EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinafikiria kupendekeza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa uchaguzi ambao mbunge au diwani akifa au kujiuzulu hakutahitajika uchaguzi mdogo. Badala yake katika mfumo huo (proportional representation) unaotumika pia Marekani na Afrika Kusini, chama kilichoshinda katika jimbo husika, kitapewa mamlaka ya kuteua mwanachama wa kurithi nafasi iliyoachwa wazi kwa kutumia orodha ya wanachama wake.
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifafanua utekelezaji wa uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wa Aprili mwaka huu na kufafanua kuwa, mfumo huo utasaidia kupunguza usumbufu na gharama za kurudia uchaguzi. Mbali na mfumo huo, pia kinafikiria kupendekeza kuanzishwa kwa mfumo mwingine wa uteuzi wa wagombea wa vyama ambao Mukama alisema unatumika Ujerumani, ambapo vyama vyote vya siasa vitatakiwa kuteua wagombea wake siku moja.
Alikiri kuwa sababu ya mfumo huo mpya wa uteuzi wa wagombea wa vyama, ni kuzuia tabia ya baadhi ya vyama kusubiri uteuzi wa chama kimoja na kuchukua wagombea wa chama hicho walioachwa. "Huwezi kukaa kusubiri wanaokataliwa na CCM, kwa sasa tunamfumo wa uteuzi sawa na ule wa kupanga magoli (mfumo unaotumiwa na vilabu vya soka kupanga matokeo kumpata mshindi)," alisema Mukama.
Chama hicho pia kwa mujibu wa Mukama, kinafikiria kuwafikisha katika vyombo vya kisheria watu waliokituhumu kuwa kimetumia zaidi ya Sh bilioni 3 katika uchaguzi mdogo wa Igunga. Mukama ambaye alikataa kutaja fedha zilizotumiwa na chama hicho katika uchaguzi huo, alisema taarifa hizo za kutumia fedha nyingi, zililenga kukifitinisha chama hicho kwa wananchi.
HabariLeo | CCM kupendekeza mfumo mpya wa uchaguzi