CCM: Kodi Hapa Vp?

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Wakuu wote tulimsikia Nape na makada wa CCM na hata TRA walipokuwa wakikomalia kodi kutoka mshahara/ posho ya Dr. Slaa ya 7m, Inaonyesha dhahiri hawa jamaa walikuwa na uchungu kweli na the so called ukwepaji kodi. Sasa kuna jambo ambalo nadhani they need to be more serious kwa sababu it is really serious. Idd Simba anasema malipo ya sh milioni 285 yaliyoingizwa kwenye account yake yalikuwa ni consultancy fee!!!!! Well and good, Idd Simba ni kada wa CCM na amewahi kushika nyadhifa nyingi serikalini na kwenye chama. Sasa basi ningependa tuone utaratibu ule ule ikiwezekana zaidi ukitumika kukomalia kodi yetu kutoka hii the so called "consultancy fee" iliyoingizwa kwa Idd Simba. Nape, Kitillya, Mkulo plsssssssssssss!!

Mods: Pls msiichanganye hii kwenye thread nyingine at least for some 3 days:

Iddi Simba ajibu tuhuma dhidi yake

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Idd Simba amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, akisema mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi, akisema serikali ilijulishwa kila hatua.

Huku akitoa madai ya kughushiwa kwa saini ya Meneja wa UDA, Bw. Victor Milanzi kuonesha kuwa mnunuzi alielekezwa kuweka fedha katika akaunti binafsi, Bw. Simba alisema kuwa kutokana na mchakato wa uuzwaji wa UDA kufuata sheria na taratibu za nchi kadri zinavyojulikana, si sawa kusema kampuni hiyo imemilikisha hisa zake isivyo halali wala kuwa imetapeliwa fedha zake.

Akizungumza na Majira juu ya sakata hilo, hasa tuhuma kuwa alipokea sehemu ya malipo ya ununuzi na fedha hizo kwenye akaunti yake binafsi, Bw. Simba alisema kuwa fedha hizo hazihusiani na ununuzi na uuzwaji wa UDA, bali masuala mengine kati yake na Simon Group Ltd.

Bw. Simba ambaye amewahi kuwa kiongozi mwandamizi serikalini, alisema kuwa taarifa za mchakato wote wa uuzwaji wa UDA alikuwa akiziwasilisha serikalini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na kwa Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma (CHC).

Alisema kwa mujibu wa kanuni za UDA, madaraka ya uuzaji wa hisa ambazo hazijagawiwa yako mikononi mwa bodi ya wakurugenzi, ndiyo maana bodi iliendelea na mchakato wa kumuuzia Simon Group kwa mujibu wa sheria na mkataba wa mauzo ukafanyika, huku hisa hizo zikilipiwa, hivyo si kweli kwamba ziliuzwa kiholela.

"Mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa sheria na kanuni. Tulikuwa tunapata ushauri wa wanasheria katika mchakato mzima. Hao wanaodhani na kusema kwamba Simon Group imetapeliwa na kwamba haikumilikishwa hisa za UDA kihalali si sawa, kwani uuzwaji ulifanyika kwa mujibu wa kanuni na sheria tunavyozielewa.

"Kibaya kilichotokea ni kwamba baada ya Simon Group kuhalalishiwa ununuzi wa hisa hizo na kulipia malipo ya kwanza ya milioni 285, mwenyekiti (wa Simon Group), Bw. Robert Kisena akataka kuingia katika utendaji wa kampuni na uongozi wake, hata kabla ya AGM (mkutano wa wanahisa wa mwaka).

"Alipokatazwa kufanya hivyo na kushauriwa kwamba asubiri mpaka taratibu zikamilike, akaingia kwa nguvu kwenye majengo ya kampuni (UDA), kinyume kabisa cha taratibu. Hapo ndipo vurugu zilipotokea. Alipohojiwa hajakamilisha malipo ya pili kama ilivyotakiwa alidai kuna pesa alishalipa katika akaunti yangu mimi Idd Simba, kwa mujibu barua aliyoandikiwa na uongozi wa UDA," alisema Bw. Simba na kuongeza;

"Moja, barua ni ya kughushi, kwa sababu Meneja wa UDA, Milanzi hakuandika barua wala hakukuwa na maagizo yoyote ya yeye kulipia hisa zake kupitia akaunti binafsi. Hilo jambo lisingewezekana.

"Lakini ieleweke kwamba muda mrefu kabla ya tukio hilo na katika shughuli ambazo hazihusiani hata kidogo na UDA, zilizotokana na ushauri wa jumla wa kibiashara aliotaka kutoka kwangu, alikuwa anastahili kulipa fedha zangu binafsi. Nilitoa amri ya kulipia katika akaunti yangu, alifanya hivyo kwa awamu tofauti kadri nilivyotoa maagizo."

Akizungumza mbele ya mwanasheria wake, Bw. Simba alipoulizwa iwapo watu hawawezi kuhoji mgongano wa maslahi ulio wazi katika suala hilo, la Simon Group kununua hisa katika shirika (UDA) ambalo yeye ni mwenyekiti wa bodi, huku pia wakati huo huo yeye akitoa ushauri wa kibiashara kwa kampuni iliyotaka kununua UDA, alisema;

"Ndiyo wanaweza kuhoji...lakini sasa mimi si mtumishi wa umma, pale UDA mimi si mwajiriwa. Mimi nauza maneno, natoa ushauri. Ukija kutaka ushauri siwezi kukutalia. Lakini kwenye bodi tulikuwa serious sana. Tatizo ni kwamba mwanzoni sikutilia maanani sana tabia ya Robert Kisena, kwa sababu mimi nilikuwa na hamu sana mzawa achukue UDA, siyo kila kitu nchi hii anachukua mwekezaji mgeni," alisema Bw. Simba.

Alisema kwamba inasikitisha kuona mpaka sasa serikali haijachukua hatua yoyote kuinusuru UDA, akionesha matumaini yake kwa CHC itachukua hatua za haraka kurejesha hali ya kawaida katika shirika hilo muhimu la usafiri Dar es Salaam, pia kwa kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo.

Wakati Bw. Simba akisema kuwa fedha zilizowekwa katika akaunti yake binafsi hazina uhusiano wowote na uuzwaji wa UDA, Bw. Kisena amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hawakuwahi kuwa na shughuli nyingine tofauti na hiyo ya ununuzi wa shirika hilo la umma.

Akinukuliwa katika moja ya magazeti ya kila siku jana, Bw. Kisena alisema kuwa walilipa fedha hizo katika akaunti ya Bw. Simba, kama sehemu ya malipo ya ununuzi wa UDA, kutokana na maelekezo ya uongozi wa UDA, akisema kuwa anazo nyaraka zinazoonesha hivyo.
 
Idd Simba ni mwizi tena mzoefu, akamatwe, afilisiwe, tumechoka kuibiwa
 
wote wawili ni wizi tu, dili limekwenda vibaya sasa wanageukana.
 
Eti Consultancy fee hebu Muogope Mungu tena na Ramadhani hii unadanganya kweupe!
 
Back
Top Bottom