CCM kumng’oa Mukama; Wabunge walioipinga bajeti kukiona

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza, mara Mukama, Mara Lowasa, Mara Chenge, Mara JK, mara Mwigulu, Mara Nape etc. Ongezeni list, sasa si waanze tuwaone? mbona wanabwabwaja maneno tuu?
 
Nimekupenda sana profesa, uko deep sana katika kuliokoa ili sikio la kufa ccm lisilosikia dawa,
nakuomba sana prof vijana utuache na chadema yetu, usituaribie kabisa maana kama wametupuuza baada ya kuwaweka madarakani leo ndo waone umehimu wetu?? La asha mbaya zaidi chadema washatutwaa.
Mbaya nyingine tumeshuudia wazazi wetu katika hali mbaya iliyokuwa created na hao ccm wakiangaika ata kuuza mchicha, mandazi n.k kutuudumia tukiwa shule leo tumekua watu sijui kama watatubadilisha
yani inshort prof. Angalia 2015 tutalinda kura zetu vituoni ili baada ya kuizika ccm, tulete sheria za china, venezuela pia irani dhidi ya almost ccm yote kwani policy yao ni kuifisadi hii nchi mpaka ibaki fukara.
Eeh mola kimbiza muda to 2015 mapema tubadili serikali maana hawa ccm wanaakikisha wanakomba mpaka hata hatma ya watoto wa kitanzania walondani ya matumbo ya mama zao

Kashorobana, Makupa na Andrews, Ukiachilia mbali ghadhabu za haya tunayoyashuhudia katika chama tulichokuwa na matumaini nacho na sasa hakiko vizuri, na ukiachilia mbali ushabiki wa kisiasa, na ukizingatia wengi wa wanasiasa wa sasa wameingia kipindi ambacho Chama Kimekuwa na Matatizo na Hakina Ubora ule uliokuwa nao miaka iliyopita, bado CHADEMA na vyama vingine vitakavyokuwa na Nguvu baadae vinapaswa kujifunza kwa mazuri hasa ya mfumo wa CCM wa kuweza kuwafikia wananchi wengi, na kuepuka na kurekebisha yale yanayopelekea madhaifu an mapungufu, mfano kuepuka mfumo unaopeklekea kuwepo kwa upendeleo wa makusudi bila kufuata viwango na sifa za uongozi, ikiwiana kabisa na tabia ya kulindana hata kama mwenzako kaoza kiasi gani kwa kisingizio cha kulinda chama (ambacho ndio chanzo cha kifo cha chama chenyewe). Na CHADEMA iwe tayari kuafikiana na mfumo ambao haujazoeleka, kwa kuwa wengi wa viajana ambao wamekuwa tayari kuingia kwenye siasa tofauti an miaka ya nyuma, wana mawazo mapya na fresh, na hawafanyi mambo yao kwa mazoea, bali kwa kile wanachoamini kinawezekana na wanataka wakiamini kifanyike sasa na si baadae. hivyo basi, speed na acuace katika every political move, one mistake could lead to serious issues with youths.
 
Tatizo ni Mwenyekiti Dhaifu hilo la Kumsingizia Mukama ni Kumuonea tu.. Wawaombe Wapinzani wawasemee kumuanika Mwenyekiti wao na wakiona kama Mwenyekiti wao kaukubali Udhaifu wamuondoe other ways watatimuana wote wakijua wanaweka mambo safi chama na serikali kiendelee kupendwa bila Kujua Tatizo Kubwa ni Mr. Dhaifu
 
MKAKATI wa kumng’oa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, anayedaiwa kushindwa kukiendesha chama umeshika kasi, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Mbali na Mukama, baadhi ya wabunge pia wanataka wenzao waliogoma kuipitisha bajeti ya serikali nao kushughulikiwa kwa kukisaliti chama.

Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa baadhi ya wabunge na wanachama wanataka Mukama aachie ngazi au afukuzwe.


Duru za kisiasa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa matumaini ya wanachama wengi wakiwamo vigogo wa chama hicho waliyokuwa nayo kwa Mukama wakati anaingia madarakani yamefifia.


Katibu mkuu huyo aliyeingia madarakani kwa mbwembwe ndani ya CCM miaka miwili iliyopita, anadaiwa kushindwa kabisa kukijenga chama kama ilivyotarajiwa na badala yake ametengeneza mpasuko mkubwa ndani ya chama.


CCM kwa sasa inakabiliwa na makundi makubwa mawili yenye wafuasi wengi, moja ni lile linaloongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, ambaye amebaki na kundi linalojinadi kama wapinga ufisadi na kundi jingine ni lile linaloongozwa na hasimu wake kisiasa, Edward Lowassa, linalopingana na dhana ya kujivua gamba.


Mukama pia anadaiwa kushindwa kukiimarisha chama na kuruhusu wanachama wengi kukihama chama hicho kwa kile kilichoelezwa kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya CCM.


Kiongozi huyo anabebeshwa lawama kuwa ameshindwa kusimamia dhana ya kujivua gamba wakati yeye ndiye aliyeanzisha hoja hiyo kupitia tume aliyoiongoza kufanya utafiti kubaini sababu za CCM kupata kura chache za urais na kupokwa majimbo mengi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.


“Unajua, Mukama ndiye aliyekuja na matokeo ya utafiti kwenye Kamati Kuu na Halmashauri Kuu. Alibainisha sababu kadhaa za chama kushindwa, lakini sababu kubwa tume yake ilibaini ni pamoja na chama kukosa mvuto kutokana na baadhi ya makada wake, Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz kuhusishwa na ufisadi.

Akaja na mapendekezo kwamba makada hao wavuliwe nyadhifa zao.


“Leo ameshindwa kusimamia kile alichokiamini, badala yake chama kimekuwa kikipiga vita ya maneno tu, mara kutoa siku 90, mara tumeongeza, mara haijulikani. Matokeo yake tumezalisha makundi yanayokitafuna chama,” alisema kada mmoja ambaye ni mjumbe wa NEC.


Kada huyo anasema kuwa baadhi ya makada wanaotuhumiwa kwa ufisadi waliandaliwa barua za kutakiwa kuachia nyadhifa zao lakini hilo lilishindikana kutokana na utendaji mbovu wa Mukama.


Makada wengine wanamlinganisha Katibu Mkuu Mukama na mtangulizi wake, mzee Yusuf Makamba, kwamba licha ya kuwa na elimu ndogo ya darasani, amemzidi Mukama kiutendaji.


Dalili za CCM kumchoka Mukama zimejionyesha hivi karibuni katika moja ya vikao vya wabunge wa CCM ambapo baadhi walifikia hatua ya kusema katibu mkuu wao amechoka kimawazo, bora aachie ngazi sasa.


Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mjini Dodoma zilisema wabunge walikuja juu wakati walipokuwa wakijadili hali ya kisiasa ndani ya chama chao na kuwekeana msimamo wa kuiunga mkono Bajeti ya mwaka 2012/2013.


Mmoja wa viongozi waandamizi wa CCM, aliliambia gazeti hili kuwa katibu mkuu sasa hashirikishwi katika baadhi ya mambo baada ya kubaini kuwa hana uwezo wa kukiimarisha chama.


“Angalia katika mikutano yote inayofanywa na chama kwa sasa hata ule wa Jangwani ulikuwa na watu wengi, Mukama hakuwepo. Ingawa alikuwa nje ya nchi, lakini hata kama angekuwapo, asingepata nafasi ya kuhutubia kwani hana uwezo wa kuongea hadharani.


Kada mwingine wa CCM alimshmabulia Mukama kwa madai kuwa amekuwa akiropoka vitu ambavyo wakati mwingine hana utafiti navyo.


“ Mfano ni wakati wa kumuaga marehemu Bob Makani. Alitoa historia ya ajabu kuhusu waasisi wa CHADEMA, matokeo yake, Freeman Mbowe, alimuumbua pale alipotoa ufafanuzi kupinga kauli yake,” alisema.


Wabunge walioipinga bajeti kukiona

Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa kuna mpango wa kutaka kuwawajibisha baadhi ya wabunge waliokiuka msimamo wa pamoja wa wabunge wa CCM juu ya kuipitisha bajeti.

Bajeti hiyo ya serikali iliyopitishwa Ijumaa wiki hii kwa kura 225 za ndiyo huku kura 72 zikiikataa, kwa kupiga kura za hapana, zaidi ya wabunge 54 hawakuhudhuria mkutano huo.


Kuna taarifa kuwa wabunge waliogoma kuhudhuria kikao hicho bila taarifa na wengine waliokataa kuipitisha bajeti hiyo huenda wakakumbana na mkono wa chama ambacho katika siku za hivi karibuni kimekuwa kikihaha kujinusuru kutoka katika minyukano ya makundi yanayohasimiana.


Inasemekana baadhi ya wabunge wanataka wenzao wajadiliwe na ikiwezekana wawajibishwe ili kujenga nidhamu chamani pamoja na kudumisha uwajibikaji wa pamoja.


Wabunge hao wanatarajiwa kujadiliwa na kikao cha wabunge wa CCM ambacho kinatarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mara baada ya kuwasilishwa kwa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.


Wabunge wanaoonekana kuwasaliti wenzao ni Luhaga Mpina (Kisesa), Deo Filikunjombe (Ludewa) na Kangi Lugola (Mwibara).
Waswahili wanasema penye ulaji hapakosi walaji na mti wenye nyuki wengi ndio penye asali.kinachotokea ndani ya ccm ni sababu za ubinafsi uliokithiri na tamaa ya madaraka zaidi waliyonayo waheshimiwa viongozi walioko CCM.baada ya serekali kuwa na loop holes kwenye usimamizi na kupelekea viongozi wachache waanze kutajirika either kwa njia halali au zisizo halali kumesababisha viongozi wenzao wagutuke usingizini.hii imesababisha kila kiongozi agombania nafasi za juu zaidi ili nae apate ulaji.ndo tatizo linalotokea mfano ndani ya kamati kuu ya ccm.atleast kila mjumbe anaitaka ile nafasi ya mukama.mukama alitoa ripoti ya kumchafua lowassa na wenzake akiwa na malengo ya yeye kufaidika zaidi na sio kuleta solution ya tatizo.hata mwananchi wa kawaida mtanzania ambaye hana uongozi ndani ya ccm anafahamu umaarufu wa mh lowassa,rostam na chenge.kwamba hata kama angefanikiwa kuwaondoa ndani ya ccm anafahamu effects ambazo chama kingezipata hasa wakati huu wapinzani wanapokuwa wanazidi kugain power.ndo angekiua kabisa chama wakati alipewa jukumu la kushauri namna na kukujenga chama.kwasababu ya kutaka madaraka ili afaidi akatoa ushauri ambao alijua wenye nia mbaya kama yake ndani ya cc ya ccm ni wengi hivyo atapata support kubwa.lowassa aliwahi kusema tatizo la yeye kusulubiwa lilikuwa ni madaraka hivyo ikabidi ayaachie kwa wanaopigania.mukama kama yeye alivyopata madaraka kwa kusulubu wenzake na yeye muda wake umefika.kasahau walioko chini wake wote wanataka kuwa alipo yeye.
Suala la ufisadi wanalopigia kelele baadhi ya viongozi walioko ndani ya ccm ni njia tu ya wao kufanikisha mahitaji yao na sio kwasababu ya kuitakia mema ccm au wananchi.wanapiga kelele kuchafua wenzao mafisadi kwasababu waliwazidi ujanja na akili.wanatamani wangekuwa ni wao.sis wananchi tunahitaji serekali itupatie mahitaji muhimu yanayotakiwa ili tuendelee.viongozi ambao wanaitwa sio mafisadi mbona wameshindwa kusaidia wananchi kupata maendeleo?au nao inabidi kwanza waibe ndio watuletee maendeleo?au wanataka kutudanganya kuwa pesa zilizopangwa kusaidia wananchi mafisadi walizikwapua hivyo hawana njia ya kusaidia kuleta maendeleo.?tunaona afadhali hata lowassa wanayemwita fisadi anasaidiasaidia makanisani.
Uchu wao wa madaraka ndio unaosababisha wao kutokutoa ushirikiano na wakubwa zao ili tu washindwe na wao wapate nafasi ya kurithishana.nchi inashindwa kuendesheka manake kila aliyeko chini anatake aliyeko juu ashindwe ili apate sababu ya kujitwalia madaraka.
Tunawaona wanavyojeuza jengo la bunge sehemu zao za mapumziko badala ya kuwa ndio sehemu zao za kutupigania sisi wananchi.wanahongwa pesa kidogo siku za kupitishwa kwa bajeti wakiingia ndani ni Kura za ndio tu.huwa hata hawajui kilichoandikwa kwenye hizo hotuba manake wamelala.then wanaamka wakati wa kupiga kura.wanauza nchi na wananchi wake milioni 40 kwa tamaa zao.
Yote yana mwisho wake na tuombe Mungu sana atupe viongozi wazuri manake kutokana na umaskini wetu sisi wananchi uliokithiri umekuwa unatufanya tukubali kuuza kura zetu kwa kuhongwa.Be blessed!
 
Back
Top Bottom