CCM: Kamati Kuu Kukaa Chini Dar

Ni bora wasiamue chochote cha kurekebisha mparaganyiko ktk safu zao. Hii polepole inaweza kutoa mwanya kwa wananchi kudai nchi yao kutoka kwa mafisadi maana hicho kikundi cha wachache kinaweza kutufikisha mahala ambapo tutaona hata DJ ni bora akatuongoza.
 
Hivi WaTanganyika mnakubaliana na hizi kauli za kuwa Vyama vya upinzani hamjawa tayari ?
Maana Zenji kasi yao wanasema hata wakiamshwa usiku wa manane kupiga kura basi Sultani CCM haoni ndani ni out tena anatupwa mbali sana ,na kila siku ziendavyo ndivyo inavyozidi kuwekwa pembeni na kuambiwa imetosha baba ,Wazenji wanataka kuizima na kuipunguza CCM EMPIRE na kuibakiza huko Tanganyika ,ila juhudi zikifanywa hata baadhi ya mikoa wanaweza kuipunguza CCM EMPIRE ,yaani Mikoa mitatu mikuu ikipunguzwa basi itakuwa hatua si ndogo ,tuikomboe Kilimanjaro Arusha,Mtwara ,Tanga ,Dar es salaam,Mwanza ,Mbeya na Kagera na mikoa mingine kumega mega ,mbona 2015 Usulutani wa CCM utakuwa umebakiza mikia tu.
Wewe unapenda sana kuzungumzia mstakabala wa CCM Zanzibar, lakini mbona hukamilishi story yako kwa kueleza nini mbadala- sasa. Wacha nikusaidie kidogo. CUF haimo kabisa mawazoni mwa Wazanzibari walio wengi. Kama CCM inapigwa chini, ujue CUF inapata kipigo mara mbili. CUF (katika hali yake ya hivi sasa) siyo chama ambacho Wazanzibari wanakikubali. Huo ndio ukweli wa mambo.
 
FMES nakubaliana na wewe lakini naomba kuuliza niprocess gani itatumika katika ku-identify kiongozi fisadi etc kwa kuwa hivi sasa kuna a lot of spin out there!

Mkuu Susuviri,

- No matter the spin, sidhani kwamba hapa JF tumewahi kudanganywa nani ni fisadi na nani sio, you know that hapa huwa tunawapekua nje ndani nafikiri Mh. Zitto anaweza kuwa shaidi wangu on that of what we do here. Kwa hiyo usiwe na wasi wasi mkuu,

- Isipokuwa tu, kwenye hili la kuwajua viongozi wetu kwamba nani ni nani, nia na madhumuni ni kuweka all the info out there ili wakati wa uchaguzi utakapofikia wananchi waamue wenyewe wanachagua kiongozi wa aina gani, kwenye uchaguzi wa 2005 kule BCS tuliweka wazi yote mapema ndio maana hatushangai yanayoendelea sasa.

Sisi hapa ni kuweka habari, halafu wananchi kuamua either kusuka au kunyoa, lakini bila ya kumlaumu mwingine au visingizio kwamba hawakujua.

Respect.

FMES
 
- The dataz zaidi nilizozipata sasa hivi ni kwamba kikao hicho pamoja na agenda zake zingine, pia kitatoa tamko rasmi la chama kuhusiana na jimbo la uchaguzi lililo wazi la Busanda.

- Lakini pia kuwepo kwa kikao cha Kamati ya Maadili ambacho Makamba, Chenge na Rais Kikwete ni moja ya wajumbe wake, kunaleta maswali mengi sana, among wachunguzi wa siasa nchini kwamba kunani hasa? Kwa sababu kama the main agenda ni jimbo la Busanda, basi haikuwa lazima kwa Kamati hii kukutana sasa, je kuna nini?

FMES!
 
...tusubiri tuone, hizi ni siasa za Chama Cha Mafisadi ambazo zimeshazoeleka. Kila watu wanapotarajia jipya ndipo wanapokuja na kituko zaidi!!
 
Wewe unapenda sana kuzungumzia mstakabala wa CCM Zanzibar, lakini mbona hukamilishi story yako kwa kueleza nini mbadala- sasa. Wacha nikusaidie kidogo. CUF haimo kabisa mawazoni mwa Wazanzibari walio wengi. Kama CCM inapigwa chini, ujue CUF inapata kipigo mara mbili. CUF (katika hali yake ya hivi sasa) siyo chama ambacho Wazanzibari wanakikubali. Huo ndio ukweli wa mambo.

Napenda kuzungumzia uhai wa Sultani CCM kwa sababu ameshafikishwa ukingoni na dalili za wazi zinaonekana ni wakati tu umibakia wa kubwagwa na chini ,Chama mbadala sio Mzanzibari bali dunia nzima inajua kuwa ni CUF ,naona unauliza mbona mchana haukuitwa usiku ?
CUF sasa hivi ina nguvu kuliko wakati wowote ule kule Zanzibar hilo halitaki mjadala ,maana uchumi wa dunia umetetereka na ujue na CCM nayo haina mshiko ,huo ndio ukweli ,halafu kule hivi sasa wananchi hawatizami uchumi wa Nchi wala umeme upo au haupo maana siku mbili hizi wamewawashia umeme na maji kwa sababu ya uchaguzi wa magogoni ,yaani mambo yenu ya kitoto kabisa ,jamani wakati wa kupewa peremende umekwisha na hilo ndio moja litakaloelezwa katika huo mkutano wa mafisadi kuwa wakati wa kubebana umekwisha na hautarejea tena ,watu wanakwenda mbele ,hivyo kitakachozungumzwa huko ni kuwa uchaguzi unaokuja utakuwa wa haki na usawa mambo ya kutegemea polisi na majanjawids umepitwa na wakati aliyepora ndio keshapora ,kwa ufupi awamu ya Kikwete na Karume ndio awamu ya mwisho kutumia mbinu za kukwapua kura na kubadilisha matokeo ,kwa chaguzi zijazo kila chombo kitatakiwa kuchunga dhamana yake ,usifananishe Tanzania na Zimbabwe au Kenya au Nchi zingine za Kiafrika utakuwa unakosea sana, Tanzania namna inavyotaka sifa haswa huyu JK Mrisho basi utaona mambo yatakavyowabadilikia jamaa zako ambao wanaona ,mbinu za kutumia polisi kukimbia na masanduku ya kura utazidi kutumika na kuwanufaisha wafuasi wa Sultani CCM.
CCM imeshasoma kuwa Nchi haiwezi kuendeshwa na matokeo ya wizi na kulazimisha utawala ,maana kufanya hivyo itakuwa hata heshima baina yao inapungua ,tumeona ni jinsi gani CCM imeweza kutwaa madaraka katika uchaguzi uliopita ,malipo yake ndio haya tunayopigiana nayo makelele ,maendeleo hakuna ,viongozi wote wameingia kwa rushwa hakuna anemsikia mwenziwe kila mmoja ni mbabe ,hakuna anaemsikiliza Kikwete kwa vitendo maana wote asiejua hili analijua lile ,viongozi wanaogopana kila mmoja anamwona mwenziwe ana marazi ya umeta.
Tusiandikie mate sikiliza dongo litakalorushwa na Kikwete yaani mtashangaa ,yeye mwenyewe atajiweka katika kundi la kuwa yupo tayari kushindwa au kukubali matokeo yatakavyokuwa ,lakini kwiba hakwibi tena ,atatizama hatima ya Mwenyezi Mungu itakavyoangukia akishinda au akishindwa ataamini kuwa haki imetendeka na ndio gumzo kubwa atakalowaambia wenziwe wakiwemo CCM-Zanzibar kuwa haiwezekani kila siku waambiwe ni wezi ni lazima uchaguzi uendeshwe kwa haki bila ya manung'uniko kutoka upande wowote atakae shinda awe ameshinda kwa ridhaa ya wananchi na sio nguvu za dola.

Hivyo kama unategemea internate za ofisi na ulaji wa CCM basi anza kufungasha na kutafuta mradi utakaokuwezesha kuonekana tena hapa JF la si hivyo ndio utupe buriani kabisa.
 
Wakuu kwa hekima ya kawaida tu ni lazima sasa tukubali na kuwa tayri kusikia tamko kuu, kama mlivyosema ninyi wenyewe cc ndiye mwanzo na mwisho wa ccm basi ni vema tuisikie nayo ikinena kuwa rushwa ni vita ya umma na ccm ndiye mpiganaji kiongozi na siyo mtu binafsi. Ni lazima tuiisikie kauli ya cc ktk kukuza demokrasia ndani ya ccm kwa kuruhusu kila atakayependa kupambana na jk ruksa lakini wao kama cc wanamuunga mkono jemedari aliyeko kwani katiba inamruhusu na ameshafanya kazi kwa kiwango cha kuaminika kwa jamii. Hii ni fursa sahihi kwa m-kiti kuweka sawa nchi hasa baada ya akina mwakyembe na rostam kunyoosheana vidole, zenj na mafuta yao n.k
pasaka njema watumishi wa mungu.
 
Jamani mimi naomba mnisaidie kidogo tu, Hivi pale CC ni nani wa kumnyoshea mwenzake kidole!!! Kama yupo hebu tusubiri tuyasikie
 
Jamani mimi naomba mnisaidie kidogo tu, Hivi pale CC ni nani wa kumnyoshea mwenzake kidole!!! Kama yupo hebu tusubiri tuyasikie

- Mkuu Nsesi, naomba kutofautiana na wewe hapa, kwa kawaida huwa wananyoosheana sana vidole huko CC, kwa mfano wakati wabunge wa Arusha walipokamatwa, safari ya kwenda kwenye ubunge wa jimbo dogo Mbeya, Butiama, Richimonduli kwa hiyo tusiwapuuze kabisa maana hiki kikao ndio mwanzo na mwisho, katika siasa zetu za bongo hiyo ni reality sio my opinion na it the only thing we got.

- Sasa tujaribu kuwapa moyo wenye nia njema na taifa lakini wanabanwa huko CC.

Respect

FMES
 
- The dataz zaidi nilizozipata sasa hivi ni kwamba kikao hicho pamoja na agenda zake zingine, pia kitatoa tamko rasmi la chama kuhusiana na jimbo la uchaguzi lililo wazi la Busanda.

- Lakini pia kuwepo kwa kikao cha Kamati ya Maadili ambacho Makamba, Chenge na Rais Kikwete ni moja ya wajumbe wake, kunaleta maswali mengi sana, among wachunguzi wa siasa nchini kwamba kunani hasa? Kwa sababu kama the main agenda ni jimbo la Busanda, basi haikuwa lazima kwa Kamati hii kukutana sasa, je kuna nini?

FMES!

Kuna umbeya nimesikia kwamba RA ameandika barua ya kujiuzulu nyadhiva zote ndani ya CCM, including ubunge. Wapekenyuzi wa mambo wanahisi kwamba barua yake "itakubaliwa" (kwa sababu iko inline na tamko la JK la mtu kuchagua siasa au biashara) ... na kuna suala la huenda Dr Mwakyembe "atawajibishwa"
 
Makalla hamjui Kitine enzi za ukachelo wake, ametumwa tu na wakubwa zake alopoke mambo; wakati Kitine akiwa kachelo nambali moja Amos Makalla alikuwa anauza matofali na vigae pale mbezi Tiles kwahiyo hajui sababu zilizowafanya wakubwa zake wasimchukulie hatua huyu Kitine!! Nadhani waliogopa kuwa huyu kachelo mstaafu anataalifa zao nyingi ambazo angeweza kuziweka hadharani na kusababisha kwa msemo wa leo kuwa mahali hapa pasingetosha!! Kwahiyo makalla aelewe kuwa Kitine hakuonewa huruma bali hao wakubwa zake walikuwa wanalinda uchafu wao usianikwe hadharani kwani ndani ya CCM na serikali yake kuna uchafu mwingi sana!!
 
Last edited:
Asante Sekenke!

That sounds good. Tatizo nililonalo na Tanzania Daima ni kuwa ni gazeti zuri sana linapokuwa na makala za Mwanakijiji na Ngurumo period. Ukiondoa michango ya wazalendo hawa wawili, Mwanakijiji na Ngurumo, Tanzania Daima ni rolling stone isiyo na msimamo unaoeleweka: ni udaku plus umamluki usiofanana na "Sauti ya Watu" wala msimamo wa CHADEMA!
 
"That sounds good. Tatizo nililonalo na Tanzania Daima ni kuwa ni gazeti zuri sana linapokuwa na makala za Mwanakijiji na Ngurumo period. Ukiondoa michango ya wazalendo hawa wawili, Mwanakijiji na Ngurumo, Tanzania Daima ni rolling stone isiyo na msimamo unaoeleweka: ni udaku plus umamluki usiofanana na "Sauti ya Watu" wala msimamo wa CHADEMA'

*******************

FATAKI: Kwa umamluki nakusapoti moja kwa moja, ni dhahiri baadhi ya makala na story zake za mbele (hasa ktk gazeti lao la Jumapili) hupenyezwa na mafisadi.
 
Hivi WaTanganyika mnakubaliana na hizi kauli za kuwa Vyama vya upinzani hamjawa tayari ?
Maana Zenji kasi yao wanasema hata wakiamshwa usiku wa manane kupiga kura basi Sultani CCM haoni ndani ni out tena anatupwa mbali sana ,na kila siku ziendavyo ndivyo inavyozidi kuwekwa pembeni na kuambiwa imetosha baba ,Wazenji wanataka kuizima na kuipunguza CCM EMPIRE na kuibakiza huko Tanganyika ,ila juhudi zikifanywa hata baadhi ya mikoa wanaweza kuipunguza CCM EMPIRE ,yaani Mikoa mitatu mikuu ikipunguzwa basi itakuwa hatua si ndogo ,tuikomboe Kilimanjaro Arusha,Mtwara ,Tanga ,Dar es salaam,Mwanza ,Mbeya na Kagera na mikoa mingine kumega mega ,mbona 2015 Usulutani wa CCM utakuwa umebakiza mikia tu.
NNAAAAAM bado sana kunahitajika miaka kumi zaidi.kwa mtaji wa kuruhusu democrasia ndani ya chama ndipo upinzani utakuwa umekomaa.
 
Wajuzi, Naomba kuuliza:
Hivi kamati ya maadili imewahi kufanya nini significant katika kuhakikisha kuwa Chama tawala kina steer the country in the RIGHT direction kimaadili? Najaribu kutafakari matukio mbalimbali ya ukosefu wa maadili ambayo yamelifikisha taifa pahala pabaya na sikumbuki kusikia hatua zozote decisive licha ya maneno matupu ya hapa na pale.
SAMAHANI MAANA KUULIZA SIYO UJINGA WAKUU.
 
Mkulu FMES, bado hakuna nyeti iliyopenyeza toka kwenye kamati ya maadili? walikuwa wanamjadili nani kule? ndugu yangu Dkt.Harisson Mwakyembe au Rostam Aziz?? najua hawawezi kumgusa Rostam Aziz kama chama lakini wanaweza kumgusa Mwakyembe kwasababu si mfadhili(kwa mtindo wa kifisadi) wa chama wala si fisadi.
 
Wajuzi, Naomba kuuliza:
Hivi kamati ya maadili imewahi kufanya nini significant katika kuhakikisha kuwa Chama tawala kina steer the country in the RIGHT direction kimaadili? Najaribu kutafakari matukio mbalimbali ya ukosefu wa maadili ambayo yamelifikisha taifa pahala pabaya na sikumbuki kusikia hatua zozote decisive licha ya maneno matupu ya hapa na pale.
SAMAHANI MAANA KUULIZA SIYO UJINGA WAKUU.

sina uhakika na sidhani kama wameshafanya lolote! maana kila siku wanachama wao hawaishi kutwangana, kupigana vijembe vya hapa na pale. na ikitokea mtu kuhoji kulikoni mambo yanaenda ndivyo sivyo ? mzee makamba atakwambia ni mambo ya ccm waachiwe ccm wenyewe.......au kama hiyo haitoshi atakwambia wewe unayeuliza hivyo umefungiwa rizki na Mungu mbinguni na duniani, ( vitu ambavyo haviingi akilini ). Mbaya zaidi usimuulize Chiligati!
 
Yaani uongozi wote wa CCM is a joke! Pale wamewekana mafisadi wote alafu wanataka kutueleza nini? Hiyo kamati ya maadili wangei-dissolve tu na wasiwe nayo maana hakuna cha maana wanachofanya zaidi ya kuendeleza majungu!
 
Tatizo leo ni tarehe 20 angalkau tungesikia kesho ndio watafunga kikao au kainzi kamepigwa fagio. Itabidi sasa tutumie vinyonga.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom