CCM kumeguka ni muhimu kwa Taifa!

Jamani tusiwe vipofu ktk hoja ambayo ni muhimu..Field marshall Es kasema ukweli mtupu ambao hauhitaji maelezo mengi..
Kama CCM ni kisiki itakuwaje mtu usubiri hadi kimeguke!.. hali hiyo itatokana na kitu gani? tusubiri hali ya hewa ya ukame ama!..
Kama alivyosema kuanzishwa kwa vyama vya Upinzani kulitokana na Ulazima uliotakiwa toka nchi za nje na CCM walijenga vyombo hivi kuuhadaa Ulimwengu.. Mrema na Seif Sharrif walitoka wakiwa na uhakika na nafasi za juu zenye posho na mshiko safi kama vile wako CCM.. tatizo lilikuja tu pale tamaa za kibinadamu zilipoingia kwa hawa jamaa. Mrema aliona upenyo wa kuweza kushinda Uchaguzi, akafanya kweli nje ya makubaliano.. Seif Pia aliona upenyo wa kuchukua Uongozi Zanzibar, CCM wakabadilisha Uwakilishi ktk serikali ya Muungano...Bahati yake ni kwamba hadi leo jhii bado ni tishio kubwa kwa CCM lakini wmeshamtafutia dawa..
CCM haiwezi kumeguka kirahisi wakubwa zangu kwani kila mkulu alipo ndani ya CCM anakatiwa chake kisawasawa, huku nje hakuna nuru na wale wote waliojaribu kujimegua wamerudi wenyewe..
Wee fikira tu majuzi Kikwete amekebehi UJAMAA wakati huu ndio mwongozo wa chama chake na Imani ya chama inasema - Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru!..
Lakini la kuchekesha viongozi wote ndani ya chama walimpigia makofi na kumshangilia wakati akikitukana chama chake mwenyewe akitumia neno Upinzani..Na ajabu kubwa ni kwamba Upinzani hawakurudisha majibu.
Mkuu wangu kisiki hiki hakiwezi kuondoka bila zana maalum za kung'oa visiki na watu wenye moyo na imani kubwa isiyofungamana na woga wa Uchawi..
CCM sio tu kisiki cha mkorosho, hiki ni kisiki sawa na ule mbuyu wa St. Peters, njia panda kwenda Masaki.
Tumejenga barabara kuuzunguka, measure zetu ni kutazama kama uwezekano wa usafiri bado unawezekana bila kukiondoa kisiki hicho..

Mkuu Bob,

Heshima mbele mkuu kwa kuuona ukweli, sina la kuongeza mkuu!
 
Vyama havikuanza kwa sababu nchi fulani ilidai vianzishwe.
Kuna watu wangapi machachari walipinga mfumo wa chama kimoja tangu mika ya sabini wakabatizwa jina la wahaini wakalala mbele nje ya nchi?
Enzi zile ukibatizwa au ukiitwa muhaini umekwisha.
Akina James Mapalala walianza hii kitu mika ya 80 kabla MWalimu Nyerere hajatamka kwamba "Si dhambi kuongelea juu ya vyama vingi"
Watu walidai mfumo wa vyama vingi na nature"Time " ikatusaidia kwa sababu ilikuwa upande wetu.

Kila kitu kina Timing yake.
Museven alisubiri Rais Obotte afanye kosa la kijinga la kumuua Jenerali wake maarufu, baada ya yeye Museven kupenyeza umbeya kwamba Jenerali yule alitaka kumpindua Rais Obotte ili atawale Uganda.
Bili kuchunguza Obotte aliamua kutungua Elkopta ilo mbeba yule Jenerali na kumwua.
Ndipo Museven alipomtumia Ujumbe wa wazi Rais Obotte kwamba sasa umekwisha, umefanya kosa la kijinga la kujiharibu.

Kusubiri mvua ilegeze udongo kuzunguka kisiki chetu cha mpingo ili Majembe shoka na sepetu zifanye kazi si makosa ya kiufundi.
Siku zote ukitaka mambo yakunyookee fuata mkondo wa nature, maji siku zote yanafuata mteremko huku yakipinda pinda na kukwepa vizuizi vyote.
Hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi sana kudai katiba itakayojadiriwa na Wabunge wale wale wa CCM.

Janja ni kutafuta akina Dr Slaa na Kabwe wengi ili kujaza nguvu Bungeni.
Tumekwisha ona kwa vitendo kwamba nguvu ya wananchi hushinda Uwingi wa Fedha, Umaarufu wa kisiasa, Ubabe wa akina Tossi na Virungu vya FFU na Polisi kwa pamoja.

Kuhubiri mambo mazito kama wizi wa EPA huko Vijijini ni upuuzi wa karne.
Huko vijijini watu wanataka uwaambie namna utakavyo wamaliza maKatibu kata na makatibu tarafa wajifanyao miungu watu.
Watu wanataka waambiwe namna ya kukomesha uonevu ufanywao na serikali za vijiji na watendaji wao kupitia ofisi za CCM.
Wanavijiji hawana hamu yeyote ya kusikia sijui njemba gani huko Dar imekamatwa kwa kuiba Benki kuu??!!!
Hakuna mwananchi yeyote wa kijijini au kule Manzese kwa Mfuga mbwa anaye hisi na kujisikia kwamba fedha ya BOT ana hisa nayo.

Wakati tunasubiri mvua ilegeze kisiki ugomvi chetu cha mpingo hatulali,Bongo zetu zinachemka kutafuta agenda kali kama ya Baraka Obama ya kuamsha nyoyo za wananchi wote wa Tanzania ili wasaidie juhudi za mwisho za kuking'oa kisiki kilicholegea tayari.

CCM inajilegeza yenyewe kwa kukumbatia umalaya mwingi wa kisiasa.
Hawalegei kwa kutaka kulegea, ila ni katika juhudi za kuendeleza undava ndipo wanashitukia wanakumbatia na kujishika kwenye nyufa badala ya vigingi.
 
Vyama havikuanza kwa sababu nchi fulani ilidai vianzishwe.

Hivi vyama tulilazimishwa na wafadhili, ndio maana CCM ikapata mwanya wa kujiingiza huko, mafanikio yaliyokwisha patikana ni madogo sana kulinganisha na time iliyokwisha pita, toka Mwalimu aseme maneno yake yale mpaka leo ni miaka karibu 15, hakuna hata dalili kwamba CCM itameguka,

Kwamba ati CCM wameshalegea? I do not think so huwa wakitetereka wanajipanga upya, wanakaa chini na kutafutana uchawi na kuja na nguvu mpya, Freeman, Dr.Slaa, Zitto, Mnyika, Lisu, na Mwanakijiji hawawezi kuwashinda CCM, hivi ni wananchi gani wenye akili timamu watawapa power ya taifa hawa watu sita tu, walioko mijini?

CCM watameguka under what threat? Kushindwa jimbo la Tarime peke yake? CCM inajua kua ili kuwa sawa na wafadhili ni lazima kuwe na percent fulani ya wabunge wapinzani bungeni, kwa hiyo majimbo kama ya Zitto, Ndesamburo, na Dr. Slaaa hayataguswa, infact hata Tarime CCM ilishauriwa kutoenda lakini ubishi wa wachache ambao sasa wanatakiwa kuondolewa.

Tusingependa kukatishana tamaa, lakini pia hatuwezi kupandishana mikenge na hope zilizolegea, Obama is another story of its own haina uhusiano wowote na siasa za bongo, huko USA wananchi hawana mchezo wakikupa nafasi ukishindwa hukutoa tu kwa kura, na sio kusubiri umeguke! Sisi kura zetu hununuliwa kwa pilau!

Wakuu tuwapeni wananchi hope zenye uhai, na zinazowezekana hapa bongo, sio ndoto za alinacha, maana wananchi tumechoka sana! Tumesikia ya kutosha!
 
Jamani mawazo ya Mwanakijiji hata wengine tusioandika mara kwa mara tulisha yafikiria kwa undani na tukaandika. Nawarejesha katika moja ya thread zangu chache sana, iliyopo katika jukwaa la siasa tarehe 14 October : 10:25 yenye kichwa cha habari '2009 - kisiasa' muone nilisema nini

2009-Kisaiasa

--------------------------------------------------------------------------------

Kwa kuwa naamini kuwa; Tunaweza kutofautiana katika mitizamo ya kisiasa lakini sote ni sharti tuishi na kutumika kwa ajili ya MAendeleo ya watu na Taifa kwa ujumla.

Na kwa vile Chama chetu cha Mapinduzi kimeonekana kuwa sasa kimepoteza imani toka kwa wananchi wengi (ndani na nje ya CCM) na hatuoni dalili za kujirekebisha.

Na kwa sababu mwakani tuna muda mfupi wa mwaka kabla ya uchaguzi mkuu, basi tunapaswa kupanga sasa mkakati madhubuti usio na unafiki ili kuwapata Viongozi ambao UTII WAO UTAKUWA KWA WANANCHI KWANZA KABLA YA CHAMA WALA URAFIKI.

Sijui ninyi mnafikiria nini, mimi niko njia panda ama:-

1. Tuwashinikize kwa nguvu zote, kila siku, popote, kwa namna yeyote ya amani vyama vyote vya upinzani Tanzania (wavunje vyama vyao) waungane na tupate mgombea na mwenza wake wanaofafa na kukubalika halafu sote tuwapigie kampeni iliyoenda shule kwa ajili ya kupokea ushindi 2010.
au

2. Tunaoona kuwa CCM ya sasa imepoteza mwelekeo lakini bado tuna nafasi kuliko vyama vingine vya sasa vya upinzani, tujimegue kwa kishindo na kuunda chama tukiite mfano :- CCM-Wananchi na tuwateuwe wawili wasio na mawaa na wenye uwezo wa kuongoza tuwapigie kampeni ya kitaalamu kujiandaa kurejesha Tz katika kuelekea ustawi wa Wananchi.

Pengine wengine mna mawazo tofauti yote yanakaribishwa maana nimeona kuwa siwezi kuendelea kuugua moyoni kwa jinsi ninavyokaa kimya tu wakati nakufa na tai-mbano ya CCM shingoni.

________________
Suala la wapinzani kutotaka kuwa pamoja mpaka leo hii linaendelea kunipa wasiwasi kuwa kuna mapandikizi ndani mwake!
 
Kibunago.. asante sana kwa kutukumbusha!

Hebu angalia kinachotokea Afrika ya KUsini leo hii; Kuna mtu miaka miwili iliyopita aliyeota njozi kuwa ANC - Chama kilichoongoza harakati za ukombozi, chama cha Mandela kumeguka wakati na yeye bado yuko Hai?


S Africa's ANC loses top official
Delegates at the breakaway conference in Johannesburg
The formal launch of the new party is expected next month

The former head of communications for South Africa's ruling African National Congress (ANC) has resigned from the party to join a breakaway movement.

Smuts Ngonyama was quoted as saying he was unhappy about a recent disrespect of authority in the ANC.

The ANC split follows a bitter power struggle between party leader Jacob Zuma and former President Thabo Mbeki.

The ANC forced Mr Mbeki to step down as president in September - a move which angered some of his allies.

The ANC issued a statement saying they welcomed Mr Ngonyama's decision and wished him luck.

At a press conference on Thursday, Mr Ngonyama said he wanted to contribute to South Africa's development, and thought he could best do so by joining the new Congress of the People.

Naming problem

"I now believe that the Congress of the People is a welcomed addition to our political landscape," he said, according to the South African Press Association.


NEW PARTY NAME CHALLENGE
1: South African National Congress, challenged by ANC as too similar to its name
2: South African Democratic Congress, already registered by another party
3: Congress of the People, refers to an event when the ANC's Freedom Charter was signed

How the ANC came to split

"We have the opportunity to ensure that the dream of non-racialism, non-sexism, and a united, prosperous South Africa remains within our reach."

Observers expect a number of other senior ANC members to resign ahead of the launch of the breakaway party, scheduled for December.

The party's registration has been delayed because the name it had initially chosen, the South African National Congress, was challenged by the ANC, while the second choice name - the South African Democratic Congress - had already been taken.

The ANC says it intends to oppose the group's third choice, as the Congress of the People refers to an event when the Freedom Charter - a document considered the cornerstone to the way the ANC governs - was signed in 1955.

"If they register their name with the IEC [Independent Electoral Commission], that's when the opposition will start," ANC spokesperson Ishmael Mnisi said.

The new party is led by former Defence Minister Mosiuoa Lekota and the former premier of Gauteng Province, Mbazima Shilowa.
 
The ANC split follows a bitter power struggle between party leader Jacob Zuma and former President Thabo Mbeki.

The ANC forced Mr Mbeki to step down as president in September - a move which angered some of his allies.

Hapa ndipo hoja yangu ya katiba inapoingia, Mbeki hakuwa na power ya ajabu kama ya rais wetu, alipothibitishwa na mahakama kwamba anahusika na kuchochea kesi against Zuma, hakuwa na jinsi ila kuwajibika. Sasa hapa the big picture imetengenezwa na small details ambazo wabongo kwa kawaida huwa hatuzijali sana na matokeo yake huwa tunashindwa kujenga picha kubwa, nani hapa bongo anaweza kuwa na power struggle na rais wetu mwenye nguvu za ajabu? Ni nani anaweza kuwa na ubavu wa kugombea uenyekiti wa CCM taifa na kumshinda the sitting rais wetu wa Jamhuri?

Labda kuna something nina-miss!
 
Jamani tusiwe vipofu ktk hoja ambayo ni muhimu..Field marshall Es kasema ukweli mtupu ambao hauhitaji maelezo mengi..
Kama CCM ni kisiki itakuwaje mtu usubiri hadi kimeguke!.. hali hiyo itatokana na kitu gani? tusubiri hali ya hewa ya ukame ama!..
Kama alivyosema kuanzishwa kwa vyama vya Upinzani kulitokana na Ulazima uliotakiwa toka nchi za nje na CCM walijenga vyombo hivi kuuhadaa Ulimwengu.. Mrema na Seif Sharrif walitoka wakiwa na uhakika na nafasi za juu zenye posho na mshiko safi kama vile wako CCM.. tatizo lilikuja tu pale tamaa za kibinadamu zilipoingia kwa hawa jamaa. Mrema aliona upenyo wa kuweza kushinda Uchaguzi, akafanya kweli nje ya makubaliano.. Seif Pia aliona upenyo wa kuchukua Uongozi Zanzibar, CCM wakabadilisha Uwakilishi ktk serikali ya Muungano...Bahati yake ni kwamba hadi leo jhii bado ni tishio kubwa kwa CCM lakini wmeshamtafutia dawa..
CCM haiwezi kumeguka kirahisi wakubwa zangu kwani kila mkulu alipo ndani ya CCM anakatiwa chake kisawasawa, huku nje hakuna nuru na wale wote waliojaribu kujimegua wamerudi wenyewe..
Wee fikira tu majuzi Kikwete amekebehi UJAMAA wakati huu ndio mwongozo wa chama chake na Imani ya chama inasema - Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru!..
Lakini la kuchekesha viongozi wote ndani ya chama walimpigia makofi na kumshangilia wakati akikitukana chama chake mwenyewe akitumia neno Upinzani..Na ajabu kubwa ni kwamba Upinzani hawakurudisha majibu.
Mkuu wangu kisiki hiki hakiwezi kuondoka bila zana maalum za kung'oa visiki na watu wenye moyo na imani kubwa isiyofungamana na woga wa Uchawi..
CCM sio tu kisiki cha mkorosho, hiki ni kisiki sawa na ule mbuyu wa St. Peters, njia panda kwenda Masaki.
Tumejenga barabara kuuzunguka, measure zetu ni kutazama kama uwezekano wa usafiri bado unawezekana bila kukiondoa kisiki hicho..
Mkandara,
Narudia tena nukuu yangu. CCM ni kapu lililokwishafumka kwenye makalio yake. Ushahidi tosha ni hiyo kauli ya mheshimiwa kupigiwa makofi aliposema kufuata ujamaa ni uchizi. Unawezaje kutukana misingi iliyofukisha hapo ulipo? Unawezaje kukiuka dira iliyokufikisha hapo ulipo halafu udhani kuwa unaweza kusalimika kama chombo cha kuongoza dola? Yote hayo yanayopigiwa makofi ni dalili za kufumka kwa kapu lakini wale waliomo ndani yake hawalioni hilo. Ndio maana ukikemea ufisadi unaonekana adui. Tunaweza kudhani kuwa kisiki hakiondoki njiani lakini kumbe kisiki chenyewe kimeshaoza ndani. Ni kazi tu ya kukipiga teke na kitapotelea pembeni. Ukiangalia mkondo wa historia utakubali kuwa kutokuwa na dira ni dalili tosha kwamba CCM imeshafikia ukingo wake na it is just a matter of time. Tarime was the beginning, sasa hivi Musoma mambo ni moto kwa CCM. Time is not on CCM's side, believe me!
 
Nilipotoa tamko kuwa CCM ni adui wa Maendeleo ya Tanzania na Watanzania, sikuwa nimekosea wala kupungukiwa kitu. Huo ni ukweli muutake au musiutake!

Kama kuna kitu ambacho Mwanakijiji kakieleza vizuri ni hiki hapa

Hilo ndilo linalohitajika kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi. Hata hivyo haliwezi kutokea hadi pale baadhia ya "vigogo" wa chama hicho hasa wakongwe au wale ambao wamejikuta wakiwekwa pembeni kutokana na misimamo yao watakapoamua kujitoa ndani ya chama hicho na kuanzisha chama kingine. Hili litawezekana tu pale ambapo wakongwe walioko CCM watakapotambua mioyoni mwao kuwa CCM siyo mama yao. Pale watakapotambua kuwa wanaweza wasife wana CCM lakini watakufa wakiwa ni Watanzania!

Sasa hivi heshima kubwa ambayo baadhi yao wanayo (kama alivyosema Mzee Kawawa miaka ile) ni kuhakikisha kuwa wanakufa wakiwa wana CCM pia. Wengine kati yao wameapa kabisa kuwa liwalo na liwe wao ni "wana CCM mpaka kufa". Nakumbuka wengine wetu tuliimba nyimbo za "naapa naahidi mbele ya Chama, Mapinduzi nitakulinda mpaka kufa". Lakini ahadi hiyo ni ya uongo kwani utii na mapenzi yetu kama raia wa taifa letu hayawezi kamwe kuwa kwa mtu, idara, taasisi au chama cha kisiasa. Mapenzi na utii wetu wa kwanza na wajuu zaidi ukiondoa ule ulioko kwa muumba wetu ni kwa nchi yetu.

Wazo hili litakapoingia ndani ya viongozi wa CCM hasa wale ambao kweli wanaamini mabadiliko yanahitajika haitawachukua muda kuamua kujitoa ndani ya CCM na kuanza harakati za kuleta mabadiliko ya kweli.

Hapa tunarudi tena kwenye ile ibara maarufi ya CCM, ibara ya 15.1 ambayo inatamka wazi kuwa wajibu wa mwanaCCM ni kwa CCM kwanza na wala si kwa Taifa.

Sasa nikimsoma FMES na kauli yake kuwa kamwe ndani ya CCM hakutatokea mvutano au kumeguka kama Madela alivyotupa tafsiri sanifu ya kumeguka na kumegwa, natatizwa na hoja ya FMES kusema kuwa msukumo pekee wa kuleta mabadiliko ya Katiba utatoka kwa Wananchi ambao wengi wao kwa ridhaa, unyonge au mazoea wamejisalimisha haki zao kwa kuipa nguvu CCM.

Labda nimkumbushe FMES mambo mawili matatu ili atambue kuwa msukumo kutoka nje ya CCM pekee kudai katiba hautoshi.

Mchungaji Mtikila katika kesi yake ya kutaka kuwepo kwa mgombea huru, alipata ushindi mahakamani ambao umesema kuwa mgombea binafsi na huru wa chama ni haki ya kila Mtanzania. Sasa ili kauli ya mahakama iwe sheria kwa jinsi katiba ya Tanzania ilivyojengwa, ni lazima Bunge lipitishe muswaada wa kubadilisha katiba na kuweka kifungu hicho. Ni nani mwenye kura nyingi ndani ya Bunge? ni CCM. Na pale wana CCM wengine watakapojifanya a Joe Lieberman, kuvuka mstari na kwenda upande mwingine, vikao maalumu vya kichama hufanyika na vitisho hufanywa hapo kwa papo kisha kura zote kwa sauti moja husema CCM!

Lakini bahati mbaya ya Watanzania ni kunukuu kauli za viongozi kadhaa wa Tanzania ambao si mara moja au mbili wametoa kauli kusema kuwa CCM ina dhamana na uamuzi wa mwisho. Kama hilo halijatosha ni kauli zinazosema kuwa kama CCM haioni jambo lolote kuwa ni tatizo na hasa kuhusiana na katiba, basi CCM kama chama tawala hakioni ulazima au umuhimu wa Katiba kubadilishwa kwa kuwa kina madaraka na Katiba ni safi kabisa kwa Tanzania kwa mujibu wa CCM.

Kauli hii ya Serikali ambayo ilitolewa ndani ya Bunge kwenye bunge mwaka jana ilitolewa na Mama Mary Nagu ambaye alisema kuwa katiba ni safi kabisa.

Labda nijinukuu mazungumzo ambayo nimeyafanya pembeni ya JF baada ya kuandika ile thread ya Azimio Jipya. Nimekukwa na mawasiliano na ndugu kadhaa (Yohana wa Mnyika akiwamo) kulizungumzia suala hili la kudai katiba mpya na ukweli ni kuwa nimekuja kugundua kwa sikuwa pekee yangu.

Peter Maina, Issa Shivji, Robert Kisanga, Joseph Warioba, Barnabas Samatta, Francis Nyalali, Sefu Hamad, Ibrahim Lipumba, Tanganyika Law Society, Law Reform of Tanzania na watu wengine wengi wamekuwa kwenye huu mchakato wa kuzungumzia Katiba mpya, lakini kizingiti kimekuwa ni CCM na ugumu wa CCM kukubali kuwa kuna haja ya kuunda katiba mpya kwa ajili ya manufaa ya Tanzania na Watanzania na si CCM na Wana CCM.

Najinukuu nilichoandika mwezi wa March 2008

Sun, Mar 2, 2008 at 7:58 PM
subjectKatiba Project
mailed-bygmail.com
hide details Mar 2 Reply

Wapendwa,

Miezi miwili na nusu iliyopita, nilikuwa na mazungumzo marefu na XXXXX kuhusiana na Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mazungumzo yetu yalikuwa ni kufuatilia mchakato wa gumzo la pale kijiweni na ombi rasmi la XXXX kuwa pamoja na kuwa yupo siriasi na kazi yake, lakini suala la Katiba tumuite.

XXXXX na mimi tulipitia majina ya wachache ambao tulionelea kuwa wanaweza kuwa "siriasi" kwenye huu mradi na hivyo tukakubaliana tufanye mawasiliano na kuanza gumzo.

Naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kuandika na kukutanisha kama nilivyoombwa na XXXXX kufuatilia ujenzi wa kikundi hiki ambacho ni huru wa kufungamana na vyama vya siasa na lengo lake kuu ni kuujenga Utaifa na kumpa mwananchi wa Tanzania haki na uhuru wa kweli.

XXXXX utaniwia radhi kwa kujivutavuta kwangu kutuma waraka huu kwa hawa ndugu kuhusiana na hili. Lakini nafikiri kujivutavuta kwangu kumesadia kutupa picha na msukumo mpya au wa ziada katika kuanza harakati hizi za kutafiti ni njia gani zinabidi kufanyika na ni ushirikiano wa namna gani tutafute ili kuleta msukumo wa kuleta mabadiliko ya Katiba yetu ambayo hayajafanyika tangu vipengele vya mwisho kubadilishwa mwaka 1984 na kufuatiliwa na viraka mara kwa mara.

Najua tumekuwa na mazungumzo hapa na pale miaka nenda rudi kuhusiana na Katiba ya Tanzania . Nafikiri ni wakati muafaka kuanza kuweka mawazo yetu na kutafuta wataalamu wa kisheria ili kuleta msukumo huru usio ambatana na chama cha siasa kuhakikisha kuwa Katiba ya Taifa letu la Tanzania ni kwa faida ya mtanzania na si chama chenye madaraka au kikundi kidogo ambacho hiushia kujitwalia nguvu na mamlaka ya dola na kiserikali.

Aidha dhumuni lingine ni kuhakikisha kuwa Katiba ya Tanzania inabainisha kwa dhati mihimili mikuu ya Serikali (Executive, Legislative and Judicial) kwa kuzipa nguvu za kisheria kuwajibishana na kutoa haki na usawa.

Matukio makubwa mawili ambayo ni ya ziada kutoa nguvu ya kudai Katiba mpya ni yale ya kuanguka na kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na Muafaka wa Kenya uliofikiwa majuzi.

Mtagundua kuwa katika suala la Waziri Mkuu na kuvunjwa kwa baraza la mawaziri, uundwaji mpya umetumia watu ambao ni wabunge na hivyo kuondoa fursa ya watu ambao si Wabunge ambao ni wataalamu wa mambo mbali mbali kama uchumi, fedha, biashara na menginewe kukosa kuwekwa katika nafasi hizo nyeti kutokana na mapungufu ya Katiba.

Yaliyotokea Kenya ni somo. Mkumbuke kuwa kutokana na tafurani na vurugu zilizotokea, kumesukuma kufanyika mabadiliko ya lazima ya Kikatiba ambayo yamehitimika kwa Raila na Kibaki kutia sahihi makubaliano ya Muafaka kuunda Serikali ya Mseto.

Hivyo basi naomba wote mpokee waraka huu kama kianzio cha mazungumzo na wale ambao watakuwa tayari kuendelea na harakati nawaseme hivyo. Wale ambao hawatakuwa na muda au nia ya kushiriki, pia tutaomba mseme hivyo ili kazi ya kubadilishana mawazo na harakati zianze.

Matumaini yetu mimi na XXXXX ni kutumia msukumo katika jamii yetu kudai Katiba mpya. Kazi hii si ndogo au nyepesi na katika kujivutavuta kwangu nimebaini kuwa wengi wamejaribu kufanya hivyo kuanzia vyama vya upinzani, taasisi za haki na sheria na wananchi wa kawaida.

CCM kupitia Serikali yake, imetangaza rasmi kuwa Katiba ni safi kabisa, lakini hata aliyekuwa Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu Joseph Warioba ametamka hivi kaibuni kuwa kuna haja ya kuundwa kwa Katiba mpya na si kuendelea kuweka viraka.

Basi naomba tukae tutafakari na tuanze mdahalo na mchakato wa kuweza kufanya kazi hii.

Sasa utaona kuwa katika harakati zetu, nasi tumekumbana nahali halisi na tumekuwa kama fisi tukiotea mkono uanguke maana kuunyofoa pekee ni mgumu, hivyo kurudia maneno ya Madela wa Madilu ni kuwa kazi ya kuibomoa CCM na hata kuleta katiba mpya haitatokana na nguvu za nje pekee bali ni hata mfukuto wa ndani mithili ya Volcano.

Upinzani na hata sisi wananchi, tulichokosea awali ni kuamini kuwa CCM wangekuwa ni watu wenye Utu na kufuata Haki na hivyo kujenga mandhari sawa ya kuleta maendeleo ya Taifa. Ulipoanza Upinzani, iwe ni kwa hiyari yetu wenyewe au kwa mashinikizo, hakuna aliyetegemea kuwa CCM ingekuwa na undumilakuwili wa hali ya juu kiasi hicho. Labda tulichosahau ni ile tabia ya kuwa kigeugeu tuliyoiona kwa lile kundi la G-55 ambalo lilipewa baraka na Mzee Malecela na kisha wakaja mgeuka baada ya kutikiswa na maswali kutoka kwa Mwalimu Nyerere na hivyo kumuachia Mzee Malecela na Kolimba laana ya kuandikiwa kitabu.

Sasa kujua kuwa CCM inafanya mambo kwa manufaa yake na uimara wake pekee ni jinsi gani kila jambo linaloihusu CCM linavyofanyiwa kazi kupatiwa ufumbuzi. Jiulize ni vipi Somaiya anatoa pesa mfukoni kugharamia kamkutano ka UVCCM kufanya uchaguzi kama si kuwa CCM ina wenyewe na ina lindwa na Ufisadi na Uharamia?

Lakini Wanafunzi kuomba mikopo inakuwa nongwa, wastaafu kudai haki yao wanafanywa wehu na wahaini, wagonjwa kuhitaji dawa wanaachwa wanaangamia, wafanyakazi na waalimu wanadai mishahara ili kukidhi ukali wa maisha wanapewa vitisho na kukebehiwa.

Mkandara kadai kuwa wengine wanaogopa kuisakama CCM kwa kupoteza pensheni, kwani penshini si inatoka Serikalini na si CCM, hivyo kikija chama Kingine hiyo Pensheni bado ipo na hata kama ndani ya CCM kutameguka, mafao na pensheni bado yapo!

Ni uoga, unyonge na mara nyingine uzandiki kama si unyenyekevu wa kitumwa ambao baadhi ya Wana CCM wanaogopa kusimama kidete na kuvuruga chama na mshikamano wake wa kinafiki. Hivi vijikauli vya Kingunge kutishia watu au ule woga eti watakwisha kisiasa una maana gani na nguvu gani kwa watu kama Mzee Msuya, Salim, Billali, Malecela, Kafanabo, Mang'ula, Warioba, Seleli, Mwakyembe, Killango, Manyanya, na wengine wengi ambao tunajua kwa kweli wamechoka kudhihakiwa na kunyanyaswa na chama walichokitolea kiapo cha maisha?

Hivi leo unataka niambia na ni kweli unathibitisha kuwa CCM ina nguvu na wana CCM ambao wanajiita wanamageuzi, wanashindwa kuweka kiapo chao na utii wao kwanza kwa Taifa na katiba na kukimbilia kuinyenyekea CCM, imani, ahadi na upuuzi wake?

Sisi wote tumetoka na kuchipuliwa kisiasa na CCM. Wengine wetu pamoja na kuipenda kwa yale iliyoyafanya kale, imefika wakati imetubidi tuwe wakweli na tuweke maslahi ya Taifa mbele na si ya CCM au marafiki wa CCM.

Tunachotaka ni wale ambao wako ndani ya CCM kuanza kukimegua chama huku sisi nasi tukiweka nguvu kukimega na kukimomonyoa bila kuogopa nguvu za madaraka ya Rais ambaye sasa hata kama ndani ya Chama watasema hatumtaki, kuna uwezekano akatumia mabavu.

Labda kilichotokea Zanzibar 2000, Rwanda 1994 na kinachoendelea Congo kwa miaka 10 kinabidi kitokee Tanzania ili tuweze kusonga mbele maana sikio la kufa CCM halisikii dawa na njia pekee ni kulikatilia mbali.

Uchungu na damu ya Wananchi itakapomwagika, ndipo pale Watanzania kwa ujumla tutakapoamka na kukitokomeza CCM. Sawa na yale mawe ya kule Chunya au Wazee Wastaafu waliolala barabarani kudai hakio zao, tunawataka wale wanaojiita CCM mageuzi, waanze kurusha mawe bila woga au aibu na wagalegale barabarani.
 
Kusubiri CCM imeguke siyo strategy. Ni majaaliwa. Kitakachofuata baada ya CCM kumeguka kama tunavyo wish hakitakuwa kizuri. CCM inaweza kung'olewa mchana kweupe!!! Tunahitaji vitu viwili tu; Watu wenye nguvu na Strong organization.

Strategy yetu iwe ni kutafuta na ku-recruit watu imara na kujenga organization. CCM is no longer an organization. Ni kundi la watu wanaounganishwa na kitu kimoja tuuu! Maslahi. Hivi ni maajabu gani yaliyotokea huko Kigoma (Kigoma yote inaweza kwenda kwa wapinzani ikiwa watajenga organization - angalia historia ya voting Kigoma kaskazini, Kigoma kusini na Kigoma mjini), huko Tarime, Pemba, Moshi, n.k. Kwa nini hatuwezi kukirudia hicho cha tarime huko DSM, Mwanza, Mbeya, etc? Tatizo ni organization.

Chukua mfano wa Kigoma! Kigoma kaskazini sasa hivi ni Chadema, Kigoma kusini ilishachukukliwa na upinzani. Kigoma mjini hali kadhalika. Na chaguzi zote ukiangalia voting pattern utagundua upinzani unatakiwa ushinde. Lakini uimara wa organization za upinzani bado ni tatizo kubwa, let's face it. Kaburu was the hope, na kama angeendelea no moto alioanza nao (kabla ya kununuliwa), Kigoma yoote (mkoa mzima) leo ingekuwa upinzani. Tuanzie hapo! Sasa hivi majimbo kama kasulu magharibi already ni low hanging fruit kwa upinzani. Kina zito wangejichimbia katika kujenga organization strong, 2010 Kigoma kuna viti vinne vya upinzani visivyokuwa na shida kabisa kuvipata. Tunahitaji kuwa na wagombea wenye mvuto na wanaokubalika kama kina Zitto na hiyo inatakiwa iwe kazi namba moja.

Wapo wanaosema nguvu ya CCM iko vijijini. Hilo nalipinga. Udhaifu wa vyama vyote leo uko vijijini. Hivi ni metropolitan gani ambapo upinzani umeshinda?? Wananchi wa vijijini wanaonekana kuwa stupid loyalists wa CCM. Lakini vile vile tukumbuke hawa wa vijijini ndo wepesi zaidi kuwabadilisha. Mjini ndo vimejazana vikundi maslahi na watu kibao wanaonufaika na cheotic situation iliyopo leo. Hao hawatataka mabadiliko. Mijini wamejaa ma middle class wa Tanzania wanaofanya kazi kwenye ma NGOs ya Kimataifa, Makampuni makubwa ya kimataifa, Mashirika ya serikali yaliyobaki na ndani ya serikali yenyewe. Hao si waleta mabadiliko.

Mabadiliko yataanzia kwa wakulima vijijini na huko nikuhakikishie CCM imebaki kihistoria tuuu! CCM ni mti ambao mizizi yake huko vijijini imeshaliwa na mchwa. Tatizo ni nani yuko tayari kuchimba huko chini??

Turecruit watu (Zitto, slaa, Mbowe, Lissu, n.k. bado hawatoshi!) halafu tujenge organizations (CCM is no longer an organization). CCM itaanguka yenyewe!!!
 
KipimaPembe,

Nguvu za giza za CCM ni kali mno, huyu Kaburu, Hiza, Lamwai, Kasyupa na wenginewe hata kina Mrema, Lipumba, Mbowe, Mtikila na Makaidi, hawawezi kusimama kidete kama hawatapata usaidizi ndani ya CCM.

Kitu inaitwa ulua ndio inaua wengi, angalia wanavyoandamana kupewa cheki za mugawo wa chama, wakikosa kwa kuambiwa hazina haina pesa, vyama hivi vitakufa kifo cha mende!
 
Hatuwezi kusubiri CCM imeguke, bali tunashiriki kuhakikisha inamegukaa yenyewe kwa kuimomonyoa kidogo kidogo.

Kwa wane wanaokumbuka mchezo wa "kula mbakishie baba" utakumbuka jinsi watoto wakiwa wamezunguka hiki kijiti kilichosimikwa katikati ya rundo la mchanga. Lengo ni kuchukua mchanga kidogo kidogo hadi mtu yule ya mwisho atakayesababisha kile kijiti kianguke.

Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anachukua mchanga kidogo na kupunguza kinga ya kijiti. Lakini kijiti kitakapoangua kinaanguka kwa sababu ya kuelemewa na uzito wake kwa sababu ya mvuto wa asili wa dunia (gravitational force). Lakini pia huwezi kuelezea kuanguka huko bila kuelezea kilichofanywa na watoto kuangusha.

Hivyo haitoshi kusubiri passively CCM eti imeguka huo utakuwa ni mkakati mbovu; bali ni kushiriki katika kuhakikisha kuwa inameguka kwa kila mtu kutumia nguvu zake, vipaji vyake na uwezo wake to chip out kile ambacho CCM inasimamia ili hatimaye ianguke kutokana na kuelemewa na uzito wake.

Kuanguka kwa CCM kutatokea naturally lakini kutalamishwa na matukio kadhaa.
 
Hatuwezi kusubiri CCM imeguke, bali tunashiriki kuhakikisha inamegukaa yenyewe kwa kuimomonyoa kidogo kidogo.

Kwa wane wanaokumbuka mchezo wa "kula mbakishie baba" utakumbuka jinsi watoto wakiwa wamezunguka hiki kijiti kilichosimikwa katikati ya rundo la mchanga. Lengo ni kuchukua mchanga kidogo kidogo hadi mtu yule ya mwisho atakayesababisha kile kijiti kianguke.

Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anachukua mchanga kidogo na kupunguza kinga ya kijiti. Lakini kijiti kitakapoangua kinaanguka kwa sababu ya kuelemewa na uzito wake kwa sababu ya mvuto wa asili wa dunia (gravitational force). Lakini pia huwezi kuelezea kuanguka huko bila kuelezea kilichofanywa na watoto kuangusha.

Hivyo haitoshi kusubiri passively CCM eti imeguka huo utakuwa ni mkakati mbovu; bali ni kushiriki katika kuhakikisha kuwa inameguka kwa kila mtu kutumia nguvu zake, vipaji vyake na uwezo wake to chip out kile ambacho CCM inasimamia ili hatimaye ianguke kutokana na kuelemewa na uzito wake.

Kuanguka kwa CCM kutatokea naturally lakini kutalamishwa na matukio kadhaa.


hii kali ya leo, tufundishane kujenga na sio kubomoa. Kama kuiondoa sisiemu madarakani muwashawishi wananchi waiondoe kwani ndio walioiweka. Kila mmoja kuimomonyoa kwa nafasi yake huo si uh*i*i fulani hivi? Tunasambaza mchanga na sisiemu itadondoka wakati na nchi ikiwa imepoteza mengi, kwani ukisambaza mchanga wakati wa kurudisha haurudi wote. Itakuwa ndio mchezo, na CHADEMA nayo itaondolewa kwa mchezo huo huo.
 
Hatuwezi kusubiri CCM imeguke, bali tunashiriki kuhakikisha inamegukaa yenyewe kwa kuimomonyoa kidogo kidogo.

Kwa wane wanaokumbuka mchezo wa "kula mbakishie baba" utakumbuka jinsi watoto wakiwa wamezunguka hiki kijiti kilichosimikwa katikati ya rundo la mchanga. Lengo ni kuchukua mchanga kidogo kidogo hadi mtu yule ya mwisho atakayesababisha kile kijiti kianguke.

Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anachukua mchanga kidogo na kupunguza kinga ya kijiti. Lakini kijiti kitakapoangua kinaanguka kwa sababu ya kuelemewa na uzito wake kwa sababu ya mvuto wa asili wa dunia (gravitational force). Lakini pia huwezi kuelezea kuanguka huko bila kuelezea kilichofanywa na watoto kuangusha.

Hivyo haitoshi kusubiri passively CCM eti imeguka huo utakuwa ni mkakati mbovu; bali ni kushiriki katika kuhakikisha kuwa inameguka kwa kila mtu kutumia nguvu zake, vipaji vyake na uwezo wake to chip out kile ambacho CCM inasimamia ili hatimaye ianguke kutokana na kuelemewa na uzito wake.

Kuanguka kwa CCM kutatokea naturally lakini kutalamishwa na matukio kadhaa.

I support MKJJ

Do you know that Mwakyembe, Kilango, Malecela, Pinda are as deadly wafisadi as Rostam EL, JK, etc???

Could you start another thread to deeply discuss abou these people whom many Tanzanian thinks are innocent while in real case they are not! They are not after people, they are not for interest of Country! they are acting as dimlights, sometimes they are angry s'time there as quite as Lady Jay Dee!

Brother you may understand what I mean, we should starts as many threads as we can to discuss personals in CCM.

I can not start threads no one will repsond, I have only 1thank and 6 posts you know old is gold!

Englisher

''English is not our mother land!''
 
hii kali ya leo, tufundishane kujenga na sio kubomoa. Kama kuiondoa sisiemu madarakani muwahsawishi wananchi waiondoe kwani ndio walioiweka hao. Kila mmoja kuimomonyoa kwa nafasi yake huo si uh*i*i? fulani hivi. Tunasambaza mchanga na sisiemu itadondoka wakati na nchi ikiwa imepoteza mengi, kwani ukisambaza mchanga wakati wa kurudisha haurudi wote. Itakuwa ndio mchezo, na CHADEMA nayo itaondolewa kwa mchezo huo huo.

mama hii ndiyo inaitwa siasa! ukielewa siasa utaona kuwa kumomonyoa na kukidhoofisha chama kingine ni sehemu ya mkakati wa ushindi. siasa haiko katika kujenga chama bali kukidhoofisha ili upate nafasi ya kujenga nchi. CCM ni chama cha siasa na kudhoofishwa ni sehemu yake.

Wao CCM wanaelewa dhana hii vizuri ndio maana hawajengi vyama vya upinzani au kuvifanya vikomake, wanachofanya ni kuvidhoofisha. Mkakati huo ukitumiwa dhidi ya CCM unang'aka na kuuita uh uni ? Ama kweli ashakum si matusi.
 
mama hii ndiyo inaitwa siasa! ukielewa siasa utaona kuwa kumomonyoa na kukidhoofisha chama kingine ni sehemu ya mkakati wa ushindi. siasa haiko katika kujenga chama bali kukidhoofisha ili upate nafasi ya kujenga nchi. CCM ni chama cha siasa na kudhoofishwa ni sehemu yake.

Wao CCM wanaelewa dhana hii vizuri ndio maana hawajengi vyama vya upinzani au kuvifanya vikomake, wanachofanya ni kuvidhoofisha. Mkakati huo ukitumiwa dhidi ya CCM unang'aka na kuuita uh uni ? Ama kweli ashakum si matusi.


Si afadhali ungekuwa uhuni! ni uh*i*i. Ndio maana sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, kwa sababu ua ush***i wa the so called siasa za Tanzania.

Ningekupa shavu kama ungesema upinzani uzistrengthen sera aka polisi zake ili kuzidhoofisha za sisiemu. Hii ya kusema kila mtu alipo afanye awezalo kuimomonyoa sisiemu ni uh*i*i.

Kwa mfano kwa mpango huu tumtegemee daktari afanye nini ili kuimomonyoa sisiemu? nesi na mwalimu je?
 
Si afadhali ungekuwa uhuni! ni uh*i*i. Ndio maana sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, kwa sababu ua ush***i wa the so called siasa za Tanzania.

Ningekupa shavu kama ungesema upinzani uzistrengthen sera aka polisi zake ili kuzidhoofisha za sisiemu. Hii ya kusema kila mtu alipo afanye awezalo kuimomonyoa sisiemu ni uh*i*i.

Kwa mfano kwa mpango huu tumtegemee daktari afanye nini ili kuimomonyoa sisiemu? nesi na mwalimu je?

sitaingia huko kwa kuita majina hivyo (nimeanza kuona kawaida ya aina fulani hivi). Kama kila mmoja atasubiri mtu mwingine amuambie jinsi gani ashiriki basi itakuwa ni kazi.

NI nani anawafunza siafu kuleta chakula kwenye ghala yao? Au ni nani huwafundishwa mbwa mwitu kuwinda kwa makundi? Kuna vitu vingine unahitaji kujijua wewe ni nani na nafasi yako ni nini. SIyo wote wataweza kuwa lead dogs, si wote watakuwa siafu askari na si wote watakuwa malkia.. lakini kila mmoja katika nafasi yake atashiriki.

La maana ni kuanza kujiuliza "katika mabadiliko ninayoyataka katika nchi yangu, mimi nina nafasi na jukumu gani katika kuyaleta mabadiliko hayo?". Jibu la swali hilo linaweza kumuongoza mtu kujua ni nini anatakiwa kufanya.
 
sitaingia huko kwa kuita majina hivyo (nimeanza kuona kawaida ya aina fulani hivi). Kama kila mmoja atasubiri mtu mwingine amuambie jinsi gani ashiriki basi itakuwa ni kazi.

NI nani anawafunza siafu kuleta chakula kwenye ghala yao? Au ni nani huwafundishwa mbwa mwitu kuwinda kwa makundi? Kuna vitu vingine unahitaji kujijua wewe ni nani na nafasi yako ni nini. SIyo wote wataweza kuwa lead dogs, si wote watakuwa siafu askari na si wote watakuwa malkia.. lakini kila mmoja katika nafasi yake atashiriki.

La maana ni kuanza kujiuliza "katika mabadiliko ninayoyataka katika nchi yangu, mimi nina nafasi na jukumu gani katika kuyaleta mabadiliko hayo?". Jibu la swali hilo linaweza kumuongoza mtu kujua ni nini anatakiwa kufanya.

Jukumu la kupiga kura na kuchagua kiongozi anayeonekana anaweza leta mabadiliko chanya (kupiga hatua kwendea maendeleo) kwa watanzania kiuchumi, kiasiasa na kijamii kwa ujumla.

Sishawishiki wala sitashawishi kumomonyoa kwani ni kujenga tabia inayoweza momonyoa hata familia pale panapokea tofauti kati ya baba na mama. Siasa za kumomonyoa si siasa, ni sawa na kufitinisha ili kushinda. Ubaya wa kufitinisha ni kuwa utakurudi na kuna siku na wewe watakufitini. Kwa hiyo ni vyema kutafuta sustainable way kuliko huko mumomonyoa. Chadema wameanza na operation Sangara.
 
1.
natatizwa na hoja ya FMES kusema kuwa msukumo pekee wa kuleta mabadiliko ya Katiba utatoka kwa Wananchi ambao wengi wao kwa ridhaa, unyonge au mazoea wamejisalimisha haki zao kwa kuipa nguvu CCM. Labda nimkumbushe FMES mambo mawili matatu ili atambue kuwa msukumo kutoka nje ya CCM pekee kudai katiba hautoshi.

- Rev msukumo kutoka kwa wananchi unapoaswa kua the final resort ya kubadili anything katika taifa, ikifikia mahali ukawa hautoshi basi the nation is either politically dead au ina wananchi waliokufa kisiasa, meaning kwamba hawaelewi chochote as far as siasa ya taifa lao is concerned, na sitaki kuamini kwamba Tanzania tumefikia huku tayari.

- Kuna mifano michache sana ipo ambayo iko wazi kwamba wananchi wakiamua katiba itabadilika, kwa mfano wananchi hawakutaka wabunge wajiongeze marupurupu, hii ishu ikakwama bungeni na haijasemwa tena, Richimonduli, na hii juzi ya EPA, kama sio kilio cha wananchi haya yasingefanyika, lakini inawezekana hata wananchi hawaelewi kwamba ni shinikizo lao ndio limefanikisha.

2.
Mchungaji Mtikila katika kesi yake ya kutaka kuwepo kwa mgombea huru, alipata ushindi mahakamani ambao umesema kuwa mgombea binafsi na huru wa chama ni haki ya kila Mtanzania. Sasa ili kauli ya mahakama iwe sheria kwa jinsi katiba ya Tanzania ilivyojengwa, ni lazima Bunge lipitishe muswaada wa kubadilisha katiba na kuweka kifungu hicho. Ni nani mwenye kura nyingi ndani ya Bunge? ni CCM. Na pale wana CCM wengine watakapojifanya a Joe Lieberman, kuvuka mstari na kwenda upande mwingine, vikao maalumu vya kichama hufanyika na vitisho hufanywa hapo kwa papo kisha kura zote kwa sauti moja husema CCM!

- Again inakuja pale pale tu kwenye nguvu ya wananchi, bunge lililompiga chini Lowassa na wenzake ni hili hili la CCM, na wabunge walisimama kidete knowing wanawawakilisha wananchi ambao wengi a walikuwa wanaunga mkono msimamo wao, na hili lilikuwa linathibitishwa na our media ambao walikuwa mbele sana na kelele!

- Kabla ya kuwatosa kina Lowassa, kilifanyika kikao maalum cha wabunge wa CCM, ambapo Makamba alijaribu sana kuwatisha wabunge waikatae ripoti, guess what? wabunge walimjia juu Makamba na kumtaka akae pembeni, he did kwa sababu hawezi kushindana na nguvu ya wananchi, inayowakilishwa na wabunge. I mean I understand your concern, lakini yakuogopana yalishapitwa na wakati,

3.
Lakini bahati mbaya ya Watanzania ni kunukuu kauli za viongozi kadhaa wa Tanzania ambao si mara moja au mbili wametoa kauli kusema kuwa CCM ina dhamana na uamuzi wa mwisho. Kama hilo halijatosha ni kauli zinazosema kuwa kama CCM haioni jambo lolote kuwa ni tatizo na hasa kuhusiana na katiba, basi CCM kama chama tawala hakioni ulazima au umuhimu wa Katiba kubadilishwa kwa kuwa kina madaraka na Katiba ni safi kabisa kwa Tanzania kwa mujibu wa CCM. Kauli hii ya Serikali ambayo ilitolewa ndani ya Bunge kwenye bunge mwaka jana ilitolewa na Mama Mary Nagu ambaye alisema kuwa katiba ni safi kabisa.

- Again, Hosea alisema amechunguza Richimonduli na kuona hakuna tatizo, and then what happened next? Nagu can say anything she wants, serikali na CCM wanaweza kusema anything they want, lakini one thing hawawezi kushindana na nguvu ya wananchi, iliyokusanywa pamoja na uongozi imara wa upinzani, Mkuu unajua Chiluba by the time anamtoa Kaunda kwenye power alikuwa ameshalala jela mara nyingi sana, matokeo yake ni kwamba alikuwa na nguvu ya wananchi karibu wote nyuma yake, ni nguvu ya wananchi tu ndiyo inayoweza kuibadili katiba, au anything katika taifa, ikishondwa basi hakuna hope tena!

4.
Labda nijinukuu mazungumzo ambayo nimeyafanya pembeni ya JF baada ya kuandika ile thread ya Azimio Jipya. Nimekukwa na mawasiliano na ndugu kadhaa (Yohana wa Mnyika akiwamo) kulizungumzia suala hili la kudai katiba mpya na ukweli ni kuwa nimekuja kugundua kwa sikuwa pekee yangu.Peter Maina, Issa Shivji, Robert Kisanga, Joseph Warioba, Barnabas Samatta, Francis Nyalali, Sefu Hamad, Ibrahim Lipumba, Tanganyika Law Society, Law Reform of Tanzania na watu wengine wengi wamekuwa kwenye huu mchakato wa kuzungumzia Katiba mpya, lakini kizingiti kimekuwa ni CCM na ugumu wa CCM kukubali kuwa kuna haja ya kuunda katiba mpya kwa ajili ya manufaa ya Tanzania na Watanzania na si CCM na Wana CCM.

- Kati ya hawa wote uliowataja mkuu, kwangu ni mmoja tu angalau anaweza kuwa na credibility na wananchi, naye ni Shivji tu, sasa CCM itakubali vipi kurekebishwa na watu wake, ambao wwamekula na kushiba wakiwa ndani ya CCM, hawakuona umuhimu wa kubadili katiba, lakini baada ya kutupwa nje ndio wameona umuhimu, unajua things like this sometimes hata viongozi wa CCM hujichekea tu!

I mean kuacha Shivji tu, nani mwingine hapo anaweza kuwa anwakilisha mawazo ya wananchi wengi wa Tanzania?
 
1.
Sasa utaona kuwa katika harakati zetu, nasi tumekumbana nahali halisi na tumekuwa kama fisi tukiotea mkono uanguke maana kuunyofoa pekee ni mgumu, hivyo kurudia maneno ya Madela wa Madilu ni kuwa kazi ya kuibomoa CCM na hata kuleta katiba mpya haitatokana na nguvu za nje pekee bali ni hata mfukuto wa ndani mithili ya Volcano. Upinzani na hata sisi wananchi, tulichokosea awali ni kuamini kuwa CCM wangekuwa ni watu wenye Utu na kufuata Haki na hivyo kujenga mandhari sawa ya kuleta maendeleo ya Taifa. Ulipoanza Upinzani, iwe ni kwa hiyari yetu wenyewe au kwa mashinikizo, hakuna aliyetegemea kuwa CCM ingekuwa na undumilakuwili wa hali ya juu kiasi hicho. Labda tulichosahau ni ile tabia ya kuwa kigeugeu tuliyoiona kwa lile kundi la G-55 ambalo lilipewa baraka na Mzee Malecela na kisha wakaja mgeuka baada ya kutikiswa na maswali kutoka kwa Mwalimu Nyerere na hivyo kumuachia Mzee Malecela na Kolimba laana ya kuandikiwa kitabu.

- Hapa tupo ukurasa mmoja kwa sababu udhaifu wetu wananchi umeuweka wazi kabisa na ndio ukweli wenyewe, ahsante for this!

2.
Sasa kujua kuwa CCM inafanya mambo kwa manufaa yake na uimara wake pekee ni jinsi gani kila jambo linaloihusu CCM linavyofanyiwa kazi kupatiwa ufumbuzi. Jiulize ni vipi Somaiya anatoa pesa mfukoni kugharamia kamkutano ka UVCCM kufanya uchaguzi kama si kuwa CCM ina wenyewe na ina lindwa na Ufisadi na Uharamia?

- CCM sio chama cha charity au kusaidia vilema, ni chama cha siasa chenye nia moja tu nayo ni kukaa kwenye power milele, sasa kuacha matatizo ya hapa na pale, ukweli ni kwamba kwenye hilo lengo as chama cha siasa they are doing a good work, kuweza kurudi kwenye power for the last 45 years,

- Off course, inaeleweka sana kuhusu matatizo ya uongozi ndani ya CCM, lakini kama wanarudi kwenye power kila uchaguzi, ni vigumu sana kwao kujirekebisha. Hili la Somaiya, bado nashindwa kulielewa vizuri exactly what is the fuss, is it kwamba chama cha siasa Tanzania kikipewa msaada na mzungu inakua sawa lakini sio kupewa na Wahindi, or what, maana ninaamini kwamba vyama vyote nchini vinapewa misaaada na wafadhili mbali mbali, wazungu, Wahindi, na Wazawa pia, au kwa sababu huyu Mhindi ni a proven mhalifu?

3.
Lakini Wanafunzi kuomba mikopo inakuwa nongwa, wastaafu kudai haki yao wanafanywa wehu na wahaini, wagonjwa kuhitaji dawa wanaachwa wanaangamia, wafanyakazi na waalimu wanadai mishahara ili kukidhi ukali wa maisha wanapewa vitisho na kukebehiwa.

- Hapa tupo ukurasa mmoja, haya ni mapungufu ya uongozi wa CCM, sasa yalitalkiwa kutuunganisha wananchi ili kudai mabadiliko, lakini gues what? wananchi wengi tunaamini kuwa hayatuhusu, lakini ukweli ni kwamba kuna siku yatatukuta na sisi, au wanaotuhusu!

4.
Mkandara kadai kuwa wengine wanaogopa kuisakama CCM kwa kupoteza pensheni, kwani penshini si inatoka Serikalini na si CCM, hivyo kikija chama Kingine hiyo Pensheni bado ipo na hata kama ndani ya CCM kutameguka, mafao na pensheni bado yapo! Ni uoga, unyonge na mara nyingine uzandiki kama si unyenyekevu wa kitumwa ambao baadhi ya Wana CCM wanaogopa kusimama kidete na kuvuruga chama na mshikamano wake wa kinafiki. Hivi vijikauli vya Kingunge kutishia watu au ule woga eti watakwisha kisiasa una maana gani na nguvu gani kwa watu kama Mzee Msuya, Salim, Billali, Malecela, Kafanabo, Mang'ula, Warioba, Seleli, Mwakyembe, Killango, Manyanya, na wengine wengi ambao tunajua kwa kweli wamechoka kudhihakiwa na kunyanyaswa na chama walichokitolea kiapo cha maisha?Hivi leo unataka niambia na ni kweli unathibitisha kuwa CCM ina nguvu na wana CCM ambao wanajiita wanamageuzi, wanashindwa kuweka kiapo chao na utii wao kwanza kwa Taifa na katiba na kukimbilia kuinyenyekea CCM, imani, ahadi na upuuzi wake?

- Haya maneno ni makali sana na ukweli ni karibu na matusi, kwa sababu kumbuka hata wewe kule nyuma umekubali kwamba haya unayoyasema hapa kwa ukali ndio pia matatizo yetu wananchi wa kawaida hata mkashindwa kufanya anything serious as of makubaliano yenu kuhusu kulilia mabadiliko ya katiba,

- Tanzania ni taifa letu sisi wananchi, kama kuwajibika ni wajibu wetu sisi wananchi sio hao viongozi, hatuwezi kuwasukumizia mzigo wengine wakati tatizo ni letu wananchi, kwenye hili mkuu hapana, ni sisi wananchi ndio tunaotakwia kujipanga na kutafuta njia ya kuleta mabadiliko, lakini hatuwezi kutupia mpira wengine, wewe mwenyewe umesema kule nyuma kuhusu G-55, jinsi mwishoni walivyobaki Malecela na Kolimba, wengine wote wamekimbia, sasa kweli unaamini kuwa hawa viongozi wengine unaowashambulia hapa hawakuuona huo mfano?

5.
Sisi wote tumetoka na kuchipuliwa kisiasa na CCM. Wengine wetu pamoja na kuipenda kwa yale iliyoyafanya kale, imefika wakati imetubidi tuwe wakweli na tuweke maslahi ya Taifa mbele na si ya CCM au marafiki wa CCM. Tunachotaka ni wale ambao wako ndani ya CCM kuanza kukimegua chama huku sisi nasi tukiweka nguvu kukimega na kukimomonyoa bila kuogopa nguvu za madaraka ya Rais ambaye sasa hata kama ndani ya Chama watasema hatumtaki, kuna uwezekano akatumia mabavu.

- Rev sina uhakika kama hii ni lugha ya kumshawishi yoyote aliyeko huko ndani ya CCM kutikia wito wa kuimegua CCM, maneno yako mengi hapa yana ukweli flani, lakini ni makali mno mkuu mpaka yanatisha, lakini bado in reality mazingara yetu bongo kisiasa na kisheria, hayakubaliani kabisa na huu ukweli wako, kwamba walioko ndani waanze kuimegua CCM kwa sababu ya shinikizo la walioko nje, kwa maoni yangu bado Tanzania hatujafikia huko!

6.
Labda kilichotokea Zanzibar 2000, Rwanda 1994 na kinachoendelea Congo kwa miaka 10 kinabidi kitokee Tanzania ili tuweze kusonga mbele maana sikio la kufa CCM halisikii dawa na njia pekee ni kulikatilia mbali.
Uchungu na damu ya Wananchi itakapomwagika, ndipo pale Watanzania kwa ujumla tutakapoamka na kukitokomeza CCM. Sawa na yale mawe ya kule Chunya au Wazee Wastaafu waliolala barabarani kudai hakio zao, tunawataka wale wanaojiita CCM mageuzi, waanze kurusha mawe bila woga au aibu na wagalegale barabarani.

- Ya kumwaga damu sina uhakika nayo na binafsi nisingependa kwenda huko, lakini kama ni ya kulilia mabadiliko ya taifa ni lazima yaanzie na sisi wananchi, kwenye hilo hatuwezi kukwepa our responsibility as wananchi, siamini kwamba kuna mmoja kule ndani anatakwia kuanza kwanza halafu wengine ndio tufuatie, nafikiri unaijua vizuri historia za uhuru au mabadiliko ya wkeli kwa wananchi, sina uhakika kama yaliwahi kuanzia ndani.

Mkuu Rev, great darasa lakini punguza ukali kidogo, maneno ni makali sana, otherwise ninaamini kwamba ni muhimu sisi wananchi wenyewe ndio tukabeba mzigo wa kudai mabadiliko, kuliko kutegemea wachache huko ndani ya CCM!, au kuwakaripia CCM wameguke kwa sababu yetu wananchi tuliowachagua na kuwaweka kwenye power for the last 45 years, huu ni mzigo wetu wananchi wa Tanzania, tena wote sio mzigo wa anybody else.

Ahsante!
 
Mjadala unaenda vizuri:

a. CCM inaweza kuanguka kutokana na migongano na mikinzano ya ndani yake (internal conflicts and contradictions). Hili linatokea pale ambapo Chama kinakuwa ndani yake kinamigongano ambayo haiwezi kupatanishwa. Hili ndilo limetokea ANC.

Kwa Tanzania nafasi ambayo ilikuwepo kwa CCM kuwa na mgongano huu ilikuwa ni kwenye suala la Richmond. Mjadala uliotokea kufuatia ripoti ya Kamati Teule uliashiria ufa katika Chama, ufa ambao ulikuwa unaelekea kukigawa chama. Ndani ya Bunge kulikuwa na pande mbili zilizokuwa dhahiri ambazo kwa wote tunaofahamu zilikuwa zimechukua aidha upande wa Lowassa au upande wa Mwakyembe. Naamini upande wa Lowassa walikuwa ni CCM loyalists na upande wa Mwakyembe ni wale kina reformers.

Tatizo lao hata hivyo ni kuwa wale wa Lowassa walikuwa na nguvu kwenye chama (as a whole) na wale wa Mwakyembe walikuwa na nguvu Bungeni tu (ambako wangeweza kusema chochote bila kupata adhabu yoyote).

Kama Lowassa angeamua kujitoa CCM nina uhakika kabisa angepata wafuasi wengi kweli kutoka CCM; Upande mwingine kama Mwakyembe, Selelii, Mama Kilango n.k nao wangeamua kujitoa wangepata wafuasi wengi zaidi kwa wananchi.

Hata hivyo pande zote hizo zingesubiri sana kuona JK anakuwa upande gani. Sentiments zake baada ya Lowassa kuzira Uwaziri Mkuu inaonekana JK angekuwa upande wa EL kwani alikuwa more sympathetic kwake kuliko kwa kina Mwakyembe.

b. CCM inaweza kumeguka kutokana na nguvu zilizo nje yake (outside forces). Nguvu hizi kimsingi nakubaliana na FMES zaidi kuwa zitatokana na shinikizo la wananchi kufuatilia jambo moja kubwa nalo ni mabadiliko ya Katiba. Tatizo hapa ni kuwa CCM tayari imeamua kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba mwakani na hivyo kumeza kabisa hoja ya Katiba mpya.

Kwa kuteka hoja ya mabadiliko ya Katiba (nasema "kuteka" kwa sababu mara kadhaa sasa serikali imetoa tamko rasmi kuwa hakuna haja ya mabadiliko ya katiba kwani iliyopo inajitosheleza) CCM inajitengenezea uwanja wa kushinda kwa urahisi na hivyo hata wapinzani wakisema "tunataka Katiba Mpya" CCM inasema hakuna haja "tayari tunaifanyia mabadiliko katika mswada wa "mabadiliko ya 22 ya Katiba" na wale wenye mapendekezo wayatoe kwa wizara ya Katiba na Sheria."

Hivyo, hoja ya mabadiliko ya Katiba haiendi popote kwani ni hoja ambayo CCM wameshajua kuwa itawatengenezea ujiko mkubwa zaidi kuliko mambo ya ufisadi. HIvyo kama kuna nguvu nje ya CCM basi siamini kuwa zitatokana na mjadala wa Katiba, CCM is too smart for that.

c. CCM itaweza kuangushwa kwa namna ya (a) endapo Wabunge wakereketwa na watetezi wataamua once and for all kufuatilia kashfa ya Meremeta, Deep Green, Mwananchi, Twin Towers, BoT forgotten funds etc. Wabunge wa CCM ambao hawajui nini kinaendelea watakapoingia na kuanza kufuatilia hili na baadaye kuja na ripoti nzito itakuwa ni uthibitisho wa ufisadi wa CCM kama chama na siyo kama mtu mmoja mmoja.

Endapo itaoneshwa pasipo shaka kuwa Chama cha Mapinduzi kilitumia nafasi yake ya kuongoza serikali kujichotea mabilioni ya shilingi kwa shughuli zake za kisiasa basi hilolitawapa viongozi wakongwe na wengine wa CCM uamuzi kama "it is worth to save the ship or to jump out and find another way to sail". CCM hapa itameguka kutokana na kuzidiwa/kuelemewa na kashfa zisizoisha. Kuna watu watachoka na CCM kama ilivyo na naaamini kati ya watu hao watakuwa ni vigogo (hapa simaanishi katibu wa CCM wa Wilaya ni watu ambao aidha wamewahi kuwa mawaziri au wabunge au viongozi wa kitaifa wa chama- hiyo ndiyo definition yangu ya kigogo)

d. Lakini pia CCM inaweza kulazimishwa kumeguka nje ya madaraka. Baada ya kushindwa viti vingi vya Ubunge na kujikuta nje ya madaraka CCM inaweza kujikuta ikilazimika kujigawa ili kuwa na kile ambacho naweza kusema ni "CCM Asili" na CCM - Mabadiliko" (Kibunago alilisema hili pia).

Katika hili sheria na Katiba zinabakia vile vile kinachotokea ni wananchi wanaamua kufanya walichofanya Wamarekani nacho ni kuhakikisha kuwa chama tawala hakirudi na wabunge wake jinsi walivyo. Msingi wa hili hata hivyo ni uelewa wa wananchi.

Katika mazingira ya sasa ambapo radio huru bado hazijaenea ni vigumu sana kuwafikia wananchi wengi na kuwapandikizia hoja ya mabadiliko. Bado Tanzania tunategemea sana radio kama chombo cha awali cha kupashiana habarri. Lakini hili peke yake halitoshi kuleta mabadiliko kwani ingekuwa hivyo miji mikubwa ndiyo ingekuwa na wapinzani wengi kama ilivyo nchi nyingine (Nairobi na Harare ni mifano ya miji ya wapinzani).

Katika kesi ya Tanzania naamini mabadiliko yetu yatatokea vijijini (hence the name) na siyo mijini. Mtu anayefikiri kuwa Tanzania itabadilika toka mijini kwenda vijijini hajaielewa vizuri historia ya Tanzania. Mara zote siasa za Tanzania zimeanzia vijijini/nje ya miji mikubwa (angalia historia ya wanasiasa wa Tabora, Mwanza, Songea, Nyasa huko n.k). Bado vijijini ndiko mabadiliko ya kisiasa ya kuisambaratisha CCM yataanzia. Hili lina sababu yake (sitajaribu kuichambua leo).

Vyovyote vile ilivyo hata hivyo, kama kweli tunataka Taifa letu lianze mwendo mpya na mwelekeo mpya kuelekea mafanikio ya kweli, uhuru wa dhati na nafasi sawa kwa watu kufanikiwa CCM ni lazima kitoke madarakani. Na kutoka huko kuje kwa namna yoyote ile ni bora lakini la msingi ni kuhakikisha kuwa CCM haipewi Urais na Bunge kwa wakati mmoja. Katika kufikia lengo hilo nafasi ya vyama vingine vya kisiasa haiwezi kupuuziwa, nafasi ya taasisi za kiraia haiwezi kupuuziwa, na kwa hakika nafasi ya wananchi wenyewe kuleta mabadiliko hayo haiwezi kupuuziwa.

Ushahidi wa kuimomonyoa ndiyo unaonekana kwani kuna mambo ambayo CCM isingeweza kuyafanya kama ingekuwa ni miaka michache iilyopita. Sasa hivi CCM na watawala wetu wanajua kabisa kuwa hawawezi tena kutawala kwa amri au vitisho kwani wananchi hawakubali kirahisi rahisi.
 
Back
Top Bottom