CCM kumtwisha mzigo Lowassa Arumeru Mashariki

naona una matatizo ya kufikiri ndo maana hunielewi . Kama hujui historia ya wameru nyamaza .

Wacha kashfa na ukabila wewe, wapi we umesoma hiyo historia,Acha kuleta historia zenu za vilabuni hapa.
 
Mkuu ritz Siafikiani na wewe ila ushauri kwa mimi ningependelea abaki kama hidden technical organizer kwanini,
CDM itatumia mapungufu mengi na ya chama cha CCM kwa jina la EL na ndipo CCM itakaposhindwa ilo jimbo na kumbuka watu wa AR sio mbumbu ingawa huyu jamaa ana power kubwa ila nguvu ya umma ni mbaya zaidi hata akitumia dola aitasaidia pale AR panaitaji technical analysis ya ushindi wa mezani sio wa nguvu. mimi nashauri atafutwe kijana mwenye mvuto na kidogo alionekana bungeni ni afadhali kushinda hawa wazee na EL abaki kama Hidden organizer. ni mawazo tuu.

Mkuu Gerlad,

Labda nikuulize ukipewa nafasi hutoe ushauri kwa CCM nani angoze mapambano Arumeru, ungempendekeza nani?
 
Kama Lowassa anajipanga kwa ajili ya uraisi 2015 ni bora akiepuka hicho kikombe cha kubeba msigo wa kuwa Campaign Manager, maaana hali halisi ya lile jimbo inajulikana na ushindani ulivyo mkali, sasa kama CCM wansema anakubalika halafu bahati nzuri wakaibuka na ushindi mwembamba hawaoni kama watakua wameushusha umaarufu wa Lowassa?....
Ushauri: kama amejipanga kugombea uraisi 2015 ni bora aukwepe huo msalaba anaotaka kutwishwa.....
 
Wanabodi,

Chama cha Mapinduzi (CCM) kina mpango wa kumbebesha mzigo mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kwenye mapambano ya kuchukuwa Jimbo la Arumeru Mashariki..

Sababu zinazotolewa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM pamoja uongozi wa CCM Arusha, ni kwamba Lowassa ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Arusha.

Machi 9 mwaka huu kampeni zinaanza na Aprili Mosi upigaji kura utafanyika.

Wananchi kadhaa wa Arumeru, wanaozungumzia uchaguzi huo mdogo wa Arumeru wanasema wazi Lowassa, ndio pekee anayeweza kujibu na kusikilizwa na jamii inayoishi katika jimbo hilo.

Ikielezwa kwamba Slaa, ana ushawishi mkubwa kwa wakazi wa Arusha, ushawishi ambao unaweza kupanguliwa na Lowassa pekee miongoni mwa makada wa chama tawala.

Arumeru kuna makabila makubwa mawili Wameru 66% na Wamasai, ambao wengi wanamkubali sana Lowassa.
W

ameru wataancha kumkubali mmeru mwenzao? hamjui kuwa hata binti yake aliolewa na mtoto wa sumari ambae ni mmeru mwenzake? umasai amejipachika tu!!
 
Mkuu Gerlad,

Labda nikuulize ukipewa nafasi hutoe ushauri kwa CCM nani angoze mapambano Arumeru, ungempendekeza nani?
Unajua kwangu mimi Arumeru ndio Arusha yenyewe wameitenganisha tu ili mradi kuijenga majimbo mengi zaidi. Lakini kama Chadema watamtumia zaidi Lema na Dr.Slaa ktk hotuba na kampeni sioni kabisa CCM wataweza vipi kutoka maana Lowassa pamoja na kumtetea sana Bibie ilikuwa aibu tu kwa chama. Pengine wachukue nguvu waliyoitumia uchaguzi mkuu 2010 lakini tu wakumbuke wakati huo Lema hakuwa na nafasi sasa hivi msema ovyo huyu akipewa Ugali wa EL mbona kuweka mboga itakuwa rahisi..
 
Mkuu Gerlad,

Labda nikuulize ukipewa nafasi hutoe ushauri kwa CCM nani angoze mapambano Arumeru, ungempendekeza nani?

Sendeka, January, Magufuli hata Sita na Simaba Chawena na yule mama simfahamu ila uwa anakaimu uspika pale bungeni anasauti kali kali ivi akitoa michango bungeni na kuna mbunge flani wa nzega ambaye uwa against na ccm mara kwa mara na baadhi wenye mvuto hapa na sema ivi ni wote wanakwenda kuvamia arusha kama CDM akuna mweshimiwa pale ni kukutumikia chama kwanza ueshimiwa baadae na EL anakua anafacilitate ndani kwa ndani asijitokeze itakua bomu kwa ccm ata kama Sita na EL wanatofautiana cha msingi chama kwanza hayo mengine baadae.
 
naomba wamlete.utakuwa wakati muafaka wa kuendeleza ile hadith ya richmond aliyoianza pale kwenye kikao cha nec ya m.a.g.a.m.b.a.anayodai kabla ya kusaini ule mkataba alimpigia simu baba mwanaasha.itakuwa imekaa njema sana
 
Guys hapa kuna kitu tuweni makini kutoa ushauri wa Bure utawafaidisha CCM! Nina shaka hii thread imeletwa ili kupima upepo toka kwa think tanks then wautumie kuamua.
Kumtumia Lowasa katika hili kuna uwezekano ikawa kwa male go mawili.
I) wamtumie ili kupima nguvu yake ikoje hasa wanapoelekea uchaguzi Dec,NA kama akishindwa basi iwe sababu ya kumchinjia baharini.Na ikiwa atashinda then wajue what to do and how given nguvu waliyoiona.
ii)kwa kufilisika ki-strategy wanaweza kuwa wameingiza baridi ya Slaa,NA kudhani kuwa Lowasa atawaokoa! Man a tunasiki Ingunga kilivyonuka wakamwita Rostam!

Ushauri wangu.Zama za Lowasa zimeisha!kuendelea kumfikilia katika uongozi wa Taifa hili mie naona ni mawazo mgando, watumie Majembe ya maana! E.g Magufuli,mtoto wa Makamba,etc
 
Mkuu Gerlad,

Labda nikuulize ukipewa nafasi hutoe ushauri kwa CCM nani angoze mapambano Arumeru, ungempendekeza nani?

ritz hivi agrey mwanri yupo wapi? huyu jamaa ni jembe mno CCM akuna mfano naye mpelekeni Arumeru plse huyu anaweza kubadilisha upepo mzima wa AR cause jamaa ana Data na ashindwi hoja pia kuelezea mchakato mzima wa maendeleo ya arumeru

List
Mwanri agenda maendeleo ya wana Arumeru na bajeti yake kwa ujumla Alamashauri zote
Magufuli Agenda mabarabara kwa ujumla Arumeru
Simbachawena Agenda Bungeni kwa ujumla na majibu ya CDM kwenye mikutano yao
Sendeka huyu ni mzuri wa kupinga au kujenga hoja hata kama ni za kweli na zikawa si za kweli
January agenda kujenga hoja ya posho na kodi za nyumba kwa wapangaji
Kinana agenda kuweka wazee wote Arumeru kukisupport chama
Sita agenda Ufisadi yeye aliruhusu mijadala na bila yeye yasingekuwepo ivi sasa izi atazijibu ikiwa chadema itatumia kama ngao yao
Na vijana wengine wakiwepo pia wakina mama na mabinti wabunge waende kupiga kambi bila kujali nyadhifa zao.

Ila mzee CCM Du watu wenye mvuto wakutafuta namna hii ikiwa mna wabunge 300? kuna kazi ya ziada ya kukisafisha chama wengi waliopo ni matumbo yao chama washakisahau kabisa maoni

Nitakuja tena baada campaign kuisha.
 
tukutane baada ya uchaguzi.
 
Unajua kwangu mimi Arumeru ndio Arusha yenyewe wameitenganisha tu ili mradi kuijenga majimbo mengi zaidi. Lakini kama Chadema watamtumia zaidi Lema na Dr.Slaa ktk hotuba na kampeni sioni kabisa CCM wataweza vipi kutoka maana Lowassa pamoja na kumtetea sana Bibie ilikuwa aibu tu kwa chama. Pengine wachukue nguvu waliyoitumia uchaguzi mkuu 2010 lakini tu wakumbuke wakati huo Lema hakuwa na nafasi sasa hivi msema ovyo huyu akipewa Ugali wa EL mbona kuweka mboga itakuwa rahisi..
Meru ni tofauti na Arusha. Nawashangaa watu wanaofananisha Arusha NA meru.
Wameru ni kama wamachame, na wanasikilizana lugha zao na wamachame ila asili ya makabila hayo ni wamasai walihamia arround 17th century.
Wameru na wachaga huwa hawapatani sana kifikra. Kanisa la kilutheri ndio kama local government ya wameru, na wameru wamekuwa wakitaka kuwa na dayosisi yao tofauti na dayosisi ya kaskazini. Mkuu Lyatonga alishawahi kusuluhisha mgogoro huu na kuna kundi la wameru lilimchukia kwa kurejesha dayosisi kwa wachaga.Enzi hizo alikuwa CCM.

Kuhusu kupeleka wachaga kupiga kampeni, ni bora wampeleke Mkuu Slaa mwenyewe..... huyu wameru watamsikiliza kuliko Mbowe au Mrema AU Lema..... wameru haswa wazee wako very sensitive kwa wachaga kuwatawala, mara nyingi huwaambia waishie hukohuko Arusha mjini..... kwani huko wachaga ndiyo wamejazana kuliko Meru.

Kuhusu Lowasa, ni ukweli kuwa Lowasa atamfunika Cmpaign manager yeyote atakayetokea CDM. Hii haina ubishi, ukibisha hii utakuwa unajidanganya. Ila binafsi simfagilii Lowassa, bora tukose jimbo. Huu uchaguzi utakuwa very close, hakuna atakayeshinda kwa kishindo... sahauni hilo!

Disclaimer: Wazee na wameru asilia ndiyo maoni hayo yana apply kwao, ila vijana wengi na wapo na Joshua Nasari, hili halina ubishi. Kwa hiyo, hii ni kama Igunga.... vijana na wageni versus Wazee na wenyeji asilia.
 
nimekupenda kwa uwelewa wako ndg yangu ila watu hawataki kusikia ukweli. Nakugongea thnx.
 
Lowassa hatwishwi mzigo kutokana na sababu mbili. Kwanza, yeye akiwa Mmeru aliyejifanya Mmasai Arumeru ni kwao. Pili ni kivyele wa marehemu Sumari. Hivyo CCM wanamtuma samaki majini. Sababu ya ziada ni kwamba Lowassa kama fisadi aliyekubuhu ana pesa nyingi ya kuhonga wapiga kura na tume ya uchaguzi ili kuchakachua matokeo. Upo hapo?
 
Kijana akiwaza sawa na wazee basi kijana atakuwa kadumaa kiakili kwani anatakiwa kuwaza zaidi ya wazee.
 
Mara shujaa, mara mwizi, mara gamba, mara mwanasiasa mashuhuri. Yote mnasema nyie. Yetu maskio.
 
mheshimiwa ritz kwa taarifa yako EL ni Mmeru original jina lake halisi ni Edward NDOSSI kama hujui baba yake alihamia Monduli enzi za utawala wa wakoloni (waingereza) baada ya kuhusika na mauaji ya watu katika eneo la Ngarenanyukii.kwa hoja yako EL ni kweli ana influence sana na Wameru kutokana na uhusiano huo.Na pia atatumia karata ya KKKT dhehebu ambalo linaoongoza kwa uwingi wa waumini katika jimbo hilo.
 
Inaelezezwa kwamba uamuzi wa CCM Mkoa wa Arusha, wanachama wa Arumeru na wa Arusha kwa ujmla kumtaka Lowassa, kuongoza jahazi katika kampeni hizo za Arumeru.

Umetokana ukweli kuwa changamoto nyingi ambazo zinahitaji mtu jasiri kama Lowassa, kuzitolea ufafanuzi.

Inasemekana CCM Arusha wanakwenda Arumeru na kauli mbiu moja tu kurejesha jimbo letu. Mambo mengine baadae.

Mpaka hapa naona unatoa habari kama mchambuzi aisyekuwa na moni yake . Nimependa sana analysis yako lakini naomba pia uweke Moni yako binafsi.

Wewe kama Mwana CCM au mtaka mabadilio au mwana CUF au mwananchi asiyeegemea upande wowote kisiasa unasema kuhusu hilo ......
 
Back
Top Bottom