CCM: Kamati Kuu Kulikoni Tena?

"Huwezi kukata tawi la mti ukiwa umelikalia..."

Baba Enock, kukata tawi la mti ukiwa umelikalia inawezekana. Abunuwasi aliweza kufanya hivyo!
 
Rev.Kishoka,

..hizi kelele za wana CCM dhidi ya mafisadi ni jitihada za kutafuta madaraka tu.

..inashangaza kwamba wananchi wamesahau jinsi wanamtandao wa CCM walivyokuwa wakimwandama Frederick Sumaye kwamba ni fisadi, na kwamba tukiwachagua wao ufisadi utakwisha.


..hata Mkapa naye aliingia kwa gia ya kupigana na ufisadi uliokuwa umekithiri wakati wa awamu ya Mzee Mwinyi ambaye naye aliingia na makelele ya fagio la chuma.

..sielewi sababu za kuendelea kuichagua CCM kwa mategemeo ya kuutokomeza ufisadi, wakati imeishatoa maraisi watatu sasa walioshindwa ktk vita hiyo?

..inawezekana wana JF wengi "hawajala chumvi" vya kutosha, lakini kwa baadhi yetu ahadi ya vita dhidi ya ufisadi tulipewa kwa mara ya kwanza na Raisi Alli Hassan Mwinyi. kwa maoni yangu serikali za CCM kimelishughulikia suala hili kwa miaka takriban 24, au awamu 5 za uongozi, na hali inazidi kuwa mbaya.

NB:

..lakini hata ukiuweka ufisadi kando na kuangalia utendaji na rekodi ya serikali za CCM sidhani kama unaweza kuridhika hata kidogo.

..tuangalie sekta za kilimo, afya, elimu, uvuvi, biashara, viwanda, umeme, nishati, madini, usafirishaji etc. Hivi kweli wananchi mmeridhika?

..ukitaka kujua kwamba nchi imewashinda CCM angalieni jinsi vijana toka vijijini wanavyomiminika mijini bila ujuzi wowote na bila shughuli ya maana ya kufanya.
 
- Wakuu salaam mbele sana na heshima pamoja, ni kwamba Rais ameahirisha kikao hadi kesho kuanzia saa mbili asubuhi na kitakuwa ni kwa siku nzima ya kesho, yaani Jumamosi Tarehe 12/9/2009.

- Samahani sana kwa usumbufu wa kuwaweka kwa muda mrefu maana leo tulikua safarini kutoka Iowa, kuelekea Minnesota, halafu na sasa tupo njiani kurudi tena Iowa, kabla ya kuruka kwenda New York Jumapili.

- Kwa hiyo tutaangalizia kesho yatakayojiri huko kwenye kikao, leo kuna habari za Makamba kudai na yeye anawaunga mkono wabunge wapiganaji, I mean this is hillarious!

Anyways, naona kuna maswali na hoja hapa zinatakiwa kujibiwa, ngoja tuziangalie kwanza na kuzijibu, otherwise tupo pamoja sana wakuu!

Respect.

Field Marshall Es!
 
- Wakuu salaam mbele sana na heshima pamoja, ni kwamba Rais ameahirisha kikao hadi kesho kuanzia saa mbili asubuhi na kitakuwa ni kwa siku nzima ya kesho, yaani Jumamosi Tarehe 12/9/2009.

- Samahani sana kwa usumbufu wa kuwaweka kwa muda mrefu maana leo tulikua safarini kutoka Iowa, kuelekea Minnesota, halafu na sasa tupo njiani kurudi tena Iowa, kabla ya kuruka kwenda New York Jumapili.

- Kwa hiyo tutaangalizia kesho yatakayojiri huko kwenye kikao, leo kuna habari za Makamba kudai na yeye anawaunga mkono wabunge wapiganaji, I mean this is hillarious!

Anyways, naona kuna maswali na hoja hapa zinatakiwa kujibiwa, ngoja tuziangalie kwanza na kuzijibu, otherwise tupo pamoja sana wakuu!

Respect.

Field Marshall Es!
duh!hiyo ya makamba mkuu IMENITISHA!ni makamba huyo huyo aliyemtamkia Nnauye habari ya ''ALIYEFUNGIWA DUNIANI.............''
 
'Vocal' CCM MPs react to President Kikwete's latest anti-corruption remarks:




MPs from the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) who have been at the forefront of the national anti-corruption drive, have welcomed President Jakaya Kikwete's latest affirmation of his government's resolve to fight graft.

Several CCM members of parliament, interviewed separately by THISDAY yesterday on their reactions to the president's ground-breaking tete-a-tete with ordinary Tanzanians via radio and television on Wednesday night, said they were both "impressed and invigorated" by his remarks.

Same East legislator Anne Kilango Malecela said she found encouragement in Kikwete's newly-reaffirmed position on the fight against graft.

�We strongly applaud the president's commitment to tackle this problem. We have been very heartened by his comments...very much," Ms Kilango told THISDAY by phone from the United States where she is currently on a brief visit.

She said the president has shown courage and a personal resolve to win the high-profile war against corruption, which has become endemic in Tanzania.

All right-thinking MPs should continue to fully support the government's anti-corruption drive, she remarked.

"We are behind him (President Kikwete) 100 per cent. We will not falter in our push for true reforms aimed at strengthening our party (CCM). The president should keep the faith...we are with him all the way," she added.

Kilango was this year presented with the "Tanzania Woman of Courage Award" by the US Embassy in Dar es Salaam for her own vocal stance against grand corruption.

She said any threats to her own safety would not stop her continuing to publicly demand that powerful individuals in the country answer questions about corruption.

Source: Thisday 12/9/2009
 
We have been very heartened by his comments...very much," Ms Kilango told THISDAY by phone from the United States where she is currently on a brief visit.
OK kazi za majuu nini hizo! Sikuona sababu za kupigia mstari United states wala brief visit...ama ni msisitizo....! Duuu kali hii ya week enda
 
Rais Kikwete awakuna
wapambanaji wa ufisadi



*Kilango:Ametupa faraja kupambana zaidi
*Shellukindo:Ameweka sawa ya Richmond



WAANDISHI WETU
Dar es Salaam

SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuhutubia Taifa na kufafanua juu ya masuala mbalimbali mazito ya kisiasa na kitaifa hususan vita vya ufisadi nchini, wabunge mbalimbali wa CCM hasa walio mstari wa mbele kupambana na ufisadi, wameipokea hotuba hiyo kuwa ni dira mpya.

Mbunge wa Same Mashariki-CCM, Anne Kilango Malecela, amelazimika kuzungumza akiwa ughaibuni kusisitiza kuwa msimamo wa Rais Jakaya Kikwete, kuhusiana na mapambano dhidi ya ufisadi hasa ahadi yake ya kuruhusu Serikali kukosolewa kwa nia ya kusahihisha makosa, umewapa faraja wabunge wanaopambana katika vita hivyo.

Akizungumza kwa simu kutoka Iowa, Marekani aliko kikazi, Kilango ambaye ni mmoja wa wabunge wachache ndani ya CCM wenye msimamo usioyumba, alisema Rais Kikwete ameonyesha ujasiri na kwamba wabunge makini wako nyuma yake.

“Kwa kweli tunampongeza sana Rais Kikwete kwa msimamo wake kuhusiana na ufisadi. Nimepata taarifa kupitia kwenye mtandao na kuwasiliana na wenzangu Tanzania, kwa kweli tumefarijika sana na msimamo wake ambao tunaufahamu siku zote,” alisema. Kilango alisema vita dhidi ya ufisadi ni vita vyenye changamoto nyingi ambazo wamekuwa wakipambana nazo na kwamba hata Rais Kikwete naye amekuwa akikumbana na changamoto nyingi, lakini ameonyesha ujasiri wa hali ya juu kubaki na msimamo wa kutounga mkono uhujumu wa fedha za wananchi.

“Tuko nyuma yake kwa moyo mmoja. Hatutapunguza kasi katika kutafuta mabadiliko ya dhati na yenye nia ya kukiimarisha chama chetu cha CCM (Chama Cha Mapinduzi) na Rais wetu asikate tamaa, tuko pamoja naye,” alisema. Alisema kutokana na furaha aliyoipata kutokana na kauli ya Rais Kikwete, Kilango anasema kwamba kwa sasa bado yuko katika maombolezo ya msiba wa ndugu yake lakini amelazimika kuzungumza hadharani kuonyesha furaha aliyoipata kutokana na msimamo wa Rais.

Alisema amekuwa kimya kwa muda mrefu, lakini Watanzania watarajie kishindo kikubwa mara atapoamua kuzungumza tena hadharani kutokana na kujiandaa kikamilifu kuitetea nchi yake. “Wasione nimekaa kimya, mimi nitajitokeza na kuibua mambo mazito kama Tsunami na watu najua mtatikisika na waandishi mtapata mambo ya kuzungumza,” aliahidi.

Kilango ambaye alitunukiwa tuzo ya mwanamke jasiri kutokana na kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa, alisema Rais Kikwete amekipa uhai mpya Chama Cha Mapinduzi na kwamba sasa chama kinazidi kuwa na nguvu kubwa. “Kwa kuimarisha chama, tunamhakikishia Rais Kikwete kwamba tutamsaidia kwa nguvu zetu zote bila kuchoka wala kuogopa misukosuko. Amegusa nyoyo zetu,” alisema.

Katika mazungumzo yake ya juzi usiku, Rais Kikwete alibainisha wazi kwamba katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na aina zote za uhalifu hana mchezo. Hata alipoulizwa swali kwamba kuna watu wanalindwa kwa kuwa amekuwa na mahusiano nao, Rais alionekana kuwa jasiri kwa kusema wazi kwamba katika ufisadi hana rafiki wala ndugu na kwamba wahusika wanalifahamu hilo.

Mbunge wa Bumbuli-CCM, William Shellukindo yeye aliguswa na ahadi ya Kikwete kulimaliza suala la Richmond.

“Nampongeza sana Rais kwanza ametuthibitishia kwamba anafahamu kuwa Serikali inalazimika kuleta majibu kuhusu maazimio ya Bunge mwezi Novemba. “Na serikali ikituletea majibu ya kuridhisha sisi tutafurahi sana maana suala hilo litakuwa limefikia mwisho ili tuweze kuendelea na mambo mengine....Sisi katika kamati yetu (Nishati na Madini) tuliazimia na tumesema tutaendelea kusimamia haki hadi mwisho.”

Akizungumzia suala la wabunge wa CCM kutoelewana, Shellukindo alisema hilo ni suala la afya kwa chama tofauti na watu wanavyoona ni tatizo.

“Hiyo ni afya ya kisiasa maana katika wabunge zaidi ya 200 wa CCM huwezi kuwa na wabunge wote wenye mawazo yanayofanana. Sasa hili la kuwepo kwa msigano ni tatizo la baadhi ya wabunge wasiofahamu kutofautisha hoja na mahusiano. Mbunge anaweza kuwa na hoja na sisi mara zote hatuzungumzii mtu binafsi tunazungumzia hoja.

“Kwa mfano kama suala la Richmond lilikuwa ni azimio la bunge na wote wa CCM na wapinzani tulikubaliana katika hilo. Sasa lazima tujue kwamba wale waliochukuliwa hatua wana wabunge marafiki zao na wao wanaweza kuwa na hoja tofauti na mtazamo tofauti. Hili ni suala la kawaida na siyo tatizo wala mgawanyiko hasa kwa wale tunaoelewa.

Mbunge wa Mbozi Mashariki, CCM, Godfrey Zambi, mmoja wa walioshikia bango sakata la Ticts, alisema hotuba ya Kikwete imewaweka sawa:

“Labda niseme kwamba siku zote sisi wabunge tumechaguliwa ili kutetea maslahi ya umma. Kazi hii haiwezi kuwa ya wapinzani peke yao ni kazi ya wabunge wote. “Kama mimi ningekuwa mroho wa madaraka ningekwenda upinzani tangu mwaka 2000, lakini niliamini kwamba ni vyema kuikosoa serikali nikiwa ndani ya chama changu CCM. Lazima katika hili tuelewane na ninashukuru kwamba Rais ameliweka vizuri.

Mmoja wa wabunge vinara wa sakata la Richmond, Lucas Selelii-CCM Nzega, alimsifu Kikwete kwa kutangaza msimamo wa kutowaonea haya mafisadi. “Tunamshukuru sana Rais ameutangazia umma wa Watanzania msimamo wake na wa serikali yake. Lazima kama viongozi wa CCM na viongozi wa wananchi tujifunze kusoma ishara za nyakati. Naamini Rais hilo analijua na ndiyo maana kauli yake mmeisikia naamini ametuwekea njia na mwelekeo wa tunakokwenda,” alisema.


Source: Kulikoni 12/9/2009.
 
duh!hiyo ya makamba mkuu IMENITISHA!ni makamba huyo huyo aliyemtamkia Nnauye habari ya ''ALIYEFUNGIWA DUNIANI.............''

- Tupo pamoja hapo mkuu, amenukuliwa na baadhi ya magazeti ya leo, it is hillarious!

Respect.

FMEs!
 
Engineer;Marshal ES,

Siku hizi umegeuka Hussein Yahaya kujifanya unatabiri yale ambayo ni obvious?Hayo uliyoyaandika hapo juu nayo ni breaking news!

- Kwanza heshima yako mkuu, sasa kama ulikuwa unayajua mbona hukuwahi kuyasema huko nyuma? Nimetoa dataz sio utabiri mkuu kuna tofauti kubwa sana kati ya dataz na utabiri, vipi ni stress za kampeni nini mkuu? Slow down mkuu maana sasa unazidi kushuka hadhi, ni vyema hata huyu mgombea wako akakupumzisha au akatangaza mapema sana kwamba hahusiki na wewe, maana kila siku ya Mungu unapofungua kinywa chako humu JF unamuongezea maadui,

- Again hizi ni dataz sio utabiri kama wako wa kushindwa kwa Mwakyembe huko Kyela, ndio maana mafisadi wanakuja kukutana huko huko kwenu kila wakati, ni kwa sababu ya mkoa kuwa na wananchi wenye mawazo ya kitabiri tabiri kama yako mkuu, yaani umejaa utrabiri wa kwenye mabao mpaka dataz kwako zinakuwa ni utabiri tu Bwa! ha! ha! unachekesha kweli!, pole sana mkuu na stress za kampeni!

Vipi mmeking mabakuri mangapi huko kwa ajili ya huyo mama yako?

Akifanya JK eti mkinga mabakuri lakini akifanya mzee au mama, unamwaga masifa yasiyo na maana.

Ila mimi namkubali mama Kilango, angalau anajua kukinga bakuri na sio kubwabwaja tu majukwaani, huku wananch wanaumia.

- Unajua kama US inaweza kwenda China kuomba zile hela za Stimulus package ya George Bush ya dola Billioni moja na nusu, sisi wananchi wa Tanzania hatuna njinsi ndugu yangu na hasa ukiangalia kwamba serikali yetu ndio hiyo, maana kama dunia ya kwanza US wanakinga bakuli itakuwa sisi bongo au husomi international news mkuu umebakia na news za Kyela tu?

- Mkuu kwa kawaida huwa ninatafuta hela za charity ya mke wangu, inayowasomesha watoto wengi wasio na uwezo kule Musoma na Arusha, hasa kata ya Mugumu, kwa hiyo kumsaidia mpiganaji yoyote nyumbani haijawahi kuwa tatizo na wala si kuvunja sheria za Jamhuri yetu au yoyote ile duniani unless kama ni sheria mpya unataka kuiweka huko Kyela baada ya kumtoa Mpiganaji Mwakyembe, Bwa! ha! ha!

- Ninamkubusha tena mgombea wako kwamba kama kweli anataka kushinda uchaguzi ujao, basi ni vyema aseme mapema kwamba hahusiki na wapambe kama wewe mkuu maana huwezi kumsaidia yeye wala jimbo la Kyela, wakati unapiga piga pumba hapa, mafisadi wamechagua mkoa wako kuwa ni mahali maalum pa vikao vyao.

- Unapaswa kusema hivi, afadhali Mpiganaji, Mheshimiwa Mama Kilango anakinga bakuli na matokeo yanaonekana kwa wananchi jimboni, kuliko wengine ambao hela hazifiki kwa wananchi.

Respect Mkuu.

Field Marshall Es!
 

- Hii ni thread ya kamati kuu na wapiganaji mkuu, Bwa! ha! ha! great thinkers wengine bwana inachekesha sana!, kama unanihitaji kule chini niite nitakuja kukupa majibu mkuu, ya tulipofikia na ile project ya nguvu kazi maana watu wako njiani kuruka sasa.

- Masa nilidhani a great thinker kama wewe, knowing kwamba ninasafiri na mpiganaji, utauliza some serious questions kuhusu masilahi ya taifa ili nimpe huyu mpiganaji, wewe unaona hii ni saa ya kuonyesha great thinking yako inapoanzia na kuishia, pole sana mkuu!

Respect.

FMEs!
 
Masa nilidhani a great thinker kama wewe, knowing kwamba ninasafiri na mpiganaji, utauliza some serious questions kuhusu masilahi ya taifa ili nimpe huyu mpiganaji, wewe unaona hii ni saa ya kuonyesha great thinking yako inapoanzia na kuishia, pole sana mkuu!

Umeniboa kupigia vimstari US na short visit...ulifikiri kuwa ujumbe usingefika? unapaka rangi mno ....
 
Sidanganyiki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

HAKUNA MAKAMANDA WA UFISADI NDANI YA CCM.

You are either "with them" or "against them". NUKTA.....

Huwezi kukata tawi la mti ukiwa umelikalia...


- Mkuu heshima yako sana, I hope hii yako sio April Fool bali ni a great thinking, maana kama that is the case basi wa-Tanzania wote tunakukubali ufisadi hakuna hata mmoja anayepinga,

- I mean tutaupingaje ufisadi huku tumeukalia kwa kuwachagua viongozi mafisadi kila siku?, that is a great thinking bro!

Respect.

FMEs!
 
Umeniboa kupigia vimstari US na short visit...ulifikiri kuwa ujumbe usingefika? unapaka rangi mno ....

- Huko ni kukurupuka kwako mkuu, nenda kwenye original story utakuta hiyo mistari, huo muda sina mkuu, maana nimeanza kwenda majuu nikiwa na miaka kama mitatu, na robo tatu ya maisha yangu nimeishi majuu, si kuenda majuu nikiwa mtumzima kwamba sasa ninalimbuka na kuanza kupigia mistari majuu, au sikutokea mikoani na kupita tu Dar nikielekea Airport kwenda majuu.

- Kwa hiyo ni simply kwamba umejiboa mwenyewe na kukurupuka kwako!

Respect.

FMEs!
 
maana niemanza kwenda majuu nikiwa na miaka kama mitatu, na robo tatu ya masiha yangu nimeishi majuu si kwenda majuu nikiwa mtumzima

Hakuna anayehitaji kujua hili, kuna waliozaliwa majuu kama wewe na miaka mitatu yako ulichelewa!
 
Hakuna anayehitaji kujua hili, kuna waliozaliwa majuu kama wewe na miaka mitatu yako ulichelewa!

- Kisiasa maana yake ni message sent na imefika inapotakiwa, sasa tunaweza kurudi kwenye hoja muhimu kwa masilahi ya taifa mkuu?

- Au hakuna maswali tena niendelee na kurudi kwenye shughuli za masilahi ya taifa?

Respect.

FMEs!
 
- Kisiasa maana yake ni message sent na imefika inapotakiwa, sasa tunaweza kurudi kwenye hoja muhimu kwa masilahi ya taifa mkuu?

- Au hakuna maswali tena niendelee na kurudi kwenye shughuli za masilahi ya taifa?

Respect.

FMEs!
naona hakuna maswali mkuu!
uzuri wa masanilo ni kwamba ni mtu muelewa sana.hahaha
maharage ya mbeya haya.MAJI MARA MOJA TU
 
Back
Top Bottom