Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Mkuu Kitila,
Heshima mbele, maneno yako mengi ni ya kishujaa sana, kuna mzee mmoja aliyekwua CCM aliyafuata maneno yako exactly, akajiunga na waasisi wa upinzani na kuanzisha upinzani, akiwa CCM alikuwa vyeo vingi vya bure hasa kwenye bodi ili kumpa kula, alipotoka tu CCM wakamnyofoa vyote, na kubaki tupu!
Ambacho hakujua ni kwamba wenziwe wote aliojiunga nao, either walikuwa wameshachota kule CCM na kuwa na miradi binafsi mikubwa kwa hiyo hawakuwa na wasi wasi na mlo, au wengine walikuwa ni mapandikizi wa CCM tu, masikini mzee wa watu akaishia kua lofa hoe hae huku wenziwe wakipeta tu, siku moja mdogo wake ambaye naye alikuwa na vyeo huko CCM, naye akawa frustrated kidogo na Diria, akaamua kutoka na kuingia upinzani,
Ninakumbuka huyu mzee, yaani kaka mtu akimlilia sana mdogo wake asifanye, makosa kama yake ya kurukia upinzani na abaki huko huko CCM, maana wakati bado, alsema nilifikiri wakati ulikuwa umefika, lakini sikuwa-read vizuri wananchi wa Tanzania kwamba bado hawako tayari kwa mabadiliko.
Ninamkumbuka sana huyu mzee, ambaye sasa ni marehemu, maneno yako Kitila ni ya kishujaa sana, lakini sio kwa mazingara ya bongo, sawa kama unavyosema kwamba ni vyema kuwa-recruit wapya kwa ajili ya the future, ni idea ambayo hapa JF kwenye quick fix kama za Europe na USA, haikubaliki kwa hiyo ni kaaazi kweli kweli!
Mzee FMES,
Kwanza naomba usichukulie binafsi kutumia maneno yako kujenga hoja zangu kuwa ni vita baridi, maana hapa watu hawachelewi kuanzisha zogo!
nikirudi kwenye jibu lako kwa Kitila, kinachonitatiza kutokana na kauli yako ambayo ndiyo hali halisi ya mfumo wetu wa Siasa na Uongozi ni ile dhana ya kusema mtu anakuwa mwanasiasa au kiongozi ile "ale" au ajipatie!
Je kujituma na kutumikia Taifa kuna nafasi gani tena? Jee kulitumikia Taifa kwa moyo kwa kuwa mtu ni mzalendo na mwaminifu wa nchi yake kunageuzwaje kuwa mradi wa kujipatia mali?
Nafahamu fika wewe ni mmoja wa wale wanaolipinga Azimio la Arusha, ingawa sijawahi kuelewa kwa maoni yako ni kwa nini unalipinga Azimio la Arusha. Lakini nitakuambia hivi, kwenye Azimio la Arusha ambalo lilivunjwa kwa kuundwa kwa Azimio la Zanzibar, ndiko kulikoandikwa miiko ya uongozi kuzuia watu kukimbilia uongozi kuwa ni sehemu ya kujipatia kipato ama kwa kutumia nafasi zao za kazi au kujipangia manufaa ya binafsi na si ya Taifa.
Huyo mzee unayemzungumzia, namfahamu, nami nilishawahi kumpa saluti yangu kwa kuwa jasiri na kwenda Upinzani.
Tatizo la uoga na unafiki wa WanaCCM wengi ambao ni viongozi, wabunge na wawakilishi ni kuwa wamekimbilia kazi zao si kulitumikia Taifa, bali ni kujipatia kipato na kushughulikia maslahi binafsi!
Hili ndilo tatizo kuu na ndio maana wengi wao wanaingia kwenye mtego wa kuogopa kuihama CCM au kufa masikini kwa kuwa wameshajenga nadharia kuwa ni lazima wawe na mali nyingi au uhakika wa mali na mapato ili waweze kulitumikia Taifa.
Badala ya Viongozi na WanaCCM kufanya kazi na kulitumikia Taifa na kuacha mapato au kipato kiwe matokeo ya kazi zao, wao wameweka maslahi na kipato mstari wa mbele kuwa ni muhimi kabla ya kufanya kazi yeyote.
Ndio maana niliposema CCM ni adui wa Maendeleo ya Tanzania na Watanzania ni kutokana na hii sasabu nyingine iliyozaa utamaduni wa watu kukimbilia siasa kama tegemeo pekee la kujipatia MAISHA BORA.
Ugonjwa na Utamaduni huu umeliharibu Taifa letu. Kama Mwanakijiji alivyoeleza, Watanzania tumeshazoea kuishi KIFISADI na KIHUJUMU na hivyo vita dhidi ya Ufisadi na Uhujumu inakuwa ngumu kwa kuwa tumefanya mazoea ya kuishi kwa kutegemea mapato ya ziada na ya ujanja ujanja na si kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Narudia tena nilichomwambia Pasco na wewe kuwa ni mpaka pale baadhi ya Viongozi waasisi na walioko madarakani wa CCM watakapoachana na woga na kuukumbatia Utamaduni huu mbovu wa unyonge wa mali kuwa ndio kigezo cha kuogopa kuondoka CCM na kufanya kilicho sahihi, Tanzania kamwe haitaweza kuendelea au kupata mafanikio inayoyataka.
Utamaduni huu pamoja na kuwa unawaathiri Watanzania wengi hata wale walioko katika vyama vya upinzani, lakini kama tunataka uharamia huu uishe mara moja na si kutumia miaka 100 kubadilika, atakayeweza kulibadili hili na kufuatwa kwa urahisi kabisa ni CCM!
Ndiyo maana nimekuwa mkali kwa wanaojiita CCM mageuzi kwa kuwa wanaukumbuatia mfumo mbovu kulitumikia Taifa!