CCM kumtwisha mzigo Lowassa Arumeru Mashariki

Ohoooo anaenda nyumbani kkufanya Kampeni manake nilisikia Lowasa si Mmasai, Lowasa inasemekana kuwa ana asili ya Meru so sitashangaa akirudi nyumbani kwao kufanya kampeni
 
Kama CCM watampeleka Mtuhumiwa namba Moja wa Ufisadi katika Hiyo Kampeni nitajua kweli chama kimefilisika na kilichobaki ni Kanyaga Twende!!
 
Safari ya kumtafuta mbunge wa Arumeru Mashariki inapoongozwa na FISADI aliyekubuhu matokeo yake ni kupatikana mbunge mpya ambaye naye atakua ni FISADI mtarajiwa katika shughuli zake na uwepesi wa kudai posho.

A big political blander at a conception stage!! Vyama vya upinzani, nafasi ndio hiyo basi kaunganishe nguvu zenu kwa mgombea mmoja kama ambavyo James Mbatia alivyowahi kupendekeza huko nyuma.
 
Nakubaliana na hoja yako, HIYO ni sababu tosha Dr. Slaa kachomooa Kugombea Arumeru alijuwa hataweza kupangua makombora ya Lowasa wakati wa kampeni. POLENI CDM huu utakuwa uchaguzi mdogo wa tatu kulalia pua; kumbukeni IGUNGA, UZINI

Jaribu kuwa mkweli kwa Arusha ccm hawaiwezi CDM hata wamfufue nyerere aje kuwapigia kampeni
 
Kama lowasa akiachiwa meru ,hakika ccm itashinda hili halina ubishi hata kidogo ( iwapo tu sioi sumari atakuwa mgombea ) . Wameru siku zote wanaomba kwa Mungu nawao watoe rais wa hii nchi na karata yao ni kwa lowassa . Wanaamini kama sioi atakuwa mbunge na lowassa rais watapata maendeleo kwa haraka jimboni kwao ,hili halina ubishi hata kidogo . Kwa upande wa chadema wanahitaji kazi ya ziada ili waweze kuwashawishi wameru .

NB . LOWASSA NI MKWE WA SIO SUMARY.

Lowasa ataenda na sera gani? Wakati hana mvuto kwa mlala hoi yeyote?
 
Hivi CC ya magamba inakaa lini, si nasikia huyu jamaa (EL) wanamtengenezea tuhuma (zenye ushahidi) ili wamtimue?
 
Inaelezezwa kwamba uamuzi wa CCM Mkoa wa Arusha, wanachama wa Arumeru na wa Arusha kwa ujmla kumtaka Lowassa, kuongoza jahazi katika kampeni hizo za Arumeru.

Umetokana ukweli kuwa changamoto nyingi ambazo zinahitaji mtu jasiri kama Lowassa, kuzitolea ufafanuzi.

Inasemekana CCM Arusha wanakwenda Arumeru na kauli mbiu moja tu kurejesha jimbo letu. Mambo mengine baadae.
 
Lowasa for presdent 2015.

Kaskazini tunaq bahati kweli tulifikiri tutapata vikwazo kumbe uchaguzi wa arumeru umetusafishia njia.

Kambi inayompinga lowasa ndani ya magamba imepigwa bao la kisigino na pia naanza kuwa na imani na tb joshua.
 
Mtamadi sana huyo but hauziki!
Mnalipwa ngapi?

Fisadi ni fisadi hata aweje?
Yeye mwenyewe kwake ilibidi aombe mkuu wa kaya akamnadi
Ameishiwa huyo hana mpya
 
Mkuu Ephata, ongoza jopo kubwa la Machalii Arusha kwenda Arumeru Mashariki kwa kazi moja tu; KUWAKOMBOA WANANCHI HAO kuondokana na kudhalilika kimaisha kule kulikosababishwa na MAFISADI PAPA ndani ya Chama Cha Magamba CCM.

Kimsingi, ni vema wakajulishwa kwamba ugumu wote huo wanaouona leo yooote ni kazi ya MAFISADI yakiwa yamesababishwa na na mapacha watatu , Chenge, Rostam Aziz pamoja na Edward Lowassa wakisaidiwa na baba yao Magogoni kama walivyonukuliwa wakidai katika miezi ya hivi karibuni tu.
 
Arumeru is another republic . Tokea ile laana ya kuwaua wale wamishenari na kuwazika alafu kuwafukua baada ya siku 3 na kuwafanyia tohara hii kitu haitawaacha paka watubu.
 
Jamani mi nipo Arusha kwa sasa na hali inavyoonyesha Chadema inanafasi kubwa sana ya kushinda kiti hiki cha ubunge endapo watamsimamisha Nasary kwa sababu kila ukipita mitaa ya arumeru ni Nasary,Nasary tu.
Na wanachosema ni kwamba huo mtoto wa Sumari hawawezi mchagua sababu hajawai ishi meru huyo huwa anakuja kwenye matukio ya kifamilia siku 2,3 then kageuza Dar.
So itabidi kwanza aanze kujitambulisha kwanza then ndo anze kampeni na wakati huo mda utakua ushaisha.
 
Arumeru is another republic . Tokea ile laana ya kuwaua wale wamishenari na kuwazika alafu kuwafukua baada ya siku 3 na kuwafanyia tohara hii kitu haitawaacha paka watubu.

Ulichokiandika kinauhusiano gani na mada tafakari kidogo kabla hujaandika pumba zako hapa.
 
Ulichokiandika kinauhusiano gani na mada tafakari kidogo kabla hujaandika pumba zako hapa.

naona una matatizo ya kufikiri ndo maana hunielewi . Kama hujui historia ya wameru nyamaza .
 
Inaelezezwa kwamba uamuzi wa CCM Mkoa wa Arusha, wanachama wa Arumeru na wa Arusha kwa ujmla kumtaka Lowassa, kuongoza jahazi katika kampeni hizo za Arumeru.

Umetokana ukweli kuwa changamoto nyingi ambazo zinahitaji mtu jasiri kama Lowassa, kuzitolea ufafanuzi.

Inasemekana CCM Arusha wanakwenda Arumeru na kauli mbiu moja tu kurejesha jimbo letu. Mambo mengine baadae.

Mkuu ritz Siafikiani na wewe ila ushauri kwa mimi ningependelea abaki kama hidden technical organizer kwanini,
CDM itatumia mapungufu mengi na ya chama cha CCM kwa jina la EL na ndipo CCM itakaposhindwa ilo jimbo na kumbuka watu wa AR sio mbumbu ingawa huyu jamaa ana power kubwa ila nguvu ya umma ni mbaya zaidi hata akitumia dola aitasaidia pale AR panaitaji technical analysis ya ushindi wa mezani sio wa nguvu. mimi nashauri atafutwe kijana mwenye mvuto na kidogo alionekana bungeni ni afadhali kushinda hawa wazee na EL abaki kama Hidden organizer. ni mawazo tuu.
 
Back
Top Bottom