Elections 2010 CCM Kuilalamikia Chadema NEC

Basi kama ni suala ya kuanza kampeni kabla ya muda, CUF pekee ndo watabaki kwenye uchaguzi, kwa hiyo kama ni haki kutendeka basi tubakishe CUF wapigiwe kura za ndio ay hapana kuunda serikali.

Cha msingi CCM walikimbia kabla ya filimbi wakati hakuna pumzi la kutosha safari hii. Hivyo acha waendelee wanaume kufanya mambo.
 
Chadema Tulikuwa tunamwosha Mwalimu tu. Naona Wanataka kuficha suti. CCM ninyi tumieni tu hiyo NEC. Msije kufanya kosa mnalotaka kulifanya mwaka huu hapakaliki. Unapofanya dhuluma sana kunasiku inafika mwisho unaowadhulumu wanachoka wanaamua kuchukua sheria mikononi kama wananchi wanavyofanya kwa vibaka.

Twendeni kwenye kampeni, acheni kulalamika kama hamnazo. Shughulikieni matatizo yenu ya Rushwa na wizi. Dr. W. P. Slaa ni Raisi hata mmbane Vipi. Mlibana sana kwa Maalimu Seif mwaka huu mnaachia, ila Huku bara tunazoa mwaka huu. Jiandaeni kuwa wapinzani muonje joto ya Virungu vya Polisi. Mtalia sana kwa sheria kandamizi mlizoziweka wenyewe.
 
Labda ni kueleze sina sababu ya kuleta za kuleta maana hata sizijui hizo za kuleta. Mwishoni nimesema two wrongs......Lakini pia CCM wanaweza kuwa na hoja kuwa wao walikuwa kwenye mkutano wao wa KICHAMA ambao unahusisha wanachama wa chama husika na ridhaa alikuwa akiiomba ndani ya CHAMA. Lakini hili la Slaa ni kwamba ridhaa inaombwa kwa Watanzania. Ingawa kiuhalisia ni vigumu kuwaomba wananchi udhamini bila kuwaeleza utawafanyia nini, lakini wakati wa kuomba udhamini huo unaweza kuwa umepitiliza kwenye kampeni kama utagusia CHAMA kingine. Its abit technical lakini hili lisitufanye viziwi kuwa hatutambui uwepo na mamlaka ya Taasisi zetu. Maana kama hatutaheshimu taasisi zilizopo kisheria basi kwa vyovyote vile malengo yetu pia yanakuwa ni yenye mashaka.

Mkutano wa kichama uliishia kwenye ukumbi. Watu wanahoji, alipoenda Uwanja wa Jamhuri pale Dodoma alienda kuhutubia wana CCM ama wananchi? Agenda pia haikuwa kuomba ridhaa, bali walisema wanamtambulisha mgombea Urais na mgombea mwenza.

Baada ya hapo safari ikaendelea kwenda Unguja ambako Karume alidai kuwatambulisha Dr. Shein na Dr. Bilal.

Hivyo vyote havikuwa vikao vya chama, ilikuwa ni mikutano ya hadhara na wala si kuomba ridhaa ya wanachama, maana chama kilishawateua tayari.
 
Sasa ngoma inogile, vikonngwe vimeshikwa pabaya, kisu kimefika kwenye mfupa. Sasa CCM wameshachanganyikiwa. Hii ni dalili nzuri saaana ya mwanzo wa mwisho wa chama cha majambazi.
 
Sasa ndio wakati ule wakati ambao CCM wanatakiwa kutambua kuwa hawana hati miliki ya nchi hii na kwamba mgombea wao kuanza kampeni mapema ni halali bali kwa wengine ni haramu.

Tatizo kubwa la CCM ni kuwa kumbukumbu zao ni ndogo sana na hawana kiongozi wa kuweza hata kukumbuka kuwa mgombea wao alianza kampeni hata kabla ya Dr. slaa. Kwa wao kulalamika ni njia mojawapo ya kumuumbua mgombea wao mwenyewe. poor guys
 
You nailed it bro. it is all about entitlement ndiyo kinachowasumbua CCM.
 
Katika taarifa ya habari ya TBC1 saa mbili usiku huu, makamu mwenyekiti wa CCM bara Pius Msekwa amenukuliwa akisema kwamba Chadema wameanza kampeni kabla ya muda.

Kutokana na hilo, katibu wa CCM taifa, Yusufu Makamba atapeleka malalamiko yao huko tume ya taifa ya uchaguzi, yaani NEC.

Mambo yameanza. Ngoma inogile.

Kinachowapa CCM "hedeki" ni kuwa, wakati Rais Slaa "akila" vichwa lukuki viwanjani, wao wanamalizana kwa RUSHWA kwenye "kula" za maoni!
 
Ni kosa na aibu sana kwa mkubwa kulia mbele ya watoto wanachokifanya sasa Kina Makamba na Msekwa ni kuwakatisha tamaa hata wanachama wao, kama viongozi hawajiamini wafuasi watakuwaje.

Zile tambo za Makamba kusema hawamuogopi Slaa hatuzisikii zinaanza kwisha polepole kinyume chake wanaanza kulialia ha ha ha haaaa.
 
HIvi wamesahau hotuba ya JK baada ya kuchukua fomu toka NEC wiki iliyopita... ? wamesahau kauli zake kuwa "kama mkituchagua".. au tuwawekee na video kuwakumbushia.. au ndiyo yale ya "kunya anye kuku, akinya bata...."
 
Katika taarifa ya habari ya TBC1 saa mbili usiku huu, makamu mwenyekiti wa CCM bara Pius Msekwa amenukuliwa akisema kwamba Chadema wameanza kampeni kabla ya muda.

Kutokana na hilo, katibu wa CCM taifa, Yusufu Makamba atapeleka malalamiko yao huko tume ya taifa ya uchaguzi, yaani NEC.

Mambo yameanza. Ngoma inogile.
Kwa maoni yangu, huu ni msimamo binafsi wa Mzee wetu, Yusuph Makamba, uwezo wake wa kufikiri, unajulikana wazi, kwa kifupi ni mropokaji tuu japo kwa mijubu wa wadhifa wake, baadhi ya kauli zake zinaweza kuchukuliwa kuwa ni kauli za chama.

CCM kama chama, hakiwezi kulalamikia hili la kampeni za mapema kwa vile kwenye hili, CCM ndiye kinara. Mji wote wa Dodoma, umepambwa kwa matangazo ya CCM, Chakua Kikwete, nikamuuliza kiongozi mmoja wa CCM, mbona mambo yameanza mapema?, akanijibu, matangazo hayo, yamewekwa na watu baki tuu wenye mapenzi mema na CCM, na sio CCM kama chama. Hata yale mabango makubwa yanayosimamaga over head accross Nyerere Rd kumbe pia ni ya wasamaria tuu wenye mapenzi mema.
 
Katika taarifa ya habari ya TBC1 saa mbili usiku huu, makamu mwenyekiti wa CCM bara Pius Msekwa amenukuliwa akisema kwamba Chadema wameanza kampeni kabla ya muda.

Kutokana na hilo, katibu wa CCM taifa, Yusufu Makamba atapeleka malalamiko yao huko tume ya taifa ya uchaguzi, yaani NEC.

Mambo yameanza. Ngoma inogile.
yaani uko right kabisa tusubiri tuone mabo yatakuwaje mwezi novemba
 
Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa NEC awe makini tu. Jana alijibu vizuri kwamba hana wala hajapokea malalamiko yoyote juu ya hilo. Akasema wazi kwamba wao kama Tume shughuli rasmi wanazianza baada ya tarehe 19 mwezi huu.
Sielewi ni kwanini JK amewaweka wale wazee wawili wahafidhina Msekwa na Makamba kwenye nafasi zile nyeti za CCM!!
 
Labda ni kueleze sina sababu ya kuleta za kuleta maana hata sizijui hizo za kuleta. Mwishoni nimesema two wrongs......Lakini pia CCM wanaweza kuwa na hoja kuwa wao walikuwa kwenye mkutano wao wa KICHAMA ambao unahusisha wanachama wa chama husika na ridhaa alikuwa akiiomba ndani ya CHAMA. Lakini hili la Slaa ni kwamba ridhaa inaombwa kwa Watanzania. Ingawa kiuhalisia ni vigumu kuwaomba wananchi udhamini bila kuwaeleza utawafanyia nini, lakini wakati wa kuomba udhamini huo unaweza kuwa umepitiliza kwenye kampeni kama utagusia CHAMA kingine. Its abit technical lakini hili lisitufanye viziwi kuwa hatutambui uwepo na mamlaka ya Taasisi zetu. Maana kama hatutaheshimu taasisi zilizopo kisheria basi kwa vyovyote vile malengo yetu pia yanakuwa ni yenye mashaka.

Kama hiyo ndiyo maana ya kampeni basi Chadema wameanza miaka mitano iliyopita. Nani asiyekumbuka operation sangara, je ilikuwa kampeni ama si kampeni? Tusianze kubabaika hapa. CCM wamefanya kampeni yao kwenye mikutano ya chama ndani ya ukumbi, lakini ikatangazwa na TV station zote, lengo ni nini kama si kuwafikia watanzania wote? Chadema wamefanya mikutano yao ya chama kwa kuwaita wanachama na wapenzi wao kwenye viwanja vya wazi, shida iko wapi? Kampeni ni pale NEC itakaposema GO! Tuache mchecheto, kama sasa tu ccm mnalalamika sasa Chadema wakifika vijijini itakuwaje? Leo wamepatikana.
 
Hili ni tatizo lazima tuliseme. CCM km wamefanya kampeni ni kosa na haimaanishi basi na CHADEMA wafanye. Kuna sheria na suala la msingi ni kuangalia sheria zinasemaje? Ukweli kinachofanyika ni kampeni. Mf km wafanyakazi nipeni kura zenu, kina mama nk. Dr Slaa sio wa kwanza kuomba wadhamini lakini style inayotumika ni kampeni. Kwahiyo km CCM wamelalamika, kwanini CHADEMA hawakulalamika??? Ni vyema kama kuna sheria sote tujifunze kuishi kwa sheria maana two wrongs...

hebu toka hapa na wewe..usitie watu hasira
 
Mkutano wa kichama uliishia kwenye ukumbi. Watu wanahoji, alipoenda Uwanja wa Jamhuri pale Dodoma alienda kuhutubia wana CCM ama wananchi? Agenda pia haikuwa kuomba ridhaa, bali walisema wanamtambulisha mgombea Urais na mgombea mwenza.

Baada ya hapo safari ikaendelea kwenda Unguja ambako Karume alidai kuwatambulisha Dr. Shein na Dr. Bilal.

Hivyo vyote havikuwa vikao vya chama, ilikuwa ni mikutano ya hadhara na wala si kuomba ridhaa ya wanachama, maana chama kilishawateua tayari.

Kaka usiwafundishe zaidi, waache waende NEC kushitaki. Huko ndiyo watakuwa wanajimaliza zaidi - sisi wananchi tushaamua mabadiliko na haturudi nyuma. Wenye akili CCM washajua kuwa upepo ushabadilisha uelekeo.
 
HIvi wamesahau hotuba ya JK baada ya kuchukua fomu toka NEC wiki iliyopita... ? wamesahau kauli zake kuwa "kama mkituchagua".. au tuwawekee na video kuwakumbushia.. au ndiyo yale ya "kunya anye kuku, akinya bata...."
tuwekee hiyo video tafadhali
 
Chama Cha Mapinduzi chawabana watendaji wakuu wa mawizara na taasisi za serikali kuelezea mafanikio ya Serikali ya CCM wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi Oktoba 2010.
Pichani Katibu mkuu wizara ya maji na umwagiliaji Christopher Sayi (katikati) akielezea juu ya utekelezaji wa malengo ya wizara yake DSM ktk kipindi cha Miaka Mitano Iliyopita ya Serikali ya Awamu ya Nne Agosti 2, 2010. Wengine ktk picha ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mbogo Futakamba (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka Y a Majisafi na Majitaka DSm (DAWASA) Archard Mutalemwa kushoto katika picha.
Naona CCM wana mikakati kila kona 'kupiga kampeni kabla ya kipindi rasmi cha kuanza kampeni za uchaguzi', ikiwemo kuwabana watendaji wakuu kuelezea 'mafanikio ya ilani ya CCM kupitia 'malengo ya wizara/taasisi za serikali', Tanzania Broadcasting Corp kurusha Live mkutano mkuu wa CCM, vijana kutembeza fomu za mgombea Urais wa CCM kupata wadhamini, mabango wa 'wanaowatakia mema CCM' ktk mabarabara ya Dodoma n.k n.k
Je Memba wa JF mnasemaje kuhusu watendaji wa serikali kuburuzwa kuipigia chapuo CCM?
 
Back
Top Bottom