CCM itavuka changamoto hizi; Kidumu Chama cha Mapinduzi!

Kaleta hoja na kama kuna watu wanaona hoja za ndugu yetu huyu ni dhaifu zioneshwe hivyo; kuzipuuzia au kumuita yeye majina hakufanyi hoja nyingine kuwa na nguvu. Turudi kwenye hoja hujibiwa kwa hoja!

Mkuu Mimi nilivyoelewa hapa huyu hajaleta hoja hapa kuijadili, ameleta suggestions zake anavyotaka mambo yawe... Nathani watu from their opinions wanamueleza not in too many words kwamba haiwezekani..... He does not have a Case
 
7. mwenge wa uhuru utumike kuimarisha uzalendo na uwajibikaji wa raia katika kushiriki michakato mbalimbali ya kidemokrasia na kuamsha ari ya kisiasa kwa wale amabo ari hiyo imeshuka (rejea idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura)

Wewe ni mbunge wa kuchaguliwa au wa viti maalum? Nimekutoa kasoro hizi:

1. Unaandika kama unavyoongea (your punctuation is poor)
2. Ni mwongo fulani hivi.

Haya tuje hiyo hoja yako namba 7:

1. Nchi gani duniani iliyofanikisha kukuza uzalendo wa watu kwa kutumia mwenge?
2. Nani anakagua mapato na matumizi ya mwenge?

Wabunge aina yenu, mnatubebesha mzigo wananchi. Nyie uwakilishi wenu ni mnadani kwenye :hungry::hungry:
 
Mbunge wa CCM, ana hoja! Zaidi ni vema kuwepo na link ya moja kwa moja toka kwa viongozi na wananchi. Kwa muda mrefu hili limekuwa ni tatizo na hasa pale viongozi wanapoamua kuwapangia wananchi wao nini cha kufanya.

CCM inapaswa kubadilika toka katika mfumo wake wa sasa wa uongozi, iwapo inahitaji kurejesha imani yake kwa vijana. Ni jukumu la CCM kujua vijana wa sasa wanahitaji nini na wanataka nini, hii itaweza kufanikiwa tu iwapo chama, kupitia wabunge wake kushiriki katika shughuli za kila siku za vijana na kujua matatizo yao na namna gani wataweza kujatatua.
 
La kuvunda halina ubani.
 
watu wengi hapa JF ni wakurupukaji tu si wajadili hoja. mh. ana hoja tena kubwa sana. na usipojua how to play a political game utaishia kumuona kama anaongea njozi zake lakini, i belive the guy is smart.

mi sijaridhika na mkakati wake wa kutumia mwenge wa uhuru kuhamasisha kwani itawagharimu sana kama wataamua hivyo kwa sababu ulishachokwa sana na wadau. kama watatumia mbinu nyingine, i agree. best wishez mbunge wangu
 
Kaleta hoja na kama kuna watu wanaona hoja za ndugu yetu huyu ni dhaifu zioneshwe hivyo; kuzipuuzia au kumuita yeye majina hakufanyi hoja nyingine kuwa na nguvu. Turudi kwenye hoja hujibiwa kwa hoja!

Mwanakijiji, nadhani hututendea haki sisi tuliochukua muda wetu kutafakari na kumjibu mleta hoja kwa hoja ambazo si yeye mwenyewe wala mtu mwingine wa upande wake ameweza kuzijibu. Kwa hiyo si fair kutuweka kwenye kapu moja na wale ambao wame-blast hoja ya jamaa bila kutoa maelezo yao!

kweli mkuu, ..... hoja zake naona ziko wazi.... lakini watu wameng'ang'ania kuzipuuza.............

baki kwenye hoja.......... nina wasiwasi kama chama chenyewe kina utashi wa kutosha kufanya hayo aliyoshauri/aliyopendekeza.... inavyoonekana yeye hakubahatika kupata uwaziri ndio maana anawapongeza wenzake..... lakini nin shauku pia ya kuhoji yeyey kama si waziri na nakumbuka pia aliwahi kusema kuwa ni mwanachama wa kawiada ndani ya ccm na si mjimbe wa kikao chochote chenye nguvu ndani ya ccm.... sasa katika subordinate status kkama hiyo ndani ya chama kikibwa, kikongwe, well established na bureaucratic kama ccm atapenyezaje ushawishi wake huo?........ labda atusaidie kama ana mkakati maalum anaofikiria kuutumia ndio unaomfanya kuwa optimistic kiasi hiki kuwa ccm itavuka.... aulete nasi tumchangie mawazo.......... thanks and best wishez...................

Mkuu,

Watu tuliowengi tumejaribu kumweleza huyu jamaa kuwa ..kweli inawezekana anayo wish list nzuri..lakini hiyo siyo wanayoitaka CCM Kwa hiyo, hakuna mtu ndani hicho chama (hasa wale viongozi wa juu) anayeweza kuuunga mkono hoja zake kwa kuzichukua na kuzifanyia kazi. CCM imebaki kama kikundi cha mafia na kila mtu anaangalia tumbo lake na anakula kwa urefu wa kamba yake. Katika mazingira hayo, jambo lolote linalolenga kuziba mianya ya hao wenye kiu ya kula kama vile hawatakufa halina nafasi mbele yao. Labda aje atueleze yeye atawezaje kuyafanya hayo ambayo hata babu zake walionza na TANU wamenyoosha mikono!
 
Kaleta hoja na kama kuna watu wanaona hoja za ndugu yetu huyu ni dhaifu zioneshwe hivyo; kuzipuuzia au kumuita yeye majina hakufanyi hoja nyingine kuwa na nguvu. Turudi kwenye hoja hujibiwa kwa hoja!

Mbunge wa CCM, ana hoja! Zaidi ni vema kuwepo na link ya moja kwa moja toka kwa viongozi na wananchi. Kwa muda mrefu hili limekuwa ni tatizo na hasa pale viongozi wanapoamua kuwapangia wananchi wao nini cha kufanya.

CCM inapaswa kubadilika toka katika mfumo wake wa sasa wa uongozi, iwapo inahitaji kurejesha imani yake kwa vijana. Ni jukumu la CCM kujua vijana wa sasa wanahitaji nini na wanataka nini, hii itaweza kufanikiwa tu iwapo chama, kupitia wabunge wake kushiriki katika shughuli za kila siku za vijana na kujua matatizo yao na namna gani wataweza kujatatua.

Heshima mbele mkuu,

Hivi unamaanisha hadi sasa kuna mtu yeyote ndani ya CCM ambaye hayajui matatizo ya chama na Taifa kwa ujumla wake? Kama wapo basi..tufwile nyambala!!!

Kwa jinsi washabaki wa CCM wanavyojieleza inaonesha kitu kimoja kikubwa...kwamba CCM wanao uwezo mkubwa wa kuainisha matatizo na changamoto zinazowakabili, shida inakuja kwenye kutafuta suluhu. Badala ya kutuorodheshea changamoto..nilidhani kuna mtu atatuletea walau roadmap ya kichina. Sijaona hata mmoja. Inakuwa kana kwamba tumbo la CCM limekuwa tasa..hakuna tena uzao ulio na upeo wa kujenga mikakati ya kulikomboa taifa. Kimebakia kizazi kilicholaaniwa na kulowea kwenye ulafi na ufisadi..Hiyo laani ndiyo inayoifikisha CCM kwenye mwisho wake soon!
 
Mkuu,

Watu tuliowengi tumejaribu kumweleza huyu jamaa kuwa ..kweli inawezekana anayo wish list nzuri..lakini hiyo siyo wanayoitaka CCM Kwa hiyo, hakuna mtu ndani hicho chama (hasa wale viongozi wa juu) anayeweza kuuunga mkono hoja zake kwa kuzichukua na kuzifanyia kazi. CCM imebaki kama kikundi cha mafia na kila mtu anaangalia tumbo lake na anakula kwa urefu wa kamba yake. Katika mazingira hayo, jambo lolote linalolenga kuziba mianya ya hao wenye kiu ya kula kama vile hawatakufa halina nafasi mbele yao. Labda aje atueleze yeye atawezaje kuyafanya hayo ambayo hata babu zake walionza na TANU wamenyoosha mikono!

Heshima mbele mkuu,

Hivi unamaanisha hadi sasa kuna mtu yeyote ndani ya CCM ambaye hayajui matatizo ya chama na Taifa kwa ujumla wake? Kama wapo basi..tufwile nyambala!!!

Kwa jinsi washabaki wa CCM wanavyojieleza inaonesha kitu kimoja kikubwa...kwamba CCM wanao uwezo mkubwa wa kuainisha matatizo na changamoto zinazowakabili, shida inakuja kwenye kutafuta suluhu. Badala ya kutuorodheshea changamoto..nilidhani kuna mtu atatuletea walau roadmap ya kichina. Sijaona hata mmoja. Inakuwa kana kwamba tumbo la CCM limekuwa tasa..hakuna tena uzao ulio na upeo wa kujenga mikakati ya kulikomboa taifa. Kimebakia kizazi kilicholaaniwa na kulowea kwenye ulafi na ufisadi..Hiyo laani ndiyo inayoifikisha CCM kwenye mwisho wake soon!

mkuu DC
nimekusoma katikati ya mistari na nimeona unachozungumza na kwa ufasaha. mimi naona ccm inaponzwa na ukubwa na ukongwe wake kiasi kwamba hata dhahabu ingeletwa na mmoja wa wanachama wake wadogo itatupiliwa mbali kama kinyesi. ila naona kama mh. mbumge ni mmoja wa vijana wanaokitakia chama chao a bright future. yeye kajitokeza, wengine bado wamejificha chini ya mbawa lakaini naamini wapo. mimi mwenyewe ni mwana ccm lakini sijainuka kwenye active politics. naamini tukiinuka wote na kushikamana pamija na hawa wachache waliopata nafasi (japo si kubwa sana) kama hii ya ubunge, tunaweza kusanmbaza influence na kukijenga chama chetu ngazi za chini na miongoni mwa makundi kama ya vijana yanayomyima usingizi mheshimiwa huyu
 
Heshima mbele mkuu,

Hivi unamaanisha hadi sasa kuna mtu yeyote ndani ya CCM ambaye hayajui matatizo ya chama na Taifa kwa ujumla wake? Kama wapo basi..tufwile nyambala!!!

Kwa jinsi washabaki wa CCM wanavyojieleza inaonesha kitu kimoja kikubwa...kwamba CCM wanao uwezo mkubwa wa kuainisha matatizo na changamoto zinazowakabili, shida inakuja kwenye kutafuta suluhu.
Tatizo sio kutafuta suluhu, CCM inaanzia kwenye ngazi ya shina, tawi n.k. Kwa muda mrefu CCM imekuwa ikiweka uzito mdogo katika ngazi za chini, labda kwa kujiamini ama kutokana na kukumbatia wenye uwezo, hivyo kuzorotesha uhai wa chama. Ni vema kwa CCM kurudi nyuma na kutumia misingi yake katika kuboresha chama.

Kitu kingine, ni kwa viongozi wa sasa wa chama, wengi wao wakati umewapita! Ni vema kwao kujiondoa ili kupisha damu mpya yenye mwelekeo wa sasa.
 
Mkuu from my experience humu Jamvini you are in the wrong place i think this is the wrong audience for you...... Most people hapa wamechoka na SAME OLD SAME OLD STORIES; and they want Change am sure hata wewe since umekuwa hapa jamvini since 2009 umeona hayo.

In that sense then we should change the motto to "This is where Chadema dares to talk openly"
 
What I said was people are Tired of Same Old Same Old Stories and the need Change...... I did not say where that change will come from lakini kutoka kwenye jibu lako inaonyesha deep down you know that Change can come from chadema
 
of course CHADEMA is the only solution for the better life of all tanzanians
 
Sasa umeleta Hoja kama mbunge au kama mwanachama na kada wa CCM ambaye ni mbunge.
Naona mawazo yako yamekaaa zaidi kujenga chama badala ya jimbo hata unalowakilisha. kama jina lako linavyosema ulitakiwa kuongea uliyayasema kwa mtazamo mwingine.

1. kupeleka itikadi ya chama kwa kundi la vijana amabo wanonekana kushabikia mambo wasiyoyajua vizuri hali inayotafsiriwa kuwa vijana hawakitaki tena chama cha mapinduzi japo uzoefu unaonyesha kuwa vijana wamekuwa hawatabiriki siku zote na katika nchi mbalimbali - VIjana hawataki itikadi ya CCM wala CHADEMAau CUF . LOwasa juzi kasema vijana wanchukia CCM sababu hawana ajira. Lakini kuna ukweli lowasa kaukwepa sababu anazozijua . Haata hizo ajira haziwezi kupatikana kama kuna RICHMOND,EPA, RADA. etc.

2. chama kijikite katika kujenga taswira ya kuaminika machoni pa wananchi ikiwa ni pamoja na kujiweka kando na matendo yanayoweza kukiunganisha na mamabo yanayopigwa vita nchini kwa sasa kama ufisadi nk. Kama nilivyosema hapo juu Taswira ya kuaminika inatakiwa kuanza kuwashughulikia MAFISADI.Inaonekana kuna double standard ya SHERIA CCM. Sheria ya ya Prof Mahalau na Chenge na Sheria nyingine kwa ajili ya mpendazoe. Huku sheria nyingine akifanya maigizo na Liyumba, Mramba. Hapa CCM hawezi kuaminika

juhudi zisizo za dhahiri sana zifanywe kwenye idara za usalama wa taifa na vyombo vingine vya dola kuweka mizania ya chokochoko za udini, ukabila na uzanzibari katika urari ili kupunguza taratibu na hatimaye kumaliza kabisa hofu iliyoanza kujengeka ya kukua kwa hali hizo zisizoendana na utamaduni wa siasa zetu- CCM kama bado inaufuata ujamaa ikajifunze kwa wachina Idara ya usalama wa Taifa ya china ilivyosaidia kukuza Uchumi na teknolojia ya china. Tunataka kuona Idara ya usalama inakitengo cha Uchumi na Teknolojia. Sio vitengo cha siasa na kufatilia itikadi za watu. haya ndo yanatakiwa kuwa mawazo wabunge wa karne hii.

Kifupi kama wabunge wenyewe weye majority ndo nyie business as usual wish 2015 come tommorow.
 
Mkuu, vijana wanajua vizuri sana mambo yanayowahusu... kwa kuanza hivi tu kwangu mimi ni kwamba wewe ndio hujui vizuri... kuna upuuzi mmoja wanasiasa wengi mnao.. you think kwamba you are just think tanks by default. wewe ndio hujui vizuri sir, remember hata ukienda kule kijijini kwenu waweza kudhani kwamba watu hawajui vizuri, in fact they know but its our attitude that put them off
100.1% right
 
Mimi namshauri kama kweli huyu ni mbunge kwenye celebrum na medula oblngata yake aondoe memory ya itikadi za chama Badala yake a overwwite space ilokuwa na itikadi ya chama na real requirement za jimbo lake.

  • Tutashangaa tukikuuliza idaidi ya shule zasekondari na primary zilizopo jimboni mwako ukawa hujui

  • Utachekesha kama Mbunge unasisitiza Itikadi ya chama wakati hujui idadi ya madaktari walimu au wanafunzi waliopo jimboni mwako

Je muheshimiwa mbunge toka upate ubunge unaweza kutupa japo takwimu zozozte chache za jimbo lako?
 
ndugu watanzania wenzangu

kwanza nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwatakia utumishi mwema wenye mafanikio mawaziri wote walioteuliwa katika wizara mbalimbali pamoja na wasaidizi wao. nawahalkikishia pia ushirikiano wangu katika kutimiza majukumu yemnu mliyokabidhiwa kwa manufaa ya serikali ya CCM na taifa zima kwa ujumla.

hivi karibuni tumeshuhudia gumzo pana na refu lililohusishwa na kitendo cha wabunge wa chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma wakati mh. rais akianza kusoma hotuba yake ya kuzindua bunge la 10.

binafsi niseme wazi kuwa sikushtuka wala kushangaa. nilikuwa nimeishajiandaa kwa tukio lile kwani ilishajulikana kuwa ingekuwa vile. ila nilichoona ni kuwa kuna mambo ambayo wanaCCM tunapaswa kujifunza na kuwa tayari kama tunataka chama chetu kivuke wimbi hili la mabadiliko. mambo hayo ni kama ifuatavyo
1. kupeleka itikadi ya chama kwa kundi la vijana amabo wanonekana kushabikia mambo wasiyoyajua vizuri hali inayotafsiriwa kuwa vijana hawakitaki tena chama cha mapinduzi japo uzoefu unaonyesha kuwa vijana wamekuwa hawatabiriki siku zote na katika nchi mbalimbali

2. chama kijikite katika kujenga taswira ya kuaminika machoni pa wananchi ikiwa ni pamoja na kujiweka kando na matendo yanayoweza kukiunganisha na mamabo yanayopigwa vita nchini kwa sasa kama ufisadi nk.

3. chama kupitia serikali yake kijitahidi kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayotokana na ilani yake ya uchaguzi ili kidhihirishe kwa vitendo utashi na uwezo wa kusimamia juhudi za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini

4. kwa wakati huu chama kijitenge kabisa na hatua yoyote ya kukaa na chadema ama chama chochote kingine kujadili jamabo lolote la kitaifa na iwapo itaonekana vyema basi chama kichukue hatua chenyewe bila kushirikisha chamas kingine

5. chama kiimarishe ushirikiano na vyama vya CUF na vingine vilivyo vidogo ili kujihakikishia kuungwa mkono na wadau anwai wa maendeleo

6. juhudi zisizo za dhahiri sana zifanywe kwenye idara za usalama wa taifa na vyombo vingine vya dola kuweka mizania ya chokochoko za udini, ukabila na uzanzibari katika urari ili kupunguza taratibu na hatimaye kumaliza kabisa hofu iliyoanza kujengeka ya kukua kwa hali hizo zisizoendana na utamaduni wa siasa zetu

7. mwenge wa uhuru utumike kuimarisha uzalendo na uwajibikaji wa raia katika kushiriki michakato mbalimbali ya kidemokrasia na kuamsha ari ya kisiasa kwa wale amabo ari hiyo imeshuka (rejea idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura)

8. kujitahidi kulipatia ufumbuzi suala la mambi ya kuasisiwa mchakayo wa kuandikwa katiba mpya lakini bila uharaka na kupeleka turufu yake kwa wapinzani wa CCM

kuna mengi, lakini kwa haya machache niseme kuwa Tanzania yenye ufanisi tele inawezekana chini ya CCM

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZU

Na sisi tusio wa CCM ujumbe wako kwetu ni nini?
 
Tatizo sio kutafuta suluhu, CCM inaanzia kwenye ngazi ya shina, tawi n.k. Kwa muda mrefu CCM imekuwa ikiweka uzito mdogo katika ngazi za chini, labda kwa kujiamini ama kutokana na kukumbatia wenye uwezo, hivyo kuzorotesha uhai wa chama. Ni vema kwa CCM kurudi nyuma na kutumia misingi yake katika kuboresha chama.

Kitu kingine, ni kwa viongozi wa sasa wa chama, wengi wao wakati umewapita! Ni vema kwao kujiondoa ili kupisha damu mpya yenye mwelekeo wa sasa.

Umeona Kibunango..unerudia kile kile ninachokisema. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CCM..kila mtu ni kujisemea na kutoa wishes zake kuanzia kwenye shina hadi taifa. Wanachama wanaongea tu hakuna anayewasikiliza..mtendaji mkuu wa serikali analilia tu...Mwenyekiti huyo anafanya kuchekacheka..Kwa ufupi CCM imegota. Inahitaji nguvu kubwa sana tena kutoka nje kuiondoa kwenye hilo tope. Labda nikikumbushe kuwa katika hili suala la CCM, principle of inertia ndiyo inayofanya kazi. Kwa hiyo hata wakiendelea kutumia dola kushinda uchaguzi...hawawezi kubadilika kwa lolote labda wapate nguvu ya ziada kutoka nje. So far, siioni hiyo nguvu zaid ya vita vya kunyang'anyana vikuku na vidagaa!
 
ndugu watanzania wenzangu

kwanza nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwatakia utumishi mwema wenye mafanikio mawaziri wote walioteuliwa katika wizara mbalimbali pamoja na wasaidizi wao. nawahalkikishia pia ushirikiano wangu katika kutimiza majukumu yemnu mliyokabidhiwa kwa manufaa ya serikali ya CCM na taifa zima kwa ujumla.

hivi karibuni tumeshuhudia gumzo pana na refu lililohusishwa na kitendo cha wabunge wa chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma wakati mh. rais akianza kusoma hotuba yake ya kuzindua bunge la 10.

binafsi niseme wazi kuwa sikushtuka wala kushangaa. nilikuwa nimeishajiandaa kwa tukio lile kwani ilishajulikana kuwa ingekuwa vile. ila nilichoona ni kuwa kuna mambo ambayo wanaCCM tunapaswa kujifunza na kuwa tayari kama tunataka chama chetu kivuke wimbi hili la mabadiliko. mambo hayo ni kama ifuatavyo
1. kupeleka itikadi ya chama kwa kundi la vijana amabo wanonekana kushabikia mambo wasiyoyajua vizuri hali inayotafsiriwa kuwa vijana hawakitaki tena chama cha mapinduzi japo uzoefu unaonyesha kuwa vijana wamekuwa hawatabiriki siku zote na katika nchi mbalimbali

2. chama kijikite katika kujenga taswira ya kuaminika machoni pa wananchi ikiwa ni pamoja na kujiweka kando na matendo yanayoweza kukiunganisha na mamabo yanayopigwa vita nchini kwa sasa kama ufisadi nk.

3. chama kupitia serikali yake kijitahidi kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayotokana na ilani yake ya uchaguzi ili kidhihirishe kwa vitendo utashi na uwezo wa kusimamia juhudi za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini

4. kwa wakati huu chama kijitenge kabisa na hatua yoyote ya kukaa na chadema ama chama chochote kingine kujadili jamabo lolote la kitaifa na iwapo itaonekana vyema basi chama kichukue hatua chenyewe bila kushirikisha chamas kingine

5. chama kiimarishe ushirikiano na vyama vya CUF na vingine vilivyo vidogo ili kujihakikishia kuungwa mkono na wadau anwai wa maendeleo

6. juhudi zisizo za dhahiri sana zifanywe kwenye idara za usalama wa taifa na vyombo vingine vya dola kuweka mizania ya chokochoko za udini, ukabila na uzanzibari katika urari ili kupunguza taratibu na hatimaye kumaliza kabisa hofu iliyoanza kujengeka ya kukua kwa hali hizo zisizoendana na utamaduni wa siasa zetu

7. mwenge wa uhuru utumike kuimarisha uzalendo na uwajibikaji wa raia katika kushiriki michakato mbalimbali ya kidemokrasia na kuamsha ari ya kisiasa kwa wale amabo ari hiyo imeshuka (rejea idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura)

8. kujitahidi kulipatia ufumbuzi suala la mambi ya kuasisiwa mchakayo wa kuandikwa katiba mpya lakini bila uharaka na kupeleka turufu yake kwa wapinzani wa CCM

kuna mengi, lakini kwa haya machache niseme kuwa Tanzania yenye ufanisi tele inawezekana chini ya CCM

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZU

Wewe uliyepewa ukuu, jina lako pia ni fisadi, mapenzi yako taimizwe huko CCM tu; hapa si forum ya CCM, na pia wengi hatuhitaji kusikia hizo geresha zenu za miaka nenda miaka rudi!!! Watanzania wana uchungu sana kwa maumivu ambayo serikali imewaletea na inaendeleata kuwaletea hadi 2015; so kama unataka kuheshimiwa na kusikilizwa, bora usemee hizo bla bla zako CCM forums....hapa tunahangaika na jinsi ya kujikomboa kwenye kongwa mlilotutwika; Bye mbunge wa CCM na NEC
 
Back
Top Bottom