CCM Kugawanyika?

1.
Mtu wa Pwani,

Wazee liacheni jina la Mtu wa Pwani, huyo ni his own man, huwa anasimama na kuhesabiwa, sasa nashangaa kuona watu wakilitumia jina lake kwa malalamiko yasiyo na hoja za msingi, toeni hoja zenu wakuu muacheni huyu MP maana yeye anajiweza kusimamia hoja zake, wekeni zenu wakuu!

Mimi binafsi nachukizwa na huu mtandao wa uliopo humu ndani ya JF. Nafikia mahali napata hisia labda JF imetiwa mfukoni mwa CHADEMA na huenda ni mfadhili mkubwa wa JF.

Wakuu hebu mfikiri kabla ya kuandika, humu ndani kuna wananchi wenye uchungu na nchi yao, tena kwa misimamo mbali mbali, kuna mpaka wanaomlilia Lowassa, aendelee kuwa pm wetu, kina KGTZ, je na yeye ni Chadema? Mbona mawazo yake ya kumtetea lowassa hayajafutwa? Wakuu nafikiri wakati umefika muangalie vizuri kama zeni ni hoja au ni viroja?

Kuna ufisadi mkubwa sana unafanywa na baadhi ya JF members humu ndani tena kwa baraka za PainKiller.
Kwa mfano, fuatilia postings za Mstahiki jinsi zinavyoyumbishwa.

Painkiller, ameanza majuzi tu kuwa mod, sasa malalamiko yanatoka wapi? Mkuu umekuwa ukijaribu ku-create hoja ambazo hazifikii level ya kukubalika na wananchi wengi hapa JF, sasa unajaribu kutafuta mob justice kwa kuandika maneno ya uchonganishi kati ya members hapa, kila kukicha una mapya, mkuu weka hoja tu hapa Jf ni hoja yako tu, na sio filimbi nyingi bila hoja!

JF ni safi, na tutaendelea kumkoma nyani tu mpaka kieleweke mkuu, huku tukitofautinana kimawazo na kihoja, hakuna short cut hapa to fame!
 
1.

Wazee liacheni jina la Mtu wa Pwani, huyo ni his own man, huwa anasimama na kuhesabiwa, sasa nashangaa kuona watu wakilitumia jina lake kwa malalamiko yasiyo na hoja za msingi, toeni hoja zenu wakuu muacheni huyu MP maana yeye anajiweza kusimamia hoja zake, wekeni zenu wakuu!

Wakuu hebu mfikiri kabla ya kuandika, humu ndani kuna wananchi wenye uchungu na nchi yao, tena kwa misimamo mbali mbali, kuna mpaka wanaomlilia Lowassa, aendelee kuwa pm wetu, kina KGTZ, je na yeye ni Chadema? Mbona mawazo yake ya kumtetea lowassa hayajafutwa? Wakuu nafikiri wakati umefika muangalie vizuri kama zeni ni hoja au ni viroja?

Painkiller, ameanza majuzi tu kuwa mod, sasa malalamiko yanatoka wapi? Mkuu umekuwa ukijaribu ku-create hoja ambazo hazifikii level ya kukubalika na wananchi wengi hapa JF, sasa unajaribu kutafuta mob justice kwa kuandika maneno ya uchonganishi kati ya members hapa, kila kukicha una mapya, mkuu weka hoja tu hapa Jf ni hoja yako tu, na sio filimbi nyingi bila hoja!

JF ni safi, na tutaendelea kumkoma nyani tu mpaka kieleweke mkuu!

NADHANI FMES UNADAKIA TU HOJA NA WALA HUJUI UNACHOKIONGEA HAPA. NILIKUTAKA UTHIBITISHE UWONGO WAKO KULE KWENYE THREAD INAYOMHUSU ANNA KILANGO UMEKWEPA, SASA UMEKUJA KUJIINGIZA HAPA. NASISITIZA NENDA KATOE MAJIBU KAMA KWELI WEWE HUJASEMA UONGO.

MIMI SIONGEI MANENO MATUPU, NINA USHAHIDI WA YALE NINAYOSEMA. KUNA MAFISADI HAPA NDANI YA JF NA HUENDA WENGINE NI CORRUPT KABISA. INAWEZEKANA WEWE SIO MMOJA WAO LAKINI KWA KUTOKUJUA KWAKO UMEINGIA KWENYE MSAFARA WA MAMBA.

NASISITIZA KUNA UFISADI NA MAFISADI. NIMETOA MFANO ANGALIENI HOJA ZA MSTAHIKI ZINAVYOYUMBISHWA, NEED I SAY MORE?
 
Kama Lowasa ana washauri wazuri ni vema aachie na ubunge pia. Kwa hali ilivyo sasa hivi, itabidi Lowasa awe na ujasiri wa kiibilisi kuweza kusimama bungeni na kuchangia mjadala wowote utakaokuwa unaendelea. Kwa waliomwona siku analalama kabla hajatangaza kuwa amemwomba Rais ajiuzulu, midomo ilimkauka kabisa na kama si Sitta kuingilia kati kumwokoa baada ya Seleli kumtaka athibitshe magazeti ya udaku yaliyotumika kama ushahidi, huyu mzee alikuwa anakwenda kuanguka chini.
Hata hawa wanaompamba sasa hivi kuwa alikuwa hodari na sifa nyingi asizostahili soon wataachana naye.

Mkulu hilo lioja lako mkuu ni zito na linanivutia sana ila CCM hawaoni hivyo.
Huyu mtu kweli ataweza changia nini huko bungeni kwa namna alivyojiambisha,watu wakamchambua kama karanga na kumkanyaga kama zulia la sebureni, au ni katika kuongeza tu idadi ya wapiga mihuli Bungeni?Akina "Naunga hoja kwa 100%"
Kuna wate walituhumiwa tu kula pesa cha chama wakatimuliwa sasa huyu na wezake wamekula mabilioni yetu bado wanatazamwa tu au kwa vile sio mapesa ya Chama?
 
MIMI SIONGEI MANENO MATUPU, NINA USHAHIDI WA YALE NINAYOSEMA. KUNA MAFISADI HAPA NDANI YA JF NA HUENDA WENGINE NI CORRUPT KABISA. INAWEZEKANA WEWE SIO MMOJA WAO LAKINI KWA KUTOKUJUA KWAKO UMEINGIA KWENYE MSAFARA WA MAMBA.

__________________
Toa boriti ndani ya jicho lako kabla hujaelekeza kidole kwa mwenzio

Mkuu nimekusikia, na la ninashukuru kuwa quote hizi mbili zimeandikwa na wewe mtu mmoja!
 
Kuna wate walituhumiwa tu kula pesa cha chama wakatimuliwa sasa huyu na wezake wamekula mabilioni yetu bado wanatazamwa tu au kwa vile sio mapesa ya Chama?

Nyangumi,
Kwa CCM pesa ya serikali kuliwa ruksa, kwani haina mwenyewe. Tatizo ukiigusa hela ya Chama na hasa kwa wewe sio mtandao, hapo unajitafutia makuu yakhe!
 
Hii kali! Sasa kitaitwa chama gani? Labda ni Chama Cha Mafisadi na Wachovu (CHAMAWA). Mimi nafikiri hiyo jeuri ya kutaka kuunda chama inatokana na wao kudekezwa na kudhani kwamba kuwaondoa kwenye uongozi ni adahbu toshelezi na uporaji mkubwa walioufanya. Halafu najiuliza wanachama wao watatoka miongoni mwa watanzania waliochoka haw hawa? THUBUTU!
 
Lowassa, R.Aziz, Nazir Karamagi, Dk. Ibrahim Msabaha, Kingunge Ngombale Mwiru, Joseph Mungai, Basil Mramba, Zakia Meghji, Dk. Juma Ngasongwa, Anthony Diallo, Harith Bakari Mwapachu, Ritha Mlaki, Dk. Charles Mlingwa , Abdissalaam Issa Khatib , Ludovick Mwananzila, Dk. Luka Siyame, Gaudence Kayombo, Zabein Mhita na Daniel Nsanzugwanko.

Hawa wote ni Mamillionea waliotengenezwa kama ilani ya chama tawala ilivyosema..hata hivyo bado lengo ni tunahitaji mamillionea 100 by 2010, ktk jitihada za kuondoa Umaskini Tanzania.

JF PAWE MAHALA PA UKWELI NA SI USHABIKI, KTK HILI LILILOTOKEA NI NA MENGI YA MFANO WAKE HALIMAANISHI KUWA HAPA TZ HAKUNA WATU SMART KTK CCM NA VYAMA VYA UPINZANI,VIVYO HIVYO NI DHAHIRI KUWA WAPO WATU WACHAFU KTK MAKUNDI HAYA YA WATZ NDANI YA CCM NA NJE YA CCM.

HAWA MAKADA WALIOJIUZURU NA WALIOACHWA KTK BARAZA JIPYA KUNA WATU WASAFI NA WACHAPA KAZI LAKINI PIA WAPO WACHAFU NA WAZEMBE KTK KAZI, NIENDE MBELE KWA KUTAMBUA KUWA KTK HAWA WAPO MASIKINI NA MATAJIRI KATU YAO LAKINI WENGINE NI WAHANGA WA NGUVU YA SYSTEM HIVYO KUONDOLEWA KWAO NI SHINIKIZO NA TAARIFA POTOFU AMBAZO JK ANAPEWA JUU YAO,MWISHO NIWAOMBE WANA JF KUONA HARAKATI CHAFU ZA MEDIA YETU TZ KTK KUWAPONDA NA KUWAANGAMIZA WANASIASA MACHONI PA JAMII KWA SHINIKIZO LA MATAJIRI AMBAO WANAWAONA WANASIASA HAO WALIKUWA VIKWAZO KWAO,ALL IN ALL HII NI VITA YA UBUNGE 2010 NA URAIS WA ZENJ 2010. MAOFISA WA USALAMA WENGI WANJIANDAA KUSTAAFIA KTK SIASA HAPO NDIPO TATIZO LINAPOANZIA.
NIMEWASILISHA KWA MOYO WA KIZALENDO
 
Kugawanyika CCM? dont think so... somo kubwa linalopatikana kutoka CCM ni namna wanavyovuka ktk mitikisiko mikubwa, hii si mara ya kwanza, wakati wa mzee rukhsa hali kama hii ilijitokeza sambamba na sakata la serikali ya Tanganyika wakati wa G55 lakini mwote humo jahazi limeelea salama salimini...

Wanaoishi kwa tamaa ya fisi kutegea mkono wa mwanadamu utaanguka kalagabaho!
 
Lowassa, R.Aziz, Nazir Karamagi, Dk. Ibrahim Msabaha, Kingunge Ngombale Mwiru, Joseph Mungai, Basil Mramba, Zakia Meghji, Dk. Juma Ngasongwa, Anthony Diallo, Harith Bakari Mwapachu, Ritha Mlaki, Dk. Charles Mlingwa , Abdissalaam Issa Khatib , Ludovick Mwananzila, Dk. Luka Siyame, Gaudence Kayombo, Zabein Mhita na Daniel Nsanzugwanko.

Hawa wote ni Mamillionea waliotengenezwa kama ilani ya chama tawala ilivyosema..hata hivyo bado lengo ni tunahitaji mamillionea 100 by 2010, ktk jitihada za kuondoa Umaskini Tanzania.

JF PAWE MAHALA PA UKWELI NA SI USHABIKI, KTK HILI LILILOTOKEA NI NA MENGI YA MFANO WAKE HALIMAANISHI KUWA HAPA TZ HAKUNA WATU SMART KTK CCM NA VYAMA VYA UPINZANI,VIVYO HIVYO NI DHAHIRI KUWA WAPO WATU WACHAFU KTK MAKUNDI HAYA YA WATZ NDANI YA CCM NA NJE YA CCM.

HAWA MAKADA WALIOJIUZURU NA WALIOACHWA KTK BARAZA JIPYA KUNA WATU WASAFI NA WACHAPA KAZI LAKINI PIA WAPO WACHAFU NA WAZEMBE KTK KAZI, NIENDE MBELE KWA KUTAMBUA KUWA KTK HAWA WAPO MASIKINI NA MATAJIRI KATU YAO LAKINI WENGINE NI WAHANGA WA NGUVU YA SYSTEM HIVYO KUONDOLEWA KWAO NI SHINIKIZO NA TAARIFA POTOFU AMBAZO JK ANAPEWA JUU YAO,MWISHO NIWAOMBE WANA JF KUONA HARAKATI CHAFU ZA MEDIA YETU TZ KTK KUWAPONDA NA KUWAANGAMIZA WANASIASA MACHONI PA JAMII KWA SHINIKIZO LA MATAJIRI AMBAO WANAWAONA WANASIASA HAO WALIKUWA VIKWAZO KWAO,ALL IN ALL HII NI VITA YA UBUNGE 2010 NA URAIS WA ZENJ 2010. MAOFISA WA USALAMA WENGI WANAJIANDAA KUSTAAFIA KTK SIASA HAPO NDIPO TATIZO LINAPOANZIA.
NIMEWASILISHA KWA MOYO WA KIZALENDO
 
E Lowassa kujitenga na timu yake CCM-Mtandao?Akigombea urais 2010 atapita?
Lowassa si zaidi ya CCM. CCM ndiyo imemfikisha aliko na akipata kiburi cha kuanzisha chama hakito-hit mbele za watanzania. Naamini Lowassa anaiheshimu sana CCM na hawezi kuisaliti hivyo. Mawazo yangu ni kuwa Lowassa ataendelea kubakia CCM na siku zinavyoenda watanzania watayasahau mabaya yake (labda) kama ambavyo wameanza kusahau ya Ballali na hali inaweza kurejea shwari. Ukweli ulio wazi ni kuwa hali bado ni tete kwake anachosubiria ni kusafishwa na ripoti ya uchunguzi ya madai dhidi yake.

R.Aziz,Bw. Nazir Karamagi Dk. Ibrahim Msabaha,Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ,Joseph Mungai,Bw. Basil Mramba, Zakia Meghji ,Dk. Juma Ngasongwa ,Anthony Diallo,Bw. Harith Bakari Mwapachu,Ritha Mlaki, Dk. Charles Mlingwa , Abdissalaam Issa Khatib , Ludovick Mwananzila,Dk. Luka Siyame,Gaudence Kayombo ,Zabein Mhita na Daniel Nsanzugwanko.
Ni mawazo tu mkuu. Ni vema kuwa huu ni mtizamo wako. Ila kumbuka ripoti ya BoT ikitoka utaelewa kwanini baadhi ya hawa huwaoni tena kwenye system. It's the matter of time. Labda ripoti iwe 'cooked'. Vinginevyo wait and see. Sioni wa kuanzisha CCM yake hapa na ika-hit kuliko 'the original CCM'.

Ni mawazo tu,

Invisible
 
Kugawanyika CCM? dont think so... somo kubwa linalopatikana kutoka CCM ni namna wanavyovuka ktk mitikisiko mikubwa, hii si mara ya kwanza, wakati wa mzee rukhsa hali kama hii ilijitokeza sambamba na sakata la serikali ya Tanganyika wakati wa G55 lakini mwote humo jahazi limeelea salama salimini...

Wanaoishi kwa tamaa ya fisi kutegea mkono wa mwanadamu utaanguka kalagabaho!

Masatu,
Nimefurahia quote yako. What you are saying is absolutely right. Jambo ambalo mimi halinifurahishi ni kuwa mtu akiongea jambo ambalo liko in favor of serikali au CCM huoneka kana kwamba hakustahili kuingia humu JF. Kuna baadhi ya wachangiaji hapa hawajui jambo jingine lolote zaidi ya 'kuponda' hata yale yaliyo mazuri. Tena kana kwamba hawaelewi watajitokeza sasa hivi kupinga ninayosema.
 
Back
Top Bottom