CCM kumeguka ni muhimu kwa Taifa!

Tatizo hapa ni kuwa CCM tayari imeamua kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba mwakani na hivyo kumeza kabisa hoja ya Katiba mpya.

Kwa kuteka hoja ya mabadiliko ya Katiba (nasema "kuteka" kwa sababu mara kadhaa sasa serikali imetoa tamko rasmi kuwa hakuna haja ya mabadiliko ya katiba kwani iliyopo inajitosheleza) CCM inajitengenezea uwanja wa kushinda kwa urahisi na hivyo hata wapinzani wakisema "tunataka Katiba Mpya" CCM inasema hakuna haja "tayari tunaifanyia mabadiliko katika mswada wa "mabadiliko ya 22 ya Katiba" na wale wenye mapendekezo wayatoe kwa wizara ya Katiba na Sheria."

Hivyo, hoja ya mabadiliko ya Katiba haiendi popote kwani ni hoja ambayo CCM wameshajua kuwa itawatengenezea ujiko mkubwa zaidi kuliko mambo ya ufisadi. HIvyo kama kuna nguvu nje ya CCM basi siamini kuwa zitatokana na mjadala wa Katiba, CCM is too smart for that.

Mkuu MMJ,

Heshima mbele, ninakubali hoja zako nyingi kwenye hii post kwa sababu zinajitosheleza, lakini bado nina tatizo kidogo hapo juu kuhusu katiba na CCM,

- Tunao mfano mzito sana wa ripoti ya Hosea na Richimonduli, kwa sababu ni clear kwamba Lowassa alijaribu kuwa too smart kama unavyowabatiza CCM hapa, lakini mbele ya nguvu ya wananchi hakuweza kutushinda,

Sasa hata kwenye hili la katiba, CCM haiwezi kushindana na nguvu ya wananchi iliyoshikamana na kusimama imara, lakini one thing sisi wananchi hatuwezi kutegemea nguvu ya wanachama wachache ndani ya CCM, kutusaidia kuleta mabadiliko kwa wananchi wote wa Tanzania, infact historia iko wazi kwamba tunahitaji kuwa waangalifu sana maana kwa mtaji huo wa watu wachache tunaweza kuangukia kwenye ule mtego uliotaka kuwapata wa-China na lile kundi la watu wanne.
 
Mkuu MMJ,

Heshima mbele, ninakubali hoja zako nyingi kwenye hii post kwa sababu zinajitosheleza, lakini bado nina tatizo kidogo hapo juu kuhusu katiba na CCM,

- Tunao mfano mzito sana wa ripoti ya Hosea na Richimonduli, kwa sababu ni clear kwamba Lowassa alijaribu kuwa too smart kama unavyowabatiza CCM hapa, lakini mbele ya nguvu ya wananchi hakuweza kutushinda,

Sasa hata kwenye hili la katiba, CCM haiwezi kushindana na nguvu ya wananchi iliyoshikamana na kusimama imara, lakini one thing sisi wananchi hatuwezi kutegemea nguvu ya wanachama wachache ndani ya CCM, kutusaidia kuleta mabadiliko kwa wananchi wote wa Tanzania, infact historia iko wazi kwamba tunahitaji kuwa waangalifu sana maana kwa mtaji huo wa watu wachache tunaweza kuangukia kwenye ule mtego uliotaka kuwapata wa-China na lile kundi la watu wanne.

mzee ES.. unaposema "sisi wananchi" unazungumai watu gani hasa?

JF ina wanachama (waliojiandikisha) wapatao 7000 hivi: Hii ni sawa na asilimia 0.0175 ya Watanzania wote (nikichukulia watanzania milioni 40). Hawa ndio "sisi wananchi"?

Wana CCM wenyewe hawazidi milioni tano (hapa nazungumzia wenye kadi) ambayo nayo ni sawa na asilimia 12.5 tu ya Watanzania?

Je unazungumzia wapiga kura? Waliopiga kura mwaka 2005 ni karibu watu milioni 12 hivi ambayo ni kama robo moja ya Watanzania wote (25 percent). Je ni hawa unaowazungumzia kuwa ni "Sisi wananchi"?

Mapema mwaka huu tumeambiwa kuwa asilimia 31 ya Watanzania hawajui kusoma na kuandika. Asilimia 31 ya Watanzania ni watu milioni 12.5! Yawezekana hawa ndio hao hao waliopiga kura?!! Je ni hawa unaosema "sisi wananchi"?

Je yawezekana ni kundi la wasomi wenye shahada Tanzania ambao wanauwezo wa kuchambua mambo kisomi? Tanzania ina watu wasiozidi milioni moja ambao wana shahada au stashahada na ukiongeza waliofikia kidacho cha sita na kupitia sekondari au elimu zaidi ya ile ya msingi unaweza kupata watu karibu milioni kumi hivi (makisio ya juu), ni hawa ndio tunawategemea kupaza sauti zao au ni watu gani hao?
 
Sisi wananchi, ni kwamba wabunge walipotaka kujiongeza marupu rupu, kulitokea sauti nyingi sana against, kuanzia media, institutional mbali mbali za taifa, NGOs, Wasomi, na Wananchi wa kawaida, ambao walihojiwa sana na our media na kutoa mawazo yao wazi kwamba hawakubaliani na kiu hiyo ya wabunge, hoja ikasitishwa hapa ni moja ya maana yangu ya sauti za sisi wananchi.

Sasa katika kesi ya kubadili katiba, kwanza ni lazima wananchi walio wengi wa Tanzania, wa kila level kuanzia mijini mpaka kijijini wahamasishwe na inawezekana sana kwa mfano uliotokea Kenya, viongozi wa huko walidhani wananchi ni wajinga wakataka kuibadili katiba ya Jamhuri wka manufaa yao, lakini kuna wananchi walioala macho kuhamasa wananchi wenzao, kuanzia mjini mpaka mashambani, guess what ile referendum ya kifisadi fisadi ya viongozi wakuu wa huko ikakataliwa na wananchi karibu wote waliopiga kura.

Sasa hapa kuna ku-deal na task ya kuhamasisha, ambapo ndipo hasa panapoweza kuleta ugumu, lakini ishu muhimu ya taifa kama ya kudai mabadiliko ya katiba ni lazima iwajumuishe wananchi wa ngazi zote, hakuna excuse kabisa on this one.

Sisi wananchi ina maana wananchi wote wa Tanzania, na sisi JF tukiwemo!
 
..

Sasa katika kesi ya kubadili katiba, kwanza ni lazima wananchi walio wengi wa Tanzania, wa kila level kuanzia mijini mpaka kijijini wahamasishwe na inawezekana sana kwa mfano uliotokea Kenya, viongozi wa huko walidhani wananchi ni wajinga wakataka kuibadili katiba ya Jamhuri wka manufaa yao, lakini kuna wananchi walioala macho kuhamasa wananchi wenzao, kuanzia mjini mpaka mashambani, guess what ile referendum ya kifisadi fisadi ya viongozi wakuu wa huko ikakataliwa na wananchi karibu wote waliopiga kura.


Unaweza vipi kuwahamasisha watu milioni 40? Na ni nani huyo ambaye atakuwa na mvuto wa kuweza kuwashawishi watu wote hivyo wakakubaliana naye? Mtu huyo/watu hao wako upinzani au wako ndani ya CCM au kila mmoja anajihamasisha mwenyewe au tunafanya kuhamasishana sisi kwa sisi? Kama lengo ni kuwafikia watu wengi ina maana ni lazima kuwa na njia rahisi na ya haraka kwani kuhamasishana mmoja mmoja inaweza kuchukua karne!


Sasa hapa kuna ku-deal na task ya kuhamasisha, ambapo ndipo hasa panapoweza kuleta ugumu, lakini ishu muhimu ya taifa kama ya kudai mabadiliko ya katiba ni lazima iwajumuishe wananchi wa ngazi zote, hakuna excuse kabisa on this one.

Bado tunarudi tunaweza vipi kuwajumuisha wananchi wa "ngazi zote"? Naomba upendekeze njia rahisi, ya haraka, na inayoweza kuwafikia wananchi wa "ngazi zote".

Sisi wananchi ina maana wananchi wote wa Tanzania, na sisi JF tukiwemo!

Mzee sisi JF ni 0.0175 ya Watanzania wote. Na hapa tunaamini kuwa tumekusanya watu wenye kupata habari, wasomi, wanafunzi, watumishi, wanasiasa n.k Sasa wale wengine "wa ngazi zote" nani atawahamasisha? Hapa penyewe ukiangalia suala la Katiba tu, umeona watu wanajadili? Utakuta kuna watu 10 tu hapa ambao wanaweza kujadili haja ya katiba mpya wengine ni watazamani tu!

Chochote kitakachoibadilisha nchi lazima kianze na CCM kwa ubaya au kwa uzuri. Njia nyingine ni ndefu kweli; mimi naangalia njia ya mkato.
 
Mjadala mzuri sana huu, ni moja ya mijadala michache hapa JF kwa siku za karibuni watu wanajenga hoja kwa umbali huu pasipo kutoka nje ya mstari. Kwa mtazamo wangu Kuimega CCM na kukuza upinzani ni mahitaji yanyoshindana na yanalazimika kutokea kwa wakati moja, vinginevyo utakuwa mchezo wa hatari mno ikiwa tutakwenda na nyenzo moja na kuacha nyingine.

Na wakati mwingine tunaisingizia CCM na kuipa uwezo mkubwa mno ambao haina! Kwenye vichwa vyetu 'tumewaumba" kana kwamba ni watu wenye weledi mkubwa mno wakati ni watu wa wastani mno. Dhana kwamba Wapinzani hawezi kuunda serekali kwa kuwa ni wachache sikubaliani nayo ni sehemu ya dhana mbaya amabazo zimezoeleka katika kunyanyapaa Wapinzani. Kama unazungumzia watu imara wa kuongoza serekali basi ni sawa na kujitukana, watu kama JK,Chiligati,makamba,Ngeleja, mudhir na wengine kama hawa ni kipimo cha ubora cha chama kuwa na watu kuweza kuongoza nchi basi iko namna! Kama ni hawa tu basi Upinzani ulipaswa kuchukua nchi kitambo sana!Tatizo tunapoiangalia CCM tunaitanua mno kana kwamba CHADEMA ikija itabidi ije na jeshi lake, majaji wake, makatibu wakuu wake, Benki kuu yake na warasimu wake. Tuangalie wafanya maamuzi tu(wanasiasa) utaona kuna uwezekano mkubwa ajabu. Mkazo ni kwa wananchi,upinzani kujipanga na kuwa na rasilimali za kutosha basi mchezo unaisha hata leo.

CCM inapaswa kuondolewa kwa kupigwa mtungo, kuibomoa na kuiondolea uhalali na kuimarisha upinzani ambao kwa maoni yangu vipo vyama vinakaribia kuiva na kushika madaraka kamili, mwanakijiji muda mfupi utakuja kugundua njia ya upinzani ndio fupi zaidi. Kimefika kipindi ambacho jamii yenyewe ina uchu wa kuasi na nguvu hii ni ziada ya CCM na uhuni wake,kukumbatiwa na vyombo vya dola,katiba mbovu na uchawi.Hawa ni weupe kabisa na wanafungika kirahisi.
 
Field Marshall Es,

Mkuu shukran sana na nakubaliana na wewe 100 kwa 100. Mjadala huu unakwenda vizuri sana..Mwanakijiji mkuu wangu shukran pia kwa kuzingatia kwamba ipo haja kubwa ya kufahamu kwanza WATU yaani wananachi wanaozungumziwa hapa ni kundi gani!...
Kulingana na Mazingira ya nchi yetu kihistoria inasemekana mabadiliko mengi yameanzia vijijini (sina hakika) lakini usemi huu unakosa kiungo muhimu sana kinachowawezesha wananchi wa vijijini kusimama..

Nikitazama toka Uhuru wetu ulianza kupiganiwa mijini ambako kulikuwa na watu wachache toka mijini waliofahamu kwamba Waingereza walikuwa wameishika nchi yetu under protectorate na hawa ndio walioweza kuitumia sheria kuanzisha vyama. haikuwa rahisi kujenga vyama hivyo chini ya sheria ngumu sana na wakaweza kupenyeza hadi vijijini ambako ndiko nguvu ya Uhuru ilipojitokeza wazi.
Pamoja na uwezo wa Muingereza kujaribu kuondoa ama kudhoofisha nguvu ya viongozi waasisi wa vyama hivi ikiwa ni pamoja na kupoteza ajira zao ndani ya serikali ya mkoloni, viongozi wetu walisimama imara kutangaza haki ya wananchi ambao wengi vijijini hawakufahamu kutokana na mazingira ya huduma za elimu tuliyopewa..

Kwa hiyo leo hii nikiitazama CCM kama vile mkoloni Muingereza aliyepo madarakani, kulingana na historia ni wajibu wetu sisi wakazi wa mijini ama labda niseme wasomi ambao tayari tumekwisha fahamu dosara kubwa zilizomo ktk Katiba tuzijengee hoja ambayo inakubalika kwa wananchi wote katika mazingira tunayoishi.
Tatizo kubwa ambalo nimeliona toka zamani ni kwamba viongozi wa leo hawako serious na Mageuzi ya Kiutawala. Mara zote mahojiano makubwa ya Mageuzi ya Utawala yamekuwa yakizungumzia miundo ya vyama, sheria zinazowafunga kamba za shingo viongozi ndani ya vymama vya Upinzani kama vile wagombea binafsi na kadhalika.

Sheria ambazo zimetoa uhuru mdogo kwa vyama vya Upinzani na kadhalika. Kifupi kila malalamiko yanayowekwa mbele ya wanananchi yanahusu kundi fulani la watu ama vyama vya Upinzani na hayana direct impact kwa wananchi..
Mfano mkubwa ambao nimewahi kuzungumzia sana humu siku za nyuma ni hilo AZIMIO la ZANZIBAR. Azimio hili kama lilivyokuwa Azimio la ARUSHA limekuwa ngome halisi la Ubepari nchini na limejengewa majeshi na sheria zote kulilinda. Na kwa bahati nzuri Azimio hili linawagusa wanannchi wote toka mijini hadi vijijini lakini limekosa sauti kutoka mijini ama wasomi wetu kulijengea hoja ya Mageuzi ktk Utawala..

Wabunge wetu, Wasomi wetu, Vyama vya Upinzani pamoja na viongozi wake wameshindwa kulizungumzia hili kabisa na pengine wanaogopa sheria ya kuondoka kwa Azimio hili kwani ndilo linalowasukuma wao kugombea viti vya Uongozi. Watu wamepoteza roho zao kwa kutaka kushika madaraka, wametumia uchawi wa nguvu ya dola kupandikiza kitu kinachoitwa FITNA kuwadhoofisha wapiganaji wengine ili mradi target kubwa ya kupata ushindi sio kuwaongoza wananchi bali kupata wao nguvu kisheria kuwa ktk kundi la Untouchables..
Wakuu wangu nimewahi kuliweka swali hili mbele ya viongozi wengi kama wanaweza kusimama na kupinga Azimio la Zanzibar... Mkuu hakuna! hakuna sio tu viongozi hata vyombo vya habari vimeshindwa kupiga adhana kuwaita waumini wa haki kulitazama swala hili na jinsi gani linavyo affect Utawala bora nchini. Azimio ambalo kwa mara ya kwanza katika Historia ya Uongozi DUNIANI..tumeona Rais wa nchi akifungua kampuni akiwa Ikulu na kujiita Mjasiriamali (Entrepreneur)...wengine kina Mwinyi wakiwatumia wake zao kuficha uchafu wao...yote chini ya jina la Azimio.
Viongozi wote duniani huacha biashara zao wakiingia Ikulu ama huanza biashara wakitoka Ikulu lakini kwetu Tanzania, viongozi WOTE chini ya Azimio la Zanzibar wameanzisha mashirika yao wakiwa madarakani..
Hali ambayo leo hii toka vijijinini, Madiwani wanachukua majengo ya serikali na kuanzisha biashara..Taasisi zote za serikali zimekuwa vyombo vya biashara badala ya kuwa vyombo vya Huduma na kila unapokwenda kuna mkono wa kiongozi wa serikali ambaye Azimio la Zanzibar limemkabidhi madaraka yanayolenga maslahi yake mwenyewe..
Matatizo yote ya Kiuchumi leo hii nchini yanatokana na Uongozi mbaya! Na Uongozi mbaya usingekuwepo kama sio Azimio la Zanzibar.. kwani Azimio hili linakebehi roho za viongozi kutazama haki yake na familia yake ama haki ya wananchi kwa Ujumla...

Mageuzi ya Utawala siku zote yanatakiwa kuwa na sura tofauti na ile iliyotangulia zaidi ya sera zinazowakilishwa. Na ndio maana kila raia wa nchi hii anaamini kabisa kuwa hata wakija CUF, Chadema ama chama kingine chochote ktk Uongozi watayafanya sawa na viongozi wa CCM..
Wananchi wanahofia zaidi matendo ya viongozi wetu kiutawala zaidi ya kile wanachoweza kuwaletea (Maendeleo)..Kwa hiyo tunapotaka mabadiliko ktk Katiba ni lazima tu Identify vipengele ambavyo vitawavuta wananchi wote toka mijini hadi vijijini.. let's find a common goal.

Hata wakati wa Uhuru wananchi wote walifunga wagon nyuma ya TANU sio kwa sababu walifikiria TANU itawaletea maendeleo zaidi ya Muingereza isipokuwa TANU ingewaletea Utawala tofauti na ule wa Muingereza - FREEDOM...
 
Qote: Mwanakijiji

Njia nyingine ni ndefu kweli; mimi naangalia njia ya mkato.

Mkuu MMJ,

Hii quote yako, inabadili maana nzima ya huu mjadala na kuipa uhai mpya hoja yako ya msingi katika hii thread.
 
Kabla ya kuanza kujadili mjadala huu kiakili ningeomba vitu viwili.......Mwenye katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na katiba ya CCM naomba.
Ili pindi nitakapokuwa naandika lolote najua narefer kwenye katiba zetu. Unaweza kuni PM nikuelekeze wapi pa kuvidropu......Aksanteni.

Ps: Mkulu FMES tutatwangiana baadae ukipata nafasi......
 
1. kulingana na historia ni wajibu wetu sisi wakazi wa mijini ama labda niseme wasomi ambao tayari tumekwisha fahamu dosara kubwa zilizomo ktk Katiba tuzijengee hoja ambayo inakubalika kwa wananchi wote katika mazingira tunayoishi.

2. Tatizo kubwa ambalo nimeliona toka zamani ni kwamba viongozi wa leo hawako serious na Mageuzi ya Kiutawala. Mara zote mahojiano makubwa ya Mageuzi ya Utawala yamekuwa yakizungumzia miundo ya vyama, sheria zinazowafunga kamba za shingo viongozi ndani ya vymama vya Upinzani kama vile wagombea binafsi na kadhalika.

3. Sheria ambazo zimetoa uhuru mdogo kwa vyama vya Upinzani na kadhalika. Kifupi kila malalamiko yanayowekwa mbele ya wanananchi yanahusu kundi fulani la watu ama vyama vya Upinzani na hayana direct impact kwa wananchi..

4. Mfano mkubwa ambao nimewahi kuzungumzia sana humu siku za nyuma ni hilo AZIMIO la ZANZIBAR. Azimio hili kama lilivyokuwa Azimio la ARUSHA limekuwa ngome halisi la Ubepari nchini na limejengewa majeshi na sheria zote kulilinda. Na kwa bahati nzuri Azimio hili linawagusa wanannchi wote toka mijini hadi vijijini lakini limekosa sauti kutoka mijini ama wasomi wetu kulijengea hoja ya Mageuzi ktk Utawala..

5. Wabunge wetu, Wasomi wetu, Vyama vya Upinzani pamoja na viongozi wake wameshindwa kulizungumzia hili kabisa na pengine wanaogopa sheria ya kuondoka kwa Azimio hili kwani ndilo linalowasukuma wao kugombea viti vya Uongozi.

6. Watu wamepoteza roho zao kwa kutaka kushika madaraka, wametumia uchawi wa nguvu ya dola kupandikiza kitu kinachoitwa FITNA kuwadhoofisha wapiganaji wengine ili mradi target kubwa ya kupata ushindi sio kuwaongoza wananchi bali kupata wao nguvu kisheria kuwa ktk kundi la Untouchables..

7. Wakuu wangu nimewahi kuliweka swali hili mbele ya viongozi wengi kama wanaweza kusimama na kupinga Azimio la Zanzibar... Mkuu hakuna! hakuna sio tu viongozi hata vyombo vya habari vimeshindwa kupiga adhana kuwaita waumini wa haki kulitazama swala hili na jinsi gani linavyo affect Utawala bora nchini.

8. Azimio ambalo kwa mara ya kwanza katika Historia ya Uongozi DUNIANI..tumeona Rais wa nchi akifungua kampuni akiwa Ikulu na kujiita Mjasiriamali (Entrepreneur)...

9. wengine kina Mwinyi wakiwatumia wake zao kuficha uchafu wao...yote chini ya jina la Azimio.Viongozi wote duniani huacha biashara zao wakiingia Ikulu ama huanza biashara wakitoka Ikulu lakini kwetu Tanzania, viongozi WOTE chini ya Azimio la Zanzibar wameanzisha mashirika yao wakiwa madarakani..

10. Hali ambayo leo hii toka vijijinini, Madiwani wanachukua majengo ya serikali na kuanzisha biashara..Taasisi zote za serikali zimekuwa vyombo vya biashara badala ya kuwa vyombo vya Huduma na kila unapokwenda kuna mkono wa kiongozi wa serikali ambaye Azimio la Zanzibar limemkabidhi madaraka yanayolenga maslahi yake mwenyewe..

11. Matatizo yote ya Kiuchumi leo hii nchini yanatokana na Uongozi mbaya! Na Uongozi mbaya usingekuwepo kama sio Azimio la Zanzibar.. kwani Azimio hili linakebehi roho za viongozi kutazama haki yake na familia yake ama haki ya wananchi kwa Ujumla...

12. Mageuzi ya Utawala siku zote yanatakiwa kuwa na sura tofauti na ile iliyotangulia zaidi ya sera zinazowakilishwa. Na ndio maana kila raia wa nchi hii anaamini kabisa kuwa hata wakija CUF, Chadema ama chama kingine chochote ktk Uongozi watayafanya sawa na viongozi wa CCM..
Mkulu Bob,

Darasa zito sana mkuu, sasa ni kutafakari tu na kuamua kama ni kusuka au kunyoa!
 
Ndugu wenye uchungu na nchi, kwa maoni yangu tunaposema wananchi tunazungumzia wale wenye kuona uozo uliopo nadni ya jamii yetu, kuuweka hadharani na kuhamasisha wananchi kuukemea na kuuondoa. Tuna mifano mizuri ya kina Dr Slaa, Dr Mwakyembe, Mama Malecela, Mh Zitto na wengine wengi ambao waliibua issue ambazo kutokana na support ya wananchi zimeweza kutufikisha mahali fulani.
Kama tukizungumzia katiba, ni wazi sana kuwa sio kila mwananchi anaweza kuelewa umuhimu wa mabadiliko ya katiba kwa nchi, lakini kuna watanzania wachache waliosomea mambo ya katiba na wanajua uozo uliopo ndani ya katiba yetu, na kama wakipewa uhuru wa kutueleza wazi na kuwaelewa basi tunaweza kuchagua kuwaunga mkono au kutowaunga mkono. My point is wawili wakileta hoja ambaoyo milioni 40 tukaiunga mkono na kuipigania ndio nguvu ya wananchi hiyo.
Wakati tume ya Nyalali ilipokuwa inakusanya maoni kuhusu suala la vyama vingi, kuna watu walidhani kuwa kutokuwa na elimu kwa watanzania kutafanya kazi nzima iwe ngumu, lakini ukiangalia ripoti ya nyalali na jinsi wataalamu walivyoanalyse yale maoni, tunaweza kusema walikusanya sauti ya wananchi. Hili hata kwenye katiba linawezekana.
 
Mwanagenzi, Katiba ya Tanzania ipo hapa: National Website of the United Republic of Tanzania na ile ya CCM inapatikana Chama Cha Mapinduzi - CCM

Mjadala unaenda vizuri; Naona tumerudi kwenye angle ya "wasomi" kama chachu ya kuleta hayo mabadiliko na hasa madai ya Katiba mpya.

a. Hivi kuna mahalii popote Tanzania ambapo pamekusanya wasomi wengi kama dar? Je kati ya vyama vyote vya kisiasa ni chama gani kimekusanya wasomi wengi wa Katiba na sheria nyingine kama CCM? Hivyo tunapozungumzia "wasomi" hawa watii wa Chama maDrs, Ma Professors, n.k wanakuwa wapi?

Hivi kama Prof. Safari akidai Katiba mpya na Dr. Mwakyembe akidai katiba mpya ni yupi unafikiri atakuwa anavutia watu wengi wa kawaida? LEo hii Lipumba, Mbatia, Mrema, Mvungi, Mbowe, Kabwe, n.k wakiamua kudai Katiba mpya (something they have already done in so many ways and venues) na akitokea Mzee Malecela, Kingunge, Dr. Masha, Rostam Aziz, n.k kuanza kudai katiba mpya unafikiri ni kundi lipi litakuwa limefanya kitu ambacho ni cha ziada na kuvutia watu zaidi?

Bado naamini kabisa kuwa Tanzania kihistoria na kimtazamo tuko tofauti sana. Mara nyingi tumefanya makosa ya kulinganisha Kenya na Tanzania, au Zimbabwe na Tanzania. Our political psyche has been formed quite differrently than that of the other people in the region.

Kwangu mimi naamini CCM is more to Tanzanians what ANC is to South Africans. Kinadharia naweza kuona the validity of your propositions that Tanzanians as a people should demand a new constitution. However, realistically such an effort has been proven to be futile in the last 15 years.

Bila ya CCM kukumbatia haja ya Katiba mpya na kufanya kuwa ndiyo agenda yao njozi ya Katiba mpya will be a "mere illusion, to be desired but never to be realized!"
 
Wachangiaji, kwa hiyo hakuna mjuaji wa kujua mahala pa mimi kuipata katiba ya nchi yetu au ndio hivyo tena haina maana ikiwa inapigwa mateke na mwenye kuiongoza nchi?
 
Wachangiaji, kwa hiyo hakuna mjuaji wa kujua mahala pa mimi kuipata katiba ya nchi yetu au ndio hivyo tena haina maana ikiwa inapigwa mateke na mwenye kuiongoza nchi?

yupo, soma vizuri post namba 51
 
Asante MMKJJ kwa makala yako. Kuingoja CCM imeguke ni sawa na fisi anayemfuatia binadamu kwa nyuma akigoja mikono inayoning'inia ianguke kwa jinsi inavyocheza akiamini imevunjika na bado kidogo tuu itaanguka.
Nakiri tunahitaji katiba mpya sio tuu ili kusawazisha uwanja kwa kupata level playing ground. Bali tunahitaji katiba mpya ambalo chimbuko lake ni watu wenyewe.

Katika wana CCM- waliopo hakuna viongozi bold enough wa kudai katiba mpya from within. Japo nakiri wako wakina Prof. Harison Mwakyembe ambaye ni Mtaalamu wa katiba na anayajua wazi mapungufu ya katiba yetu tena from contutionakism poit of view hana jeuri ya kudai katiba mpya from within.

Spika Sita ni bold. Kitendo cha kumwambia rais awe mkali kidogo baada ya kulihutubia Bunge ni uthibitisho wa boldness ya baadhi ya wana CCM katika masuala ya maslahi ya taifa. Ndani ya chama its the other way round hapa ni maslahi ya chama tuendelee kutawala.

Hakuna wanaCCM watakaothubutu kudai katiba mpya kasababu ikipatikana katiba mpya. The playing ground itakuwa level. Kama playing ground itakuwa level na tayari wanajua weakness yao, they know for sure they'll be beaten on their own game,huku bado wana njaa. Chama chao majeruhi kweli nani atakubali?
Katiba iliyopo yenye sheria, taratibu na kanuni za kuifavour si ni mtaji mkubwa wa kujihakikishia unaendelea kutawala na kuendeleza ulaji?.

Mabold wa CCM kama akina Warioba, Kaduma, Butiku hawa wanaweza lakini sasa ni wazee peke yao hawawezi bila vijana na vijana kina Mwakiyembe, Anne Kilango na kina Sita ndio hao bado wananjaa wanataka kuendelea kula mpaka washibe ni leo? Hiyo CCM itamegeka leo?!. Makinda yenye kuonyesha cheche-za mabadiliko kama Nape ndiyo hayo yananyofolewa mabawa ili yasiruke, kuna kitu hapa?.

Watanzania wamechoka na CCM siku nyingi. Wanapoangalia ni chama gani wanaweza kukiamini kuikabidhi nchi, hawaoni any serious party hivyo wanaamua bora zimwi likujualo wanaishia kuichagua C[CM.

Kwa 2010 wakati ndio huu. Apatikane mpinzani mmoja tuu kama Mhe.Zitto asimame na rais Kikwete. Wapinzani wote waungane nyuma yake. Amini usiami jamaa atashinda the Obama style na CCM itapigwa chini bila hata kumeguka.

Upinzani wa Tanzania needs serious reorganization now than ever because the wind of change is sweeping accross. If not now, then when? na 2010 ndiyo hiyo!.
 
Asante MMKJJ kwa makala yako. Kuingoja CCM imeguke ni sawa na fisi anayemfuatia binadamu kwa nyuma akigoja mikono inayoning'inia ianguke kwa jinsi inavyocheza akiamini imevunjika na bado kidogo tuu itaanguka.

Hatuwezi kuingoja CCM imeguke, tunatakiwa kushiriki katika kuisababisha imeguke. We are not passive but active in setting up the eventual break up of CCM.

Nakiri tunahitaji katiba mpya sio tuu ili kusawazisha uwanja kwa kupata level playing ground. Bali tunahitaji katiba mpya ambalo chimbuko lake ni watu wenyewe.

Bado unanirudisha kule kule kwenye square one. Kama CCM haiko tayari kuwa na Katiba mpya, hitaji la Katiba mpya ambalo ni dhahiri kwa watu wengi litaendelea kuwa hivyo tu, hitaji.

Katika wana CCM- waliopo hakuna viongozi bold enough wa kudai katiba mpya from within. Japo nakiri wako wakina Prof. Harison Mwakyembe ambaye ni Mtaalamu wa katiba na anayajua wazi mapungufu ya katiba yetu tena from contutionakism poit of view hana jeuri ya kudai katiba mpya from within.

Hili ndilo kosa; hivi unafikiri kulikuwa na watu ndani ya CCM walioweza kudai Richmond na Kamati Teule? Unafikiri wale waliotokea na kudai kuwajibishwa kwa Waziri Mkuu na watumishi wengine walikuja hivi hivi; kila kitu ni mkakati. Tukitaka wabunge wa CCM wachague kilio cha Katiba mpya inawezekana.

Spika Sita ni bold. Kitendo cha kumwambia rais awe mkali kidogo baada ya kulihutubia Bunge ni uthibitisho wa boldness ya baadhi ya wana CCM katika masuala ya maslahi ya taifa. Ndani ya chama its the other way round hapa ni maslahi ya chama tuendelee kutawala.

Hapana si kweli; ndani ya CCM kuna mbegu za mabadiliko ambazo tumeshiriki kuzipanda na pole pole zinakua. Na sitoshangaa CCM inataka kufanya "mabadiliko" ya Katiba lakini watakapoleta hoja hii bungeni itageuka ni ya "Katiba mpya" mark my words..



Hakuna wanaCCM watakaothubutu kudai katiba mpya kasababu ikipatikana katiba mpya. The playing ground itakuwa level. Kama playing ground itakuwa level na tayari wanajua weakness yao, they know for sure they'll be beaten on their own game,huku bado wana njaa. Chama chao majeruhi kweli nani atakubali?

Wapo wana CCM ambao watakuwa ni wanufaikaji wa kwanza wa Katiba mpya.

Katiba iliyopo yenye sheria, taratibu na kanuni za kuifavour si ni mtaji mkubwa wa kujihakikishia unaendelea kutawala na kuendeleza ulaji?.

Hicho ndicho kizuizi kilichopo sasa hivi, na ndiyo sababu ya kuweza kushawishi wana CCM kuona picha zaidi ya manufaa ya muda ya CCM.


Mabold wa CCM kama akina Warioba, Kaduma, Butiku hawa wanaweza lakini sasa ni wazee peke yao hawawezi bila vijana na vijana kina Mwakiyembe, Anne Kilango na kina Sita ndio hao bado wananjaa wanataka kuendelea kula mpaka washibe ni leo? Hiyo CCM itamegeka leo?!. Makinda yenye kuonyesha cheche-za mabadiliko kama Nape ndiyo hayo yananyofolewa mabawa ili yasiruke, kuna kitu hapa?.

believe me, hata walioshiba nao husikia njaa; usiwe na shaka kuna kundi la CCM ambalo linasubiri kupata ile "cheche" tu ya kuwasha moto wa mabadiliko.


Watanzania wamechoka na CCM siku nyingi. Wanapoangalia ni chama gani wanaweza kukiamini kuikabidhi nchi, hawaoni any serious party hivyo wanaamua bora zimwi likujualo wanaishia kuichagua CCM.

Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa tu.

Kwa 2010 wakati ndio huu. Apatikane mpinzani mmoja tuu kama Mhe.Zitto asimame na rais Kikwete. Wapinzani wote waungane nyuma yake. Amini usiami jamaa atashinda the Obama style na CCM itapigwa chini bila hata kumeguka.

Zitto hawezi, umri haumruhusu na linapokuja suala la uongozi wa nchi sidhani kama anastahili kuwa Rais kwa wakati huu. As a matter of fact watu wafuatao (nitachambua siku moja) hawastahili kuwa viongozi wa nchi yetu kwa kadiri wataendelea kuwa walivyo sasa: Mbowe, Lipumba, Mrema, Seif, Prof. Safari, Mtikila, na Mbatia. Ubunge yes, Urais NO.


Upinzani wa Tanzania needs serious reorganization now than ever because the wind of change is sweeping accross. If not now, then when? na 2010 ndiyo hiyo!.


point nzuri sana.
 
Zitto hawezi, umri haumruhusu na linapokuja suala la uongozi wa nchi sidhani kama anastahili kuwa Rais kwa wakati huu. As a matter of fact watu wafuatao (nitachambua siku moja) hawastahili kuwa viongozi wa nchi yetu kwa kadiri wataendelea kuwa walivyo sasa: Mbowe, Lipumba, Mrema, Seif, Prof. Safari, Mtikila, na Mbatia. Ubunge yes, Urais NO.

Powerful, mimi nasubiri uchambuzi tu, siku itakapofika.
 
Nakubaliana na baadhi ya maoni humu ndani ingawa nadhani ili kujua ugumu ulioko mbele yetu ni lazima turudi nyuma kidogo. CCM iliyakubali mabadiliko kwa shingo upande baada ya kuelemewa na pressure ya nje na ndani. Kwa kutambua kuwa mfumo wa vyama vingi hauzuiliki na kwa kuepusha makali, Raisi aliunda tume ya Nyalali kukusanya maoni ya wananchi kwa ujumla wao licha ya kujua kabisa kuwa maoni ya tume pamoja na wananchi hayangeheshimiwa.

Wakati tume ya Nyalali ikizunguka nchi nzima, kulikuwa na tume nyingine chini ya Mwanasheria Mkuu nayo ikitoa mapendekezo yake kwa kuzingatia maslahi ya utawala. Mambo haya yalifanyika wakati ambapo wananchi waliishi kama watumwa na kuishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao - ama ulikuwa mwana CCM au ulitengwa na kujikuta kama mtazamaji tu ukizidi kudidimia kwenye tope la umasikini. Kama ni kijana UVCCM, mzazi jumuiya ya wazazi na mama UWT. Tulitekwa.

Waliopenda kusoma nje ama kupata nyadhifa katika nchi walitakiwa kuwa na kadi ya CCM na waliotaka kuendesha biashara kwa ufanisi bila vizingiti ilibidi wawe na kadi za CCM - hiyo ndiyo ilikuwa sera ya ndani ya CCM. Matokeo yake ilikuwa ni asilimia 80% ya wananchi kukataa vyama vingi - mwananchi gani angethubutu kuipa mgongo CCM, halafu iweje. Hata hiyo asilimia 20% ya waliotaka vyama vingi walionekana wenda wazimu na wanaohatarisha amani na utulivu iliyojengwa na CCM (sic).

Ikumbukwe ni mwaka huo ambapo Afrika ilishuhudia mauaji ya kimbari yaliyochochewa na siasa za ukabila katika nchi za Burundi na Rwanda. Propaganda za CCM zilitawala masikioni mwa Watanzania kuwa vyama vingi vingeleta machafuko na vita na hata mtaala wa somo la Uraia kwa shule za sekondari ulielezea madhara ya nchi kuwa na vyama vya upinzani. Mwaka 1994 kwenye kampeni za uchaguzi CCM ilitumia turufu hiyo hiyo ya vita endapo angechaguliwa kiongozi yeyote kutoka vyama vya upinzani.

Hiyo hiyo serikali ya CCM iliyounda tume ya Nyalali ikakubali mfumo wa vyama vingi lakini ikakataa mapendekezo yote ambayo yangetoa uwanja sawa kwa hivyo vyama kushamiri. Katiba ikarekebishwa kuruhusu vyama vingi lakini kanuni zikawekwa za kuvibana hivyo vyama na kukipendelea CCM. Kuna sheria nyingi tu ambazo tume ilipendekeza zifutwe lakini kwa ujanja ujanja na bila kuzingatia maslahi ya taifa kwa ujumla ama hazikufutwa au zilivikwa viraka tu vya kiini macho.

Wakati amri zinatungwa na Bunge la nchi kusimamia taratibu za nchi na ni lazima zifuatwe na watu waliomo humo na anayekwenda kinyume nazo hupewa adhabu na mahakama, kanuni zinatungwa na chombo kilichopewa mamlaka na Bunge ili kusimamia taratibu za mahali fulani kama vile miji na mikoa, idara za serikali na kadhalika. Ni hizi kanuni zinazoendeleza uonevu kama vile polisi kuzuia mikutano ama maandamano kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu. Ni hizi kanuni hizo hizo zinazowawezesha wezi kutembea vifua juu.

Hivi sasa tunashuhudia serikali kwa kutumia kanuni zake inavyojizatiti na kuwa tayari kupambana na wanananchi hao hao walioiweka madarakani. Angalia polisi wanavyotumiwa kulinda maslahi ya CCM huku wezi wakitanua na kuzidi kula bila kunawa. Leo hii tunawaona FFU wakitanda kwenye vyuo vikuu wakiwa na silaha za moto, mabomu ya machozi na magari yanayorusha maji ya kuwasha eti kupambana na watoto wetu wanaodai haki yao. Imefika mahali hata kibabu kinatandikwa rungu na mjukuu wake.

Pamoja na yote haya kuna mtanzania anathubutu kuitetea CCM na kusema ni viongozi wachache ndani yale ndio wabaya. Wanaopiga kelele wakiwa humo ndani ni wanafiki wa kutupwa, wote wameonja nyama ya binadamu na kama manyang'au yaliyoshiba yanacheka - hayalii. Narudia kama nilivyosema kwenye posti yangu ya nyuma tusisubiri CCM imeguke, tusikae pembeni kushuhudia inameguka na tusiiombee imeguke - tuimegue na wakati wa kuimegua ni sasa.

Tuzipigie kelele jumuiya na taasisi zote zinazokumbatia CCM - makanisa, misikiti, NGOs, wahisani, mashirika mbalimbali, mahakama kwa kukaa kimya, bunge kwa kuwageuka wananchi, jumuiya za wafanyakazi, wakulima, wafanya biashara, vijijini, mijini na popote pale. A luta contunua.
 
Mag.. nadhani vyama vingi viliruhusiwa tena mwaka 1992 kabla ya mauaji ya kimbari. Wananchi asilimia 80 walikataa mfumo wa vyama vingi. Ingawa yawezekana wengi hatutaki kukubali matokeo ya uchaguzi wa rais 2005 imeonesha asilimia 80 ya wapiga kura wakiichagua CCM any correlation?

KUna imani kuwa "watu wanaichukia CCM" hii ni imani tu haina msingi. Mapenzi ya watu kwa CCM yamekuwa kama mapenzi ya mtoto kwa mama yake. Kuna mvuto mkubwa sana wa CCM hasa kwa kizazi kilichotangulia. Wazee wengi kutokana na kile wanachoamini kuwa ni hekima hawako tayari kuona mabadiliko makubwa kama ya kuipa nchi uongozi wa chama kingine. Hawa bado ndio wapiga kura wengi zaidi na walio constant.

Wazee hawa bado wanamepenzi ya TANU na CCM na bado hawajaona sababu hasa ya kubadilika hasa wanapoona serikali inajishughulisha kidogo. Wazee hawa hawataki mabadiliko ya ghafla kwani wengine wana hofu ya pension zao, miradi yao, na maendeleo ya watoto wao.

Nakumbuka wakati nashughulikia suala la vijana kule Ukraine, mzazi mmoja alimpigia simu Rais na kumbembeleza kwa kumuita "Baba" na mzee mwengine alisema "Rais ni kama Baba yetu, atusaidie". Wakati wale vijana wakililia kilichokuwa haki yao wazee wao (baadhi) walikuwa wanaibembeleza serikali kama mtu anavyombembeleza mama mkwe!

HIvyo ukweli utabakia kuwa wazi, CCM bado inawapenzi wengi zaidi, ina mashabiki wengi zaidi na licha ya kashfa zote tunazozisikia sasa ni wanachama wa CCM ndiyo wamekuwa mara zote kimbilio la serikali.

Hivyo kuleta mabadiliko kwenye Taifa letu bila kuangalia CCM ni njozi ya Alinacha.
 
Zitto hawezi, umri haumruhusu na linapokuja suala la uongozi wa nchi sidhani kama anastahili kuwa Rais kwa wakati huu. As a matter of fact watu wafuatao (nitachambua siku moja) hawastahili kuwa viongozi wa nchi yetu kwa kadiri wataendelea kuwa walivyo sasa: Mbowe, Lipumba, Mrema, Seif, Prof. Safari, Mtikila, na Mbatia. Ubunge yes, Urais NO.

Powerful, mimi nasubiri uchambuzi tu, siku itakapofika.

Naweza pia kutoa mhitasari wa uchambuzi wangu kuhusu hili: kuna Changamoto kuu mbili zinazowakabili wote hawa.

1. Katika demokrasia iliyotukuka ukijaribu kugombea urais tena wengine sasa ni zaidi ya mara mbili na bado unashindwa au hautangazwi mshindi (haijalishi hata kama mwenzako kacheza faulo) ni vyema wakati ujao ukae pembeni kutoa nafasi kwa mtu mwingine kujaribu kuja na mkakati mpya wa ama kuzuia faulo au naye kuja na faulo babu kubwa kuliko ya mpinzani wake (yaani CCM).

2. Katika wote sijaona mtu makini, shujaa na anayejitoa (seriously) toka Januari - Desemba na kila siku popote kwa kutumia majukwaa, maandiko, mitandao na vyombo vya habari na rasilimali zake akionyesha juhudi za dhati za kuunganisha vyama vya upinzani hata kama ni kwa kuomba uwezeshwa huo kufanyika na mtu wa nje au asasi isiyofungamana na chama chochote cha siasa Tanzania na kutamka waziwazi kuwa yeye na viongozi wa chama chake yuko tayari hata kutoteuliwa kuwa wagombea endapo wananchi wataona hawafai au hawana sifa kuliko wengine.
Ninachosoma katika ndimi, nyuso na maandiko ya hawa viongozi ni kupigana vita, ni ubinafsi wa kutafuta umaarufu wa vyama vyao na sio Maendeleo ya Taifa kwanza sasa wana utofauti gani na CCM?

Baadaye wengine mnaweza kuwachambua mmoja mmoja kwa madhaifu au mapungufu makubwa waliyonayo ambayo kwayo wanakosa sifa za kuwa rais anayefaa.

Kuhusu Zito; nakubaliana na Mwanajijiji kuwa huyu mwenzetu anafaa kwa kiwango alichopo Ubunge na hata pengine kuanza na Unaibu waziri lakini si urais maana bado mchanga katika issues nzito. Ana nafasi nzuri ya kukua kisiasa na kiuongozi endapo ataendelea kusimama kwa ajili ya maslahi ya umma.
Mfano: Katika kuonyesha ukomavu na misimamo katika uongozi shupavu, binafsi nilimwondolea Zito alama fulani. Kijana alivyopigwa yellow card Mjengoni kwa kuonewa kwa kuleta mada iliyoomba utafiti ufanyike kwa manufaa ya umma. Halafu baada ya kutumikia adhabu Rais tena akamteua kuwa katika kamati (isiyo na mamlaka ya kisheria) kuchunguza kilichokuwa na uhusiano na alichopigiwa yellow card! Nadhani hekima ingekuwa kukataa kabisa na kuomba kwanza aombwe msamaha kwanza.

Swala la utoaji maamuzi ya busara ni nyeti sana kwa anayetaka kuwa Rais. Mfano, ingawa Obama alikuwa pampu kubwa katika nyanja kadhaa, wachambuzi wa siasa waliona kuwa McCain alifanya kosa kubwa sana kukubali the bailing out package for wall street kinyume na kauli na mwelekeo wake.

Nina imani na ni kweli kuwa, Tanzania haina watu kumi tu, wala watu mia tu, ambao ndio tu wenye uwezo wa kuwa rais. Cha msingi ni kuacha ubinafsi na kuungana na kukubali kuchungulia kupitia madirisha mengi kwa fikra angavu miongozi mwa mamilioni ya Watanzania nani asiye na skandali za kitaifa na anayeweza kutuongoza kwa ufanisi!
 
Nimemtaja Mhe. Zito for the sake of The Obama Style. Nakubaliana nanyi. Then the other one is Mhe. Cheyo, John Memosa. Maskandali yake ya Swaziland ni by gone.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom