CCM kumeguka ni muhimu kwa Taifa!

Unataka kusema sijawahi kutoa mawazo ya kuwa solution za kuleta maendeleo Tanzania au kuboresha mfumo wa siasa?
Naomba nikukumbushe kwanza kwa kukuomba usome Marshal Plan ya Mchungaji na hasa kipengele cha Uongozi
'Marshall Plan' - Restoration and Recovery Plan for Tanzania

Kisha soma Dynamic Productivity Dynamic Productivity; Tija na Maarifa

Endelea na Why Vita vya Ufisadi will not win election Why "Vita vya Ufisadi" failed and will never win election..

KUna Money Matters Money Matters: Maendeleo, Ubunifu, Maadili na Kujitegemea

Pia kuna nyingine tatu za Focus 2010, Chadema must reform na Azimio Jipya, sizioni tena naona mods wamechanganya hoja hivyo sijapata linki zake.

Exactly ndio ninachosema nilitegemea uweke solutions maana ninaamini kwamba unao huo uwezo, sasa shukrani kwa link zako lakini ungeziwakilisha kwenye hii mada ya Mwanakijiji, ningeelewa.

NInachojaribu kuonyesha hapa ni kuwa nimekuwa nikimpigia kelele Kikwete na kumtupia lawama kwa ukali, lakini hata kama ni Amiri Jeshi MKuu, yeye si pekee katika uongozi na CCM ilipaswa kuwa makini kumuongoza hata Mkapa, Mwinyi na Nyerere. Katika hizo thread nilizokuonyesha hapo juu, solution zake si kwa ajili ya CCM, bali ni kwa ajili ya Taifa zima. Solution kwa CCM kujisafisha ni kwa watu kuacha kuoneana haya na woga na wafanye kweli ama wafukuze au wajiondoe.

- Hapa ndio yale yale, hakuna solution ila lawama tupu kwa wengine wa CCM, mkuu huko kwenye tumefikaje hapa tulipo Mwanakijiji ameshapitia kabla ya kutoa hii mada, tumetokea kwa Mwalimu, sasa anatafuta solution, kama uliwahi kuzitoa huko nyuma ilikuwa kwenye mijadala mingine lakini sio huu, lawama sio solution kwa sababu matatizo yako sio ya mwingine.

- CCM wajisafishe wasijisafishe, sio tatizo letu wananchi hapa kwenye hii mada tatizo letu ni solution kutoka kwenye shimo tulilomo tayari, kuwalaumu viongozi watano au sita wa CCM hakutatui tatizo, kwa sababu CCM they are not doing it, so what tusubiri mpaka watakapoamua kufanya kama unavyosema itakua ni lini hiyo?

I mean kama ni ukali kila mtu hapa anaweza kuutoa, lakini where is a solution kwa sisi wananchi na taifa lililoko shimoni??
 
Exactly ndio ninachosema nilitegemea uweke solutions maana ninaamini kwamba unao huo uwezo, sasa shukrani kwa link zako lakini ungeziwakilisha kwenye hii mada ya Mwanakijiji, ningeelewa.



- Hapa ndio yale yale, hakuna solution ila lawama tupu kwa wengine wa CCM, mkuu huko kwenye tumefikaje hapa tulipo Mwanakijiji ameshapitia kabla ya kutoa hii mada, tumetokea kwa Mwalimu, sasa anatafuta solution, kama uliwahi kuzitoa huko nyuma ilikuwa kwenye mijadala mingine lakini sio huu, lawama sio solution kwa sababu matatizo yako sio ya mwingine.

- CCM wajisafishe wasijisafishe, sio tatizo letu wananchi hapa kwenye hii mada tatizo letu ni solution kutoka kwenye shimo tulilomo tayari, kuwalaumu viongozi watano au sita wa CCM hakutatui tatizo, kwa sababu CCM they are not doing it, so what tusubiri mpaka watakapoamua kufanya kama unavyosema itakua ni lini hiyo?

I mean kama ni ukali kila mtu hapa anaweza kuutoa, lakini where is a solution kwa sisi wananchi na taifa lililoko shimoni??

FMES,

Bila kuonyesha ubovu wa CCM, kamwe Watanzania walio wengi hawataweza kuoanisha na kuelewa kiini cha matatizo yao.

Unakumbuka mapokezi waliopewa kina Chenge na Lowassa? ambayo yaliandaliwa na Chama? Je mapambio mengine mengiya kukisifu chama huku kinashindwa kufanya kazi zake kwa umakini kwa nini basi tusiwapashe habari Watanzania wajue udhaifu wa Chama walichokiamini ili waweze kuamka kama unavyotaka waamke na kuwajibika?

Wananchi wengi wameridhika na CCM, wameridhika kutokana na mazoea na hisia kuwa kila kitu ni heri ndani ya CCM.

Lakini ukweli ni kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kazi. Leo Chiligati anasema CCM isihusishwe na wizi wa pesa za EPA. Hilo ni sawa, kwa kuwa tunaweza tusipate ushahidi kamili wa kunufaika kwa CCM kutokana na wizi huo wa EPA, Meremeta, Kagoda, IPTL, Richmond, Rada na tuhuma nyingine nyingi za Uhujumu na Ufisadi. Lakini swali linabakia, ni nani alikuwa na majukumu na mamlaka ya kuongoza nchi na kudhibiti rasilimali na uchumi? Jibu ni Serikali ya CCM..

Hivyo kukwepa kuwajibika kwa kuwa eti hatujawakamata CCM kama Paulo Usijekuchza na sisi, si tija wala halina nguvu. Madhali uhujumu huu ulifanyika kwa zaidi ya miaka 6, ni wazi basi kuwa CCM na Serikali yake havina uwezo wa kuongoza na kulinda rasilimali za nchi, mbaya zaidi, haina uwezo wa kudhibiti, kukagua na kuhakiki shughuli za uzalishaji mali na biashara.

Sasa kwa hili, kwa nini tusiinyoshee CCM vidole na kuilamu ili wale ambao wameishi wakiridhika na kufikiri CCM ni safi waone udhaifu wa CCM na hivyo kujirekebisha na kuanza kudai uwajibikaji?

Solution yangu kwa hili swali ni hivi: Wale wanaojiita ni CCM Mageuzi wajitoe ndani ya hiki chama, maana kimeoza na ni kazi kusafishika. KIbaya zaidi ni hizi njama ambazo tumekuwa tukizisikia kwa zaidi ya miezi 10 ya kuwashikisha adabu wale CCM mageuzi kwa kuhakikisha hawapati nafasi za uongozi wala uwakilishi 2010. Kwa mtaji huo, viapo vya hawa CCM mageuzi bado ni matatani maana kama wao wanajivutavuta kuwaondoa wale wachache, basi wao ndio watakaoondolewa.

Solution ni moja, get rid of CCM!
 
FMES,

Bila kuonyesha ubovu wa CCM, kamwe Watanzania walio wengi hawataweza kuoanisha na kuelewa kiini cha matatizo yao. Unakumbuka mapokezi waliopewa kina Chenge na Lowassa? ambayo yaliandaliwa na Chama? Je mapambio mengine mengiya kukisifu chama huku kinashindwa kufanya kazi zake kwa umakini kwa nini basi tusiwapashe habari Watanzania wajue udhaifu wa Chama walichokiamini ili waweze kuamka kama unavyotaka waamke na kuwajibika? Wananchi wengi wameridhika na CCM, wameridhika kutokana na mazoea na hisia kuwa kila kitu ni heri ndani ya CCM.

- Kama umemsoma vizuri Mkandara, anasema kwamba wananchi hawajui wa kumuamini between upinzani na CCM, maana wote wwamefurahia kumalizwa kwa Azimio La Arusha, sio kweli kwamba wananchi hawajui kwamba CCM ina matatizo, tatizo ni wa kumuamini?

Lakini ukweli ni kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kazi. Leo Chiligati anasema CCM isihusishwe na wizi wa pesa za EPA. Hilo ni sawa, kwa kuwa tunaweza tusipate ushahidi kamili wa kunufaika kwa CCM kutokana na wizi huo wa EPA, Meremeta, Kagoda, IPTL, Richmond, Rada na tuhuma nyingine nyingi za Uhujumu na Ufisadi. Lakini swali linabakia, ni nani alikuwa na majukumu na mamlaka ya kuongoza nchi na kudhibiti rasilimali na uchumi? Jibu ni Serikali ya CCM..

- Haya yamefanywa na Mkapa na Mtandao wake, sio siri na wananchi wanajua fika, sasa ukiwaambia wananchi hadithi tofauti ndipo wanaamua kuwapigia CCM anyways, hela za EPA hazikuchukuliwa na CCM yote, hapana!

Hivyo kukwepa kuwajibika kwa kuwa eti hatujawakamata CCM kama Paulo Usijekuchza na sisi, si tija wala halina nguvu. Madhali uhujumu huu ulifanyika kwa zaidi ya miaka 6, ni wazi basi kuwa CCM na Serikali yake havina uwezo wa kuongoza na kulinda rasilimali za nchi, mbaya zaidi, haina uwezo wa kudhibiti, kukagua na kuhakiki shughuli za uzalishaji mali na biashara.
Sasa kwa hili, kwa nini tusiinyoshee CCM vidole na kuilamu ili wale ambao wameishi wakiridhika na kufikiri CCM ni safi waone udhaifu wa CCM na hivyo kujirekebisha na kuanza kudai uwajibikaji?

Solution yangu kwa hili swali ni hivi: Wale wanaojiita ni CCM Mageuzi wajitoe ndani ya hiki chama, maana kimeoza na ni kazi kusafishika. KIbaya zaidi ni hizi njama ambazo tumekuwa tukizisikia kwa zaidi ya miezi 10 ya kuwashikisha adabu wale CCM mageuzi kwa kuhakikisha hawapati nafasi za uongozi wala uwakilishi 2010. Kwa mtaji huo, viapo vya hawa CCM mageuzi bado ni matatani maana kama wao wanajivutavuta kuwaondoa wale wachache, basi wao ndio watakaoondolewa.

Solution ni moja, get rid of CCM!
__________________

- How do you get rid of CCM ndio hoja ya Mwanakijiji hapa, ni kwa kumeguka kwa CCM au what??

- Binafsi nina heshima sana na wanamageuzi wote kwanza kwa kazi kubwa waliyokwisha ifanya, na mazingara magumu waliyofanyia kazi zao, kuna ambao leo wanaishi kwa matatizo makubwa sana wakiwindwa na mafisadi, watalipwa na Mungu tu lakini sio sisi wananchi.
 
FMES,

Naona tunacheza Sega Dance kama si Segere Matata!

Kama Mkapa na kakundi kake ka mafisadi ndio wanaokichafulia jina Chama, kwa nini inakuwa ni vigumu kuwatoa?

Je Mkapa na kundi lake ndio wanaoshikilia bajeti na mipango ya maendeleo ya Taifa?
 
FMES,

Naona tunacheza Sega Dance kama si Segere Matata!
Kama Mkapa na kakundi kake ka mafisadi ndio wanaokichafulia jina Chama, kwa nini inakuwa ni vigumu kuwatoa?

- Wanatolewa na nani? Mkapa ambaye Mwalimu baba wa taifa mwenye nguvu za kulaani na kubariki, alisema ni malaika na ndiye aliyekwua mwenye CCM, sasa Mkapa anatolewa na nani huko CCM?

Je Mkapa na kundi lake ndio wanaoshikilia bajeti na mipango ya maendeleo ya Taifa?[/QUOTE]

- Najua kuwa ndio waliochukua hela za EPA, na ndio wenye nguvu ndani ya serikali yetu leo, si nimeona mahali humu kwamba Lowassa was the best, au si wote wamoja hao, au?
 
- Wanatolewa na nani? Mkapa ambaye Mwalimu baba wa taifa mwenye nguvu za kulaani na kubariki, alisema ni malaika na ndiye aliyekwua mwenye CCM, sasa Mkapa anatolewa na nani huko CCM?

- Najua kuwa ndio waliochukua hela za EPA, na ndio wenye nguvu ndani ya serikali yetu leo, si nimeona mahali humu kwamba Lowassa was the best, au si wote wamoja hao, au?

Then tunarudi kwenye ile hoja yangu kuwa CCM haiwezi kujisafisha na hata CCM mageuzi hawawezi kukigeuza chama ila nji amoja, wajitoe CCM.

Kama Mkapa na wafuasi wake wanaogopewa eti mteule wa Nyerere au visingizio vingine huku inajulikana wazi kuwa alishindwa kazi na anaongoa genge la wahujumu, basi wale wote wanaobakia kudai CCM ni mama yao au wao ni CCM mpaka kufa wana walakini na hivyo kamwe tusitegemee CCM ituletee mabadiliko au kuruhusu kufanyika mabadiliko yeyote kwa kuwa ndani ya chama kuna udhaifu mkubwa!
 
....CCM ni chama weak sana na wala kisiwatishe na kitatoka tuu soon or later,nakumbuka mrema alivyowapelekesha CCM uchaguzi mdogo wa Ubunge Temeke na hata juzi Tarime CCM wameonyesha jinsi walivyo weak,dawa ni kupata wajanja wanaojua issue na kupiga mdomo kama Obama then utaona CCM ilivyo maharage ya mbeya,hakuna kitu pale ni vitisho tuu na status quo na hakuna haja ya kuwalaumu wananchi wanaoipigia kura CCM maana ni swala la muda tuu,dawa ni kupata wataalam wachache tuu upande wa upinzani utaona jinsi wanachi watakavyo wageuzia kibao...wizi wa kura au utemi ni no match to charismatic leader
 
Rev.Kishoka,
Bob Mkandara,
Mtu anapojirudi na kujisahihisha na kuanza kufuata njia iliyo bora na njema, ni rahisi sana kukubalika. Hata Mchungaji, Padiri au mhubiri kama amefanya makosa na waumini tukayaona, naye akaja ungama kwetu na kwa nadhiri ya kweli akajisahihisha na kutenda yale yaliyomema, atapokelewa na kupewa nafasi ya mara ya pili.
Inapokuwa Mchungaji huyu, anafumbia macho maovu ya watu wake au yake mwenyewe na kukataa katu katu kuwa mnyenyekevu na kujisahihisha hata kuomba toba si kwa Mungu pekee bali hata kwa waumini na wafuasi wake, basi ni ama Mchungaji huyu aondolewe madarakani kwa kufukuzwa, au kupigiwa kura ya kutokuwa imani au hatari kubwa zaidi kama Mchungaji huyu ana mizizi ambayo haikatiki, ni waumini kumuachia hilo kanisa lake mwenyewe.
Sasa CCM kama ni Kanisa au Msikiti, lina viongozi, wawe Wachungaji, Mashekhe, Wainjilisti, Wahubiri, Mapadiri,Imamu au Masharifu. Wanaposhindwa kuliongoza Kanisa au Msikiti, inawapasa waachie ngazi ili wengine wenye uwezo na wenye kuaminiwana waumini, waongoze chombo hiki.
Lakini kama CCM, tuna makanisa na misikiti ambayo viongozi wake wamekwaza roho za waumini kwa madhambi ya ajabu ajabu, iwe ni wizi, uzembe, uzinzi, uasherati, ulawiti, dhuluma, unafiki, fitina au kukosa mwamko wa kiroho kuongoza makanisa na misikiti hii na hivyo kurutubisha imani za waumini wa masikiti na misikiti hii.
Mkuu wangu ni rahisi kusema lakini imani ya mtu ktk dini haitokani na mchungaji hata kidogo.. Mchungaji anaweza kukukuta wewe tayari umekwisha kuwa na imani ya dini hiyo kutokana na mafundisho ya Kitabu - Yaani Biblia ama Msahafu, kwani Mungu ni neno na neno hilo ndilo lililoandikwa ktk kitabu sio Mchungaji wala Sheikh..ndio maana siku zote hata kwenye ubishi wa dini huwa sipendi mtu aanapotumia mapungufu ya kiongozi fulani wa dini kuwachamba waumini wote...On this mkuu nipo na FMES..

Na uhakika wa maneno yangu in reality, mkuu unajua kabisa kuwa wachungaji wetu hao Masheikh na Mapadre ndio vibaka hawana hata aibu kila siku hukamatwa wakifanya mabaya tena wakiwa ktk mataji yao, lakini umeona mtu hata mmoja akiacha dini yake kwa sababu ya mchungaji ama Sheikh huyo!..nambie kweli wewe unaweza kuondoka dhehebu lako kwa sababu ya matendo mabovu ya Rev mwenzako ambaye amekana kuyatenda!
Hata ukihama msikiti ama kanisa bado utakuwa muumini wa dini hiyo kwa maana kuwa unaweza kuhama toka tawi fulani la CCM nakuhamia jingine lakini kuondoka kabisa CCM ina maana huna tena imani na msahafu wa chama CCM...Hawa ndugu zetu kina FMES tunawaweka kona kwa maswala ambayo hata sisi tungekuwa ktk hali hiyo hiyo..Kama tunashindwa wananchi millioni 40 wenye imani tofauti kuwaondoa hawa wachafu iweje iwe rahisi kwa wanachama millioni sijui 4 au 5 wenye imani sawa na viongozi wao!

Mag3,
Mkuu labda unachukulia swala la Chama kibongo bongo lakini mkuu wangu nchi za nje Ufuasi wa mrengo wa chama ni sawa kabisa na dini. Watu wanaondoka chama kwa sababu mafundisho yake yamechukua mkondo tofauti na imani zao lakini kamwe huwezi kumkuta Republican kaondoka chama hicho kwa sababu McCain kashindwa ama kiongozi fulani kibaka..
Bongo na nchi zote maskini zilizovamia mfumo wa vyama vingi naweza kuamini kuwa Mbowe akiondoka Chadema basi ataondoka na wafuasi kibao kama alivyofanya Mrema. Pia nimeona baadhi ya Wachungaji wakiondoka dhehebu fulani na kuanzisha lao wameweza kuvuta wafuasi lakini bado ni waumini wa dini ile ile..Mara nyingi kama sio zote madhehebu yametokana na tafsiri tofauti za mafundisho ya kitabu hicho lakini sio matendo ya viongozi wa dini..

Sasa tunapoomba CCM wameguke labda watumie hoja kama ile ya Kikwete kukebehi Ujamaa na Kujitegemea wakati ni mwongozo na imani kubwa ya chama chake!..Watokee hao CCM Asilia wamwambie afanye kiapo upya maanake kuukejeli Ujamaa na Kujitegemea wakati ndio njia pekee inayokubalika na chama chake kuweza kuleta mafanikio ya jamii ya Watanzania ni kukiuka kanuni muhimu ya chama..
Nje ya hapo kwa kuangalia matendo ama maneno yao viongozi ambayo hayapo ktk kitabu, kina FMES siku zote watashindwa kutuelewa..swali kubwa watakuuliza nionyeshe ni wapi ktk Katiba (mwongozo) ama ilani ya chama imesema Ufisadi ni halali na haki ya mtu..
 
Jamani naomba tuwe realistic kidogo na tuache blah blah ambazo haziwezi kutufikisha popote. Ukweli ni kuwa hivi sasa tunayo serikali ya kiimla inayoendeshwa kwa mtindo wa udikteta wa chama. Chini ya mfumo kama huu ukweli ni kuwa mabadiliko hayawezekani bila "blessing" ya hicho chama labda yatokee mapinduzi. Mapinduzi yanawezekana tu wananchi kwa wingi wao wanapoikataa serikali na kuichukia - na wataichukia tu watakapoweza kung'amua uozo ulio ndani yake.

Kwa bahati mbaya serikali ya aina hiyo hufanya mengi kwa kificho na mambo muhimu ya taifa huamuliwa kwenye vikao vya siri vya chama ambavyo hushirikisha tu wateule wake na kuwaacha kwenye mataa wananchi walio wengi. Matokeo yake inakuwa vigumu mwananchi wa kawaida kujua yanayojiri mpaka wahanga kama Mh. Dr. Slaa atokee na kuwapasha. Katiba inakuwa silaha ya kujilinda ili kubaki madarakani badala ya kuwalinda wananchi. CCM kuridhia mabadiliko itakuwa ni kama kujizika na kwa namna ninavyowajua hii kwa sasa ni ndoto kama ya Alnacha.

Inapofikia hali hii kuna njia moja tu ya amani ya kuwafanya wananchi waijie juu chama kinachoendesha serikali hiyo nayo ni kuishitaki kwa wananchi. Wengi tunabezwa kwa kupiga tu kelele na kulalama lakini tumekwishashuhudia jinsi hizo kelele zinavyoweza kumnyima mwenye nyumba usingizi. Hizi blah blah za kutafuta lawama kwa awamu zilizopita, kuwalaumu wasadizi na si mhusika ama kusema ni kakundi kadogo tu ndizo zinawapa vichwa wa "act with impunity". Ubovu wa CCM na ulafi wa viongozi wake lazima utangazwe wakati wote wananchi ambao hawajasikia wasikie.

Hiyo ndio njia murua ya kuimomonyoa CCM pole pole - hakuna anayelala milele labda mfu. Kuna watakaotukatisha tamaa kwenye hili lakini mangapi tumefanikiwa na hizi kelele zetu humu ndani ya JF. Mojawapo ya mafanikio ninayojivunia ni kuona wakazi wa kijijini kwetu walivyoitikia kelele zangu na huko CCM haipati kitu ng'o - subirini 2010. Na msafi gani angeishi ndani ya huo uvundo na atoke bila doa - haiwezekani. Mimi mag3, nitaitwa majina na nitabezwa lakini sitaacha kukilaani hiki chama cha mafisadi kilichoifikisha Tanzania, nchi ya asali na maziwa, hapa ilipo.
 
Jamani naomba tuwe realistic kidogo na tuache blah blah ambazo haziwezi kutufikisha popote. Ukweli ni kuwa hivi sasa tunayo serikali ya kiimla inayoendeshwa kwa mtindo wa udikteta wa chama.

Udikteta wa CCM haukuanza leo, wote tunajua ulipoanzia na kwamba hawa wa sasa wanaiga tu!

Anyways, I am out now!
 
Mag3,
Jamani naomba tuwe realistic kidogo na tuache blah blah ambazo haziwezi kutufikisha popote. Ukweli ni kuwa hivi sasa tunayo serikali ya kiimla inayoendeshwa kwa mtindo wa udikteta wa chama. Chini ya mfumo kama huu ukweli ni kuwa mabadiliko hayawezekani bila "blessing" ya hicho chama labda yatokee mapinduzi. Mapinduzi yanawezekana tu wananchi kwa wingi wao wanapoikataa serikali na kuichukia - na wataichukia tu watakapoweza kung'amua uozo ulio ndani yake.
Mkuu nakubaliana na wewe 100% na ndio sababu tupo hapa JF.. Hata FMES amekuwa mstari wa mbele kuelezea mabaya ya viongozi walioshika na watakaoshika madaraka..Tatizo kubwa la Tanzania ni Viongozi wabovu...
Kuwaumbua viongozi wabaya ndani ya chama chake ni kazi kubwa inatakiwa moyo na FMES kila siku amekuwa nasi sote kutupa dataz..
Kazi kubwa imebakia kwetu sisi wananchi kutumia kila njia kuhakikisha viongozi hao hawapati nafasi ya kuongoza..
 
Mbowe na kampeni zake bwana

sasa mkiiondoa hiyo CCM ndio mnataka ipewe CHADEMA na huyo MBOWE mabye kshindwa kurun lile danguro pale mjini ndio ataweza kurun nchi wa watu milioni 40?

hAO cuf NA SEFU NDIO MSISEME KABISAAA
 
FMES, Mkandara, Mag3, Mwanakijiji na wachangiaji wengine,

Nawaeleweni vizuri sana, ila kinachonitatiza ni kule kujivutavuta, kusubiri mtondogoo tuanze kufanya kazi.

Waswahili walisema cheleachelea utakuta mtoto si wako, sisi nasi tumeridhika na kasi hii ya konokono kama si kinyonga, ya kuburuza miguu badala ya kuchangamka na kuwa wepesi wa maamuzi.

Leo hii, tunaanza kuwaonea huruma na kudai tuwape nafasi au eti ndivyo tulivyo. Kama ni hivyo na ndivyo tunavyofikiri na kufanya mambo, tutegemee lini kupata mabadiliko?

Rwanda ambayo miaka 14 iliyopita walipigana mapanga na sasa hivi wataanza kutupita kwa maendeleo ya uchumi na demokrasia.

Ni lini tutaacha kutambaa na kuanza kukimbia?
 
FMES nitajie jina la pili ninalotumia hapa JF ni lipi? uje kule uliposhadadia, usikimbie.
 
FMES, Mkandara, Mag3, Mwanakijiji na wachangiaji wengine,

Nawaeleweni vizuri sana, ila kinachonitatiza ni kule kujivutavuta, kusubiri mtondogoo tuanze kufanya kazi. Waswahili walisema cheleachelea utakuta mtoto si wako, sisi nasi tumeridhika na kasi hii ya konokono kama si kinyonga, ya kuburuza miguu badala ya kuchangamka na kuwa wepesi wa maamuzi.
Leo hii, tunaanza kuwaonea huruma na kudai tuwape nafasi au eti ndivyo tulivyo. Kama ni hivyo na ndivyo tunavyofikiri na kufanya mambo, tutegemee lini kupata mabadiliko?

Mkuu Rev,

- Kama kawaida nitajiongelea mwenyewe, I have seen a lot, ile habari ya muasisi wa Upinzani niliyoisema juzi ukasema unamjua, bado mpaka leo haijanitoka kichwani, unajua mzee aliteseka sana Hospitali, hakuna kiongozI wa upinzani hata mmoja aliyejitokeza, hakuna chama hata kimoja cha Upinzani kilichojitokeza, hakuna mwananchi hata mmoja wa Tanzania aliyejitokeza, infact hata madakitari waliamua kumuacha tu ajifie.

- Nilipopewa habari nikaamua ku-get involved na kwenda kuwaomba msaada wakulu wa CCM na serikali, ambao walini-direct niende kwa aliyekua waziri mdogo wa Afya then Mama Ntimizi, finally msaada ukatokea tena mzito sana, ninamshukuru yule mama mpaka kesho, na viongozi wengi wa CCM na serikali yake wakaanza kujitokeza kwenda kumuona Hospitali Muhimbili, aliweza kuishi kwa muda wa mwezi mmoja zaidi ambao ninamshukuru Mungu kila siku kwamba I was able to help na kuona mzee wa watu akitangulia kwenye haki kwa amani, na guess what? Siku ya mazishi, viongozi wote wa Upinzani in full walikuwa kwenye safu ya mbele, walianza na Mrema akitoa maneno ya kishujaa na siasa nyingi za kuponda CCM, wenzake wote mmoja baada ya mwingine wakaja na maneno yale yale, Chadema ilikuwa under Bob Makani naye ninamungalia kwa macho mawili nikiwa pembeni mbali akitoa maneno mengi ya kashfa kwa CCM, sasa hebu tuwe wakweli mjane na watoto wa yule marehemu leo unaweza kuwaambia nini kuhusu CCM na upinzani bongo?

- Ni kweli tunataka mabadiliko, lakini mazingara bado sio sawa kwa sababu hatuko kwenye ukurasa mmoja na wananchi walio wengi na tena ni kwa sababu nyingi na mbali mbali ambazo kwetu zinaweza kua ni ndogo, lakini kwa wahusika zinaweza kua ni kubwa sana na hata kukatisha tamaa kabisa, na this ni kwa pande zote mbili yaani CCM mpaka Upinzani.

- On my part ninajitahidi kila siku ya Mungu kufanya yale ninayoweza na kwa kasi ninayoiweza, niwe mkweli simuamini anybody on this hata awe ndugu yangu maana nimeona ya kutosha, ninawaheshimu sana kina Mwakyembe, Mama K, Seleli, Sendeka, Mama M, Mkulu S, Kubenea, Zitto, Ndesamburo, na Dr. Slaaa,

- Wengi wa hawa wakulu ukiongea nao uso kwa uso, huwa wanasema kwamba kazi wanayoifanya matokeo yake hayawezi kuwa enjoyed na kizazi hiki yaani chetu, ila wanaweka msingi kwa ajili ya kizazi kijacho ninbakubaliana na this kwa 100%. Hivi karibuni nilimshuhudia kiongozi mmoja fisadi, akimuomba mmoja wa hawa viongozi wapiganaji, amsaidie kwenye kampeni ya uchaguzi wake kwa maneno yake yule fisadi, alisema "...Unajua nyinyi wenzetu mna heshima sana na wananchi...na mnakubalika sio kama sisi wenzenu!..." toka siku ile huwa sina wasi wasi tena na kazi nzito inayofanyika, ingawa sio kwa mwendo unaokubalika hapa JF.

Mkuu Rev, tuendelee kumpigia paka kengele siku tutakapoweza kuaminiana basi tutajumuika wote kwa pamoja, kutafuta the right tools na strategies ili ziweze kutusaidia zaidi kusonga mbele kwenye hivi vita vya kutafuta mabadiliko kwa ajili ya taifa letu, taifa ni letu sio la mtu mwingine ni letu sisi wananchi. Na respect kwa michango yako yote humu na kwa wote waliochangia hii thread ni darasa zito sana kwa sisi wananchi.

Ahsante Mkuu
 
Quote: GT

yaani hiki ni kchekesho sana yaani unabadili jina kisha unajipongeza mwenyewe!
ama kweli ukistaajabu ya Musa utashangaa ya Fir'aun

Quote: ???????

FMES nitajie jina la pili ninalotumia hapa JF ni lipi? uje kule uliposhadadia, usikimbie.

Haya mfungie na GT sasa tuone ubabe wako, bwa! ha! ha! ha! ha! halafu nifungie na mimi pia!

mkuu GT hebu shika simu niko hewani, this is lovely!
 
Haya mfungie na GT sasa tuone ubabe wako, bwa! ha! ha! ha! ha! halafu nifungie na mimi pia!

mkuu GT hebu shika simu niko hewani, this is lovely!

ha ha ha ha, mwanaume utakufa na kijiba, nakwambia kwa mara ingine, kama wewe unatumia majina mengi hapa sio wote. Tena unikome kabisa kunifatafata mwanaume una gubu kama nini. Unataka uonekane wewe tu, una laana nini wewe?
 
Duh! yamekuwa hayo tena!...yangu mato (macho).

Narudi kwenye mada...
Wakuu zangu tuko msitari mmoja na kama alivyosema Mag3, kuna njia mbili tu za kuiona pepo..
Moja ni hiyo ya CCM kusambaratika, jambo ambalo FMES amesema ni ndoto na haliwezekani.. binafsi namuunga mkono kwa kuzingatia maneno ya Rev. Kishoka kuwa kusubiri CCM isambraratike ni dalili za wananchi waliokosa kabisa matumaini na bila shaka ni mwendo wa kusuasua..
Njia ya Pili ni hiyo ya Wananchi kuweza kuchukua hatamu wenyewe jambo ambalo sio lazima iwe mapinduzi ya kumwaga damu isipokuwa mapinduzi ya Kifikra..
Mapinduzi ambayo tumeyaona Mbeya na Tarime, sasa chukulieni kuwa inawezekana Tanzania nzima...
 
Chimbuko la umasikini wetu wa kutisha ni utawala mbaya. Kwa mfano, ni utawala mbaya ndio umefanya tuingie mikataba ya dhahabu yetu kuchukuliwa wakati sisi tukiambulia 3% royalty peke yake. Linganisha hilo na utawala mzuri wa Botswana ambao umehakikisha taifa lao lina hisa ya 50% kwenye kampuni ya uchimbaji almasi kwao.

Chimbuko la utawala mbaya Tanzania ni CCM kuhodhi madaraka. Ni kuhodhi madaraka ndiko kunaifanya serikali ya CCM ilikatalie Bunge kujadili mikataba mikubwa ya kiuchumi inayoingiwa na taifa. Ni kulewa madaraka ndiko kunafanya CCm ipuuze kipengele cha katiba kinachosema Bunge litajadili na kuidhinisha mikataba mikubwa inayoingiwa na serikali.

Matokeo ya utawala mbaya ni pamoja wizi wa fedha za wananchi. Ulipogundulika wizi wa fedha za EPA, wananchi walitaka akaunti zote BoT zichunguzwe. Ukishajua wizi umefanyika ndani ya chumba kimoja utaachaje kuchunguza vyumba vyote? Ni kulewa madaraka ndiko kuliifanya CCM ipuuze wito huo.

Matokeo ya wizi wa fedha za wananchi ni kudorora kwa miradi ya maendeleo. Miradi mingi sana ya maji imekufa kutokana na kukosa fedha. Hili linawaongezea mno umasikini wananchi wetu. Ni sehemu ndogo sana ya Watanzania wanapata maji safi na ya kutosha. Tanzania imekuwa sasa ya mwisho Afrika karibu kwa kila kigezo. Ghana kuna umeme kila kijiji. Rawlings alifikisha umeme kila kona ya nchi. Serikali ya CCM haiwezi kufanya hivyo kwani fedha hamna. Zinaibiwa na viongozi wa CCm na washirika wao.

Kwa vile serikali ya CCM inapuuza katiba basi haisaidii kupata katiba mpya. Itapuuzwa tu vile vile.

The conditio sine qua non for development in Tanzania is the removal of CCM from power. Kuna waoga wanaosema CCM ikisambaratika na taifa litasamabaratika. Si kweli. Mbona KANU na UNIP viliondolewa madarakani na nchi za Kenya na Zambia zikazidi kuimarika?

Naudhika nikisikia mtu anasema "CCM haiwezekani". Kwa nini isiwezekane? Kuna waliosema vile vile KANU haiwezekani, na leo inabidi waone aibu. CCM inawezekana sana, tena imeshaonekana ni uchafu tu mbele ya wananchi wengi.

Tanzania ina tatizo moja kubwa sana, nalo linaitwa CCM
 
Back
Top Bottom