Ccm,kinara wa umoja na mshikamo wa kitaifa

Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
110
Waungwana nadhani mwenye macho haambiwe tazama.
Kwa muda mrefu CCM kimekuwa mstari wa mbele ktk kuhakikisha umoja na mshikamano wa Kitaifa.Kikiongozwa na KINARA WAO JK ,hakiogopi kumwaga damu kwa yeyote atakaye taka kuuvuruga UMOJA HUO.
Je ni kwanini watishie kumwaga damu badala ya kudumisha umoja na mshikamano huo kwa njia ya kutoa haki kwa wote,huduma bora kwa wote,kutokushabikia dini fulani na zinazofanana nazo.Nasema hivi kwa sababu,kuelekea maadhimisho ya miaka kumi ya kifo cha Baba wa Taifa,kumekuwa na matembezi ya hiari kwa vijana lakini kwa mshangao wangu ni VIJANA WA CCM PEKEE na kama wapo wengine ni wale ambao hawana chama(hawana msimamo wa kisiasa).JE HIYO NI NJIA SAHIHI KUSEMA KWAMBA WAPO MSTARI WA MBELE KTK KUDUMISHA UMOJA NA MSHIKAMANO?
 
Back
Top Bottom