CCM kushinda urais mwaka 2015, CHADEMA kutawala bunge!

Let us agree to disagree, binafsi ka-siasa nakafahamu kwa mbali na watanzania nawafamu kiasi; uchambuzi wa MTENDAHAKI unaukweli wa asilimia 85 kwa kuzingatia watanzania walivyo. Lengo lake si kuponda CDM kuwa hawawezi kuchukua nchi 2015, bali ni kuonyesha changamoto mbalimbali ambazo CDM lazima wazifanyie kazi na wafanye kazi kubwa ya kuelimisha wananchi.

Tunachokosea ni kufikiri kuwa bibi na babu na mdogo wangu aliyepo kule Mwabuma anayafahamu madhambi ya Magufuli kama mtu mwingine mwenye access na JF, kwa kijijini na hata hapa mjini Dar es Salaam wananchi wa kawaida wanaimani kubwa na Magufuli kuliko kiongozi mwingine yeyote wa CCM kwa sasa hata hao walioambiwa waogelee bado wanamuona kuwa ni kiongozi shujaa anayeweza kusimamia mabadiliko ya nchi hii. Kisaikolojia watu wanaufurahia ubabe wa Magufuli.

Mleta mada, kwa nilivyomwelewa mimi ni kuwa CDM wanatakiwa waunganishe nguvu zao zaidi ili kuwaelimisha wananchi kuwa hata kama atapewa urais Magufuri bado CCM kutokana na kuoza kwake hakuna jipya atakalolileta kwa wananchi kwa kuwa atakuwa ndani ya system iliyooza. Kwa mantiki hiyo nguvu kubwa inatakiwa itumike kuwaelimisha wananchi kuwa ingawa wapo wana-CCM wanaoonekana ni wasafi, lakini system ya CCM ni mbovu hivyo njia pekee ya kujinasua na matatizo tuliyonayo watanzania ni kuipiga chini CCM, na ikiwezekana waadilifu hao wachache wanaweza kuchaguliwa baadae kuongeza nguvu kwenye baraza la mawaziri la CDM pindi CDM itakapokuwa imeingia madarakani.

Tags; Ritz Pasco Makene
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom