CCM: Jembe na Nyundo ni alama sahihi kwa nyakati?

Mkulima aliyekonda kupita kiasi kwa sababu wanamtegemea kupata kura na kula lakini hawampi kitu!
 
Layout%202.jpg
 
Mi naona kwa mbele waweke picha ya jamaa baunsa akiwa kamkanyaga raia mnyonge kwa miguu then mkononi awe ameshika bastola simply kuonyesha ukatili wanaoufanya dhidi ya watanzania maskini... Na kwa nyuma waweke picha ya bangi kuonyesha hawatumii elimu bali wanakwenda kibangebange..
 
Ndugu zangu,
enzi za mwalimu CCM kilikuwa chama cha wafanyakazi na wakulima na ndio maana bendera yake ina jembe ikimaanisha wakulima na ina nyundo ikimaanisha wafanyakazi lakini sasa watu hawa hawana nafasi tena ndani ya chama.hinyo kuna umuhimu wa kubadilisha nembo hizo kwenye bendera ya CCM.
Kwa kuwa sasa CCM kimekuwa chama cha wafanyabiashara na familia zao,kuna umuhimu na bendera yao isadifu wanachama wake. je kama wewe wamekupa tenda ya kubuni nembo mbadala wa JEMBE na NYUNDO UNGEWEKA NEMBO GANI?

mimi naona ningeweka alama yapunda kabeba mzigo mzoto kuliko uwezo wake na nyuma yake kuna mtu anafimbo anapiga.
 
ndugu zangu,
enzi za mwalimu ccm kilikuwa chama cha wafanyakazi na wakulima na ndio maana bendera yake ina jembe ikimaanisha wakulima na ina nyundo ikimaanisha wafanyakazi lakini sasa watu hawa hawana nafasi tena ndani ya chama.hinyo kuna umuhimu wa kubadilisha nembo hizo kwenye bendera ya ccm.
Kwa kuwa sasa ccm kimekuwa chama cha wafanyabiashara na familia zao,kuna umuhimu na bendera yao isadifu wanachama wake. Je kama wewe wamekupa tenda ya kubuni nembo mbadala wa jembe na nyundo ungeweka nembo gani?

nyundo na jembe
 
Ninapenda kujiuliza mwenyewe na vinginevyo ni jibiwe na mana JF

Alama ya jembe na nyundo ipo mahususi kumvunja nguvu mkulima kwa kutomfungua kwamba kilimo kina fuata mkondo wa technolojia,...Jembe ndilo kimbilio tu la mtanzania na hivyo tusahau rasilimali nyingine,..... jembe limetumika miaka mingi na kunyon`gonyesha watanzania kwa kudhoofisha afya zao wakilitumia,.... Nyundo hiyo pia imetumika na mafisadi kubomoa nyumba za walala hoi na kuwaibia rasilimali,.... nyundo imetumika pia kuvunja maboxi ya kura,.... nyundo imetumika pia kuibomoa benki kuu kuchukua fedha za uchaguzi....nyudo sasa inatumika kulinda maovu...

Je bado tunahitaji Jembe na Nyundo
 
WanaJF,

Maneno hayo nimeyaazima kutoka kwenye post za Isekuu na LAT.

Nimejikuta natafakari nini maana ya alama ya Jembe na Nyundo. Je wakati haubadilishi maana? Jembe na Nyundo vimebaki, watu wamebadilika. Je sio muda wa kubadili nembo? Nadhani Umma na Kisu itafaa zaidi.

Ni ushauri tu kwa CCM.
 
Hata wasipobadili nembo naamini kwamba uhalisia unaonekana kwamba ni Tucta (nyundo) waliokataa kuwaalika kwenye sherehe za mei mosi na ndio hao hao wana akili za mbayuwayu! Ni wakulima (jembe) ambao leo hii hawana uhakika kama wanalima au la! Mvua sio za uhakika!

Najiuliza, Rostam ni Nyundo au Jembe? Ngeleja?
 
Hakika ni umma na kisu kwa ajili ya mafisadi kusosomolea vinono huku makabwela wakilala bila chochote tumboni. Hata ukiongeza na mrija sio mbaya.
 
hahahahahahahahaaa! uko juu mkuu. ni kweli ishakuwa uma na kisu siku nyingi kidogo kilichopita. selfishness. mwingine mshahara laki unusu na mwingine milioni kumi. wote watumishi wa umma na soko lao ni moja. kima cha juu hakipaswi kuwa zaidi ya m1 kwa serikali yetu na ndo heshima kwa wananchi itakuwapo. kwa sasa wala hawatakumbuka kitu na hata kama mafuta ya gari yangefika elfu 5 kwa lita kwa kuwa hutumia magari ya umma hadi kwenda sokoni na hata ukweni. sukari ikifika alfu 3 wala si tatizo pia. wamebaki kuimba tu wao watoto wa wakulima. wakatae mishahara yao na wapewe ya walimu then tuone kama hawatapunguza wizi kwa kuwa watafeel pinch tuipatayo sisi wengine.
 
WanaJF,

Maneno hayo nimeyaazima kutoka kwenye post za Isekuu na LAT.

Nimejikuta natafakari nini maana ya alama ya Jembe na Nyundo. Je wakati haubadilishi maana? Jembe na Nyundo vimebaki, watu wamebadilika. Je sio muda wa kubadili nembo? Nadhani Umma na Kisu itafaa zaidi.

Ni ushauri tu kwa CCM.

Hilo mkuu halina ubishi!!!
 

Attachments

  • uma na kisu.gif
    uma na kisu.gif
    1.2 KB · Views: 194
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom