CCM kumeguka ni muhimu kwa Taifa!

ZITTO HAJAPOTEZA WALA HAJAKOSA SIFA KUWA RAIS WA TZ!
Kwanza nakubaliana nanyi kuwa Tanzania kama Taifa tuna uhaba wa viongozi. Sababu kubwa ni hofu. Kwamba kuna baadhi ya watu waliostahili kuwa viongozi lakini kwasababu ya hofa na udhaifu wa kufikiria katika mstari mmoja wa CCM imewawia vigumu kujua kama wanaweza kuwa viongozi ktk nafasi ya Urais nje ya CCM.. Ndio maana binafsi naamini kwamba kwa kadiri tunavyokwenda, tunaweza kutoka nje ya kufikiria CCM, na kuona wanao onesha uwezo nje ya CCM. Nikweli kwamba baada ya Ushindi wa Obama zimeibuka hisia kwa kiwango cha juu kuhusu uwezekano mkubwa wa kijana au vijana wachache wenye dhamira na uwezo kuelekea dhamira zao kuweza kuliokoa Taifa hili. Ni bahati mbaya au nzuri kwamba kwa sehemu kubwa kadiri ninavyokumbana na hisia hizo, Jina Zitto limepata kuwa na nafasi kubwa.

Wanaompinga Zitto wamekuwa wanasukumwa na sababu kubwa mbili, kwanza ni umri wake usiokidhi matakwa ya kikatiba, lakini pia wamekuwa wakihoji sana uzoefu wa Zitto katika kusimamia masuala tete ya Kitaifa. Kwamba pengine utatuzi wa matatizo makubwa ya kitaifa yanahitaji uzoefu mkubwa kuliko alionao Zitto. Nionavyo mimi kwa mazingira ya kisiasa tulionayo, Zitto au mtu aina ya Zitto anaweza kuwa Rais bora kuliko Kikwete na walio wengi kama sio wote ndani ya CCM kwasababu zifuatazo;

1. Kusema Zitto hana umri unao ruhusiwa kikatiba ni sawa na kusema Watanzania wapo kwa ajili ya Katiba badala ya Katiba kuwepo kwa ajili ya Watanzania. Na mpaka sasa sioni mantiki yoyote ya msingi kwanini umri wa mgombea urais kuwa miaka 40 na sio miaka 35 au hata 30. Labda wengine watachangia uzoefu wa nchi zingine duniani ktk hili. Lakini hii bado ni changamoto kwa vijana na wazee watanzania kuendelea kutafakari kama kuna uhusiano kati ya uwezo wa mtu kuwa Rais na Umri wa miaka 40.
2. Kwamba Zitto hakuonesha umakini kukubali uteuzi wa Rais kwenye Kamati ya Bomani, na hivyo hafai kuwa Rais ni sawa nakumuonea bure kijana huyu. Labda ili tutoe hukumu halali katika hili tujiulize, Hivi ushiriki wa Zitto kwenye Kamati ya Bomani umeleta hasara na faida gani? na Je, kama asingeshiriki Taifa lingepata hasara au faida gani?. Nadhani huu ndio msingi wa kupima usahihi na ama udhaifu wa uamuzi wa Zitto. Labda changamoto inayoweza kuendelea kujadiliwa ni kama baada ya Zitto kushiriki ktk kamati hiyo anafanya nini zaidi kuhakikisha alichokitaka kinatokea kweli.

3. Ni kweli kwamba Zitto hana uzoefu kama alinao Kikwete, Lakini faida ya uzoefu ni nini?. Maana kimsingi uzoefu unamsaidia kiongozi kujua masuala mengi kwa kina na hivyo kujmweka kwenye nafasi ya kufanya maamuzi kwa haraka na kwa usahihi mara kwa mara kama sio wakati wote. Lakini ukimtazama Kikwete na walio wengi ndani ya CCM hawana uzoefu kwasababu hiyo. Zitto ni kijana anayebadilika kwa kasi katika jinsi anavyoyatazama mambo. Nikikumbuka siku ya mjadala wa buzwagi bungeni alivyokuwa anawadhibiti wabunge wa CCM kwa hoja na vielelezo kutoka kwenye mabuku mbalimbali aliyokuwa amerundika mezani kwake, ilitosha kujua kuwa kijana huyu ana uwezo mkubwa wa kupambambanua mambo...Lakini tusishau kuwa Zitto amewahi kuwa kwenye timu inayomshauri Rais wa Ujerumani kuhusu masuala ya uchumi, na Sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma, kazi ambayo hapana shaka ufanisi wake sio wakuhojika sana kama ingebidi tuzingatie umri na uzoefu wake...Na hivi karibuni tumeambiwa amechaguliwa kwenye timu ya wabunge wanaoshughulikia migogoro ya kisiasa duniani...Nakiri kwamba kama Zitto akigombea urais hii inaweza kuwa hoja, lakini bado kuna mengi ya kutafakari kuhusu nafasi ya urais mbele zaidi ya uzoefu...Kama wamarekani walivyomtazama Obama mbele zaidi ya Uzoefu wa Mac Cain, ndivyo ilivyo kwa Zitto. Kumshindaniosha Zitto na Kikwete ktk eneo la Uzoefu ni kama ambavyo mtu angemshindanisha Obama na Mac Cain katika eneo moja la uzoefu na kufanya uamuzi.

4. Lakini zaidi ya hapo, Zitto anawakilisha tabaka la wasomi vijana wazalendo, aliyeamua kufanya kazi ya kujenga upinzani tangu awali, na hakuna rekodi tofauti ktk uamuzi huo. viongozi wa namna hii hawana mizigo kama walionayo CCM ya kutoka awamu moja kwenda nyingine. Ndio maana siamini kama kiongozi mbadala anaweza kutoka ndani ya CCM. Ndani ya CCM ni visasi na malumbano ya nani ni nani katka awamu gani? basi. Nachokubali ni kwamba CCM ikipasuka itarahisisha upinzani kushinda na kujenga uongozi mbadala, lakini upinzani usije kurogwa kusumbili viongozi wa kuongoza Taifa hili kwa maana ya urais kutoka ndani ya CCM. Litakuwa kosa kubwa kutokea. Na historia itawahukumu vibaya. tunahitaji damu isiyofungamana na mizigo ya hisia chafu, fitina za awamu hadi awamu, wala mizigo ya ufisadi kutoka awamu moja hadi nyingine.

5.Kikubwa ninachokiona kwa Zitto ni kuwa mtu mwenye dhamira isiyohijika kirahisi, kijana mwenye moyo wa simba anapopambana, mwenye kutazama siasa juu ya vyama, aliyepata bahati ya kukubalika na hivyo fursa ya kushawishi mabadiliko(hii ni bidhaa adimu sana na muhimu sana), asiyehofu kufanya maamuzi magumu ambayo yanaweza yasiupendeze Umma au jamii inayomzunguka ktk wakati fulani(Unpopular decision) lakina anayasimamia, na wakati huohuo kuwa tayari kubadili maamuzi yake anapobaini hayakuwa kwenye misingi sahihi.
6. Ni kweli kwamba akiwa mwanadamu, na katika umri wa ujana anaweza kuwa na mapungufu kadhaa wa kadhaa..Lakini muhimu tutafakari Taifa letu linataka nini kwasasa? na hivyo ni kiongozi wa aina gani anahitajika kwa majukumu hayo, kisha tuwapime viongozi tulionao katka hayo...Lakini kitu kimoja muhimu ni kwamba kwa vigezo vyovyote anuai vinavyoweza kuwekwa, ni jambo dhahiri kwamba Zitto atamshinda Kikwete kwa mbali kabisa....Labda CCM ilete mtu mwingine ashindanishwe na Zitto, Siyo Jakaya Jamani!..... Huyu Kikwete?...Tuendelee kujadili.
NDIYO, TUNAWEZA!
 
From Mwanakijiji
"Zitto hawezi, umri haumruhusu na linapokuja suala la uongozi wa nchi sidhani kama anastahili kuwa Rais kwa wakati huu. As a matter of fact watu wafuatao (nitachambua siku moja) hawastahili kuwa viongozi wa nchi yetu kwa kadiri wataendelea kuwa walivyo sasa: Mbowe, Lipumba, Mrema, Seif, Prof. Safari, Mtikila, na Mbatia. Ubunge yes, Urais NO."

Kwa hiyo uchaguzi wa uraisi mwaka 2010, kura yako itaenda kwa Kikwete? (Ceteris paribas within CCM)
 
Hapa hakutakuwa na jipya kwani ikiwa Roman Empire ilianguka. Sidhani kama sisiemu ni kubwa kuliko Roman Empire au hata USA kiuchumi itaanguka kabisa na world super power itakuwa China, India etc. USA itasujudu chumi za nchi hizi.

Sasa well being ya kuishi na walionyanyuka itakuwa-determined and dependent on how you lived with them. If you gave them shit they will give you shit plus. And you know what pain is more to the one who lost good thing than one who just got it from not having it. I do not know whether one gets a good picture. Its a speculation but we are sure of, and it the most certain thing to sisiemu. They are late to act for their bad acts.

SISIEMU bye bye! Who is next!!!!
 
Mwanakijiji,
Mkuu binafsi maswali yako mengi yanazidi kupanua wigo la maswali mengine ya kufikirika, kutafuta hisia za watu nje ya sisi kuwatazama viongozi wapinzania ama vyama vya Upinzani vimeshindwa wapi kuwavutia wananchi..
Trust me, mkuu wananchi hawahitaji makubwa zaidi ya kutambua hali zao za kimaisha na kuwapa ahadi za kweli zinazoweza kubadilisha maisha yao..

Kwa mfano, tunajiuliza iweje wananachi waichague CCM (Kikwete) kwa asilimia 80 ikiwa kweli wananchi wameichoka CCM?..
Swali zuri sana, na kama nilivyosema huko nyuma ni kwamba ktk uchaguzi uliopita vyama vingi vya Upinzani walishindwa kutumia hoja zinazowahusu wananchi kila siku...Na kusema kweli sikumbuki slogan yoyote ambayo ilitumika kuwahamasisha wananchi ktk Mageuzi ya Utawala..
By the time Mkapa anaondoka nina hakika Popularity yake ilishuka chini kama huyo mzee Bush..
Kikwete ambaye kisiasa alikwisha andaliwa kama Mpinzani wa Mkapa, zikatumika historia za Uchaguzi toka mwaka 1995 kuonyesha kwamba Kikwete as a Maverick ndiye pekee anaweza kuleta Mageuzi ya Utawala mbovu wa Mkapa uliotangulia...
Wote kina Mbowe, Lipumba na sijui Mrema walishindwa kumshambulia Kikwete direct, kumhusisha na Ufisadi uliotangulia chini yake badala yake wakaweka nguvu zao kuzungumzia sera za chama CCM ambazo Kikwete aliweza kwa urahisi sana kuzi defend ikiwa ni pamoja na ahadi za Uongo..

Mkuu tujiulize ni Watanzania wangapi kwa ujumla wa hesabu yao wanataka mabadiliko ya Katiba?.. ni wangapi wanajua hata hiyo katiba kama ndio mwongozo wa Taifa! -
Pili tujiulize tena ni wananchi wangapi wanajua tofauti ya sera za chama kimoja kwenda kingine? na wangapi kati yao wanajali hata hizo sera kuwa ndio mkombozi wa maisha yao ikiwa Kiutawala pekee wameshindwa kuona viongozi bora!.

Jibu lake fupi sana, kuwa ni less than 20% na pengine 10 ya wapiga kura!..Sababu kubwa ikiwa Umaskini wa Akili na Mali (Elimu na pato la mwananchi)..
Na ndio maana kila siku wananchi wanategemea sana kutokea kwa nabii, na mchango wa viongozi wa dini zetu kuwapitisha manabii huchukua nafasi kubwa ya imani ya wananchi ambao kwao siasa ni Utamaduni mpya. Bado kabisa Tanzania pamoja na kwamba watu wengi wamesoma sasa hivi elimu dunia lakini imani ya dini na Uchawi bado imeshika nafasi kubwa ktk asilimia kubwa ya wananchi..Kwani tumekosa mwanga kupitia siasa zetu, kilichobakia ni kumwomba Mungu ama shetani..Ideology zote za Kisiasa na Kiuchimi zimekuwa zililenga maswala mazito ya Katiba na sera za chama badala ya kutazama maswala muhimu yanayowagusa wananchi kila siku...

Matukio mengi yanayoendelea nchini yanaonyesha wazi kuwa WATU na MAZINGIRA tuliyokuwa nayo hayawezi kufanana na nchi za Ulaya hata kidogo... bado watu wanaamini Ulozi na kinga pekee ya Ulozi (Fitna, chuki, majungu na voodoo) ni kusali sana na kumwomba Mungu!..hivyo kufanikiwa kwa mtu ama Taifa letu kutategemea zaidi BAHATI ama MAJALIWA yanayotokana na Mungu ama Uchawi..Na mkuu wangu Tanzania watu wanasali.. yaani kama nguvu ya wananchi ktk ibada za sala na makombe zingekuwa ktk utendaji kazi basi leo hii tungekuwa na Mafanikio japo kidogo..Na kibaya zaidi Mungu ndio kwanza anatuharakisha zaidi kwa sababu ibada zetu zinazotokana na Umaskini, Ushirikina (kumshikirisha)...

Hapa ndipo tulipo simama wakuu zangu wala tusitake kujidanganya kuijadili sana Katiba ikiwa ndani ya Katiba hiyo hakuna kitu wananchi wanaelewa...Nitarudia kusema wakati wa Mkoloni, Katiba ya Mkoloni kimaandishi haikuwa sababu ya sisi kutafuta UHURU wetu isipokuwa adha za kila siku ya maisha ya wananchi ndizo zilikuwa Politics pamoja na kwamba zimetokana na mwongozo (Katiba) ya Mkoloni...
Kifupi tu ni kwamba madai ya Uhuru wetu yali focus moja kwa moja ktk vitu ambavyo viliwafunga wananchi na kuwanyima Uhuru (Freedom), kitu ambacho wanaweza kujiona wao ktk kioo cha fikra zao kuwa hawapo huru..
Lakini nikirudi kuitazama hali halisi ya sasa hivi kiutawala, Itakuwa makosa makubwa na pengine kurudia yale yale ya mwaka 2005 kutumia mapungufu ya Katiba na ibara zake kuwahubiri wananchi ambao they careless about Katiba..Hata Zimbabwe kwenye matatizo mengi ya Kiutawala Morgan hakutumia zaidi siasa na sera za chama ZANU kutafuta Ushindi isipokuwa hali halisi ya Uchumi na hatua mbovu zilizochukuliwa Udhoofu wa kiongozi aliyepo madarakani na kadhalika, wakati ukitazama sisi Tanzania ndio kwanza kila Kiongozi wa Upinzani alikubali uchaguzi wa Kikwete..

Wakuu, mapungufu ya Katiba hayawezi kabisa kuwa kiamsho cha wananchi, na kama Field Marshall ES alivyosema Mabadiliko yoyote ya Kiutawala yatatoka kwa wananchi wenyewe ambao watalilia Mabadiliko hayo kutokana na hali halisi.. Na kwa hili nawapongeza sana Chadema walipokuja na kitu OPERATION SANGARA...Ni mvuto ambao unawagusa wananchi wote nchini bila kuitazama Katiba wala sera ya chama CCM na kama kuna uwezekano wa CCM kumeguka ni kutokana na Maazimio kama haya.. Maazimio ambayo yanawagusa wananchi wote kwa Ujumla iwe mijini ama Vijijini..
 
As a matter of fact watu wafuatao (nitachambua siku moja) hawastahili kuwa viongozi wa nchi yetu kwa kadiri wataendelea kuwa walivyo sasa: Mbowe, Lipumba, Mrema, Seif, Prof. Safari, Mtikila, na Mbatia. Ubunge yes, Urais NO.

.

Mzee Hapa noamba tutofautiane.Nasubiri uchambuzi wako
 
From Mwanakijiji
"Zitto hawezi, umri haumruhusu na linapokuja suala la uongozi wa nchi sidhani kama anastahili kuwa Rais kwa wakati huu. As a matter of fact watu wafuatao (nitachambua siku moja) hawastahili kuwa viongozi wa nchi yetu kwa kadiri wataendelea kuwa walivyo sasa: Mbowe, Lipumba, Mrema, Seif, Prof. Safari, Mtikila, na Mbatia. Ubunge yes, Urais NO."

Kwa hiyo uchaguzi wa uraisi mwaka 2010, kura yako itaenda kwa Kikwete? (Ceteris paribas within CCM)


oh..no naomba muangalie vizuri kauli yangu niliyoandika. Mara nyingi watu hawasomi hasa nimeandika nini wanainfer kitu ambacho sijaandika: Sijasema viongozi hawa "hawawezi" kuwa viongozi wa nchi yetu wala Zitto sijasema "hawezi". Jamani nachagua maneno yangu vizuri. Ndio maana nimesema nitachambua wakati wake ukifika hapa ilikuwa ni kidokezo tu. Pia nimeweka "qualifications" kubwa mbili kwenye hiyo kauli yangu.

Siwezi kumpigia kura Kikwete hata nifungiwe jiwe la kusagia shingoni, kwa kadiri ya kwamba anaendelea jinsi alivyo sasa na rekodi yake ikiwa ndiyo hii.
 
Mwanakijiji,
Mkuu binafsi maswali yako mengi yanazidi kupanua wigo la maswali mengine ya kufikirika, kutafuta hisia za watu nje ya sisi kuwatazama viongozi wapinzania ama vyama vya Upinzani vimeshindwa wapi kuwavutia wananchi..
Trust me, mkuu wananchi hawahitaji makubwa zaidi ya kutambua hali zao za kimaisha na kuwapa ahadi za kweli zinazoweza kubadilisha maisha yao..

Mkuu kwanza nakubaliana na wewe kwani nadhani tunakubaliana sana kwenye jambo moja ambalo sijakubaliana na Mzee mwenzangu FMES; kwamba kudai katiba peke yake siyo kichocheo cha mabadiliko tuyatakayo. Kuelezea haja ya Katiba mpya siyo sababu ya kuiondoa CCM kwani CCM wakija na madai hayo wao wenyewe kuwa wanataka Katiba mpya wananchi watabakia kudai nini?

NInapenda hicho ulichokisema mbele ambacho ulikianza vizuri nadhani ukakipinda kidogo mbeleni ulipotumia mfano wa Zimbabwe. Alichofanya Mugabe siyo tu kuongoza wananchi kuikataa serikali ya Mugabe bali kuikataa ZANU-PF. Hivyo haikuwa kumkataa Mugabe kama mtu au serkali kama serikali tu bali aliweza kuwaonesha kitu wananchi (hapa ndipo umepatia kama Pele) kuwa matatizo yao yanahusiana moja kwa moja na Uongozi uliopo.

Kwamba hali yao mbaya ya kiuchumi haikutoka kwa Shetani bali imetokana na uongozi na sera za chama kilichopo. Mpango wa kunyang'anya watu ardhi, kudidimiza upinzani n.k ilikuwa ni sera ya ZANU-PF.

Kwa Tanzania hata hivyo hilo litakuwa gumu kweli kwa sababu kubwa mbili:

a. Watanzania wengi wananufaika na ufisadi uliopo. Watanzania wengi tumeshazoea kuishi katika utamaduni wa kifisadi kiasi kwamba kujaribu kuiondoa CCM ni sawa na kujaribu kukata mkono unaotulisha. Leo hii watumishi, wananchi wa kawaida wanaishi maisha ya kiujanja ujanja kiasi kwamba kuwarudisha kwenye mstari itakuwa ni kama kile tulichokiimba miaka hili "mabepari walia kukatiwa mirija". Leo hii tunapozungumzia mafisadi mara nyingi tunazungumzia walioiba mabilioni; lakini wale wanaotumia nafasi zao kila siku kujinufaisha kinyume cha sheria kwa muda wa kazi, fedha za umma au vyombo mbalimbali vya umma wana sababu gani ya kutaka CCM iondoke?

Watumishi wengi wameshajua kuwa ukitaka kufanikiwa ingia serikali na ukiingia huko watu watakuonesha jinsi ya kutumia mianya iliyopo na hata kusababisha matobo ili ufanikiwe. Leo hii ziara za Rais zinatumiwa kama kisima cha kumwibia Mtanzania halafu tuwaambie hawa wasomi kuwa ukija uongozi mpya wataachishwa wizi huo kweli watatuunga mkono?
 
Mwanakijiji,

Mkuu tupo ukurasa mmoja..
nilipozungumzia Morgan na Zimbabwe nimeutumia mfano huo kwa ufupi sana..Kumbuka Morgan hakutumia sana slogans za kisiasa maanake unapozungumzia sera, katiba na kadhalika ndipo unapokigusa chama. Lakini kama utazungumzia Matatizo yaliyopo kisha ukawaeleza wananchi matatizo haya yanatokana na nini na nani basi moja kwa moja hukumu yao inaashiria chama lakini mind You ujumbe unahusu (Nini na Nani) issue iliyopo na mtu fulani.. in this case Uchumi na Mugabe. Kwa hiyo hata kama Mugabe angekuwa chama tofauti bado adha za wananchi Kiuchumi bado ingeendelea kutokana na msimamo wake...

Hii ndio Tofauti iliyopo ktk siasa za nchi yetu na upofu huo wa kuelezea mapungufu ya kiongozi yameweza kujenga hoja kwamba pengine wapo viongozi ndani ya CCM wenye uwezo mzuri kuliko Kikwete..na focus ya wananchi imelenga zaidi kumtafuta nabii toka CCM kwa sababu hadi leo hii hakuna kiongozi nje anayezungumzia matatizo ya wananchi wenyewe moja kwa moja na kuyatafutia dawa. Kumbuka Mrema mwaka 1995 aliweza vipi kupata kura za wananchi?.. CUF mwaka 2000 wote hawa wali attack the real issue zinazowahusu wananchi..
Hivyo mostly wananchi wanataka kusikia wewe kama kiongozi utafanya nini tofauti kwao na sio kuwapa takwimu za GDP kama ndio scale to measure socio -economic status wakati elimu, afya, na huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na miundombinu (vitu ktk maisha yao ya kila siku) vinazidi kuporomoka..Hayo maendeleo yanayozungumziwa ni ya takwimu ambazo zinaonyesha hali yetu kuwa nzuri wakati wananchi wanazidi kusaga lami..

Mkuu watu wanaofaidika na siasa za CCM sasa hivi ni wachache sana. Hii imani ya kwamba watu wengi wanafaidika na siasa hizi ni dhana potofu. Dalili zote za uchumi unaokufa zinajionyesha.. Kupanda kwa maisha, interest rate, kupungua kwa ajira ni ishara tosha kabisa kuwa melikebu yetu ya uhcumi imeanza kuchukua maji mengi..Kiutaalam siku zote meli inapotaka kuzama deck yake hupanda juu kuliko kawaida wakati nyuma ikizama taratibu (kumbukia sinema ya Titanic) na ukiweza kupima scale utafikiria kwamba meli inapaa..
Mkuu hawa wote wanaofaidika na hali hii ni wale waliokimbilia deck wakdhania kwamba watapona ama kuwa wa mwisho kufa maji..Ni sawa kabisa na viongozi wa Zimbabwe ama wafuasi wa ZANU walivyofikira wakati wakichukua mali za Wazungu..Dalili zote zilionyesha nchi inaporomoka hawakutaka kuamini leo hii huko Zimbabwe ni Ujambazi mtupu lkama Somalia.. Kufurahia kwa wachache majambazi wenye nguvu ya dola haina maana kuwa Zimbabwe na Somalia zinapiga hatua mbele..
Mkuu, inawezekana kabisa kuibomoa CCM kwa kusimamia mambo ambayo yanawagusa wananchi wengi moja kwa moja. Na kwa bahati nzuri kuna uwezekano mkubwa kwamba sasa hivi population kubwa ya wananchji ipo mijini na sio vijijini tena. Kila mji mkuu wa wilaya, mkoa na hata miji yetu mikubwa kwa hesabu kuna wamechukua asilimia kuwba ya wakazi tofauti na zamani.
 
Hivi sifa za urais ni zipi ambazo JK anazo na ambazo hao uliowataja hawana au ni katika kuhalalisha umateka wetu kwa CCM? Kwamba tumeshindwa kuitoa CCM madarakani haina maana kwamba inakubalika au inapendwa. KANU ilibaki madarakani kwa muda mrefu wakati tafiti zote zilikuwa zinaonyesha kwamba katika watu kumi sio zaidi ya wawili waliokuwa wanaipenda na kuikubali KANU. It is much much more complicated than what you have tried to suggest.

Hilo la wanaCCM kumeguka imethibitika kwamba ni unworkable kwa sababu (i) woga na kukosa ujasiri miongoni mwa viongozi wengi wa CCM. Na woga huu unatokana na ukweli kwamba wengi wa wana CCM, hata hao mnaowaita mashujaa, wamesokomezana uchafu wao mvunguni mwa CCM. Siku wakitoka CCM tutashangaa jinsi ambavyo nao ni wachafu. Sasa ili utoke CCM inabidi uwe mnyoofu kwelikweli, sasa ni wangapi hao. Ndio maana sisi wengine tunaamini katika safari ndefu ya ku-recruit wana siasa wapya, wenye bidii na maono ya muda mrefu. (ii) vyama vingi vya upinzani havipo welcoming kwa hao wahamaji watarajiwa. Mwanasiasa yeyote anayetegemea siasa pekee kama njia ya maisha yake, ambao ndio wanasiasa wetu wengi walivyo, hawezi kuondoka sehemu bila kuhakikishiwa usalama wake kisiasa na kimaisha huko aendako. Akigundua kwamba huku aendako kuna uwezekano mkubwa zaidi ya nafasi ya kufanya siasa (eg) ubunge kuliko huko alipo sasa, ataondoka, tena haraka. Lakini wengi wa wanasiasa wa CCM, hasa wabunge, wakipiga hesabu wanaona uwezekano wa kupata ubunge tena ni mkubwa ndani ya CCM kuliko wakienda huko upinzani. Hili linawakwaza. Yote hii ni kwa sababu wabunge wengi wa CCM walichaguliwa kupitia mgongo wa chama chao na JK. Ukiwanyan'anya CCM wakabaki wenyewe wachache sana wanaweza kupata ubunge na hili wanalijua.

Ambacho wabunge wengi wa CCM hawajaelewa ni kwamba mwaka 2010 JK hatakuwa mtaji tena. Kwa wale waliopita kwa sababu walishikwa mkono na JK wataliwa kwa sababu JK mwenyewe itabidi ajihangaikie. In fact 2010 kujaribu kupiga kampeni kupitia mgongo wa JK itakuwa counterproductive kama ilivyokuwa kwa Bush uchaguzi uliopita.
 
oh..no naomba muangalie vizuri kauli yangu niliyoandika. Mara nyingi watu hawasomi hasa nimeandika nini wanainfer kitu ambacho sijaandika: Sijasema viongozi hawa "hawawezi" kuwa viongozi wa nchi yetu wala Zitto sijasema "hawezi". Jamani nachagua maneno yangu vizuri. Ndio maana nimesema nitachambua wakati wake ukifika hapa ilikuwa ni kidokezo tu. Pia nimeweka "qualifications" kubwa mbili kwenye hiyo kauli yangu.

Siwezi kumpigia kura Kikwete hata nifungiwe jiwe la kusagia shingoni, kwa kadiri ya kwamba anaendelea jinsi alivyo sasa na rekodi yake ikiwa ndiyo hii.

Read this book: "It is not what you say that matters, it is what people hear"! Sasa mzee kama wewe unaandika hivi na watu wanaelewa vile, mwenye shida hapo ni nani: is it the sender or the receiver of the message?
 
Mkuu kwanza nakubaliana na wewe kwani nadhani tunakubaliana sana kwenye jambo moja ambalo sijakubaliana na Mzee mwenzangu FMES; kwamba kudai katiba peke yake siyo kichocheo cha mabadiliko tuyatakayo.

Mkuu MMJ,

Ninachosema hasa ni kwamba kama kuna choice between kumeguka kwa CCM na kubadili katiba, ninachagua kubadili katiba,

kwa sababu CCM haitakuja kumeguka hivi karibuni na kwangu hii sio political strategy kwa wananchi wanaoataka mabadiliko kwa taifa lao, na nisichopenda kuliko yote ni maneno ya kudanganyana humu forum wakati ukweli wa ground zero bongo wala haufanani kabisa na haya maneno mengi ya kishujaa humu ndani,

So far ninaridhika sana na maneno mengi ya FDR na Mkandara, kwa sababu yako samba samba sana na ukweli wa siasa za bongo, sasa kama kuna kazi inatakiwa kufanywa on mabadiliko, ni lazima kuanzia na analysis za hawa wakuu kwa maoni yangu, lakini siwazuii wanaotaka kudanganyana.
 
Quote: FDR

atashinda kwa kura nyingi kwa sababu kuu mbili

1. Anaopambana nao nje ya ccm siyo strategist wazuri ktk mingoling ya siasa zetu na hasa pale ccm inapokuwa united front against mpuuzi yeyote mbele yao, hofu yangu ni wapainzani kupungua bungeni hilo ninaliona kwa kasi linakuja.

2. Wa-tz tumejaaliwa kutafakari beyond mashaka ya kibinadamu, na kama utapiga kura kwa kufuata mtindo huu basi jk atashinda na wabunge wake maana wapiga kura wasio na jazba kama tarime kamwe hawawezi kumpitisha mpinzani ambaye kwao daima anaonekana ni mtu asiyetayari kuongoza na kutawala zaidi ya kulalama.

Ni maoni yangu tu kama mtz na mzingatia wasifu wetu asilia.
__________________
"TWENDE PAMOJA, INAWEZEKANA... ." – FDR.Jr"
 
Mkuu MMJ,

Heshima mbele sana, na hili chini ni darasa zito sana kwa wasielewa vizuri siasa za bongo, maana wengi tunafikiri bongo ina siasa za Europe na USA, hebu kuleni darasa hili:-


Quote:- Mwanakijiji

1. Mag.. nadhani vyama vingi viliruhusiwa tena mwaka 1992 kabla ya mauaji ya kimbari.

2. Wananchi asilimia 80 walikataa mfumo wa vyama vingi. Ingawa yawezekana wengi hatutaki kukubali matokeo ya uchaguzi wa rais 2005 imeonesha asilimia 80 ya wapiga kura wakiichagua CCM any correlation?

3. KUna imani kuwa "watu wanaichukia CCM" hii ni imani tu haina msingi. Mapenzi ya watu kwa CCM yamekuwa kama mapenzi ya mtoto kwa mama yake. Kuna mvuto mkubwa sana wa CCM hasa kwa kizazi kilichotangulia. Wazee wengi kutokana na kile wanachoamini kuwa ni hekima hawako tayari kuona mabadiliko makubwa kama ya kuipa nchi uongozi wa chama kingine. Hawa bado ndio wapiga kura wengi zaidi na walio constant.

4. Wazee hawa bado wanamepenzi ya TANU na CCM na bado hawajaona sababu hasa ya kubadilika hasa wanapoona serikali inajishughulisha kidogo. Wazee hawa hawataki mabadiliko ya ghafla kwani wengine wana hofu ya pension zao, miradi yao, na maendeleo ya watoto wao.

5. Nakumbuka wakati nashughulikia suala la vijana kule Ukraine, mzazi mmoja alimpigia simu Rais na kumbembeleza kwa kumuita "Baba" na mzee mwengine alisema "Rais ni kama Baba yetu, atusaidie". Wakati wale vijana wakililia kilichokuwa haki yao wazee wao (baadhi) walikuwa wanaibembeleza serikali kama mtu anavyombembeleza mama mkwe!

6. HIvyo ukweli utabakia kuwa wazi, CCM bado inawapenzi wengi zaidi, ina mashabiki wengi zaidi na licha ya kashfa zote tunazozisikia sasa ni wanachama wa CCM ndiyo wamekuwa mara zote kimbilio la serikali.
Hivyo kuleta mabadiliko kwenye Taifa letu bila kuangalia CCM ni njozi ya Alinacha.
 
Hilo la wanaCCM kumeguka imethibitika kwamba ni unworkable kwa sababu (i) woga na kukosa ujasiri miongoni mwa viongozi wengi wa CCM. Na woga huu unatokana na ukweli kwamba wengi wa wana CCM, hata hao mnaowaita mashujaa, wamesokomezana uchafu wao mvunguni mwa CCM. Siku wakitoka CCM tutashangaa jinsi ambavyo nao ni wachafu. Sasa ili utoke CCM inabidi uwe mnyoofu kwelikweli, sasa ni wangapi hao. Ndio maana sisi wengine tunaamini katika safari ndefu ya ku-recruit wana siasa wapya, wenye bidii na maono ya muda mrefu. (ii) vyama vingi vya upinzani havipo welcoming kwa hao wahamaji watarajiwa. Mwanasiasa yeyote anayetegemea siasa pekee kama njia ya maisha yake, ambao ndio wanasiasa wetu wengi walivyo, hawezi kuondoka sehemu bila kuhakikishiwa usalama wake kisiasa na kimaisha huko aendako. Akigundua kwamba huku aendako kuna uwezekano mkubwa zaidi ya nafasi ya kufanya siasa (eg) ubunge kuliko huko alipo sasa, ataondoka, tena haraka. Lakini wengi wa wanasiasa wa CCM, hasa wabunge, wakipiga hesabu wanaona uwezekano wa kupata ubunge tena ni mkubwa ndani ya CCM kuliko wakienda huko upinzani. Hili linawakwaza. Yote hii ni kwa sababu wabunge wengi wa CCM walichaguliwa kupitia mgongo wa chama chao na JK. Ukiwanyan'anya CCM wakabaki wenyewe wachache sana wanaweza kupata ubunge na hili wanalijua. Ambacho wabunge wengi wa CCM hawajaelewa ni kwamba mwaka 2010 JK hatakuwa mtaji tena. Kwa wale waliopita kwa sababu walishikwa mkono na JK wataliwa kwa sababu JK mwenyewe itabidi ajihangaikie. In fact 2010 kujaribu kupiga kampeni kupitia mgongo wa JK itakuwa counterproductive kama ilivyokuwa kwa Bush uchaguzi uliopita.

Mkuu Kitila,

Heshima mbele, maneno yako mengi ni ya kishujaa sana, kuna mzee mmoja aliyekwua CCM aliyafuata maneno yako exactly, akajiunga na waasisi wa upinzani na kuanzisha upinzani, akiwa CCM alikuwa vyeo vingi vya bure hasa kwenye bodi ili kumpa kula, alipotoka tu CCM wakamnyofoa vyote, na kubaki tupu!

Ambacho hakujua ni kwamba wenziwe wote aliojiunga nao, either walikuwa wameshachota kule CCM na kuwa na miradi binafsi mikubwa kwa hiyo hawakuwa na wasi wasi na mlo, au wengine walikuwa ni mapandikizi wa CCM tu, masikini mzee wa watu akaishia kua lofa hoe hae huku wenziwe wakipeta tu, siku moja mdogo wake ambaye naye alikuwa na vyeo huko CCM, naye akawa frustrated kidogo na Diria, akaamua kutoka na kuingia upinzani,

Ninakumbuka huyu mzee, yaani kaka mtu akimlilia sana mdogo wake asifanye, makosa kama yake ya kurukia upinzani na abaki huko huko CCM, maana wakati bado, alsema nilifikiri wakati ulikuwa umefika, lakini sikuwa-read vizuri wananchi wa Tanzania kwamba bado hawako tayari kwa mabadiliko.

Ninamkumbuka sana huyu mzee, ambaye sasa ni marehemu, maneno yako Kitila ni ya kishujaa sana, lakini sio kwa mazingara ya bongo, sawa kama unavyosema kwamba ni vyema kuwa-recruit wapya kwa ajili ya the future, ni idea ambayo hapa JF kwenye quick fix kama za Europe na USA, haikubaliki kwa hiyo ni kaaazi kweli kweli!
 
Sikubaliani na wazo kuwa CCM inazoa kura kwa sababu ya kupendwa na wananchi walio wengi. La hasha, kuna sababu za ziada kama umasikini, ujinga, kukata tamaa, hofu na woga.

Kwanza, baada ya kuona sura zile zile miaka nenda rudi iwe ndani ya CCM ama upinzani, wananchi wengi wamekata tamaa. Hiki ndicho chanzo cha kusikia misemo kama - afadhali tubaki na CCM yetu hii tunayoijua - hii ni dalili mbaya na ya hatari.

Pili, tumejenga jamii ya watu yenye woga na iliyojifunika kwenye mwamvuli wa amani hewa. Tumebaki watu wasiojiamini kwenye kudai haki na kubaki kutegemea miujiza ama mitume ituletee hiyo haki. Si ajabu tunamngoja mwokozi kutoka CCM.

Tatu, serikali inatakiwa iwe na hofu inapoboronga ikijua wazi wananchi wanaweza wakaifukuzia mbali. Lakini wananchi wa Tanzania wameiruhusu serikali kujiimarisha kwenye ubabe kiasi cha kuwatia hofu wananchi walioiweka madarakani. Hili halikubaliki.

Nne, mara ngapi matamshi ya kijinga kama sisi watanzania ni tofauti na wenzetu, tunayasikia na kuyakubali. Ujinga wetu umejenga tabia ya ukondoo ambao umetoa mwanya wa kutotaka kujifunza kwa wenzetu kwa mifano hai kama ya Kenya na Zimbabwe.

Tano, kwa umasikini uliokithiri tumeshindwa kutambua kuwa rushwa si tu ni adui wa haki bali ni kichocheo cha umasikini. Kwa rushwa tunaipa kura CCM bila kujua athari za kufanya hivyo. Aliyetoa rushwa leo, kesho atavuna na kwa riba kubwa hicho alichokupa na kukuacha masikini zaidi. Na jambo hili linajirudia kila uchaguzi.

Mrema, Lipumba, Mbatia, Cheyo, Mbowe, Seif na wengineo - mmeishajaribu kiasi cha kutosha na sasa waachieni wengine na ikiwezekana awe moja atakayekubalika kwa wengi. Ili Tanzania ipate mendeleo ya kweli, CCM ni lazima ipigwe chini.
 
Sasa hata kwenye hili la katiba, CCM haiwezi kushindana na nguvu ya wananchi iliyoshikamana na kusimama imara, lakini one thing sisi wananchi hatuwezi kutegemea nguvu ya wanachama wachache ndani ya CCM, kutusaidia kuleta mabadiliko kwa wananchi wote wa Tanzania, infact historia iko wazi kwamba tunahitaji kuwa waangalifu sana maana kwa mtaji huo wa watu wachache tunaweza kuangukia kwenye ule mtego uliotaka kuwapata wa-China na lile kundi la watu wanne.

FMES,

Kwa nini unavunjika moyo kirahisi na kuruhusu adui akuvuruge akili kwa vitisho? Ulichokisema hapa cha kina mke wa Mao na wenzake, ndicho kinachotumiwa na CCM kukaba makoo kina Mwakyembe, Killango, Seleli, Manyanya na wengine wanaotaka kuachana na mfumo butu na chama sakala.

Umenihoji hapo awali kuwa nimekuwa mkali na kutoa maneno makali, je jukumu na wajibu huo wa kuwa mkali kwa wanaohujumu nchi ni wa nani?

Ndiyo, maneno yangu ni makali kwa kuwa ni hasira na uchungu wa kuendelea kupuuzwa na kudharauliwa. Haki yangu inanyanyaswa na kuzibwa pumzi kisa wajibu wa mwanachama wa CCM ni kwa Chama kwanza na si Taifa!

Ni aibu sana kwa wale ambao wako katika vyama vya siasa na hasa CCM na ambao wametoa viapo vya maisha kuwa kamwe wao hawataachana na CCM! Aibu hii itawaingia siku CCM uozo wake utakapokifanya kisambaratike.

Sijui hawa wazee Salim, Warioba, Kawawa, Malecela, Msuya na wenginewe ambao wanazidiwa kete kila siku na wajanja wanaomiliki CCM watasemaje na viapo vyao siku CCM itakapokuja umbuka kuwa pamoja na kutuletea uhuru na mengine yote yaliyokuwa ya maana, CCM ilibadilika kuwa jinamizi mhujumu na fisadi.

Swali langu kwa hawa Wazee ni hili, wako tayari kufa kuilinda CCM na si Tanzania? Ni maslahi gani wanayoyalinda ikiwa kwa zaidi ya miaka karibu 15 tunajua kuwa CCM imepoteza dira na muelekeo? Hivi hawa wazee wanategemea kweli na kutokuwa kwao na madaraka au kutumia busara na kuachana na CCM wataweza kuibadilisha CCM iwe kila chama tulichokishangilia February 5 ya mwaka 1977?

Wazee hawa ni heri wakihame CCM au waachane na CCM kuliko kuja poteza sifa na heshima zao na kuitwa WASALITI kwa kuwa waliogopa kukihama CCM wakati walipokuwa na fahamu zao kuwa CCM si chama cha mapinduzi wala si chama cha Wakulima na Wafanyakazi.

Sauli wa Tarsu, alikula kiapo cha milele kuitumikia Roma, akawa akiwanyanyasa Wayahudi na hata kufumbia macho vitendo viovu. Lakini siku ile alipokuwa akienda Damesiki (Damascus), Biblia inatuambia mbingu ikafunguka na Bwana Yesu akamuuliza, "ilhali vipi wawanyanyasa watu wangu? wamekukosea nini unawapa mateso?"

Sasa sisi na sauti zetu za kutaka CCM imeguke na hawa wanaojiita CCM mageuzi waachane na Roma yao, ndiyo inayolia, "kwa nini hawa wanaojiita watetezi wa haki bado wanaendelea kulewa mvinyo na CCM ambayo haiwajali Watanzania tena bali ni kujali matumbo yao na marafiki zao?

Umeniuliza maana ya kuleta mfano wa Somaiya kulipia mkutano mkuu wa UVCCM kwa kutoa shilingi milioni 400.

Nikuulize, hizo hela ni kwa mapenzi gani? ni nani ananunuliwa au analipwa fadhila na hizo hela? Iweje CCM leo iweze kupata fedha za kuendesha mkutano na uchaguzi wa jumuiya yake ambayo si jambo la msingi kwa Taifa lakini inajivutavuta kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kweli yanayowasibu Wananchi wa Tanzania na Taifa la Tanzania?

Nikianza na orodha ya haraka haraka, kuna mgomo wa wanafunzi, mgomo wa waalimu (huu sijui baada ya mwaka ndio Serikali inapata pesa na kuwalipa!), kuna wastaafu, kuna shida ya maji, shida ya umeme, madawa hakuna, njaa kila kona, ajira hakuna, ufisadi na dhuluma zinapeta, lakini kikao cha UVCCM kimepata umuhimu na ujiko wa hali ya juu (priority) na pesa zikapatika haraka ili achaguliwe mwenyekiti wa jumuiya?

Nitaongea kwa ukali kwa kuwa CCM ya leo, si CCM iliyonilea, CCM iliyonifunza kuuthamini utu na jirani, kujivunia Utaifa wangu.

CCM ya leo imezingirwa na inaongozwa na kundi la Wasaliti, Wahaini, Wazembe, Walafi, Wezi, Wavivu, Wahuni, Wanafiki, Waongo, Wahujumu, Mafisadi na sifa nyingine mbovu ambazo si njema kwa Tanzania hata wale WanaCCM ambao bado wanatongotongo kwenye macho.

Wanaojiita CCM mageuzi, tunawataka wafanye hivi kama sisi Wakristo tunavyosema tunapotubu, "wamkatae Shetani na mambo yake, kazi zake, fadhila zake na wema wake" watubu kuwa walikosea na wanapaswa kuoshwa, nasi tutawasamehe na kuwaenzi kama mashujaa.

Kinyume cha hapo, wataendelea kunuka uozo na kuoza kama vile kapu la samaki linavyovunda kwa samaki mmoja kuoza.
 
Katika wana CCM- waliopo hakuna viongozi bold enough wa kudai katiba mpya from within. Japo nakiri wako wakina Prof. Harison Mwakyembe ambaye ni Mtaalamu wa katiba na anayajua wazi mapungufu ya katiba yetu tena from contutionakism poit of view hana jeuri ya kudai katiba mpya from within.

Spika Sita ni bold. Kitendo cha kumwambia rais awe mkali kidogo baada ya kulihutubia Bunge ni uthibitisho wa boldness ya baadhi ya wana CCM katika masuala ya maslahi ya taifa. Ndani ya chama its the other way round hapa ni maslahi ya chama tuendelee kutawala.

Hakuna wanaCCM watakaothubutu kudai katiba mpya kasababu ikipatikana katiba mpya. The playing ground itakuwa level. Kama playing ground itakuwa level na tayari wanajua weakness yao, they know for sure they'll be beaten on their own game,huku bado wana njaa. Chama chao majeruhi kweli nani atakubali?
Katiba iliyopo yenye sheria, taratibu na kanuni za kuifavour si ni mtaji mkubwa wa kujihakikishia unaendelea kutawala na kuendeleza ulaji?.

Pasco,

Boldness! That is a critical word You have used my friend.

Ndio, ndani ya CCM hakuna watu Bold tena. Wakati kina Jumbe, Sefu Hamad na hata Malecela na Kolimba walipoweka mataruma ya kupingana na CCM, Nyerere aliwapandia vibaya na wengi wao wakapagawa na kuogopa.

Katika moja ya vitu ambavyo daima nitamkosoa Mwalimu Nyerere pamoja na mapenzi yangu kwake, ni hili la kutuachia watu wenye nidhamu na woga na makende laini kama sufu.

Mwakyembe na hata Sitta, hawana ubavu kusimama kidete na kukidindia chama chao na kutaka kijinyooshe.

Hata kama wana madhambi, wao wanakiogopa CCM kuliko kuwaogoa wananchi wa Tanzania ambao wamewapa dhamana ya kuongoza Taifa.

Ni mpaka pale mmoja wao au baadhi ya hawa Wana CCM watakapoachana na paranoia na fear syndrome ya kuangamizwa na CCM kama kina Sefu, Malecela na Jumbe walivyofanyiwa, ndipo tutakapoona mabadiliko ya wazi na ya kweli.

Nafasi ya hawa ndugu kufanya hilo, iko sasa kuliko wakati mwingine wowote. Najiuliza ni lini wataacha kucheza nalenale na kufanya kweli? Kama wao kweli ni Wazalendo na Wanamapinduzi, basi hawataogopa iwe ni mzuka wa Nyerere au kushikiwa bango na CCM.

Nawapasha sisi wananchi tunatega masikio, tuwasikie wakifanya maamuzi magumu.
 
Rev. Kishoka,
Mkuu taratibu mkuu wangu taratibu.... ebu pumua kidogo kabla hujasoma yangu maanake nataka utazame upande wa pili wa shilingi hiyo ya watu kama Field Marshall Es..
Nitakupa mfano wa dini yako mwenyewe ambayo nina hakika wewe ni Rev na utaweze kunipa somo vizuri..
Hivi kama viongozi wa Kanisa wakiwa na mapungufu yote uliyoyaandika hapo juu... wewe kama muumini wa dini ya Kikristu utajiondoa ktk dini hiyo kwa sababu ya matendo ya viongozi hao!
Je, Biblia uliyofundishwa itakuwa na mafundisho yapi muhimu ktk kukuongoza wewe ikiwa matendo ya binadamu wachache waliochaguliwa ama kubahatika kuongoza ndio wametumia vibaya msahafu huo kujineemesha..
Navyofahamu mimi mtu kama Field Marshall ES ni muumini wa kweli wa CCM isipokuiwa anaelewa mapungufu ya baadhi viongozi wa chama chake na hawezi kukiharamisha chama kizima kwa sababu ya matendo machafu ya baadhi ya viongozi waumini wa msahafu ule ule wa chama CCM..
 
Pasco,

Mwakyembe na hata Sitta, hawana ubavu kusimama kidete na kukidindia chama chao na kutaka kijinyooshe.

Hata kama wana madhambi, wao wanakiogopa CCM kuliko kuwaogoa wananchi wa Tanzania ambao wamewapa dhamana ya kuongoza Taifa.
.

Hao wananikumbusha aliyosema Skakespeare; It is a tale told by an *****, full of sound and fury signifying nothing. It's like a poor player who struts and frets his hours on the stage and then is hear no more.

They definitely wouldn't dare, they dont have the nerve !!
 
Rev. Kishoka,

Hivi kama viongozi wa Kanisa wakiwa na mapungufu yote uliyoyaandika hapo juu... wewe kama muumini wa dini ya Kikristu utajiondoa ktk dini hiyo kwa sababu ya matendo ya viongozi hao!
Je, Biblia uliyofundishwa itakuwa na mafundisho yapi muhimu ktk kukuongoza wewe ikiwa matendo ya binadamu wachache waliochaguliwa ama kubahatika kuongoza ndio wametumia vibaya msahafu huo kujineemesha..

Mkandara,

Pamoja na kwamba ulikuwa una"respond" kwa post ya Rev. lakini imenibidi niingilie. Najua kuna ambao wameilinganisha CCM na baba au mama, lakini hii ya kuilinganisha na dini ni kiboko. Pia kwa wana CCM inawezekana kuna wanaoiweka kwenye mizani ya dini - sasa hii inafungua pandora box ambayo naomba daima ibaki imefungwa. Tukielekea huko, basi hakuna tena haja ya kuipinga CCM lakini sote tunatambua kuwa CCM hiyo hiyo ndiyo imetufikisha hapa tulipo pamoja na kubadilisha viongozi. Something has to be wrong in CCM other than Kikwete, Lowassa, Chenge and others including FMES.

Waliojaribu kupiga kelele wamenyamazishwa na sasa wametulia. Wako wapi Kilango, Mwakyembe, Seleli, Nape na wengineo. Kabla yao tulikuwa na akina Kasaka, Mzindakaya na wengine wengi tu. Mfumo unaonyamazisha upinzani dhidi ya uovu na wakati huo huo kuukumbatia uovu huo kwa kulindana ndiyo sera ya ndani ya CCM. Kama vile chama cha siasa hakiwezi kuchukua nafasi ya baba ama mama, dini ndiyo kabisa na nakusihi uombe msamaha kwa hilo.
 
Back
Top Bottom