CCM katika hali mbaya Arusha; kigogo mwingine (Bananga) atimkia CHADEMA

Nimeupenda sana ujumbe wake huyu bwana. Kwa hakika kama trend itakuwa hivi tunaweza kujikuta hadi kufikia 2014 tunatakiwa kurudia uchaguzi wa madiwani na wabunge wengi sana kwa kuwa wengi wao watakuwa wameshahamia CHADEMA. Kwa hili tutapaswa kumshukuru na kumpongeza Kikwete kwa kusaidia kuindoa CCM madarakani.

Nawaomba mtambue kuwa hata siku moja MUNGU hakushuka duniani kuleta mabadiliko! Nyakati zote alitumia watu either positivel or negatively, hivyo JK ni mmoja wapo wa watumika! Mpango wa Mungu juu ya MAUMIVU ya Watanzania unachkua kasi towards 2015! Mkono wake umeingia ndani! Kinachoendelea ni kuchanganyikiwa kamba kwa waliokuwa wanaijenga BABYLON TOWER! Leta Jembe, analeta mwiko! nk. Kweli tutamweka JK historiani, kwa kuondoka na CCM! Dalili zilionekana pale tu alipoingia Madarakani! Kumbukeni Siku 30 za MAAMUZI MAGUMU! Hotuba yake Bungeni, Na tafsiri ya SURA zake mbalimbali! Tujipange kwa MABADILIKO ili nasi TUSIYAPOKEE kwa hamaki na kusababisha kuchanganyikiwa!
:rockon:
 
Karibu sana bwana Bananga,hapo ndio nyumbani kwenu, hakika sasa umefika kwa nduguzo,Mungu akubariki sana kwa maamuzi yako mazuri, Amina!!!
 
ally bananga mfuasi mwingine wa el sina imani na na wewe kabisa ccm we na millya mlikuwa mnatumikia el na mtoto wake ""cadet" fred lowassa anyway karibu cdm but tutakaa na nyie kwa tahadhari kubwa

kweli huyu ndiyo mbaya kuliko,tafadhali viongozi hili wimbi la wana-ccm ambao hawakuwa safi kuja cdm kuweni makini.yamkini kuna jambo
 
MTOTO-FRIJI-OPENI RIDHIWANI KIKWETE APUPUTISHA WATOTO WA WALALAHOI KUKIMBIA UVCCM NA KUJITAFUTIA MAKAZI YA KISIASA CHADEMA, BILA HATA YA BABA YAKE KUONA KERO

Ridhiwani Kikwete anakiua CCM kwa kupuputisha vijana kibao chamani humo. Hadi tunapofikia mwaka mpya wa fedha 2012 tunatarajia kuona zaidi ya 65% ya UVCCM wakikihama chama cha Baba Ridhiwani Kikwete kutokana na tabia mbaya ya huyu kijana kwa vijana wenzake ambao wazazi wao HAWANA MAJINA katika chama hicho wala serikalini.

Kama huamini hili ninalolisema basi kasubiri kidogo uone KUMBUNGA CHA KAMANDA ndani ya M4C kila kona ya nchi hii. Subiri uone akina Mchungaji Msigwa, Nassari, Sugu, Abwao, Vincent Nyerere, Tundu Lissu, Dada Mdee, Ole Millya pamoja na wengine wengi wanavyoendelea kucheza na chaki ya uwanja wa kisiasa.

M4C, moto mkubwa kila mahali hadi MAFISADI waduwazwe na vitendo vyao vya kutudhalilisha na umasikini wa kuchonga.
 
Usaliti na makundi ndani ya CCM yanatishia kabisa uhai wa chama na tayari yamekwisha angamiza Taifa letu, hata hivyo nafasi ya wa watoto wa wanyonge ndani ya CCM inazidi kuwa finyu, aidha ujipendekeze kwa wakubwa ili upate nafasi ya kutumikia jamii au Chama, wakati nafsi yangu haiko tiyari kusimamia uovu huu sasa nimeamua kusimamia ninachokiamini bila uoga wala unafiki, na mfano Tazameni yanoyoendelea ndani ya UVCCM ARUSHA mikono ya mtoto wa mkubwa unaumaliza umoja huo mkoani hapa. Lakini pia uzito wa serikali ya CCM kushidwa kuwawajibisha wabadhirifu na wanaotumia vibaya madaraka waliyopewa angalia ubadhirifu mkubwa hivi karibuni uliofanywa na Mawaziri na Watumishi wengine wa Umma, Angalia jinsi Serikali imelichukulia suala la Jairo kwa mzaha, ni hatari kwa Nchi yetu kwamba wakati watoto hawana madawati wako viongozi wakubwa ambao wanashindwa kuchukuliwa hatua kwa wizi wa mabilioni ya fedha. SAFI SANA KARIBU KWENYE MAPAMBANO! ASANTE JK KWA KUUA CCM! R.I.P CCM!
 
Hong era sana Chadema kwa kuokota makapi toka CCM . End element kukusanya uchafu ila musitumie vibaya msamiati wa kigogo au vigogo, maana Bananga hana sifa ya kuitwa kigogo. Labda kama mna upungufu wenye sifa ya kuitwa kigogo mpaka na Bananga nae aitwe kigogo.
 
Huu ndio ukweli.

578111_364514723586346_107238979313923_1015538_927427111_n.jpg
 
kaka karibu sana ila chonde chonde kama una mambo yako binafsi bora ujiondoe coz tutakuja kukuchoma moto bure tena hadharani

  • :rockon:
    • :yo:


 
Can someone prepare a list ya wote waliokwisha bwaga manyanga ili NAPE aweze kuwa deduct kwenye database yake iache kusoma 6mil.

Wait to hear Nape`S Comments na huyu naye alikuwa na Karipio au Ban?
 
Ndugu yetu Bananga,kwa kweli mimi binafsi nakupongeza sana kwa uamuzi wa busara kwa kukubali kuwa mfuasi wa Nuru badala ya giza.CHADEMA ni JUK yaani jeshi la ukombozi.Kwa takwimu za wanachama wapya walioingia chadema miezi miwili tu ni zaidi ya wanachama wote wa CCM waliohai na wafu.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. TAARIFA KWA VYA HABARI


“Mficha maradhi kifo humfichuwa “

Ni muda mrefu nimeitafakari dhamira yangu na sasa ni wakati muafaka kufikia maamuzi magumu, Nimeamua kuachia nyadhifa zangu zote ndani ya CCM ambazo ni, MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA, MJUMBE WA BARAZA LA MKOA UVCCM, NA M/KITI WA KAMATI YA MAHUSIANO YA UVCCM MKOA ARUSHA.

Yaliyonisukuma ni mwelekeo mbaya wa CCM kwa sasa ambao umejiondoa kuwa Chama cha wanyonge na wakulima na sasa ni chama cha kundi la watu wachache na watoto wao ndio sababu yanayoendelea sasa ndani ya CCM yanasikitisha sana.

Usaliti na makundi ndani ya CCM yanatishia kabisa uhai wa chama na tayari yamekwisha angamiza Taifa letu, hata hivyo nafasi ya wa watoto wa wanyonge ndani ya CCM inazidi kuwa finyu, aidha ujipendekeze kwa wakubwa ili upate nafasi ya kutumikia jamii au Chama, wakati nafsi yangu haiko tiyari kusimamia uovu huu sasa nimeamua kusimamia ninachokiamini bila uoga wala unafiki, na mfano Tazameni yanoyoendelea ndani ya UVCCM ARUSHA mikono ya mtoto wa mkubwa unaumaliza umoja huo mkoani hapa.

Lakini pia uzito wa serikali ya CCM kushidwa kuwawajibisha wabadhirifu na wanaotumia vibaya madaraka waliyopewa angalia ubadhirifu mkubwa hivi karibuni uliofanywa na Mawaziri na Watumishi wengine wa Umma, Angalia jinsi Serikali imelichukulia suala la Jairo kwa mzaha, ni hatari kwa Nchi yetu kwamba wakati watoto hawana madawati wako viongozi wakubwa ambao wanashindwa kuchukuliwa hatua kwa wizi wa mabilioni ya fedha.

Sababu ni nyingi sana za kwanini nimeamua kutoka CCM, nikisema niandike zote pengine itanipasa kuandika kitabu hata hivyo ninaamini kuwa nitakuwa na fursa ya kueleza mambo mengi sana kwenye mikutano ya hadhara nitakayofanya na Chama cha kipya CHADEMA.

CHADEMA, nawashukuru kwa kunipokea nawahaidi utumishi na kazi iliyotukuka, nitajifunza kwenu na pia naamini mtajifunza kwangu ili tuweze kwa pamoja kuleta matumaini kwa wanyonge.

Kwa marafiki zangu na wanachama wa CCM, msihuzunike sana kwani ninatangulia kwenda kuwaandalia makao kwani ninajua nanyi pia mko njiani mnakuja, hata hivyo sikuwahi kuwa mwema kama malaika tulipokuwa pamoja CCM naamini kuna mahali niliwakosea kama binadamu naomba msamaha kwenu na undugu wetu ubaki, lakini kama maamuzi yangu ya kwenda Chadema yatakuwa yamewauzunisha poleni sana na muendelee kuchukia kwani hatuwezi kuukwaza utu na faraja ya Mwanadamu kwa kufurahisha nafsi za watu wachache.

Asanteni sana karibuni Chadema.


Ally Bananga.
……………………
27/4/2012.
 
Karbu mana umehamia pazuri mana bajaji ulikuwanalo kwanza dogo mmebanana hamna mawazo ya kuona mbali safi hamia airtel (CHADEMA)
 
Wakifika waliotoka CCM wapangwe Dodoma, Morogoro, Singida (kidogo), Tabora, Songea, Lindi, Mtwara na wapi tena bado magamba yanatawala? Labda Pwani ah na Kagera wakaeleza kwa nini wamehama CCM nadhani tutavuna kibao huko. Wakienda wapelekwe na Prof na wasifanye mikutano pekee yao wasije wakachakachua maana kile ulichokizoea ni hatari!!!
 
Back
Top Bottom