilipoanza ilipingwa kwa nguvu sana na Serikali wakiwemo Waziri wa Sheria, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri na Wabunge wa CCM! Kiwete aliweza kusoma alama za nyakati ikabidi amwage manyanga na kukubaliana na HOJA YA KUWA NA KATIBA MPYA! Hii ndiyo KAZI ILIYO BORA KABISA ILIYOFANYWA NA CHADEMA kuwapatia Watanzania kitu chema-Katiba Mpya!
  2. Kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri baada ya HOJA YA CHADEMA kupitia Mbunge wake machachari Mhe.Zitto Kabwe baada ya CAG kuanika UOZA WA UFUJAJI WA MABILIONI NDANI YA SERIKALI YA CCM. Hoja ya KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU iliibuliwa na Zitto Kabwe pasipo matarajio ya Wabunge wa CCM na Serikali yao. Hakika wamekutwa ''OFF GUARD''! Pamoja na juhudi za kutaka kuizima hoja hii kwa mizengwe mbalimbali kupitia Spika Makinda, William Lukuvi,Pinda mwenyewe na majority ya Wabunge wa CCM bado ngoma ikabakia palepale. HII NI KAZI NYINGINE NZURI YA CHADEMA.
  3. Hivi karibuni mwanzoni wa mwaka huu wa 2012, Rais Kiwete kama kawaida yake alifanya ziara ya KUTEMBELEA NCHI ZA NJE HUKU AKINDAMANA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA SERIKALI AMBAPO MSAFARA HUO ULIGHARIMU SH.400 MILLIONI FEDHA YA WALIPA KODI. CHADEMA kwa heshima na taadhima ikaiambia Serikali msafara wa Rais kutumia Shs.400 milioni kwa mara moja ni UFISADI NA FUJAJI WA PESA YA WATANZANIA. Kiwete aliporudi alikuta hoja hiyo ikichemka jikoni na kwa maneno yake mwenyewe akasema KUNA HAJA SASA SERIKALI IANGALIE UPYA ZIARA ZINAZOFANYWA NJE YA NCHI ILI KUPUNGUZA GHARAMA. Naamini hili limeshafanyiwa kazi maana hata juzi Kiwete alivyokimbilia BRAZIL kukwepa joto la kisiasa la kutokuwa na IMANI NA PM msafara wake ulikuwa wa watu wachache sana. HIYO NAYO NI KAZI NZURI YA CHADEMA.

Inavyoelekea huko tuendako hoja na sera za CHADEMA ndizo zitazidi kutamalaki mpaka mwaka 2015 wakti CHADEMA watakapoingia IKULU rasmi.

Naomba kuwasilisha.

makoye2009, Nakuunga mkono ila pia Sema hivi, CCM wanaendesha nchi kisanii kwa kuzuga wanatumia yale cdm itakayo na wananchi. Hakuna kipya hapo. Waondoke nchi hii si yao.
 
c c m ni kama mtoto wa miaka 4 awezi kusimama mpaka asaidiwe CHADEMA MWENDO MDUNDO
 
Hiyo ipo wazi kabisa pamoja na kuwa ni vigumu kukubali wazi wazi. Kumbukeni mkubwa hakosei kwani hata akitoa hewa chafu anasingiziwa mtoto!! CDM JUUUUU
 
CDM ni kama samba la Kibrazil la 1970,s. Haponi mtu hapo!

Chadema hii ninayoifahamu? kama ile huwezi ilinganisha hata na shamba ambalo halitumiki. Chadema ni sawa na shamba ambalo halijaanza hata kufanyiwa usafi kwa maandalizi ya kilimo.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Hoja ya nne, ni Kukwama kwa hoja ya kuongezwa posho za wabunge! Yaani endelezeni list
 
sasa naona umuhimu wa 30000/= zangu nilizochangia kwa njia ya simu kwenye m4c na nitazidi kuunga mkono kila mwezi nitapunguza bajeti ya bia na kuchangia 10000/=
 
Ni kweli CHADEMA wanaonekana kuishauri na kuisisitiza serikali kuwatumikia wananchi....hii inasababishwa na makundi ndani ya CCM coz kuna wanaotaka kuona JK na mtandao wake wameshindwa....makundi haya yanapelekea hata kususia mambo muhimu kwa taifa...yanatoa ushauri negative kwa mambo ya kiuchumi na kiutendaji....but chadema kinawarudisha kwenye mstari.
 
Back
Top Bottom