CCM kulichukulia hatua gazeti lililo chapisha habari za kupotosha umma

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
ktk taarifa ya habari ya TBC ya saa mbili usiku,NAPE amesema kuwa chama cha mapinduzi ccm kitalichukulia hatua gazeti linalochapishwa kila siku hapa Tz kwa kuandika habari za kupotosha umma na kutumia nyaraka ambazo ni siri na bado hazijafanyiwa kazi na chama.
amesema kuwa gazeti hilo limeandika habari yenye kichwa cha habari CCM KUWAFUKUZA WAZEE KTK CHAMA

jamani hata mie siijui ni gazeti gani hilo
 
Nape!!!gazeti la mtanzania linamnyima usingizi!!!Magamba yamegoma vulika sasa hasira amehamishia kwenye magazeti
 
Amelitaja Gazeti la Mtanzania, alikua hana haja ya kutangaza hio, ningemwona wa maana zaidi kama ningesikia taarifa yake ikisema ameshalichukulia hatua za kisheria, ingesaundi zaidi ya kutishia kwanza. Sasa kama hatachukua hatua hapo baadae, habari hiyo itakuwa na maana gani?..............................
 
ktk taarifa ya habari ya TBC ya saa mbili usiku,NAPE amesema kuwa chama cha mapinduzi ccm kitalichukulia hatua gazeti linalochapishwa kila siku hapa Tz kwa kuandika habari za kupotosha umma na kutumia nyaraka ambazo ni siri na bado hazijafanyiwa kazi na chama.
amesema kuwa gazeti hilo limeandika habari yenye kichwa cha habari CCM KUWAFUKUZA WAZEE KTK CHAMA

jamani hata mie siijui ni gazeti gani hilo

Kaazi kweli kweli!

Sasa kama Gazeti lina Barua hiyo, hata kama imeandikwa kwamba ni SIRI, kosa ni la nani?

May be niulize swali, hivi kuna sheria ambayo inazuwia kusoma siri za chama/kampuni/organization? Mimi nilijua siri ni za serikali tu kwa kuwa zinaweza kuhatarisha usalama wa nchi. Wana sheria naomba msaada!
 
ktk taarifa ya habari ya TBC ya saa mbili usiku,NAPE amesema kuwa chama cha mapinduzi ccm kitalichukulia hatua gazeti linalochapishwa kila siku hapa Tz kwa kuandika habari za kupotosha umma na kutumia nyaraka ambazo ni siri na bado hazijafanyiwa kazi na chama.
amesema kuwa gazeti hilo limeandika habari yenye kichwa cha habari CCM KUWAFUKUZA WAZEE KTK CHAMA

jamani hata mie siijui ni gazeti gani hilo

Hilo ni gazeti "Mtanzania" la Rostam Azizi ambalo liko chini ya "Msomali" Bashe!
 
sasa hasira zinahamia ktk magazeti,ngoja tuone

Ongeza na hasira za kupigwa stop asiende Igunga kwenye kampeni na ilihali fisadi Rostam akiombwa aende kuwapa shavu! Ndo ajabu ya mafisadi, wanapiga vita ufisadi, fisadi anajivua gamba halafu huyo huyo fisadi anayechafua chama anaombwa akasaidie kufanya kampeni huku wale ambao wanaitwa wapiganaji wakiambiwa wasiende!
 
kule aliambiwa atavuruga chama
maana wanaelewa kuwa ni mvurugaji,hivi kama sio mvurugani kwanini walimzuia asiende Igunga?
 
Gamba limewashinda wanatafuta kuhamisha attention ya watu wasiwaulize mambo ya magamba
 
Back
Top Bottom